Heri ya mwaka Mpya!
Sasa umegonga zaidi ya 40 unajisikiaje? Nakumbuka nilipokuwa in my 20s Ma-Celeb walikuwa wanasema wanajisikia kama walivyokuwa in their 20s....wakaibua msemo wa 40s in new 20s. Kwangu binanafsi nakuhakikishia sio kweli kwa asilimia Mia moja, kwasababu nilipokuwa na umri nusu wa nilionao sasa, sikuwa najiamini kwenye kufanya maamuzi Kiuchumi, Kimwili na Kimahusiano(ndugu, marafiki, mpenzi) na kijamii kwa ujumla.
Kama ulichelewa kuwa na watoto basi ujue utapoteza umuhimu wa baadhi ya mahusiano na watu wengine sababu watoto wako ni muhimu zaidi kwa sasa kuliko hao watu wengine, sio hivyo tu wanao wanakupa sense ya ukamilifu na kuridhika na maisha uliyonayo na hutaki kupoteza muda kufanya mambo nje ya familia yako ulioitengeneza na Mumeo/Mkeo.
Kwa wale waliokuwa na watoto ktk umri mdogo, wanaweza kuikuta wapweke sababu watoto wamekua na wanajitegemea hivyo ktk umri wa miaka 40na unaweza kujikuta unatamani kujenga mahusiano na watu wengine nje ya Mwenza wako au kama bado upo nae basi unafurahia uhusiano wenu wa kimwili huku ukielekea umri wa kufunga Hedhi bila kuhofia Mimba aka late 40s.
Ktk umri huu ambao unakaribia nusu Karne na una watoto chini ya miaka 15....kutumia miaka yako iliyobaki na wanao na pia kujitahidi kufurahia maisha yako na mwenza wako inakuwa jambo muhimu sana kwa sababu tayari ulifanya starehe na kuishi ujana wako wote na ukaumaliza. Kwa maana nyingine ukifika miaka 50, unakuwa umeishi/maliza miaka mingi nyuma kuliko miaka ijayo/iliyobaki.
Kipindi hiki unaona thamani ya maisha, unapata kutazama nyuma na kushukuru yote uliyopitia wewe kama wewe bila wategemezi wako(watoto), hayo ukichanganya na malezi yako unawagea watoto wako bila msaada wa Bibi/Babu zao...sababu technically wanao ni wajukuu zako uliojizalia mwenyewe....haichekeshi? Soma tena kwa utulivu.
Miaka 40 hakika ni kama vile miaka 20 kihisia na kimwili, ila sasa inategemea na mtindo wa maisha ulioishi miaka 20 nyuma. Kiakili unakuwa mwepesi kushika masomo/mambo hasa ukiamua kurudi shule au kujifunza ujuzi mpya ili ubadili Career baada ya watoto kukua, hasa kama ulikuwa Mama wa kunyumba full tume kama mimi.
Tofauti ingine ni Fashion sense yako inabadilika, badiliko hili linaeza kuwa Hasi au Chanya...mie binafsi style yangu ni ile ile classic-smart-casual na sidhani kama itabadilika, Pamoja na kuwa tofauti sio kubwa sana, ni muhimu kuangalia afya yako kwa ukaribu nje na ndani kwa ajili ya umri mkubwa ujao wa miaka 80 and beyond.
Takuona tena, ukiniona bai.
Comments