Sunday, 19 July 2015

Kula Fresh Vs Natural?

Hi.....kwa mara nyingine!

Back in 2006 kulikuwa na mabishano kuhusu matumizi ya vitu ambavyo sio asili kwa matumizi ya Mwanadamu.Wengi wetu (tukisaidiwa na chunguzi mbalimbali) tuliamini kuwa matumizi ya vyakula vya Kopo, Madawa ya kutibu, aina za Sabuni, matumizi ya Microwaves n.k huenda ndio sababu ya magonjwa  Mengi yasiyotibika na kuu ni Saratani.
Miaka ikapita na tukakugundua kuwa kutokana na Maendeleo ya Teknolojia kwenye kila kitu hakuna u-natural......kwamba hakuna mtu anakula kiasilia kwasababu mazao yote yanakuzwa na Mbolea ambayo ni "man made".Ukiachilia mbali Mbolea ni Maji tutumiayo kumwagilia mimea na madawa ya kuua wadudu wanaoshambulia Mazao.....Umepata idea ya wapi naelekea ambako sitaki kufika(sitaki post ndefu).
Bado mabishano yapo au niseme yameamia kwenye utunzaji wa ngozi na Nywele. Watu wanajisifu kuwa wao ni Natural na hawataki Chemical(relaxer) kwenye miili yao lakini bado wanakunywa maji (bombani au chupani yote yanakemikali).Wanatumia Sabuni na bidhaa nyingine kusafisha nguo na miili yao. Wanakula chakula ready made(kopo au paketi).....wanapaka Manukato na kupaka Vipodozi.Wanatumia bidhaa zinazorangazwa kuwa ni "all natural" hakuna kinachotengenezwa na kukaa Dukani bila kuwa na "kemikali" ya kusaidia kiendelee kuwa salama kwa mayumizi yako.


"All natural" inalipa lakini haina maana kuwa ni "all" hata kama wameandika vikivyomo kwenye bidhaa hiyo. Kumbuka sio lazima waandike au wakuambie kuwa kuna Asilimia Kumi na Moja ya Kemikali ili kusaidia bidhaa hiyo kudumu kwa muda mrefu.
Sooooo chagua kula Fresh na sio Natural......fanya utakavyo juu ya mwili wako lakini usijitambe(bado mnatumia neno hili?) Kwamba wewe ni "natural" kwasababu hujajichubua au una-rock nywele zako bila kuosha wala kupaka Mafuta(achilia mbali relaxers).Mie ni mpenzi wa kula "natural" tangu enzi....lakini nikiwa mkweli ni kwamba nimekuwa nakula fresh na sio natural.Nikuache kwa sasa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.......babai.

Sijafa-sijaumbika....

Si nikaumwa Tetekuwanga!!!

Isije siku tunakutana ukaanza kunifokea/Suta kwanini nilisema nina ngozi nzuri wakati nimejawa na madoa ka Chui(as if unajali). So wacha nijihami mapemaa.
Sikutegemea kuwa siku moja ningeugua Ugonjwa huu so nilipoanza kuumwa nkasema Mimba nini?Unajua....unapofanya Mapenzi nyama kwa nyama na Mumeo kitu cha kwanza kuangalia ni Mimba kila unapojisikia vibaya ili nisijetumia Madawa nakuua au kulemaza Kiumbe(sio kwamba naitaka hiyo Mimba).Ndio hivyo sasa nimeugua gonjwa la Kiwahili(sio kweli).....akati nakua kuna watu (Majirani zetu) walikuwa wanatukuza magonjwa ya Kudumu kama vile Moyo,Kisukari nakadhalika.Utasikia "sie hatuumwi magonjwa ya Kiswahili kama Tetekuwanga, Typhod, Kifua kikuu na mengine yote ya kuambukiza. Tunaumwa Magonjwa ya maana kama vile Kisukari, Saratani, BP" hihihihihi.....sijui ulikuwa utoto wao au ujinga wao?Sitoki nje bila kujipaka tope(foundation) kuficha Madoa Meusi usoni....naaa hakuna kujiamini hapa.....natisha hahahaha.Next.....kipi muhimu kula Natural au Fresh?  Asante kwa kuichagua Blog hii.

Babai kwa sasa.

Monday, 13 July 2015

Chanya....Wanaume na tofauti zao (SY2)!

Hai?

Baada ya sehemu ya kwanza iliyofunikwa na Hasi (bado ninazo kibawo though)nimeona sio mbaya tukiangalia zile tofauti ambazo ni Chanya. Bila kupoteza muda twendeeee!


Wanakufia kimahama mpaka hawajielewi lakini sio ki-Romeo....hawa jamaa hawajui kuweka wazi hisia zao wazi kwa kukuambia wanakupenda na kukunidi na kukumisi kila siku, na Kamwe hutowasikia wakisema "bila wewe maisha yangu ni bure".


Utakuwa umeambiwa/umesoma mahali kuwa Mwanaume asipokuambia hivyo ujue hakupendi.....sio kweli!

Pili, wanafurahi kuonekana kama Familia, yaani siku hizi zile "date night" sijui "outings" hazipo.....kila mkitoka basi na wanenu pembeni. Ukimkumbushia "sisi"anakuambia "watoto bado wadogo kwanini tuwe wa binafsi na kujitoa wenyewe?"(family man?).

Tatu, Tangu mmefunga Ndoa hakaribishi rafiki zake ambao ni Single na ukaribu wake kwao unapungua. Sio kwamba anaogopa watakuiba bali anajihisi kuwa kwenye era nyingine ya Maisha yake.

Nne, Mara ya mwisho kukusifia ni siku ya kwanza kukuona lakini akikununulia zawadi lazma itaendana na style yao hata kama ni kwa mbali...ameisha kupata asa akusifie ilibiweje (adhaniavyo yeye).

Tano, kinachowatoa nyumbani ni Kazi au shughuli nyingine muhimu....lakini anachofurahi ni kuwa nyumbani na familia yake.

Sita, Pamoja na kuwa hawajui kuongea au kujieleza au wapi wakusisimue bado wakipanda Kiunoni hawatoki mpaka wahakikishe umegusa Kibo n....!

Saba, wahatumii "kama hutaki kunipa basi hunipendi" au kusema "mie nitaoa baada ya miaka 5" (huyu anakuambia sina mpango na wewe na sidhani tutavuka miaka 5 pamoja).

Nane, wanaweka extra protection ili wasikutie Mimba.....sio kwamba hawakupendi au wanadhani wewe una Magonjwa/Mchafu la hasha. Hawapo tayari  kuwa Baba at least not with  you (si umshukuru Mungu sasa).


Tisa, Huwasikii wakisema Mama yangu hivi au vile.....wanatambua kuwa wewe huchukui nafasi ya Mama zao na wanakuheshimu na kukuchukulia wewe kama wewe bila kutoa mifano ya Mama zao wapenzi.

Kumi, Kabla hawajafanya maamuzi makubwa/madogo wanakuhusisha ili kupata maoni yako.Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.

Friday, 10 July 2015

Baba/Mama yao Mzungu.....?

Watu(Wazungu) wanapouliza kama Mumeo/Mkeo ni Mzungu kwasababu watoto ni weusi na sio WEUSIiiiiii tii, unafurahi? Unakwazika?  au unapata (mie)nafasi ya kutoa Elimu kuwa Weusi wetu Waafrika unatofautiana na kwanini?Nilikwisha wahi gusia kuwa kuna baadhi ya watu Shuleni kwa Babuu wanadhani Baba yake ni Mzungu......nikiwa na Kibibi ambae hana rangi ng'avu sana kama Kaka yake bado watu wanadhani Baba yake ni Mzungu.

Halikadhalika watoto wakiwa na Asali wa Moyo (baba yao)bado wanauliza "is their mother white"?Inafikia mahali unachoka kutoa Elimu ya tofauti ya Weusi......jamaa wanadhani Waafrika wote tuna rangi moja kwamba wote ni Chocolate au Dark Chocolate.Ikitokea unakarangi ka Caramel au umepauka zaidi basi wewe ni mixed race(toa macho kwa mshangao)!
Sasa hili ni Jepesi kwa Mimi mkimama wa Kitanzania(sikwaziki kirahisi).....ilimtokea Mkimama mmoja wa USA ayeeee alikasirika mpaka akaamua kwenda public(youtube).....Weusi wa USA wapo verevere demaged na Ubaguzi.
Pamoja na hasira zake bado mtoto sio wake wa kumzaa.....anamtunza tu wakati anasubiri kupatiwa "a home". Imagine angekuwa kamzaa sasa.Najua Ubaguzi upo UK na hakika Wazungu ni wabaguzi sema wengi inabidi watuchukilie kama tulivyo kutokana na "sheria" dhidi ya Ubaguzi, pia hii ni 2015 sio 1920
Pamoja na kusema hivyo bado wapo baadhi hawajui tofauti yetu sisi weusi kama vile ambavyo wengi wetu(wenu hihihi) hamjui tofauti za Wazungu. Mnadhani Mzungu=Maisha mazuri/mapenzi ya kweli.Usikute tukitoka kama familia wanadhani Mimi na Asali wa Moyo ni Childminders au tume-adopt.


Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.

Tuesday, 7 July 2015

Kiswahili kwenye Matangazo UKtv

Sema, mambo!

Kiswahili kimekuwa Common sasa kama Kiinglish, yaani inakuwa taabu kuwateta watu(not that i teta watu....). Natumia Kiswahili zaidi kuficha ukali wa maneno pale wanangu wanapoleta ujinga.Mfano tupo mtaani na watoto halafu wakawa hawasikii....unawaambia "do you want to chapwa au am going to chapa you"......wanajibu "no dont chapa us" na kuacha ujinga hehehehe.Sasa ukisema neno kuchapa kwa Lugha yao bana utaitwa abuser na unaeza nyang'anywa watoto.To the nukta: Kuna Matangazo mawili ya Kiswahili moja la Holiday (lastminutes.com) na lingine la Bank linalomhusisha Mmasai(Co-operative Bank).....nenda kaguge.

Siangalii Tv kihiiiivyo ila wanangu wamenishtua niliposikia wanaimba sijui 'ninini matako'.....nkauliza "where did you learn that word?"......nikaambiwa "its only an advert mum, dont be silly".
Nka-rewind si nkakutana na Tangazo la holiday jamaa anaimba kwa Kiswahili pamoja na maneno mengine akatamka "matako".....
Lile la Bank husikii sana Kiswahili as kuna mtu anatafsiri lakini bado inafanya Kiswahili Common ka Kiingereza bana....hata sifurahii.


Hata hivyo, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Wanaume na tofauti zao....


Kuna wale wanaodhani kuwa na wewe ni "Feva" hivyo ushukuru Mungu. Aina hii huwa wanategemea uwafanyie kila kitu kuanzia kuwapikia mpaka kutafuta mbinu za kuendeleza "moto" kwenye ndoa yenu.


Unafanya yote hayo na pengine zaidi.....yeye ana-chill tu. Yaani hata ukiumwa hakutengenezei Uji. Inafikia mahali unajiuliza "nafanya yote haya kwa ajili yake, yeye ananifanyia nini?


Pili, Wanajifanya wanaujua Usawa kuliko Feminist (well wanaume pia wanaweza kuwa mafeministi as in wanasaidia kupigania Usawa kwa wote). Lakini sasa kwanini ni wewe tu ndio umnunulie Zawadi ghali na wewe kupata Kadi tu kutoka kwake kwenye ile siku yenu Maalum?


Tatu, Wazee wa Mipango aka wazito.....huyu bwana ana plans lundo halafu nzuri zinazotekerezeka lakini utekerezaji Sufuri. Sasa si unipe mgao mie nikutekerezee? Mpaka nikuombe....Aiii!Nne, Wadaku.....kila stori ya Mjini anayo yeye....kila mwanajamii wa jamii yake ama anamjua au rafiki yake ni rafiki yake. Anashadadia(bado mnatumia hili neno?) Matatizo ya wenzie na kujadili nini kifanyike ili matatizonyawaishe......wakati matatizo yake yanamshinda.Tano, Wasambaza Umasikini. Hakupendi na hana mpango na wewe anachotaka ni hizo dakika tatu za Ngono, lakini kutumia Condom ni Mwiko......huyu anaacha mabegu (uchafu)wake popote.....i mean kwa mwanamke yeyote(anapima kama anauwezo wa kuzaa).Hawa bana anaeza kuivaa Condom halafu katikati ya mchezo akaivua bila wewe kujua.......au....au kama upo nae kwenye uhusiano anajifanya "nimeshindwa kujizuia ujue wewe ni mtamu sana".....mwenyewe unaona siiiifa unatunza Kamimba.Kimbia(sikutumi ila kama haeleweki inabidi uzuie kabla haijatunga) kachukue kale kakidonge kanaitwaje kaleeee.....night after? Nani anataka "oops baby" Maisha haya?.Sita, Marafiki Mbele, Familia nyuma......umewahi kusikia msemo wa "familia Daima".....familia kwa maana ya ile unayoianzisha sio kule ulikozaliwa.


Saba, walazimisha Undugu.....usinielewe vibaya lakini kama hamchangii damu pande zote mbili huna undugu.....hao ni Jamaa tu.


Nane, Wakosoaji! Kabla hawajajua kwanini umefanya ulichofanya wanakuja full force na makritisizim yao. Uliza kwanza Mwanaume.


Tisa, wapenda watoto tu sio Mama zao. Well inawezekana kabisa hasa kama mama alikuwa "mapoozeo".....Ujue Ngono kwa wanaume WENGI huwa ni Ngono tu.


Huwa hawaweki emotions na mara zote hawaifanyi kwasababu wanakupenda.  Wanafanya ilinkumaliza haja ya mwili. Rejea namba Tano.


Kumi, niligusia jana. Wanakuwa Baba yako zaidi kuliko Mpenzi....huyu bana kila akikugusa kimapenzi unarudi nyuma na kukumbuka alivyokufokea au alivyokukataza usimshike tako"......wasifu wa Baba huu hapa"....unapoteza hisia.


Kumi na Moja, hawajui kusema ahsante(kushukuru)......hawajui kuomba Msamaha(mpaka u-demand) which inapoteza maana ya Msamaha.

Hii inakufanya  uogope kuwaacha watoto wenu kwa Wakwe.....maana kama baba yao hakufunzwa basics na wazazi wake walipokuwa Vijana....leo wamezeeka wataweza kuwafunza wajukuu?

Kumi na Mbili, watishiaji/wamikwara......"usipobadilika nakuolea mke wa pili" hehehehehe well dear nami nakuletea mume mwenza.....hii ni 2015 sio 1984 pale mama yako alitishiwa hivyo.

Kumi na Nne(13 ni namba ya Mikosi UK).....wanaolazimisha watoto waliowazaa kabla yako.....kipindi ndio anakutaka-taka(anakutongoza) au mpo pamoja......kutwa anachomekeza habari za mwanae "my baby this....my baby that......aaah mwanagu kapata mama mzuri kweli" (yaani wewe).

Unatamani kumwambia "unanipotezea mzuka bana....najua mwanao ni muhimu kwako naomba ibaki hivyo wacha ku-push on me".....as in am not interested.

Aaah sitaki Post iwe ndefu wacha niishie hapa! Ahsante kwa kuchagua blog hii.

Babai.

Monday, 6 July 2015

UK ya leo sio ile ya 1998-2006


Habari?

Unajua enzi hizo kuishi Ulaya(ya UK) ilikuwa raha sana na tulikuwa na mahela ya kumwaga.....hata mie nilikuwa tajiri Mwanafunzi.Unakumbuka enzi zile tulipokuwa summer holiday(kipindi kama hiki) unagoma kurudi kwenu na badala yake unabaki Ulaya kupiga Kazi siku 7 za Wiki ili "kufuga" pesa?Wakati wa term mtu kutoka Bongo anakuomba senti.....unamwambia nipe wiki nitakurekebishia......unaenda chukua kazi kwa Wakala na unamaliza tatizo la mtu just like upepo.Fast foward mpaka 2008.....wa Ulaya Mashariki wakaanza kumiminika nankujaza kazi zote za Mawakala tena kwa malipo chee(wanachukua mpaka £3 kwa saa)......sasa mimi Muafrika na yule Mbritish (kiwango cha malipo ni tofauti na wa Ulaya Mashariki)! nikufanyie kazi lwa £3 sijipendi??Siku hizi ni kama Bongo tu.....kama hujapata bonus kazini kwako basi utabaki na Mshahara ule ule......siku hizi hata zile overtime hazipatikani. Mkurugenzi anachukua extra hours hihihihihi.Sasa mtu akikuomba msaada na  ukamwambia....eh bana life ngumu UK samahani siwezi kukusaidia anakuona unaroho mbaya tu/umebadilika.Ndio mimi ni Matanzania muhamiaji lakini siwapendi Wahamiaji wa Ulaya Mashariki kwasababu nilizogusia hapo juu. Naiomba Serikali iweke sheria ngumu kwa Wahamiaji wa Ulaya Mashariki.Hee majuzi hapa tukaletea Mchango wa Ndoa ulioambatana na ujumbe "kwasababu Ndugu tupo wachache UK tumeamua kila Ndugu atoe £500"......kweli? Kweli kabsaaaaa......bila aibu? Nendeni mkaoane Bongo kuna Ndugu kibawooooo.


*Ndugu wa kupanga matofali(sio baba na mama mmoja). Sante kwa kuchagua Blog hii.

Babai.

Chunga Ulimi usimuudhi Mpenzi....

Hello! Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Mambo tunayoambiwa tuyafanye kwenye Ndoa ili tuishi kwa Amani ni mengi mno na yanachukua "utambulisho" wetu......halafu vipi kuhusu Ndoa yenye furaha?Mambo kama "usilopokea....soma nyakati kwanza ili usimuudhi mwenza wako", hii inakufanya uwe mtu mwingine na sio wewe.....katika hali halisi ni task itakayokukosesha furaha kwasababu utakuwa unaishi kama mtu mwingine na sio wewe.
Unasoma nyakati only kama issue unayotaka kuiwakilisha kwa mwenzio ni ya kubomoa au kujenga Ndoa yenu. Lakini mambo ya kawaida kama vile kutaniana na kuzungumzia watoto hayahitaji "kusoma nyakati".
Kingine ni kusema unavyojisikia baada ya kuvumilia vya kutosha.....ujue wakati wote sisi ni wepesi kuona makosa  madogo madogo ya Wenza wetu kuliko kuona yetu(sio rahisi kuona makosa yako).
Na ikitokea Mwenza sio mwepesi kukuambia pale unapokosea basi wewe unadhani kuwa ni kawaida tu na unasonga na maisha.Siku yakimfika shingoni anakuambia rasmi kuwa "kuna siku nitachoka kuvumilia nitabwaga manyanga".....hapo ndio unaamka na kuanza kutafuta makosa yako.
Sasa siku hizi tunaambiwa tusiwaambie Wenza wetu kuwa "tunakaribia kuchoka kuvumilia" kwasababu hiyo itawaudhi na hivyo kuharibu Amani Ndoani.Hivi unajua kuwa bila kuwa na furaha Ndoani hakika hukutakuwa na Amani?Ili kuwa na Ndoa yenye furaha ni vema kila mtu kuwa yeye na sio ku-pretend kuwa mtu mwingine ili usimuudhi Mwenza wako.Kosa likijitokeza liweke wazi na mlizungumzie na kwapamoja kutaguta namna ya kuliepuka(kosa sio cheating.....cheating haina kuzungumza).Jinsi siku zinavyokwenda na Ndoani unakuwa too comfortable to the point unapoteza hadhi ya Mpenzi unaanza kuwa Baba/Mama yake. Unaweka vijisheria vya kipuuzi vingi.....usinishike hapa.....usiongee na mimi hivyo....usivae hivi.....my FAV....SIKU HIZI HUNA HESHIMA!


Nani anataka kulala na Baba/Mama yake? Total  Kuneng'enuana off put.

Babai.