Skip to main content

Mambo 10 kuhusu Ujauzito hakuna mtu atakuambia....

 ...isipokuwa mimi!

Kumbuka kuwa sehemu kubwa ya haya mambo ni uzoefu wangu binafsi ambao unaweza kukutokea wewe pia, sasa ikikutokea usishangae na kudhani kuna "uchawi" na isipokutokea haina maana kuwa una tatizo.


Mimba sio lelemama kama ambavyo baadhi ya watu hasa wa kiafrika wavyojiaminisha. Kila mimba unayoshika ni tofauti(uzoefu tofauti) japokuwa mimba zote zinaongeza uwezekano wa Maradhi ya kudumu kwako sasa au huko mbele. Jinsi ambavyo unashika mimba mara nyingi ndivyo ambavyo unajiongezea matatizo pale utakapofikiwa umri mkubwa.  



Imagine "kuhisi" kichefuchefu masaa yote 24 kwa miezi 4, kutokuwa na nguvu mwilini, maumivu ya viungo na msuli, kichwa, mgongo, nyonga na kinena, ukubwa wa matiti yanayouma na yamekuwa makubwa yanafika shingoni na unashindwa kupumua....hapo sijazungumzia Uchungu wa kuzaaa, hofu na uhai wako na mtoto na kuzaa kwenyewe. 


Oh halafu kuna ile "maziwa kuja", ugumu wa kunyinyesha na kukesha na kichanga kwa miezi mingine 4.....halafu kuna M-baba anasema "wanawake wa bongo wanadeka sana wakiwa na mimba". anyway hii ni topic inayojitegemea, tuanze na namba Mosi;


-Mimba inaharibu afya yako na uwezekano wa kuwa na maradhi ya kudumu ambayo hujawahi kuwa  nayo kabla ni mkubwa(kwamba Mimba inaweza kuwa sababu ukawa na afya mbovu). Ndio maana ni muhimu kutoa mwili wako na viungo vya uzazi kwa Mwanaume ambae ni Mume wako na anaestahili kujitoa Mhanga kwako kwa ajili ya kumpa familia Mpya.


Pili;-Ni bahati kuvuka miezi yote na hatimae kujifungua salama na kupita Wiki 12 za mwanzo bila maambukizo(na hata kifo) kwako na kwa mtoto baada ya kujifungua.


Tatu;- Ukubwa na nguvu ya Moyo wako unaongezeka, sasa kama una matatizo ya Moyo au tayari ni Chibonge au mtu mzima (miaka 46+)ni muhimu kutambua faida na hasara kwako linapokuja suala la kushika Mimba. 


Nne;- Ukubwa wa miguu(vikanyagio huongezeka kwa size 1), wewe ulidhani ni matiti, pua, makalio na tumbo tu eti? 


Tano. Kipindi mimba ni changa unajikuta ukihitaji tendo la ndoa mara kwa mara na kila baada ya tendo unahisi kinyaa na harufu ya "ndoa" kati ya Manii  ya mumeo na Utoko wako ndio balaa inazidi. Ukisha jiswafi, utahisi kutaka tena Tendo...hii itaendelea kwa miezi yote tisa(kumi). 


Sita;-Uwingi wa Utoko unaongezeka hata ujiswafi(shije) na ni kero kubwa mno. Ila kitibabu wanashauri usijiswafi mara nyingi ili kuepuka maambukizo Ukeni na hata kumfikia mtoto. Hivyo jiswafi mara mbili kwa siku.


Saba;- Ngozi yako inakuwa "sensitive to the touch" na sio kwa uzuri....inakuwa kama inauma hivi...iwe mikono ya mumeo, Daktari, Mkunga, maji wakati wa kuoga au nguo uvaazo.


Je umewahi pitia uzoefu tofauti na ungependa wengine wafahamu? Naomba unisimulie.

Mpaka siku ingine, Bai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao