Skip to main content

Jinsi ya kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu!

Kumbuka sababu kuu ya ninyi kuwa pamoja ni mapenzi na sababu ya kufunga Ndoa ni kwavile mnapendana na mnataka kuishi pamoja kwa furaha. Ulipenda na ukataka kupendwa na kufurahia Muungano wenu. Sasa kama hiyo ndio sababu kuu, kuna umuhimu gani wa kuendelea kuishi Maisha ya ndoa wakati hakuna furaha? Utasema Mapenzi, kwasababu mapenzi hayaishi obviously, jinsi mnavyozidi kuishi pamoja ndivyo ambavyo unapata sababu nyingine nyingi kwanini unapenda Mume/Mkeo.

 

Kuna wakati unaweza usipendezwe na mumeo/mkeo kutokana na matendo yake au kutokana na jinsi alivyokujibu/ongea nawe au kafanya jambo Fulani hukubaliani nalo, hii hali hutoweka mara akiomba radhi au wewe ukiamua kudharau. Hali hiyo haiondoi mapenzi yako kwa mume/mkeo.

 

Ule msemo wa watu wa social media kuwa “my happiness comes first” au “I choose me” ni kwa wale ambao hawana Imani (hawamuogopi Mungu) ni single au wapo kwenye Ndoa mbaya za unyanyaswaji, vipigo, mateso na masimamngo. Sie wengine ambao wenza wetu wamebadilika sababu zilizo nje ya uwezo wetu Mf; wamezaa au kupoteza  kazi/mali n.k.  "your family’s happiness comes first” au tuseme “furaha  ya mkeo/mumeo comes first”, yeye akiwa na furaha, wewe pia utakuwa na furaha na hivyo watoto yenu kufaidika pia.


Sasa kabla sijakukumbusha namna ya kurudisha furaha kwenye ndoa yako(ambayo siijui), sio mbaya kama tukiangalia ni vitu gani hasa vinachangia kuondoa furaha kwenye Ndoa yenu?

 

1-Mmesahau au hamzingatii zile nguzo 5  zisome hapa , hapa na hapa kwasababu mmemzoea kupita kiasi na sasa upo tu hapo kutimiza wajibu, mmejisahau.

 

2-Unamtolea nje/unamkataa Mumeo kimwili na hii ikitokea mumeo anakosa furaha napengine kuanza kuwaza wapi unapata tendo ama hakuvutii tena au anakasoro(inategemea na kiwango cha kujiamini kwake). Kwa kifupi Mumeo ni sensitive sana kwenye kutolewa nje kimapenzi. Yanayoendelea akilini mwake hupelekea kujitenga kihisia(anakununia), akikununia wewe unanuna back au unaanza kulalamika na matokeo yake mnazozana na mwishowe kutamkiana maneno makali au kurudisha makosa ya zamani yaliyokwisha tatuliwa(malizwa).

 

3-Wakati wote upo tayari kujitetea au ku-react, ku-over-react ni kubaya sana mara zote unaachia akili yako kwenda mbali na kutengeneza “hadithi” ili kupata majibu kwanini mkeo/mumeo kauliza alichouliza, kasema alichosema n.k. Pia wakati mwingine unaweza kuwa unafanya kitu ambacho unajia wazi kabisa mkeo/mumeo akiona ataudhika na hivyo unaweka Ngao tayari kupambana(kujitetea).

 

4-Kupeana triggers kila kukicha, kila mmoja wetu anazo ni vema ukiziweka wazi ili mwenza wako azifahamu na hivyo kuziepuka ili usiwe triggered…kuanzia Ex, baadhi ya Marafiki zake, kutoka home bila kuaga, matumizi ya pesa, malezi ya watoto, kurudi nyumbani usiku wa manane n.k.


5-Umesahau kufanya yale ambayo ulikuwa unayafanya awali mlipokuwa wapenzi, wachumba na Ndoa ilipokuwa changa. Mf, wewe Mume ulikuwa unampigia simu Mkeo na mnaongea masaa yote unapokuwa break kazini, ukiwa safari hulali mpaka usikie sauti yake, ukitoka unambusu kwa mahaba na unamjulia hali kati kati ya siku na kabla ya kurudi nyumbani unamjulisha. 


Habari zako na zake ndio muhimu na sio Habari za Dunia au Siasa. Mlikuwa mnazungumzia Mipango yenu ya baadae, careers, safari n.k. Mlikuwa mnafanya mapenzi kila siku(siku hizi mnafanya ngono tu), mnaenda kulala pamoja na hata kama mmekosana hamlali bila kupeana busu nyevu la usiku mwema(na kuishia kufanya mapenzi kwa hasira?), unakumbuka?


Njoo tena ili tuone hatua unatakiwa kuchukua ili kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu.

Bai!

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao