Skip to main content

Twitter ya Elon na heka heka zake...


Ni mwaka na wiki kadhaa tangu Elon Musk alazimishwe na "Mahakama" aichukue Twitter  baada ya kutishia kuinunua 2021(for attention) na ni Mwaka  Mmoja na Wiki Sita tangu nami niachane na Twitter(nisome kama unajali ). Maisha bila twita yamekua ya kwaida na sijawahi kuhisi kutamani kuchungulia na kusalimia watu wangu ambao huwa  nawakumbuka mara kwa mara na kutabasamu kutokana na vichekesho au jinsi tulivyokuwa tunaelewana, kupishana na kushangaa pamoja. Hey I miss you on twita too.



Sasa juzi hapa nikaona habari kwamba Elon anataka kubadilisha Kindenge na kuwa Eksi(huenda tayari imekuwa hivyo), nikaudhika na kuombea Twita ikufe kabisa na kubaki kumbukumbu, maana ni aibu hata kusema niliwahi kuwa Twita tangu mwanzo miaka 17 iliyopita.


Ilikuwa jamii nzuri sana na kamwe sitoisahau kama ilivyokuwa DHB(Dar Hot Board)/DHW(Dar hot Wire), JamiiForum na Facebook. Nimesikia kuna mabadiliko mengi ambayo nilijua yatatokea kutokana na jinsi Elon anajibeba. Elon ni Bilionea ambae anapenda "attention" na ana mashabiki ambao wanaamini kuwa yeye ni JINIASI kitu ambacho kinamfanya awe tofauti  na mabilionea wengine, hiyo pia inamfanya aonekane kuwa yupo karibu zaidi na watu wa kawaida(masikini) na "anawajali" kumbe katika hali halisi anachuma kidogo walichonacho hao masikini.



Watumiaji wa Twitter wanamchukulia jamaa kama mkombozi which is sad kwasababu platform ile haimfaidii yeyote bali Elon pekee, sasa anawakomboaje bila ninyi kukomboleka? labda akianza kuwalipa watumiaji wake kwa content creation kama ambavyo Google(Aphabet) anafanya  kule Youtube na huku Blogger. Kwamba isiwe micro-blog tena na iwe blog-BLOG na kuwe na video format  itakayoruhusu watu wenye utaalam hitajika kutoa Elimu n.k. Kwasasa inaonekana(kwa mujibu wa Mashable) kumejaa soft porno, bulling, exposeeS kama pumziko baada ya stress za siasa na drama za watu kwenye maisha yao binafsi.


Twita ilikuwa  na nguvu na kujitengenezea sifa nzuri kwa  miaka 17, ilikuwa chanzo cha habari in real time kitu ambacho kilifanya Waandishi wa habari kuitumia kama kituo cha kwanza kutoa dondoo/tip/habaro kwa ufupi nahivyo wananchi kwenda kwenye News paltform kupata habari kamili. Pia ilikuwa ni kituo kizuri kwa wanaharakati na bila kusahau ilikuwa sehemu ya ya kufanyia research  kwa Content creators wa Maswala ya Siasa kwenye Paltform nyingine kama vile youtube, blogger,facebook na instaglam.


Miaka ambayo nilikuwa na bahati kuitumia Twitter (kutoka facebook  2007) na kuona mabadiliko mbali mbali ambayo yalikuwa bora na baadhi ya kuudhi, twita iliendelea kutamba kutokana na urahisi wa kutoana  kupata habari/maelezo moja kwa moja kutoka chanzoni.  Tuone Titter ya Elon itadumu kwa Muda gani. Nikiwa mkweli napenda kusem akuwa naombea sana ifeli, sijawahi kufurahia mtu kufeli ila Elon akifeli na Xtwita yake nitafurahi sana. Siku moja nitarudi nione yaliyomo....labla. Mpaka siku hiyo endelea kuwa nami huku kwa Blogger ya Google....namaanisha Aphabet Inc.




Picha kutoka kwa Mashable


Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao