Skip to main content

Saikolojia ni Sayansi rahisi, you need to heal...

...huwa wanamaanisha nini? ku-heal ndio kukoje wakati huna matatizo ya kiafya(kimwili)?


 Kuna maneno watu wa mitandaoni wanapenda kuyatumia ili kuonekana wajuzi au wana upeo ama wana akili/wasomi(kila mtu anataka kuonekana hivyo), unakuta mtu anajieleeeeeza halafu hakuna anachoelezea, anajazia tu maneno ambayo yana-sound vizuri au kisomi ama yale "clinical" yanayotumiwa zaidi ya Wanasaikolojia(wale wenye Leseni ya kutoa Huduma hiyo baada ya kumaliza masomo na kufuzu kwa kiwango cha phD) au Madaktari wa Akili


Sisi tuliosoma "Social Science" kama sehemu ya Kozi nyingine hatupaswi ku-act kama vile ni Wanasaikolojia, ni kama Sheria kuna sehemu unaijua na unaweza kuizungumzia lakini wewe sio mwanasheria, uliisoma tu kama sehemu ya Kozi yako na sio Kuisomea. Huezi amini leo ndio nimeelewa kwanini Wanasheria wa Bongo huitana "Mwanasheria Msomi".


Juzi hapa nilikuwa nasikiliza PodCast(yeah them ones) kuhusu malezi ya watoto kutoka kwa "wataalamu", kukawa na wanasaikolojia na wazazi wanabishana kuhusu namna ya kulea watoto, wawili kati yao hawajawahi kuwa na watoto ila wana-support soft ways ya kulea watoto, alie na watoto akawa anapinga na kusema watoto hawatakiwi kulelewa ki-soft muda wote, wanatakiwa kufunzwa namna ya kukabiliana na maisha kwa sababu maisha ni magumu, ukienda ki-soft kutokanana malezi yako, utashindwa kustahimili Maisha na heka heka zake....huyo mbishi ni  mimi😁(in my head).


Saikolojia ni Sayansi rahisi sana, kwamba kila mtu anaweza kujifunza mwenyewe bila kupoteza muda wa miaka kadhaa Chuoni si ndio? Watu wengi ndio wanavyoichukulia Saikolojia, unasoma gazeti/magazine ya Saikoloji kisha unatafasiri kwa Lugha yako then boom wewe ni mwanasaikolojia. Hii dharau kwenye Kona ya kuujua Ubongo, Kemikali zake(upungufu, uwingi/ukosefu), namna unapokea/tunza na kisha toa maelezo, namna unajenga tabia, tunza kumbukumbu n.k. sio Sayansi rahisi kwasababu wasomi wake wanaenda deeper zaidi ya Sayansi yenyewe,  vilevile sio Sayansi Ngumu.


                                                Picha kwa hisani ya The Guardian.


Kwa maoni yangu Wanasaikolojia wanachukuliwa poa(hawaheshimiki) Era hii ya Social Media ni  kwasababu wanapotoa huduma kwa  individual, the individual's issues huwa sio unique kwake pekee, kwamba kuna watu wengine zaidi ya 20 wanauzoefu kama huo wa mteja wako. Sasa mteja wako mmoja akija kutumia uzoefu wake wa trauma na kuchangia alichokuwa akiambiwa na Mwanasaikolojia wake, ni wazi mteja wako huyo atakuwa na uwezo wa "kutibu" watu wengine 20na, pengine zaidi kama ataamuwa kufanya kuwa Kozi maalum kwa kutumia uzoefu wa matatizo aliyopitia na huduma(tiba) aliyoipata kutoka kwako Mwanasaikilojia wake bila kusomea.


Pia kuna wanasaikolojia wanaingiza "treatments" zao na kufunza wagonjwa wao tabia mpya, badala ya kuwasaidia, wanajenga bond to the point "Sayansi" inapotea, mgonjwa anakuwa na issues nyingine due to Mwanasaikolojia mbovu mwenye ajenda zake binafsi + Big Boss (Drug Companies), vilevile usisahau baadhi ya Wanasaikolojia tayari wana matatizo ya Akili(aren't we all) so ni rahisi kuchepuka nje ya Mipaka. Hii inaifanya Sayansi hii kudharaulika, na pengine ukute sio Sayansi...No? anyways....turudi somoni.


Unapowaambia wenzako wa-go and heal, huwa unamaanisha nini hasa? Je wewe una uhakika ume-heal trauma ulizopitia? au umesikiliza Pod kama mimi ukabeba "go heal"? Hakika sote tuna some sort of mental issues, ukubwa/serious wake unatofautiana inategemeana na namna una/mekabiliana nayo...mf umedharau, umefuta akilini, Umejitenga na mtesi wako, unatumia kilevi(pombe, unga, social media,sinema/picha za matusi, ngono holela) ili kufunika issue au unapambana on an daily.


Je utajuaje kuwa umepona vidonda vyako vya Moyo, Akili au Mwili? Utaweza kuongea kuhusu yaliyokutokea kuanzia mwanzo mpaka mwisho bila kutamani/taka kulia, souti yako haitovunjika, hutotokwa na machozi tena....kibinaadamu huwa tunasema "aah nimeisha zoea siku hizi, zamani nilikuwa siwezi kuongelea hili suala bila kulia". Mosi.

-Pili, hutohisi hitaji la kutaka ku-seek attention kwa kutumia matatizo uliyopitia.

-Tatu, Mtu aki-post au akisimulia yaliyomsibu hutopata hitaji la kutaka kufananisha matatizo yako kwake ili kumfanya mhusika kuona tatizo lake sio kubwa kiviile, maana wewe ulipitia makuu.

-Nne, Utakwepa kulalamika au kuonyesha kuwa wewe ni "victim" kila unapopata nafasi au kila unapokosea/fanya makosa.

-Tano, Huwezi kutumia uzoefu wako (trauma) kama sehemu ya kujipatia kipato na badala yake unatumia kusiaida wengine kama sadaka(bila malipo).

-Hutokuwa na shinda kwenye kuunda/jenga mahusiano ya karibu na kuda mrefu na watu wengine urafiki/mapenzi


Lakini kabla hujafika hapo(ku-heal), kumbuka kuwa inachukua muda na unahitaji kufanyia kazi....kwa maana kuwa unatakiwa kuzungumzia hayo mambo mara kwa mara iwe na Mwanasaikolojia, kwenye kioo(kuongea mwenyewe na kulia kama mwehu), Familia(hii nzuri kama wote mmepitia same issue mf; Kifo cha wazazi/ndugu) au unaweza kuandika kama Hadithi endelevu(sio in one sitting mara kwa mara mpaka ukose cha kuandika), yaani kama vile unamuadithia mtu. 


Nami nimeandika weee halafu hamna kitu, oh well takuona baadae Wiki hii, 

Bbai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao