....vipi kuhusu Elimu, Dini na Familia?
Aah Elimu ni kwa ajili ya masikini kwani haina faida, sababu watoto wa vigogo wanainunua. But tunahitaji wajuzi wa afya ya Ubongo, Mwili na viungo vyake, Mifupa n.k kuanzia tupo tumboni mpaka tunafika miaka 120(yep tunafika huko as hii ni karne ya 21 sio 11).
Wajuzi wa mazingira,vyakula, sumu, Madawa, Nishati, Shetia na utaratibu wa kulinda na kupata Haki yako maka mtendwa au mtendewa jambo kinyume cha sheria n.k.
Vipi kuhusu Imani ya Dini? Nayo tumeaminishwa tu na Wazungu na Waarabu ili watutawale si ndio? Vipi Waarabu na Wazungu huko makwao ambao bado wanafuata, kuamini na kusimamia Imani hizo za Dini, wanafanya hayo ili kujitawala? Aaah ili kunyanyasa Wanawake na watoto....Achana na Uislamu/Ukristo, vipi Imani za Dini/Miungu ya kimila na Desturi?
Bado unaamini haikuwa sehemu nzuri ya kuifanya jamii husika kuwa na structure na hivyo kufanya maisha yawe rahisi kumudu hasa linpokuja suala la stress, shida na matukio mengine ambayo ni sehemu ya maisha kama vile vifo, magonjwa, ndoa, uzazi na ulemavu?
Kwanini Ndoa ndio iwe kitu ya kwanza(Pekee)kuandamwa na kutoiheshimu/kuiacha sababu "tumeaminishwa" na Jamii....unauhakika? Sio kwamba kupata mwenza umtakae ili muishi miasha yenu yote pamoja na kujenga familia ni ngumu zaidi kuliko kulala na yeyote bila kufungamana?
Enzi nilikuwa teen miaka ileeee ya 1990s, Kufunga ndoa ilihitaji Kijana awe amesimama kiuchumi au anaonyesha bidii kuwa anaenda kujiweka sawa ili aweze kuoa. Anachumbia vema tu ila haruhusiwi kumuoa binti wala kulala nae mpaka atakapo muoa, so unatunziwa future wife wako(mara nyingi huwa Masomoni)....ila ukichelewa zaidi ya Miaka 2...Shabani au Jackson anaeza kukupiku. Hii ilisaidia sana vijana wa kiume kujituma.
Sina maana Ndoa ndio mafanikio maishani(inategemea na mtu, mie binafsi Ndoa ni moja ya mafanikio yangu sambamba na Elimu, Pesa, Afya, Watoto, Umri niliofikia, nyumba ninayoishi na kupunguza unene).
Vipi kuhusu Familia? Bila ndoa unakuwaje na familia yako wewe kama wewe, sio ile familia ulikozaliwa...hao kila mmoja wao anafamilia yake. Mkiisha kuwa watu wazima mnabaki kuwa ndugu, mkikutana kila mmoja wenu anakuja na familia yake....sasa bila Ndoa familia yako iko wapi?
Unakusanya watoto wako kutoka baba/Mama tofauti kila mwezi mnakuwa familia iliyogawanyika au inakuaje? Blended family eeh, hiyo ni kwenye TV/kuigiza na kwa MamilioneaS, vinginevyo kwa nyie hoihae doesn't work.
Aah sijui hata naenda wapi na hii topic,
Anyways, Elimu, Imani, Ndoa(kuishi na mtoto wa watu kwa miaka 2 ni common law marriage) na Familia vinategemeana na vyote ni Muhimu maishani....takuona J'3.
Bai.
Comments