Friday, 31 October 2014

Kuaga au kutokuaga Marehemu!

Hiyaaaa!

Leo si Halloween bana, wacha nami niungane nao kwa kuzungumzia Wafu.


Jana tulikuwa (Mimi na Asali wa Moyo) tunaangalia Tv, mara Tangazo la Documentary ya Ebola (Ebola crisis) hilooo!


Nkasema mie sipendi kuona/onyeshwa miili ya wafu hata kama imefunikwa(hifadhiwa vizuri), kama wameenda wameenda tu hata mkituonyesha haifanyi Ebola kuwa Hatari zaidi ya ilivyo!

Mwenzangu akasema, "mie sielewi kwanini watu hupenda kwenda kutoa "Heshima" za mwisho wakitegemea kumuona Marehemu kwa mara ya Mwisho, marehemu ambae hawakuwa nae karibu kama Ndugu(wa Damu). Kwanini utake kumuona Mtu akiwa Maiti?

Nikakumbuka Msiba wa Marehemu Kanumba(Mungu akuongezee heri huko uliko, Ameen), ambao sasa umekuwa (in my head) kama "model" ya Misiba ya MaCeleb wa Bongo kwa Uwingi wa watu....*whispering* nasikia MaCeleb wa Kibongo wanaombea nao wajekuzikwa na watu wengi kama huyo nliyemtaja!

Walioshiriki walilalamika na wengine kukasirika kwanini hawakupewa nafasi ya "kumuona" Marehemu kwa mara ya mwisho!

Waingereza waliotuletea "utaratibu" wa Kuaga Marehemu kwa kuiangalia Maiti hawafanyi hivyo tena kwasababu wanakiuka Haki za Marehemu (Binaadamu) husika....unless alisema kwa maandishi kuwa anataka kuonwa akiwa hana uhai.

Sasa leo nilikuwa Duka la Madawa nasubiri Dawa(wanangu wanakohoa kwa Mashindano.....ahsanteB *nahisi umenipa pole*).

Pembeni alikuwa amekaa Mmama mmoja Mweupe(Mzungu), kachangamkaa, kama kawaida akaanza Stori...mara nikamaliza yangu (pata Dawa) nikamuaga.....akasema "am trying to be nice to everybody, because I don't know who'll look after me in a Nursing Home or Hospital".....mie nkatabasamu nkasema "aww how kind"....Do I look like a....never mind!

Point hapa ni kuwa, kwanini tunapenda kuhofia nani atanizika....nani atakuja kwenye Msiba wangu na kuishia kujenga urafiki na watu wengi ambao ni Maadui!

Hebu tujaribu kuwa nice/kind kwa kila mmoja wetu bila kurafikiana kwa kuegemea kwenye kuhofia nani atatusaidia Hospitalini au tutakapopata Udhuru mahali ambapo hakuna umjuae/akujuae.

Babai.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 29 October 2014

Wacha kuzungumzia Wanao, unatukwaza!

....ambao hatuna watoto!


Kabla sijawa na Watoto sikuwahi kukwazika ikiwa mtu anazungumzia mtoto au watoto wake. Niliona ama chukulia kuwa ni sehemu muhimu ya maisha yao.

Wakati huo nilikuwa nazungumzia mambo ambayo hayahusishi "wazazi" hivyo ni wazi mimi pia nilikuwa nawakwaza wenye watoto (in my head).

Maisha tunayoishi siku hizi "Ulayani" au Ulaya ya hapa nilipo yametawaliwa na "hofu" ya ku-offend (kukwanza) wengine.....imefikia mahali mpaka Sikukuu ya Krismasi inakwaza wasiohusika (mostly Waislamu).

Yaani ule uhuru wa kuzungumza na mtu kisha kuulizia kama anawatoto haupo tena. Ila mie huwa nauliza kwanza kabla sijaanza habari za akina B-I(initials za majina ya wanagu).....wakisema hawana watoto then siwazungumzii wanangu, wakisema wanao hapo inakuwa sherehe.

Suala la watoto linatetewa kwasababu lina umiza hisia za baadhi ya watu ambao kwasababu mbalimbali hawana watoto.

Well, binafsi nimeacha kuzungumzia na kufuatilia Siasa za Dunia, sio mpenzi wa kuzungumzia Celebs, na sipendi kuzungumzia Misha ya watu wengine.

Sehemu kubwa ya Maisha yangu ya sasa yametawaliwa/chukuliwa na Wanangu hivyo sina mengi ya kuzungumzia zaidi ya wanangu ambao wanafanya mengi ambayo sijawahi kuyashuhudia mbele ya Mcho yangu.

Meenda mchukua Babuu kutoka Vidudu,"Development officer" wake akaanza kunipa "ripoti", baada ya maongezi nikauliza kama anamtoto...akaniangalia kwa uchungu kisha akasema "bado sijabarikiwa" akaanza kulia.Babai
Mapendo tele kwako...

Monday, 27 October 2014

Feminism....

Na ugomvi wao wa nani ni "real Feminist", yupi ni "fake Feminist" anatumia U-feminist kama "PR" na yule sio "feminist enough". Women....WOMEN!!
Majuzi yaleee, well Wiki iliyopita)....nilipokuwa naandika post ya maJuzi yalee nikajihisi nakuwa Feminist!
Then nkakumbuka....Nimeitwa majina mengi sana mabaya, machafu na makali tangu nimeanza kujihusisha na "maisha " ya online mwaka 1999, yote huwa hayaniumi kwasababu najua mimi sio hayo majina wanayoniita (wote hawanijui zaidi ya maandishi/text).

Ila walipoanza kuniita "Dinah ni Feminist" kiasi cha kutosha, nikaanza kuchukia na kutamani kubishana au kujibu...."acha Uswahili" inakuja kichwani, nadharau na kupoteza Comments husika!

Binafsi sipendi kuitwa Feminist pamoja na kuwa baadhi ya "views" zangu za kimaisha zinaweza kukufanya udhanie kuwa mimi ni Feminist.

Sababu nyingine inayonifanya nichukie kuitwa "feminist" ni kibongo-bongo na baadhi ya Wamagharibi (stupid ones) U-Feminism unahusishwa na chuki dhidi ya wanaume au kutaka kuwa "sawa" na wanaume .

NAWAPENDA wanaume na kamwe sitaki kuwa sawa nao (isipokuwa Kiheshima, Kielimu na Kiuchumi) vingine wabaki navyo, ahsante nashukuru!.

Napenda, ninafurahia na kuridhika kusafisha nyumba yangu (sipokuwa kusafisha vyombo), kupamba na kuremba Kitanda chetu,....kupika na kumuandalia Asali wa Moyo chakula.
Napenda kuwa "in-control" kwenye masuala ya nyumbani ambayo wewe unayaita "kazi za mwanamke".....time to time Asali husaidia shughuli hizo kama wote tumekazika(wote tulikuwa job).

Oh! Kabla sijasahau...(Feminists lazima waniuwe kihisia hapa) ninaamini kuwa mwanamke anapojipendezesha halafu apite mtaani bila kupata "sifa" kutoka kwa wanaume au hata "ka mluzi", lazma atajishtukia.....Tunapendeza ili kuvutia wanaume, nao wanaume wanapendeza kutuvutia Wanawake....ni Nature!!Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 21 October 2014

Vita dhidi ya Ebola imeSiasa-iwa!

Kila mtu anakuja na lake, mara Wazungu wametengeneza Ebola ili "kumaliza" Kizazi cha Weusi(Waafrika)...huyu ni Mwafrika/Mweusi aweza kuwa Manasiasa au Mtaalam(daktari) n.k.

Mzungu wa kawaida (mtaani) anahoji Kwanini mnahaha na Ebola iliyoua watu Chini ya Elfu Kumi wakati Malaria inaua Mamilioni ya Waafrika kwa siku? Vipi kuhusu HIV na Umasikini ambavyo vinaondoa mamilioni ya Watu....TB je?

Karibu Miezi Nane tangu mlipuko "mpya" wa Ebola kuibuka(according to my kumbukumbu) Wamagharibi walielekeza nguvu zao Ukraine na Iraqi ambako kuna faida zaidi ya kuokoa Maisha ya Muafrika, Afrika.....mara boom wanapigana zaidi kuliko wenye Tatizo (waafrika)?!!

Mwenyewe jana nikajiuliza, kwanini US, EU na Cuba (is Cuba....never mind) wanapeleka "jeshi" la Wataalam kupigana na Ebola which ni more expensive kuliko kupeleke Vifaa na Wataalam wachache wa kutoa mafunzo kwa Locals (Waafrika).
Nikapata jibu kuwa, labda Wazungu wanajua wakiwapa Vifaa na Dawa (zile Trials) mtauza na tatizo(Ebola) litabaki pale pale na hivyo litawafikia huko waliko (EU na USA)....wanataka kulimaliza huko huko lilipoanzia lisifike kwao.
Au pengine wanashindana tu kiSiasa ili kujisifu "nani" alikuwa mstari wa Mbele kusaidia. USA wanafaidika sana na Afrika Magharibi (ukitoa Naigeria) na EU inafaidika na kwingine kote kulikobaki.

Kuna wakati napata aibu ya kuwa Muafrika kimoyomoyo, ila ukiniona mtaani ninavyojivunia Uafirika wangu wee....but kwa ndani naona SOO sana...tunatia aibu sana sometimes.
Over to you to argue kama I hate my skin or my Africanismness*(is that a word? usi-google tafadhali hihihihi).


Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 20 October 2014

Kwanini Mtoto awa wa Baba?!!

Nimekaa hapa nikafikiria(sio kweli)....limenijia tu kichwani.
Kwanini tunaaminishwa kuwa Mtoto akizaliwa ni wababa, Jina lake la ukoo lazima liwe la Upande wa Baba. Ukimpa mtoto jina lingine la mwisho....baba anakuwa Mkali au anahoji kama kuna "mwenzie"!

Kutokana na Mfumo Dume, nahisi(in my head) kuwa wali/na lazimisha hivyo kwasababu walijua/wanajua kuwa Baba ana sehemu ndogo sana kwenye Uumbwaji wa Mtoto.
Baada ya zile Dakika Tatu (if you are lucky that is) kazi yake (baba) imeisha, isitoshe Mbegu hazina Damu so mtoto kuwa na Damu ya Baba yake ni kama 0.5% hihihihihi (lazma mnipige mkinikamata wababa).
Hebu angalia suala hili kwa undani kwenye jamii bila kuhusisha Sayansi wala Dini! Kwanini hasa Babaz au ndugu Upande wa Mwanaume ndio huwa na viherehere vya kuendeleza Undugu kama sio kujishtukia kuwa hawana undugu (wanalazimisha).
Stori time: Kuna siku nipo shereheni, mkaka mmoja akaanza kutambulisha ndugu wa Mama mbali-mbali lakini baba Mmoja kuwa "yaani ukimkata huyu ukachukua Damu yake ni Asilimia Mia moja inafanana na yangu".
Nkacheka kimoyo-moyo huku najisemea mngekuwa mlizaliwa na Mama mmoja then YEAH mngekuwa Asilimia 99 ya Damu....na ile 1 ndio ya baba zenu (0.5 each) bwihihihihihihihiiii.
Wee unafikiri ni kwanini Wanaume wanapenda kusema "wee mwanamke tu"....wanataka ujione "mdogo", "huna thamani", "huna umuhimu" ili wakutawale kwa nafasi na wewe unawapa nafasi eti?!!.....duh! I sound kama Feminist sasa.....*zima Device*


Baibai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 13 October 2014

"Ngoja nitakupigia" = Stop calling me....

Za milimo?


Unawatambua wale watu ukiwapigia simu hawakawii kukuaga utafikiri wao ndio wamepiga....mnasalimiana vizuri, mara baada ya salamu...enhe nipe stori au "mamo mengine vipi?"
Upande wa pili wa Simu(uliempigia) anaanzisha stori, unamsikiliza ukingonjea kwa hamu zamu yako ije ili uongezee kwenye stori husika (uongee).....yeye anakuambia " eh bwana eh, ngoja nitakupigia" halafu kimyaa.

Baada ya Wiki kadhaa unampigia tena na kabla stori hazijachanganya yeye yulee "nitakupigia baada ya dk 20"....ndio imetoka hiyo mpaka umtafute tena.
Mtu hutakiwi lakini hukomi mpaka mtu akuambie "sitaki Urafiki/Ujamaa/kujuana na wewe"....baadhi ya watu wanakupa "ujumbe" ili "muachane" vizuri bila kusutana, ukikimbiwa once na "nitakupigia baadae"....subiri mpaka akupigie (obviously hatokupigia).

Unajua kuna watu wanapenda kuwa tegemezi kifikra.....hata sijui kama inaleta maana kwenye nilichokigusia hapo juu.
Kuna baadhi yetu tunapenda kuonekana Wema, tunajali hata mahali ambapo hapahitaji Wema wala kujaaliwa. Huitaji kushi ili kufurahisha watu(kila mtu kaja kivyake/kazaliwa kivyake) sasa ishi kufurahisha nafsi yako kwani ukifa utazikwa peke yako kama ulivyokuja.
Hopefully kuna walikutangulia wa kutosha angalau wakupokee huko utakapofikia.....but wait! Ukienda(kufa) unaenda kuanza maisha "mapya"! Au?!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 9 October 2014

Kutoboa Mtoto Masikio(Kutoga)

Ni umri gani hasa unapaswa kumtoga Binti yako Masikio? Na je yeye kutoga masikio na kuvaa Hereni ni muhimu kwake au kwako wewe Mzazi?
Mie nilitogwa nikiwa mchanga (Miezi Sita) na nilichelewa, kutokana na Imani sijui Desturi ya mmoja wa Wazazi wangu ni lazima Binti wa kwanza atogwe na kuvalishwa Dhahabu.

Binti yetu alipofikisha Miezi 3 Baba yake akasema tumpeleke akatobolewe(Togwa) Masikio, mie nikapinga na ku-suggest kuwa tumuache na akikua ataamua mwenyewe kutoga au kutokutoga.
Nikaongeza, tena atakuwa na kitu cha ku-look forward to, mf: "nikifikisha miaka 15 natoboa Masikio".....kuliko tumalize kila kitu akiwa Mchanga halafu akikua tu tunaletewa Bf au Mjukuu kabisa sababu kila kitu tumekifanya akiwa bado mtoto.
Isitoshe (in my head) tunatoboa watoto masikio kwa ajili yetu wenyewe Wazazi, yeye mtoto wala hajali kama anavaa Hereni ama hana "kitobo" cha kuweka Hereni.
Baadhi ya Wazazi huku Ulayani wanachukulia kumtoga mtoto masikio ni abuse kwasababu hajui kwanini anaumia.....mmmh! Nakumbuka kwenye Kumtahiri Babuu, niliambiwa na Dokta wangu kuwa ni "abuse".....ikabidi tuende Private.
Aaah! Adha pekee ya kuzaa Kidume ni hiyo ya kushuhudia Kichanga wako "akikatwa" aiii mwanamke nililiaaaa sikujali cha Ganzi wala nini, kitendo cha kuona mwanangu mduchuuu "anatengenezwa"....labda akiaanza kuniletea Wakwe wa Kizungu hihihihi.
The thing is, kwa mtoto wa Kiume ni tofauti na Mtoto wa kike kwenye Kutoga. Kutahiriwa sio Urembo/Vanity ni Jadi/Utamaduni.
Alipoanza Nursery nkawa nahofia(ogopa) Carer wake atakuwa anamchunguza wakati wa kumbadilisha Nepi....maana hawajui kama watoto hutahiriwa wakiwa wadogo.....Ndio! Hihihihihi I am mwehu like that.

Babai.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 8 October 2014

How to be Mum, Wife, HomeMaker and Blogger...

Mimi sijui!

Hihihihihihi huyooo unapenda kutafutiwa kisha wee unameza tu (copy and paste)!!
Mwanamke mwenye maisha kama yangu (not exactly ila kwa mbaaaali) unawezaje ku-keep up na Blog updates kila siku?
Sio blog kama hii ambapo sihitaji kufikiri bali natiririka tu. Zile ambazo unatumia akili kimtindo kwa kuvuta kumbu-kumbu (Uzoefu) na kufikiri.......aiiiii Imenishinda!
Basi nimefika nyumbani siku hivi, nawakilisha nilichoambiwa na Walimu wa Babuu.....Baba mtu wacha aanze kung'aka....."Mimi sifuati wanachotaka wao kwenye nyumba zao za Kizungu, nafundisha mwanangu nijuavyo mimi".

Nikajiuliza kwa hasira bila kutoa sauti....hihihihi "sasa ni kwanini tunampeleka mtoto shule ikiwa hatutaki kuwa kitu kimoja na Walimu wake?".

Nikasema....Asali wa Moyo, shuleni kuna Mihula (mipya imeanza August) na ili watoto waimalize vizuri, kuelewa na kwa wakati ni lazima Wazazi wa-work together na Walimu, vinginevyo mtoto atakuwa Nyuma au kuiona Shule Mbaya/Ngumu/Task.

Baadhi ya Wazazi wa Kiafrika ni waoga, mtu wa jamii ya Kizungu akikuambia jambo, unahisi kuwa anataka kuku-Zungu-rize Uafrika wako.

Badala ya kumfanya mtoto ajifunze kwa furaha akiwa comfortable na achague anachotaka kujifunza huko baadae....tunaishia kuwafanya watoto waione Shule kama "Task" na kuwa- confuse (Shuleni anaambiwa hivi, wewe unapinga unamwambia vile).

Unamlazimisha mtoto kujua mambo yaliyojuu ya uwezo wake ili aonekane na Akili sana Darasani, akishindwa unamuadhibu(bila kufanya uchunguzi kwanini hawezi)!
Au unaifanya Elimu yake sehemu ya Malipo.... "kasome kwa bidii ili upate kazi(pesa) utusaidie wazazi wako".

Niligombana na Baba (marehemu) sababu alitaka nichukue PCB, mie nkaenda kwingine kabisaaaa.....though niliipenda shule na mpaka leo napenda kusoma.
Sinilikuambia mie ni "AcademicHolic"....looking forward to my 50yrs birthday so I can do my PHD.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Friday, 3 October 2014

Blogger wapya!

Hellooooo*clear throat*....hi!


Kuna kipindi wana-blog (wapya) walikuwa wanasemwa sana, "kila mtu anaanzisha blog" baadhi ya Blogger wakaacha (mie nakaribia kuicha ile ingine maana.....takuambia siku ingine) hivyo naangukia kwenye "newbes" si ndio!!!
Kipindi naanza ku-blog 2005(kabla sijawa serious 2007), hao hao walikuwa wakilalama kuwa Watu (Wabongo) wapo nyumba, hawa-blog kama wenzao wa MBELE(hasa Wahabari na Watu mashuhuri).
Mara haooooo wote wakawa na Blogs(well baadhi).....kinachoKERA ni kuwa na habari zilezile bila kusema chanzo/Kielelezo.Mambo ya Beauty, Lifestyle, Fashion and News(kila mtu).
Aaah! Who cares....maisha ya kila mmoja wetu yapo tofauti na interesting in a way hivyo sio mbaya kuongea mwenyewe via Blog kwa matumaini kuwa mtu mmoja atasoma na kucheka au kujifunza.....asa uta-Copy vipi na Ku-paste mtindo wa Maisha na Uzoefu binafsi ya Mtu? Hihihihihihi lione!

Hata hivyo....Mbio zimepungua ila mizunguuko imeongezeka! Hivi nilikuambia Babuu kaanza shule (as if ni muhimu kwako hihihihi) anyway....basi mbio zimegeuka kuwa Mchaka-Mchaka.

Si unajua mizunguuko ya Mchaka-Mchaka? Bora mbio unakimbia mara moja unamaliza....kuliko Mchaka-mchaka.Tumbe: "Jua lile literemke mama aiyayaya iyaa iyaaa mama"......"Sijui nini na nini Pua kama Kijiko, Midomo kama Bakuli....nini na nini"!


Nikutakie Mwanzo Mwema wa Mwisho wa Wiki.


Babai.
Mapendo tele kwako...