Saturday, 30 May 2015

Msafi au Unajipenda?

Kuwa msafi ni tofauti na kujipenda.....Habari gani?Mimi sio Msaaaaafi to the point nahitaji "Tiba" ya Ushauri Nasaa, lakini napenda kusafisha Bafuni/Chooni na Jikoni (nachukia kuosha vyombo though).
Maeneo au vyumba hivyo ni muhimu sana kwangu na kwa familia yangu kwasababu  natumia muda mwingi zaidi.Unapoenda Kushundi sharti utulie kwenye mazingira Masafi, haependezi kushundi(kutoa haja kubwa) huku unahofia kupata Maambukizo.Pengine unaharakisha kutoka na kukatisha Haja yako kwasababu ya harufu ya uchafu mwingine zaidi ya Kinyesi chako.Nahitaji kweli kuelezea kuhusu usafi wa Jikoni au Mahali unapoandalia chakula?Kuna siku nilikabidhiwa Jiko...si unajua wale akina Wifi/Shemeji ukienda kuwatembelea wanataka wakutumikishe? Basi nikapewa Jiko....mwenye Jiko mwenyee anajipenda huyo!Jikoni kwake sasa.....kulikuwa na uchafu worth of 3yrs akyanani nikashindwa kupika ikabidi nisafishe jiko na maeneo ya karibu. Kwenye Sinki kulikuwa na vyombo vichafu worth of 5days(Uanaume sio kigezo cha kuwa mchafu) khaa!


Anyway baada ya upishi nikaibua sababu ya kuondoka ili nisile chakula nilichopika.


Ukitaka kujua mtu Msafi au Mchafu basi mjaji kwa kuangalia Bafu/choo na Jiko au mahali anapoandalia Chakula(sio kila mtu ana jiko). Kujipenda kimwili na Mavazi sio kithibitisho cha Usafi wa mtu.

Off i go to do my dishes.....

Babai.

Wednesday, 27 May 2015

Matiti Makubwa(asilia) Vs Madogo....

Hi!

Matiti ni fuko la Fat ambalo halina umuhimu....well zaidi ya kunyonyesha watoto. Sasa kama umemaliza kuzaa what do you do with them hasa yale Makubwa?


Sie tulionyimwa matiti bana tukimaliza kunyonyesha tumatiti twetu tunapotea, yaani unabaki na alama ya matiti ambayo hayahitaji Brazia....well inategemea na umbile la titi, maana kama yako ni yale Papai shape au Embe sindano Shape mwenzangu hadithi ni ingine.


Kwasababu ukubwa uliongezeka mara 3(mara mbili) kutoka B mpaka D na kifua kutoka 28-34inch.....yes nilikuwa 34D!!, hofu yangu kuu ilikuwa ni matiti kulala baada ya kumaliza kunyonyesha.


Lakini baada ya watoto wawili yapo pale pale kati japo sio firm kiviiiiile lakini hayajalala (too small to sleep hahahahaha to sleep).


***Faida chache za kuwa na tumatiti tudogo ni kama ifuatavyo:-

-Unanunua Sidiria Duka lolote kwa bei chee(japo huitaji one).....Ile shughuli ya kunyanyua Titi ili kujiswafi chini yake huwezi kuipata-Mambo ya kulala chali na matiti kukimbilia Kwapani haitokutokea.....usipovaa braa bado matiti yataonekana(well chuchu hihihihi).


Still better than kuonekana huna matiti kabsaa halafu chuchu zimejitokeza tumboni kama sio kiunoni.


-Siku ukitaka kuwa na matiti Makubwa ili uvae a V Top unaibua Push up bra.-Ule mstari unaojitokeza katikati ya matiti hautojitokeza sababu matiti yako hayajalala na hivyo hayahitaji kunyanyuliwa na kukutana.....utaendelea kuwa na a clear kiliveji Milele.


-Wakati wa kuneng'enuka ktk mtido wa wewe juu huna haja ya kuyashikilia ili yasimchape usoni Mpenzi wako. Pia mikono yake inakuwa huru kukamata sehemu mbali mbali za mwili na sio kushikilia matiti mwanzo mpaja mwisho wa Mzunguuko.Hata kwa ile mbuzi kagoma inaeza kuwa uncomfortable kwako kama jamaa anaenda kwa nguvu na kwa sipidi, na haujavaa Sidiria lazima yakutandike usoni au tumboni si eti...pa-pa-pa-pa(in my head...mmh).


Halafu mtu analalamika mkewe anachoka haraka kunako kuneng'enuka......hujui kuwa Matiti ni mazito(full of fat).


***Hasara za Matiti madogo

Hawahishi kukuhisi kuwa wewe ni Msagaji hasa kama huna womanly shape.

-Baadhi za nguo hazikupendezi mapaka uvae Push up Bra.


-Tumbo lako linainekana kubwa kuliko lilivyo.


Natumaini Post hii itakufanya wewe mwenye tudogo utupende tutiti twako(small chested hatupati Credit za kutosha) na wewe mwenye makubwa utaona the funny side of it badala ya kuwa offended.  Ahsante kwa kuichagua Blog hii.


*Kuneng'enuka=kufanya Mapenzi. Ni neno langu mbadala sio rasmi.

Babai.

Monday, 25 May 2015

Wanataka uwe single Milele....

Watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki).....heiyaaa! Happy Bank Holiday wa hapa nilipo.

Kama bado hujagundua basi utagundua muda si mrefu. Uhusiano wako unaponawiri tu, unaanza kusikia maneno maneno kuhusu Mpenzio au watu wanaomuhusu iwe Familiani au Kazini.

Pengine hakukuwa na vijimaneno lakini tangu umefunga Ndoa wameanza kujitenga au kuanzisha urafiki(kufahamiana na watu wengine.....wale ambao wewe hupatani nao aka maadui zako).

Au kila kitu kipo sawia na hayo hapo juu hayajawahi kutokea lakini tangu umejifungua au Mkeo kazaa basi na wao "marafiki" wanaanza kupunguza ukaribu kwako.

Marafiki hao(watu unaofahamiana nao) wote au nusu na robo yao huwa kwenye Ndoa na Familia na wewe ulikuwa the only SINGLE one or the few of that robo ya mzunguuko wenu wa urafiki.

Unaendelea ku-effort-ika(make an effort) kuwatafuta kwa simu au kutafuta muda ili kubadilishana mawili matatu kuhusu maisha yako mapya na yale ya enzi.

Hawapatikani au hawatokei kwenye mihadi ya  kufurahia siku husika, tena wala hawajali wala kuheshimu kuwa una Shughuli nyingi kwani sasa wewe ni Baba/Mama(priorities zimebadilika).

Unatafuta within yourself ili kujua umekosea wapi? Then unakuja kugundua kuwa "aaaah nina familia". Kumbe walikuwa wananipenda nilipokuwa sina Majukumu!

Sasa wananikwepa kwasababu sitokuwa free kwenda kwao ku-baby sit, kuwashauri kuhusu Ndoa zao na kuwakopesha senti(well mie....i still feel used).

Hao sio Fake isipokuwa ni watu ambao wanapenda kutumia wenzao kwa manufaa yao kwa kisingizio cha kufahamiana.....well wewe utasema Urafiki.

Shukurani kwa kuichagua Blig hii.
Babai.

Thursday, 21 May 2015

Ni kweli wa Ughaibuni wajuaji....

Ndio na Hapana.....hello, jambo kabisa?

Wengi sio wajuaji (wanajua sana)ila nadhani ni wazuri kwenye kufananisha..... ukifananisha system ya UK na Tza kwa mfano hakika uta-sound mjuaji(kumbe ni bongolala tu).Kingine kinachofanya udhani kuwa wa Ughaibuni wanajifanya wajuaji ni uhuru wa kusema, kwamba kila mtu ana Maoni yake kuhusu kila kitu kinachotokea au anachokisoma na pengine kushuhudia.Uhuru huo (ahsante nyingi kwa Gugo) unafanya baadhi yetu kuweka maoni yetu  kwenye issue yeyote ambayo tunahisi inatugusa.Nikianza kukupa (maoni yangu) mbinu za kukusanya Kodi (nita-base zaidi na system ya UK ambayo naijua lakini wewe huijui) na kuitumia Kodi hiyo kwenye kuboresha Maisha ya Watanzania waishio maisha Duni hakika utaniona nina Akili kweli na ninafaa kuwa Waziri.Kumbe katika hali halisi mie ni m-bovu wa Hisabati na Masuala ya Kiuchumi siyajui lakini ni mzuri kwenye kujieleza so nikipata "material" naweza kuyaelezea kwa urahisi na kueleweka bila kutumia "statistics".Unajua kuna tofauti kati ya Mghaibuni alielelewa kimtaani aka uswahilini na yule aliekulia kwenye mazingira ya Kati(kawaida), pia yule mtoto wa Kigogo(high life) bila kusahau alietoka Kijijini break ya kwanza London(kwa mfano).Sote tunaishi Ughaibuni maisha tofauti kabisa (inategemea na kilichotuleta)lakini Maoni yetu yanaweza kuwa sawa kwasababu System za Nchi zilizoendelea zinafanana.


Pamoja na kusema hivyo bado sehemu kubwa ya wa Ughaibuni wanajua zaidi kuliko wale ambao hawajawahi kuishi Ughaibuni.Nadhani kinachosaidia zaidi ni mchanganyiko wa watu wengi wenye "Kacha" zao tofauti ambao unakumbana nao kwenye maisha yako ya kila siku.Kujifunza au kuwa na uwezo wa kumchukulia kila mtu kama alivyo na kumsikiliza kuhusu Kacha na desturi yake(inategemea anatoka wapi Duniani).  Hali hiyo inapanua upeo wako....unajikuta unajua taratibu mbalimbali za Maisha ya watu wengi kutoka Nchi tofauti Duniani.Nyumbani(Tz) tunajichanganya wenyewe kwa wenyewe na tofauti yetu ni Makabila lakini bado tuna-share baadhi ya Desturi na Tamaduni zetu kulingana na Kabila.Hata kama kuna Mataifa mengine bado sio kwa kiasi kikubwa kama Ughaibuni. Kuishi Ughaibuni kunamfanya mhusika kujifunza mengi bila yeye kujua(bila kuingia Darasani).Usipofunzwa na Mamayo(Nyumbani) utafunza na Ulimwengu(Ughaibuni).

Babai.

Monday, 18 May 2015

Kwanini Weusi sana huenda na Wazungu?


Herooo heri ya J'3!

Unakumbuka ile vita ya Weusi na Weusi wenye rangi ng'avu(wewe unawaita Weupe) niliyoigusia hapa mawiki kibao yaliyopita?....haiwezi kuisha hasa kwa nchi hizi za mbele.Kufunga ndoa na mtu Mweupe zaidi yako ni kupoteza muda, Baadhi ya wanadamu (Weusi) wanaamini kuwa unless mwenza wako ni Mzungu.....uhusiano wenu hautodumu.Mmmh come to think of it.....Weupe(Wazungu) wengi(niwaonao) wakiamua kuoa au kuolewa huenda Darker. Umewahi kuona Wazungu wangapi wanafunga ndoa na Waafrika ambao ni a bit lighter/fair.Halafu ukifanya Uchunguzi wako binafsi ambao sio rasmi (obviously)kwenye Sosho Media utagundua au utaona walio na Wazungu kama wenza wao ni weusi sana(deep dark).Lakini pia Ndoa au Mahusiano hufikia mwisho kwasababu nyingine nyingi na Rangi sio moja ya sababu hizo.Hivi ujawahi kujiuliza kwanini wanaume wa Kizungu hujibebea wadada Weusi warembo kweli (model like kiumbo) tofauti na Wanaume Weusi ambao hujikusanyia wamama_____well hurudi home na watoto wao kila mwaka lakini Mkewe haji....kwanini?Asali wa Moyo ana-share Picha zake na watoto bila mimi hihihihi wale wale....angalau mie sio Mzungu bana.

Babai.

Friday, 15 May 2015

Adui mpende.....mpende adui yako.

Hivi wewe una adui?

Kusema ukweli kabisa mie sina adui which means mie sio adui wa mtu yeyote.....oh hello!


Kuna wakati unazungumza na watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki) na unakutana na suala la maadui......kwamba wanawazungumzia "maadui zao" na jinsi gani wanawachukia halafu unajiuliza imekuaje mpaka hawa watu wanakuwa na maadui?Adui yako anaweza kuwa mtu yeyote kuanzia nduguyo wa damu mpaka yule uliewahi kuchangia nae mwili lakini sasa ni HISTORIA iliyofutika .Sababu za hawa majamaa kuwa maadui zinayofautiana lakini chanzo mara zote (nidhaniavyo mimi) ni ukaribu wao kwako.Ndugu: Unajua Ndugu wa damu mnapokuwa watu wazima mnabadilika (mnakuwa) na ule ukaribu wenu hupungua kutokana na mmoja wenu kuishi maisha tofauti na  (mume au mke) wake.
Baadhi ya ndugu huwa bitter wakidhani kuwa huwajali tena na badala yale unajali zaidi mkeo/mumeo na "familia yake".....ni kweli halafu sio kweli kwa kisingizio cha  utahama kwenu na kumfuata mwenza wako.
Jamaa na marafiki: Huna muda tena wa kukesha nao au kufanya starehe kila mwisho wa Wiki AU kuongea kwa masaa na masaa Simuni....watadai umebadilishwa na mkeo/mumeo.Unapokuwa mtu mzima(well in your 30s aka mimi) na unakafamilia kako kuna vitu vilivyokuwa muhimu enzi za 20s havina umuhimu tena so unaachana navyo.Sasa kwasababu ulishawahi kuwa karibu na hayo makundi niliyoyataja hapo juu ni wazi kuwa hawatakuacha uendelee na maisha yako kwa amani. Wanakuwa kama wale Exes vinga'ang'anizi waishio in Past for life(move on darling life is passing you by).Makundi hayo yatafanya yote ili kujua unaishi vipi ili wakuharibie so that urudi kwao. Wakishindwa kabisa wanatumia ule ukaribu wao waliokuwa nao kwako na wakijuacho ili kusambaza chuki (kumbuka kuna mambo nyeti waliyajua kuhusu wewe).


Halafu kuna wale ndugu ambao inatokea tu hawakupendi (kabla ya u-30s)mpaka unahisi kuwa "mama alitereza" nje nini? Kwanini kaka/dada yangu kutoka baba na mama mmoja ananichukia hivi!Mie sina Adui japokuwa kuna watu (maadui wa mume wangu)wanalazimisha wawe maadui zangu hihihihi lakini sitoi nafasi.Pia nikikorofishana na mtu Familiani huwa nawaua (in my head) so wanakuwa hawa exist....siwazungumzii wala kuwaulizia na sitomwambia mtu yeyote kwanini tulikorofishana.Ukaribu wako kwao ni kuwa easy target kwa mengi mabaya ambayo ni chanzo cha Uadui. Shukurani kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Tuesday, 12 May 2015

Mvaa Vimini na mzaa ovyo....

....nani hajiheshimu?

Mambo vipi?
Uchaguzi umepita....maisha yameanza upya Jana na Pound imeshuka thamani. Maana Ijumaa ilishuti mpaka kufikia 2,900Tsh(why am i telling you this? Never mind).Kuna wakati mtu unachoka kujielezea na kuelewesha baadhi ya watu kuwa Mavazi ya mtu sio tabia na mavazi mafupi sio kielelezo cha mtu kutokujiheshimu.Natambua kuna tofauti ya ufupi wa mavazi kulingana na umri japokuwa umri sio sababu ya mtu kubadilisha style yake ambayo anadhani kuwa inampendeza kulingana na shape yake au kulingana na kuonyesha kilicho "perfect" ili kuondoa attention kwenye kile akionacho kuwa ni "imperfect" (miguu vs sura) hiihihihihi mie.Sasa unapomuita mvaa nguo fupi kuwa ni Malaya, hajiheshimu au Changudoa(uchangudoa ni kazi japo siiungi mkono) na kumtukuza mvaa mavazi marefu na ya kujificha(eti heshima) lakini ana watoto 3+ kutoka wanaume watatu tofauti unakuwa bwegelao(bongwa la mabwege).
Kabla hujachukia au kuponda vazi la mtu ambalo unadhani kuwa si la heshima....jaribu kuangalia kinachosababisha mhusika kuvaa anavyo vyaa. Pia kumbuka mwili ni wake na anauvika atakavyo kutegemeana na anavyojisikia.Kama ilivyo kwa wazaa ovyo(wake kwa waume).....kuna sababu ya wao kutoheshimu miili yao (zaidi ni Saikolojia ila wengi ni kutojiheshimu)na kujiachia bila kinga. Wanaume wengi wazaa ovyo wanajisifia "mie dume la mbegu" na wanawake hu-justify kuwa "nimeubwa kuzaa".


Basi hata wavaa nguo fupi wanasababu zao na moja nimeitaja hapo awali.

Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Thursday, 7 May 2015

Tuepushie Bunge la Kuheng'i....

...na tuepushie huyu wa sasa....amen!  Natumai Kura yangu itaongeza palipopungua 2010.

Heyaaa!

Kuna wiki moja huwa inakuwa busy sana na appointments kuliko.....Dentist....Chanjo kwa Kibibi....kuongezea Chanjo kwa Babuu....manunuzi ya viwalo vyao vya summer.Wengine (mimi) tunanunua nguo Sikukuu to sikukuu. Unafanya kubadilisha Makoti na Majaketi ya Miaka 2 iliyopita.....sio kila Majira ya mwaka yanavyobadilika mweee.Halafu mtu anakuambia "hutaki kuzaa kwasababu unaogopa maisha".....no dear naogopa gharama.


Well ukiachilia habari ya kukujulisha kwanini sijapost kwa muda kiasi, ni kwamba huu uchaguzi wa Leo unanipa Presha kimtindo.Naenda kulala ili niweze kufuatilia matokeo kuanzia saa Tatu(Tano tz).

Ahsante kwa kuichagua blog hii.

Babai.

Sunday, 3 May 2015

The Online Support....kwa Celebs!


Hata kwa sie ambao sio maCeleb is real.....unajua pale unapoungwa mkono na kupewa ushirikiano wa "kisaiba"(cyber) na kukufanya ujihisi umebebwa....unapendwa...unakubalika.


Unahisi furaha na pengine kujiona Mashuhuri(mtu wa kawaida) au kuhisi Umashuhuri wako (kwako Celeb) umeongezeka na kupata Konfisensi ya ajabu ya kufanya lolote au chochote.

Unajua ile umeweka Picha halafu unapata followers zaidi na wanakumwagia masifa.....wanaomba kuona zaidi na wewe unazimwaga picha za mapozi tafauti hihihihihi baada ya siku mbili wanakuja followers wapya(wale wale kwa account tofauti via device tofauti) na kuanza kukuponda.....unabaki kulia na kuita watu "fake friends".

Inategemea ni nini hasa kimefanya upate support ya "Fanzi" aka followers wako Online.....kuna wakati unahisi kutaka kusema ukweli wako ulivyo na sio uongo wausikiao au ku-justfy na ku-share zaidi ya unachopaswa kusema/ku-share.

Bila kuomba ushauri kutoka kwa "inner self" au bila kumsikiliza yule "sixth sense" huyooo kwa kujiamini kabisa unaenda na kuyamwaga yaliyo chini ya uvungu wa Moyo wako aka Siri zako ambazo ni muhimu kwako na sio kwa Jamii au "Fanzi" wako wanaokufuata popote ulipo Online.

Pap! Unapoteza Dignity(na bado hujazaa....mwee bora kuzaa unaacha zilipo Dignity zote pale Leba rum )....unapoteza maana...unapoteza umuhimu kwa hao ambao sasa wanakujua nje-ndani bila kukufahamu.


Unawapa nafasi watu kukujua kwa undani lakini hawajawahi kuishi na wewe achilia mbali kukufahamu.

Sio wote wanaokuchekea Mtaani wanaupendo kwako na si wote wanaokufuata online wanaku-support......wengi wao wanakufuata ili wawe wa kwanza kukumaliza "kisaiba" na wengine ni kwasababu wanataka kuhisi unafuu kuwa "aaah hata wewe unashida na matatizo....sio peke yangu au yako makuu kiliko yangu".


Kama issue yako chini ya moyo(Siri) ni muhimu kwa jamii in terms of kuelimisha  na labda kuwa Advocate wa UN then tuambie.....vinginevyo keep it to yourself.....hata wazazi wako wasijue.

Hakuna ulazima wa ku-justfy ambacho tayari kimesambaa kwa muda mrefu Mtaani(in reality) au Online.....kwasababu hata ukijaribu bado watu wataamini kilichosambaa na sio justfication yako.

Jibakizie Dignity Mrembo/Mtanashati. Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Friday, 1 May 2015

Kumbe Minimum wage ni £4 kwa Wobama


Not exactly.....
MAY Moja njema sana kwako mpendwa na ahsante kwa Kuichagua Blog hii.Kuna siku nilikuwa nasoma Forum moja hivi kuhusu Ughali wa Maisha hasa kwa sisi Mama wa nyumbani wa Muda mfupi au wale wa Kudumu(sijaji mie).Mdada mmoja akauliza ni namna gani wenzake wanabajeti vipato vya Waume zao. Yeye akadai kuwa anashindwa kabisa kubajeti Mia Tano Hamsini (£550)kwa Wiki.Akaja Mmarekani bwana (tatizo la mUS ni la wote si walijua hilo)akaanza kushusha manamba kuwa mumewe anaingiza $750 kwa Wiki na haitoshi ndio itakuwa £550.....siku pay attention kwenye Dola & Pound mpaka nimesoma hii article.
The Guardian: Congress to propose bill raising US minimum wage to $12 by 2020. http://google.com/newsstand/s/CBIw1Iu9zSEObviously hata yeye wa $750 hakuiona £ kabla ya 550 hihihihihihi oh boy kumbe Dola 750 is less than Pound 550.....Kima cha chini UK ni £6.45p Labour wakishinda inakwenda 8...kwa maana nyingine US watafikia 6.45p in 5 years......sio exactly lakini you get an idea.Bado sielewi kwanini Bidhaa za US zikija huku zinakuwa Ghali. Haa! Mie na Hisabati wapi na wapi.

Babai.