Saturday, 28 November 2015

Mzunguuko wa Ngono kwa Mwanamke...

Jambo!

Kama unakumbuka niliahidi kuwa nikipata muda nitaandika kuhusu Mzunguuko wa Hedhi ambao unaendana na Mzunguuko wa Kufanya Ngono/Mapenzi kwa Mwanamke. Nilielezea kuwa Mwanamke sio kama Mwanaume, kwamba tunakabiliana na mambo mengi ukiachilia mbali Homono(Pengine ni Homono tu).
Kuna siku Mwanamke analianzisha, inaweza kuwa mara moja au tatu kwa mwezi. Pia kuna siku mwanamke anataka kuwa Juu sio kwasababu wewe Mkibaba unataka bali mwili wake unamtuma kutaka kuwa in-control na hii inaweza kutokea mara kadhaa ndani ya mwezi lakini sio kila siku. Hali kadhalika zipo siku(ambazo ni nyingi) mwanamke anataka kuhisi kupendwa  na kujaaliwa kwa vitendo(kitandani)......vinginevyo Tendo halitokuwa na maana na halitokuwa la kufurahia.
Wale Wanawake na Wanaume mabingwa wa kuwalaumu wanawake kuwa ndio sababu ya Waume zao kutereza nje ni ama hawaujui Mwili wa Mwanamke, kwamba mwanaume ataka na kutegemea Mwanamke awe in control kila siku......au kungojea Mwanamke alianzishe ili afurahi au ajihisi Mfalme.Tusipoteze  muda sana....twende kwenye Mzunguuko (Siku 28 ndio nina uzoefu nao).


Wiki ya Kwanza(Siku ya  1-7):  Siku unayoanza Hedhi/ona damu ndio Siku ya kwanza ya Hedhi na ndio unaanza Wiki yako pia. Haijalishi imeanza saa ngapi. Unakuwa umechangamka na utahisi Akili yako imetulia na kufanya kazi vema. Unapata "ari" ya kufanya mambo tofauti au mengi-mengi.Unakuwa kind too active.

Wiki hii ni nzuri ikiwa unaenda kwa siku 2-3. Wiki hii utahisi kutaka kufanyanyiwa Mapenzi zaidi ya wewe kuwa "mtendaji".
Wiki ya Pili(Siku ya 8-14): Wiki ya Kujiamini na kuhisi kutaka, unakuwa Muongeaji kuliko siku nyingine, unahisi kumpenda mwenza wako(au kutamani kupenda kama huna), unahisi kuwa na Nguvu nyingi na hujui hata uzitumie vipi!!Hamu ya kutaka kufanya mapenzi huongezeka, unataka kuwa kwenye Control. Wiki hii Mwili wako "huchemka".....Vijana mnasema kuwa "hot", Ute wako unakuwa laini na uke "kulowa" kama vile upo tayari kwa Tendo. Wiki hii ndio Mwanamke unajiweka mwenyewe Juu, unakuwa mtendaji Mkuu na pengine kutotosheka na Tendo.Wiki hii pia ni Hatari ikiwa huna mapango wa kuwa Mama, hivyo kumbuka kutumia Kinga.
Wiki ya Tatu(Siku ya 15-22): Shughuli ya Uanamke ndio huonekana hapa, unakuwa na ama Huzuni au Hasira, msahaulifu, kila kitu unaona kero tu. Wiki hii hakuna Hamu ya kufanya mapenzi wala kufanyiwa Mapenzi. Mwenza wako asipokuchokoza na kwa kujituma kweli kweli kwenye "maandalizi" tendo linaweza likawa la maumivu/karaha. Pamoja na yote hayo bado Wikii nii salama, kwamba kama umehesabu vizuri basi huwezi kushika Mimba.
Wiki ya Nne(Siku ya 23-28); Siku Sita kabla ya kuingia Siku ya 28(siku yako ya Hedhi), utaanza Wiki hii kama ulivyokuwa Wiki ya Tatu, tofauti ni kuwa Wiki hii utakuwa na Nyege(hamu ya kutaka kufanya mapenzi) nyingi. Utakuwa Mkali na mwenye Kisilani labda.....lakini ukiguswa Kiuno tu tayari "umelegea".Ikiwa Mumeo anajua Mzunguuko wako hapa ndio huwa anakutegea.....unamjibu kwa kiburi, yeye anakuja kukushika kwa nguvu na Kukubusu, halafu unakosa la kusema unaishia kupeleka Mkono kwenye nanilihu....hihihihi. Wiki hii ndio ile "sex when angry" huwa tamu. Umewahi kumtaka Mumeo aende kwa Kasi na Kwa nguvu? yeeah, basi lazma utakuwa unakaribia Hedhi aka upo Wiki ya Nne.Hata hivyo, "hasira" nilizogusia hapa ni zele zetu wanawake kutokana na Homono, sio zile kuu na chafu. Hey Post imekuwa ndefu, wacha niishie hapa.


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Tuesday, 24 November 2015

Kulazimisha Mtoto awe na Mawazo....


Pengine ni ngumu kujua tofauti ya ku-share information kwa nia ya kuwafanya watambue "Asili" yao, wajifunze kuhusu Upande wa pili(kwa wale waishio Ughaibuni) na kuwapa watoto mawazo.
Natambua kuwa kila Mzazi ana namna yake ya kulea na kufunza wanae, na kamwe sitokufundisha namna ya kulea wanao tangu mie mwenyewe  najifunza kila siku. Lakini tukumbuke kuwa kuna "Common Sense".....huitaji Elimu wala Uzoefu kuitumia.Unakumbuka ulipokuwa Mdogo na Mama au Baba au mtu yeyote wa karibu anaanza Hadithi za "Kaka/Dada" yako aliezaliwa na kufariki.....kisha ukaanza kuwaza ingekuwaje hivi sasa kama angekuwepo? Unawaza huko aliko je anafuraha, ana-toys,? unakuwa na Maswali kibao ambayo hayana Majibu. Mtoto anakosa usingizi kwa Mawazo au Uoga na akilala anamuota "dada/kaka". Wazazi hapa hudhani/amini kuwa Mtoto ana connection na "mwenzie"....lakini ukweli ni kuwa anasumbuka Kiakili na Kihisia.

Pia umewahi kutambulishwa kwa Ndugu yako ambae Baba/Mama alizaa wakati wa "ujana" na sasa anaishi na Mzazi mwingine ambae sio Baba/Mama yako. Unaanza kuwaza na ku-wish ama ungeishi kule au yeye angekuja kuishi hapo kwenu. Unatamani kuwa Wazazi wenu wangekuwa wamoja(baba na mama mmoja). Kwa Mzazi mmoja ambae ni Mzazi wa Mtoto wa Upande wa pili huona ni Jambo jema kwamba Mtoto huyu ana-value undugu wake na mtoto yule wa kabla ya Ndoa......Ukweli ni kuwa unateseka Kiakili na kihisia kuhusu Jambo hilo.
Halafu unakumbuka ile hofu uliyokuwa nayo pale Mzazi wako anapokuambia hana Pesa na XMas imekaribia, sio tu mtakula Ugali badala ya Pilau pia hakuna Sare  Mpya za Shule, Madaftari wala Kalamu....yaani unaenda shule na Sare zako zilizochakaa. Unapata Donge rohoni(unaijua ile hali ya kutaka kulia lakini huwezi kulia, huwa kuna maumivu  si maumivu fulani sehemu ya Koo hihihihihi)....Roho inakuuma na unakosa Amani kabisa kila Baba/Mama anaporudi Mikono Mitupu na ni tarehe 22 Dec!!....kwa Mfano.
Mzazi hapaswi kumuambia Mtoto kuwa hana Pesa, hilo ni jukumu lako kwasababu wewe ndio ulieamua "kumleta" ama kwa Uzembe au kwa Kupanga. Kwanini huamishie "Hatia" zako kwa mtoto na hivyo kumpa mawazo? Kama mzazi tafuta namna kwa uwezo wako wote  na kuhakikisha unatimiza mahitaji ya Mtoto. Mtoto haitaji kujua kama una Pesa ama huna au unazipataje.Kuna wakati unakuta Mtoto anakuwa Mkimya sana(anakuwa na mawazo au depressed), lakini kutokana Umri wake unadhani kuwa hana Mawazo na hivyo ameamua tu kutulia leo(ameamua kuwa  mtoto Mzuri). Ukweli ni kuwa Mtoto anaanza kuwaza akiwa na Umri Mdogo sana kuliko tunavyofikiria.
Wazazi ndio chanzo cha Mengi Mabaya au Mazuri linapokuja suala la Ukuaji wa mtoto Kiafya, Kiakili, Kisaikolojia n.k. hivyo ni muhimu kutafakari na kujua Mipaka ya Info gani zinapaswa kuwa shared kwa umri husika.
Mtoto anapozaliwa huwa Mtupu akilini. Kila siku hujitahidi kujaribu na kufanya mengi, Mtoto huyu haitaji kuwa "feeded" masuala mengine ambayo hayamhusu kwa Umri alio nao! Muache mtoto awe mtoto.....muache awe huru. Mtoto anakabiliana na mengi katika kujifunza na hivyo haifai kuanza "kupandikiza" hatia zako za Mtoto uliemuacha kwa Baba/Mama yake, kwa mtoto huyu kwa kisingizio cha "nataka ajue kuwa ana Kaka/Dada" hai au katangulia.
Pia sio sahihi "kupandikiza" hatia za ukosaji wako wa pesa kwa mtoto kwa kisingizio cha "nataka ajue ugumu wa kutafuta" au "nataka ajifunze mapema kuhusu utafutaji wa Hela". Subiri mpaka afikishe Miaka 8, pale unapoanza kumshikisha Pocket money(pesa ya kutumia shule) tena unamfunza kutunza sio "kutafuta".Wacha niishie hapa, Nathamini na Kuheshimu Muda wako hapa,  ahsante sana kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Thursday, 19 November 2015

Era ya Kulazimishana ku-react!


Heiyaaa!

Mtu una-react kutokana na Uzito au Wepesi wa Hisia  unazopata kutokana na Tukio au Jambo fulani. Kuguswa kwako kunaweza kutokana na Upendo au Chuki au Kutojali, Kutoona umuhimu wa jambo hilo lililotokea n.k.
Kama unakumbuka Rais aliyepita alikuwa mzuri sana/Maarufu kwenye kushiriki Masuala/Matukio ya Kijamii. Naamini kufanya kwake huko kulitokana zaidi na kuguswa kwake yeye kama Mwanadamu na sio kama Kiongozi wa Nchi. Kwamba anapojitokeza Mahali, haendi kuwakilisha Taifa basi yeye na pengine Familia yake. Reaction yake kwenye Misiba ilichukuliwa kivingine....achana na Siasa(Msimamo wangu kwa JK bado ni ule ule hihihihi), ni mfano wa karibu ili unielewe.
Sasa kwenye Era hii ya Sosho Media imekuwa ngumu na pengine haikubaliki kwa baadhi yetu kuweka wazi hisia zetu kwa kuhofia kuonekana "tuna roho mbaya", "hatujali", "tunachagua matukio yapi ya kusikitika/kufurahia", n.k.Imefikia mahali wale "Magwiji" sijui "Wakongwe" (waliokuwemo kitambo kwenye Sosho Midia) kulazimishana ku-react na matokeo yake utakuta kila Blog/Site inazungumzia tukio lile lile kwa Siku kadhaa......kama ilivyo kwenye News Media. Sasa pengine Blog wanakimbiza "traffic" kwa sababu za kimapato zaidi na sio kwamba wanajali,umia au chukizwa  na tukio fulani lililotokea.
Platform kama Twita na Facebook zimekuwa zikitumika kulazimisha watu wa-react au ku-fit in na kuonekana(hata kama hawana hisia hizo) kuwa wameumia na wanajali kuhusu Tukio fulani linaloendelea kwa wakati huo.

Nitakupa Mfano mwingine. Linapotokea Shambulio au Maafa kwa Nchi kama India, Nigeria,Pakistan, Palestine, Ukrain, Russia na Israel huwa sipati hisia yeyote(nimechoka kusikitika na kukasirika), huwa si-react(nakuwa kawaida tu)....sasa silazimiki kuungana na wale walio-react kwa furaha au hasira au chuki na huruma......Hisia hailazimishwi, inajitokeza tu yenyewe.

Ikitokea umeguswa na tukio, usianze kuhamishia hasira zako kwa watu wengine na kuwalazimisha waungane na wewe au na ninyi ili "kuonyesha" kuguswa sawa wakati wanajua kabisa hawajakuswa kama ulivyoguswa wewe.

Imefikia mahali mtu unaamua ku-fit in ili uwe-protected na Magwiji uliowakuta kwenye hiyo Sosho Midia, kwamba ukienda tofauti na mtu na ukawa-attact maGwiji wanakuja kukusaidia. Umezoea ku-fit in mpaka unapoteza uwezo wa kujitetea. Ukiwa mtaani ana kwa ana na attacker au bully utafanya nini?

Labda tujaribu kuacha  Kacha ya kutaka  # zetu ku-trend kwenye Sosho Midia na hivyo ku-bully wenzetu ili wa-fit in na vile tunavyohisi sisi. Kila mtu ana haki ya kuweka/kutokuweka Hisia zake wazi, japo ni muhimu kuzingatia Sheria za unapoishi ikiwa unataka ku-share Hisia zako ambazoo ni Hasi. Tukubali kutofautiana iwe Kijinsia, Kiuchumi, Kihisia na mengineyo.Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Tuesday, 17 November 2015

Wasichana tuliokulia miaka ya 90...


....ndio tulipokea kwa nguvu zote suala la Haki za Mwanamke au Usawa aka U-Beijin. Waliopigana vita ni Mama zetu ambao hawakutaka sisi tuonewe kama ambavyo wao walionewa. Baadhi ya Mama zetu hao walikuwa na Hasira na Wanaume kutokana na "treatment" walizopatiwa na Wanaume kama Wenza wako, Wafanya kazi wenzao, Wakubwa wao kwenye Familia na Maboss wao.
Ujumbe na maana na nia ya "Ubeijing" ilikuwa nzuri na bado ni nzuri, lakini kwa baahati mbaya kwa baadhi ya akina Mama zetu hao waliziwakilisha kwetu, wasichana ambao tulizaliwa mwishoni mwa miaka ya 70s na 80s ambao ndio tumekulia era ya "Ubeijing" au niseme Miaka ya 90.
Heka heka za kupigania Haki/Usawa kwa wanawake imeanza  miaka ya 60s kwa nchi niliyopo na mafanikio makubwa yalikuwa ni kutambuliwa kwa "haki" ya mwanamke kufurahia tendo la kufanya Mapenzi, kwamba tendo hili sio kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume. Baada ya hapo ikaja suala la kutumia Kinda Dhidi ya Mimba(Kidonge).
Mkutano wa Nne wa wanawake uliofanyika Ubeijing mie nilikuwa  ndio namalizia Shule ya Secondary. Nilikuwa najivunia sana ile Hotuba ya yule Mama wa Kitanzania (nimesahau jina lake na sina mpango wa kuGugo....soma Picha hihihihi) niliona kuwa ni Mwanamke Msomi(academically smart), Shupavu na Imara.
Sasa, sisi Wasichana wa Era hiyo ndio tulikuwa wa kwanza kuweka "Ubeijing" kwenye actions kwa nguvu zote.....tulikuwa kwenye "presha" bila kujijua, tulihakikisha tunabaki shule kwa muda mrefu (sio kukimbilia kuolewa) na kuipata hiyo Elimu kama Wanaume, Era hiyo wengi  wetu tulichukua Masomo ya  "Magumu" kama vile Sayansi(nili drop katikati though usicheke), tunafanya kazi za Ufundi,Uinjinia, Urubani,Ukandarasi n.k.
Wasichana wengi tulifaulu Mitihani, hatukuwa wa kati wala mwisho tena. Tuliongoza Darasa na Mikondo. Dhamira yetu ya kujitegemea na kuongoza na kuelimisha Jamii iliendelea kukua tulipopatiwa Mawaziri wa Kike na kuona Wakurugenzi(akina Ms Mhavile and co) wakifanya mambo.
Fast Foward:...kwa Wasichana wa leo(waliozaliwa 90s wamekulia 2000s) ambao wengi wanaumri kama ule wetu miaka  ya 90, ni teens au wapo early 20s.....hawa are so relaxed! Wanajua haki zao, wanajua wanapaswa kujitegemea na how.....yaani kila kitu kipo wazi kwao hivyo hawapigani ile sanaa kama sisi miaka ya 90s.
Ni kama vile wameona "Ubeijing" haujafanikiwa kama tulivyotegemea(well tangu 1965 bado Wanawake hatujafanikiwa...safari ni ndefu). Wengi wa Era hii(2000s) wapo tayari kufanya kazi nusu siku ili wapate muda wa kuwa  na Familia zao na kuachia Jukumu la Mume kubaki palepale. "Ubeijing" umefanya Baadhi ya Wanaume kuwa tegemezi na matokeo yake mwanamke anafanya Jukumu la Baba na Majukumu yake kama Mama. Wasichana wa 2000s wanachangamoto ya  kubadilisha hili.
Wasichana wa 2000s(wanaokulia Era hii) wameanikiwa(wekea wazi) kila kitu na wao wana-choose and pick, tofauti na sisi  ambao hatukupewa Option kwasababu tulikuwa hatujui lolote kuhusu nafasi ya Mwanamke kwenye jamii ambayo ni zaidi ya Kuzaa na Kulea watoto.
Natambua wanawake wengi walikuwa wakijituma na kuongeza Kipato kwenye familia kabla ya miaka ya 90(Ubeijing era) lakini bado hawakuwa na sauti au nguvu kwenye Vipato vyao, so ni kama walikuwa "watumwa" wa Wenza wao.


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Wednesday, 11 November 2015

Mzazi kukupenda zaidi ya wenzio...


Habari ya sasa!

Kwa kawaida Mtoto wa Kwanza na yule wa Mwisho kwenye Familia nyingi hutokea kupendwa zaidi na wazazi au Mzazi......wakati mwingine wadogo/wakubwa zake. Sababu ya kuwa "favourite" angalau kwa muda hapa ipo wazi.Mtoto wa kwanza ndio kifungua Familia na huwa peke yake kwa muda mrefu au ikitokea kuna mdogo wake kaja fasta basi ile "huruma" huwafanya Wazazi waongeze attention kwa yule wa kwanza. Mtoto wa mwisho ni mdogo kuliko wote hivyo Wazazi na dada/kaka huwa over protected.


Pamoja ya kupendelewa au kupendwa zaidi bado Wazazi wengi huwa hawaonyeshi hilo kwa uwazi ili kuepusha ugomvi au kuwafanya watoto wengine kujiona hawapendwi kwa kiwango sawa. Lakini mnapofikia umri mkubwa unaweza kuona kabisa kuwa Baba na Mama wanampendelea fulani zaidi na hivyo kuanza kujenga chuki au ushindani dhidi ya mwenzenu ambae mnahisi kuwa anapendelewa.Hali hufikia pabaya, mpaka anaependelewa kuanza kujidai na kutumia kupendwa zaidi na Wazazi wake kama Silaha ya kuwaumiza wenzake hasa kwenye Masuala ya Mali ya Familia. Utakuta yeye ndio wa Kwanza kupewa Kiwanja/Nyumba, yeye ndio anaijua Bank Account ya Akiba ya Siri ya Wazazi wenu, Yeye ndio Mshikilia Hati za Assets zote Ghali za Familia n.k.Wale ambao wanadhani hawapendwi sawa na mwenzao(mdogo/mkubwa) hujenga Genge dhidi yako bila wewe na Wazazi wako kujua. Unakuwa huna sauti kwenye maamuzi ya Kifamilia......kwamba mchango wako hautwi maanani(unadharauliwa).Kama Wazazi  bado wapo Hai huwa ni rahisi kuendelea na "undugu" lakini mara tu baada ya Wazazi kutangulia basi wewe uliekuwa Favourite unakuwa umeenda na wazazi wako(ndani ya mioyo yao) japo bado una ishi.


Kwenye Familia yangu baadhi hudhani kuwa Mimi ni Favourite(sababu nilikuja Ulaya hihihihi) ukweli ni kuwa hakuna anaependelewa/aliependelewa, kama yupo basi haikuwekwa wazi na Wazazi wetu. Natambua kuwa Mimi nilikuwa Dad's Girl kwasababu ni Binti wa kwanza, sio mtoto wa kwanza.
Nilipata "presha" ya kujifunza mengi kuliko Kaka yangu ambae ndio mtoto wa kwanza. Pamoja na hilo bado sidhani kama Kaka yangu alikuwa "favourite" ya wazazi wetu kwasababu alikuwa wa kwanza kwenye kila Kitu, Kusoma Shule ya Private(miaka ya 90 kwenda Private ilikuwa Deal), kupata the best School Bag na Saa kutoka Ulaya na pia alikuwa wa kwanza Kupelewa Nje ya Nchi.
Nadhani Baba yangu alikuwa Feminist ( Ndio wanaume pia can be Feminist ujue) kimtindo....kwasababu alinisukuma kuchukua Sayansi(ambayo sikuichukua), Alinisukuma kwenye kujitegemea na msemo wake maarufu "ukimtegemea mwanaume utakuwa Mtumwa maisha yako yote", alinifunza Kunyoosha Nguo (am good at kunyoosha Suruali na Mashari) pia alinifunza Kupika Ugali(alitaka Mimi nimpikie Ugali) nikiwa as young as 8yr old.
Well, my point is mie sio Favourite Child, nadhani Wazazi(hasa baba) kama Baba wengine kwa watoto wao wa Kike, hakutaka nisumbuke ukubwani. Aliniandaa. Nampenda sana tu Baba yangu lakini sio Rafiki yangu, Rafiki yangu ni Mama yangu....haya yametoka wapi lakini sasa?
Nikija kwa Wanangu, Asali wa Moyo anasema nampendelea Binti zaidi kuliko Babuu(hii huwa inaniuma) kwasababu najua kuwa nawapenda wanangu the same but different. Nawapenda individually but mara nyingi namtetea Binti kwasababu ni Mdogo sio kwasababu ni my Fav.....Babuu ni Mbabe/Controling hihihihi typical Kaka mkubwa!


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuchagua Blog hii.

Friday, 6 November 2015

Bora alama ya Mstari kuliko F.....Miaka 20 Tangu Secondary


Mambo!

Ijumaa Mpya(ya Kwanza Mwezi huu) na Maalum kabisa kwani ni Wiki ya Kwanza tangu kuanza kwa Mitihani ya Kumaliza Kidato cha Nne Tanzania, na ndio Mwanzo wa Mwisho wa Series hii(inaonekana kupedwa/somwa zaidi), inapendeza!Utakuwa unajua by now kuwa Mie na Hisabati sio marafiki, Biology niliipenda kwenye kuandika Essay kuhusu Maambukizo au Magonjwa(niliyajua haya kutokana na Somo la Sayansikimu kutoka Msingi), mengineyo nilikuwa sielewi(nilikuwa nasinzia). Mwalimu wetu wa Biology Kidato cha Tatu-Nne alikuwa a bit Boring au alikuwa  na Mapepo(hihihi).
Yule mama alipokuwa akiingia na kufungua Mdomo "Good afternoon" mie yuleeeee Uzaramoni.....yaani macho yanakuwa mazito halafu nalala ule usingizi Mzito m paka Udenda! Nikaona aah isiwe shida bana, nikawa siingii kwenye Kipindi chake unless kuna Essay hehehehe.
Sikufanya Mitihani Miwili  nayo Hisabati na Biology, kwasababu nilijua wazi sitofanikiwa kufanya vizuri na matokeo yake nikaamua ni Bora nipate alama ya Mstari(-) kuliko li-F. Wazazi wangu hawakulijua hili mpaka baada ya Kupata Majibu. Huu ulikuwa Uamuzi Mkubwa nilioufanya katika Maisha yangu nikiwa a Teenager!!Baada ya Mitihani hiyo kupita, wanafunzi wenzangu walikuwa wakinionea huruma kuwa Mitihani Miwili ingenigharimu kwenye Points( to this day I don't know how they work out their points hihihi HISABATI).
Halafu nimeruka habari ya Mgomo wa Walimu Kidato cha Tatu, aah next week basi. Walimu pekee ambao hawakugoma  Shuleni kwetu walikuwa wa Kiswahili, English na Biology.


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Thursday, 5 November 2015

Kuzuia Mimba au Kupoteza Hamu?

Habari ya sasa!

Utasema hee Dinah mbona umeshupalia Topic hizi? Well....ninachoandika hakitobadilisha Maisha ya watu na kuwa Bora zaidi ya yalivyo sasa, lakini naweza kusaidia mtu mmoja kuelewa kwa kiasi kidogo....yule ambae ame-google "kupoteza hamu" kwa mwanamke si eti!
Kuna ulalamishi kuwa Dawa za kuzia Mimba(pamoja na matatizo mengine kwa baadhi) husababisha Mwanamke kupoteza hali ya kutaka/tamani Ngono. Hakuma chunguzi ambayo ina-support hili ila Wanawake wengi hulalamikia kuwa Hamu hupungua au hutoweka kabisa mara tu baada ya kuanza kutumia Njia za kuzuia mimba Zenye Homono(hata zisizo na Homono huingilia "hamu" ya mwanamke").

Do I look like I am busy?Ukweli ni kwamba kama hali ya kutaka  Ngono ilikuwa juu au chini basi haitobadilika......isipokuwa utaratibu wa Mwili wako ndio utabadilika na hivyo wewe Mkimama kulazimika kuanza kujifunza upya(wengi huwa hawalijui hili) namna mwili wako unafanya kazi. Tena sio Dawa za kuzuia mimba tu ndio zinasababisha hili, bali pia kuwa Mama(Kuzaa kunabadilisha Mwili na Akili).
Unapoongeza Homono ambazo zinaenda kuingilia utaratibu wa Mayai yako ili usishike Mimba ni wazi ile siku ya Kipevuka hutojisikia Nyege sana kama ilivyokuwa awali kabla hujaanza kutumia Dawa za kuzuia Mimba. Nia na madhumuni ya Dawa  hizo ni kuzuia Uwezekano wako wa kushika Mimba.
Hivyo Yai linapokuwa "tayari" Dawa za kuzuia Mimba (aina ya Homono) ndio hufanya kazi ya ziada kuzuia na hivyo kukamata (shika/teketeza) zile "sex homono" ambazo hujitokeza kipindi hiki na hivyo kukufanya utake Ngono na kutoa Ute laini ili Mbegu zisafiri kwa "amani" na hivyo kushika Mimba.(Dhumuni la Ngono ni Mimba/Kuzaliana siunajua?)


Nimekuchanganya? Tuna Homono zaidi ya Moja lakini sasa kwa vile Mie sio Msayansi siwezi kuelezea Kisayansi na hivyo nimejaribu kuelezea kibinaadamu vile ninavyoelewa mimi ili nisikuache.Nitajirudishiaje "Hamu" sasa?

Unahitaji uelewa na Ushirikiano wa Mumeo/Mpenzi wako(rejea topic Umuhimu wa Furaha ya Mke) pia tambua Mabadiliko na kurekebisha mambo kiakili(jifunze upya kona zako za Utamu/raha) na kimwili(kula kiafya, fanya mazoezi, jipende)....umewahi kujiremba (paka vipodozi) na ukafikia kwenye kupaka Lipstic/Lipgloss ukahisi hamu ya Kuneng'enuka(au ni mie tu? Najitamani hihihihihihi).

Anyway kabla hujakimbilia kukubali kuwa umepoteza Hamu, jaribu kubadilisha utaratibu wa maisha yako ya kila siku (kama nilivyogusia hapo juu) na kufanya jambo ambalo unaamini na kujua kuwa unalipenda na unalifurahia. Unapofurahia siku yako na kupata muda wako peke yako kama "mwanamke" hata kama ni Nusu hakika siku yako itakuwa Njema sana na akili yako itatulia na hivyo kupata muda wa kufikiria mambo ya kufanya na Mumeo kama wapenzi. Unapokuwa na huzuni au hasira/mawazo/hofu siku itakuwa mbaya na hakika hutotaka/tamani kufanya Mapenzi au kuwa karibu na Asali wa Moyo wako.
Kama siku imekuwa na Mishughuliko mingi  kama Mama basi jaribu kutulia na kufanya yanayohitajika kufanyika.....kamwe usijipe presha ya kuwahi kumaliza ili kupata muda wako na hivyo kumfurahisha Mumeo....kumbuka Wewe kwanza, watoto halafu ndio Baba yao. Usiwafuate wale Mume wangu kwanza, Kids halafu ndio wao...(hawajui Thamani yao).
Ukipata muda(watoto wakilala), jipatie Dakika chache za kucheza na mwili wako ili ujue wapi panafanya nini na wapi hapako kama enzi kabla hujazaa. Mfano mie.....mmh itakuwa Too much Info....achana na hili.
Ukishajijua inakuwa rahisi kumuongoza Mpenzio/Mumeo na hivyo yeye kuachana na ile Kanuni ya "paji, midomo...shingo....matiti...kiuno...nyuma yabmagoti...ingia kati".Baada ya Kuzaa mwili wa mwanamke hubadilika na kilichokuwa kinamhemesha enzi.....sasa kinaweza m-put off.Na ninyi wanawake mnaoshupaa kuwasukumia Wanawake  wenzenu Mpira wa "Wanawake ni kosa letu"....."Wanawake tunajitakia wenyewe"...."Wanawake hatujitumi". Mnapaswa kujifunza namna mwili wa Mwanamke unafanya kazi na wakati unajifunza tambua kuwa Wanawake tunatofautiana na hivyo mabadiliko unayokabiliana nayo wewe mwingine hana. Tuanze kujiheshimu na kutumia Muda zaidi ili kujijua badala ya kulaumiana hasa linapokuja suala la Ngono na Mahusiano baada ya Kuzaa.
Mwanamke  haitaji Mwanaume kufika Kileleni(kama anaujua mwili wake), lakini ili afike Kileleni akiwa na Mwanaume.....atahitaji Mapenzi na ushirikiano  wa Mwanaume  kimwili na kiakili. The moment mwanamke ana mawazo(akili haijatulia) hakutakuwa na Kilele wala kutaka/kufurahia Tendo.Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.


Babai.

Tuesday, 3 November 2015

Umuhimu wa Furaha ya Mke....


....wengi huchukulia suala hili juu juu tu, labda hushindwa kuelewa kwasababu Jamii (ikiongozwa na wanawake wenyewe) huwa  hailizungumzii sana kama wazungumziavyo Furaha ya Mume. Furaha ni hitaji la wote lakini nadhani kwa mwanamke ni muhimu zaidi kwasababu bila furaha kwake ni wazi watoto  na baba mtu hatokuwa na furaha.
Pia furaha kwa mwanamke inahusika sana kwenye masuala ya kufanya mapenzi.....kama mwanamke hana furaha ni ama hakutakuwa na Tendo au Tendo halitokuwa la kufurahia na badala yake litakuwa ni la kumaliza haja tu kwa Mwanaume(maliza nilale arrg hihihihi).
Wanaume wachache ambao wameshuhudia baba zao wakihakikisha Mama zao wanafuraha mara zote iwezekenavyo, hujitahidi na kuwa hivyo au zaidi kwa wake zao. Hawa hujua namna ya kujali  na kuheshimu hisia za mwanamke.Kwabahati mbaya sehemu kubwa ya Wanaume wamelelewa kwenye Mazingira ya kumuona Mama  ni mtu mmoja mvumilivu, mpole na muelevu.....wakati Baba Mkali na Bingwa wa kudharau. Kwamba Mama anapochoshwa na labda maudhi ya Baba na hivyo kuweka hisia zake wazi kwa "ukali".....baba hupata hasira kwanini "mwanamke" amwambie nini cha kufanya....yeye mwanaume na hivyo kuamua kukaa kimya(kumdharau Mkewe) ili yaishe.Kwasababu najua akimjibu mkewe ni wazi Ugomvi utakuwa Mkubwa kwa maana Baba hato-back down na huenda akaishia Kumpiga Mama....ili kuepusha hilo Baba anajifanya anamsikiliza Mkewe(mama) lakini ukweli ni kuwa hakuna kinachoingia akilini na hakuna atakachofanyia kazi.Sasa kwa Kijana aliekulia kwenye Mazingira kama hayo(kama nilivyogusia hapo juu) inakuwa ngumu kujua umuhimu wa furaha ya Mmwanamke kwenye Uhusiano wao. Furaha ya "mke" itakuwa na maana nyingine kabisa ambayo mimi na wewe(wanawake kama wanawake tunavyoifahamu).Kwasisi Wanawake baadhi hukua kwenye Mzingira kama hayo pia lakini tofauti ni kuwa pembeni huwa tunafunzwa namna  Mwanamke anapaswa kuwa "treated" na namna gani Mwanaume anapaswa kuwa "treated". Wanaotoa mafunzo huwa ni Watu wazima ambao tayari wamepita kwenye maisha hayo na husisitiza kuwa Waume zao  hakuwa hivyo lakini hawakuwa  na jinsi kutokana na Jamii ilivyokuwa (kipindi hicho cha nyuma)alipaswa kuolewa kwa wakati ule ambapo aliolewa(hakuwa na option).
Sasa kutokana na kukosa Option, inakuwa kama vile wanajutia na hawataki sisi Wanawake wasasa(tunaofundwa) kuishi maisha walioishi wao.....kudharauliwa, kutosikilizwa, furaha zao kutotiliwa maanani n.k.Je utamfurahishaje Mwanamke(Mke)?
Inategemea na Mwanamke husika lakini kuna yale ya Jumla ambayo kila mwanamke anahitaji ili kuwa na furaha na hivyo kuwa na Ndoa/Uhusiano mzuri:-


-Msikilize(najua tunaongea sana) lakini ni muhimu kuonyesha unamsikiliza na kumuelewa.

-Mshukuru(sio kwa kufanya Mapenzi) bali kwa lolote ambalo anakufanyia nje ya Kitanda, hata kama ni kidogo kama kukuletea Chai au kukutoa tongotongo.-Muulize kabla ya kumkosoa(wewe sio Baba yake, hajifunzi kutoka kwako) hivyo ni vema kujua kwanini jambo limefanyika badala ya kukimbilia kumkosoa.-Zika habari za Ex.....hakikisha huleti habari ambazo unajua zitasumbua akili yake(wale Funs wa kuzungumzia past lives zao kila Mgeni anapowatembelea au kila mnapokutana na watu wapya). Wote mna Past, kwanini udhani yako ni muhimu sana kujulikana kwa kila mtu?!!


-Hakikisha unajua tofauti kati ya Wajibu na Mapenzi, yupo na wewe kwasababu anakupenda......kukupenda sio Wajibu.

-Msaidie kwenye Malezi ya watoto(kama mmejaaliwa kuwa  nao), watoto wenu ni Wajibu wenu kama Baba na Mama, sio Wajibu wa Mama pekee.


-Mnunulie Zawadi once in a while hata kama ana kazi na mshahara Mkubwa kuliko wako.


Hey! Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.