Skip to main content

Huge Microphones na yupo youtube...Kero zangu.

...ndio mnaita podcasts?  wameharibu youtube eti, au nimezeeka niachane nayo kama nilivyoiacha twita? Anyways, hujambo? Unaendeleaje na u-pre-menopause?



Kama binadamu hakika kuna vitu vinakukera, binafsi nakwerwa na sehemu kubwa ya jamii ya online, hasa mamilionea na wamarekani weusi wanaoijua Afrika na kacha zake zote (nchi 57?) baada ya kwenda Ghana kwa wiki moja wa youtube na mi-microphone yao makubwa ka' wapo Mawingu FM. Halafu usinikumbushe wale wanajipanga kwenye vibox(zoom meetings) wanaanza kubishana oh my days.,,,ukute ni wivu wangu tu, maana  wanangu wakienda shule na Baba yako Kazini nabaki hapa sina hili wala lile.



Ukiachana na hao kuna wale young single men and women wanashauri/fundisha wenzao namna ya kuishi maisha ya ndoa(Well I did that when I was younger but kama unakumbuka nilishauri kuhusu mahusino na ngono nilikuwa in one na was doing it). Najua unatambua kua sio tu Ndoa ni tofauti na maisha ya ndoa, pia Ndoa sio mahusiano japokuwa mahusiano ni sehemu ya ndoa. NO? Sawa bana. By the path Dinahicious imerudi hewani jana.






Baada ya hao, kuna wale Wabaguzi ambao ni weusi, sikuwahi kuamini kuwa watu weusi ni wabaguzi na hawezi kuwa wababguzi kwasababu hawamiliki Uchumi kama Bazungu, mapaka nilipoanza kuwafuatailia Black american, kabla hawajawa ADOS na baadae AFB(confused na identifications).....tangu awali nilijua Wamarekani weusi hawatupendi Waafrika, ila aisee, jamaa wabaguzi Mzungu haoni ndani, na hakuna mtu anawashughulikia kwa kuogopa kuitwa mbaguzi.



Halafu hehehehehee kuna Malaya na wauza ngono wa kike na kiume na ma-microphone yao makubwa wanafunza wanaume namna ya kupata wanawake/wanaume. Tubaki hapa, kuna wale wazee kama mimi hapa wameoa/olewa miaka ya 90s au early 200s huko(na ndio ilikuwa mara ya mwisho ku-date) leo hii wanafunza madogo on how to date? Maam/Sir, last time you dated was 1994....labda mtusimulie(historia hahahaha) jinsi mlivyokabiliana na maisha ya mapenzi/mahusiano bila internet/simu za viganjani!!



Pia wale wanaochukua kazi za wenzao na ku-react, yaani hakuna ubunifu (own/original thoughts) zaidi ya kukosoa/kukubaliana na kazi za wenzao, kutumia kazi ya mtu kama ushahidi au reference ya unachokizungumzia sio mbaya ila kuna mipaka. Kama ilivyokuwa twita kabla ya Musk(sijui ilivyo sasa), kwamba mtu anakuja na twiti yake halafu jamii nzima inaitumia hiyo twiti kama topic na kujifunza kwa ujumla. sio kila ukiingia twita/youtube kazi yako ku-quote na kujibu,,,,,huna original thoughts.


Kero yangu ya mwisho kabisa ni Mabilionea wanaofunza wenzao "how to" kwa kuwauzia e-books, kuwalazimisha wanunue sponsor's products au kujiunga kwenye Petrion au/na kuwa members kwenye channels zao kwa malipo. 

Je una-share kero zangu au unazo zako tofauti? ongezea basi tucheke kwa pamoja.
Takuona wiki ijayo, bai baiii.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao