Skip to main content

Kutoa ushauri wa Mapenzi, Ngono na Ndoa...Elimu, Uzoefu na Mazingira vinatosha?

 

Za leo?

Muibuko wa Podcast za wakaka na dada wajuzi wa maisha ya Ndoa zimekuwa nyingi na karibu wote (kutokana na uchunguzi nilioufanya) hawajawahi kuishi Maisha ya ndoa, lakini wanashauri wenzao(hasa wanawake) namna ya kuishi na Mume. Bila kutilia maanani kywa kuna tofauti kubwa sana kati ya kuishi na mpenzi na kuishi na mke/Mume.

 

Binafsi sidhani kuwa unahitaji Elimu….kwasababu matatizo hayo hayafanani  kwa ukaribu na hakuna dalili zinazofanana kama vile Magonjwa, matatizo ya kimaisha, afya ya akili. Mapenzi na ndoa yameegemea zaidi kwenye aina ya wahusika(muonekano/kipato), malezi, mazingira na jinsi  mhusika alivyo umbwa/zaliwa(japokuwa tunazaliwa na ubongo mtupu)…tuegemee kwenye Malezi na mazingira, maana suala la kipato na muonekano ni la majaaliwa.


Pamoja na kusema hivyo Elimu kuhusu Tabia za binadamu na jinsi ubongo unavyofanya kazi inaweza ikasaidia Zaidi, ila kumbuka Ubongo ni complex na “chemical” zake zinaweza kutofautiana  kutoka kwa mtu na mtu na kutoa matokeo tofauti kulingana na tabia(mazao ya malezi) na Uzoefu(mazao ya mazingira) ya mhusika.

 

 Enzi za miaka ya 80(kabla hujanijaji kuwa nimezeeka which I am ila enzi  hizo nilikuwa mtoto) wazee walitumika kama watoa ushauri kwasababu ya uzoefu wao wa Maisha japokuwa maelekezo yao mengi yalifanana na kumkandamzia mwanamke Zaidi. Hawakujali au walikuwa hawajui kuwa kila binadamu ni tofauti sio tu kimalezi bali pia kimazingira.

 

 Nimeanza kutoa ushauri kwa watu nikiwa a teen(miaka ya 90)  tena bila uzoefu wa ngono wala Maisha ya kimapenzi na bila internet. Nakumbuka siku moja kuna Dada alinijia na kuniuliza kuwa “hivi mwanaume akikuingilia halafu akagundua upo hedhini, akasinyaa…inamaana hakupendi”...nikamwambia, Hapana huenda damu ilikuwa nyingi ukeni hivyo akashindwa sababu ya kinyaa(kumbuka kibongo bongo damu ya hedhi inachukuliwa kama uchafu).

 

 Kama Binti wa kwanza kwenye familia, nilipata bahati ya kupewa mafunzo ya ziada nje ya shule(kuniandaa kwa ajili ya Maisha ya Ndoa) na hivyo nilijuwa mambo mengi kuhusu mapenzi, ndoa na ngono kabla sijashiriki kwasababu ya ulazima wa kupewa Elimu ya awali(kufundwa)iliyotolewa na watu ambao walikua kwenye mazingira ya “kizamani” miaka ya 1900s kabla ya 1950s si unajua enzi hizo wanawake walikuwa hawapaswi kusoma….so ukibalehe tu, unaolewa.

 

 Nilipoanza kazi kwenye Kampuni ya Media, niligundua kuwa washauri wengi kuhusu mapenzi kwenye magazeti walikuwa wanaume wakitumia majina ya kike ili kufikisha ujumbe kuhusu uzoefu wa mwanake. Nilishangaa, nikacheka na kikakasirika. Hasira na Mshangao ule ndio ukazaa Dinahicious Blog, nikiwa tayari nina uzoefu na Muda.

 

 



Pamoja na kusema hayo, sidhani kama ni sahihi kushauri mtu kuhusu Maisha ya ndoa kama hujawahi kuishi kwenye Ndoa. Ndoa ni mtindo wa Maisha (ndio mnaita life style?) ambao umekubaliwa na ninyi wawili, Mungu na Serikali. Makubaliano hayo yana sheria na miiko yake ili kuboresha Maisha ya ndoa(basic na kila mtu anatakiwa kujua na kufuata) na kujenga familia. Vile vile kuna sheria, makubaliano na mipaka wanandoa wanajiwekea na kukubaliana wenyewe ili  kuboresha amani na kufurahia ndoa yao kulingana na uzoefu wa makosa waliopitia wakiwa ndoani humo.

 

 Nimeongea mengi yasiyo na maana eti? ni matumaini yangu kuwa sijakuchanganya, nia yangu ni kutaka utambue kuwa kutoa ushuri mzuri sio lazima kusomea japokuwa uzoefu utasaidia zaidi kuaminika na hivyo watu kuchukua mawili-matatu na kuyatumia na kuacha 280 yasiyowafaa.

 

 Mwisho kabisa napenda ukumbuke kuwa makini na unayosikiliza na kusoma mitandaoni, baadhi ya watoa ushauri wanataka ufanye kama walivyofanya wao ili ukosee wafurahi au kama vile wangependa ufanye hayo kwasababu wangependa wenza wao wafanye hivyo huko mbele…hivyo hakikisha unaangalia ni nani hasa anatoa Ushauri….jiulize je anatoa ushauri huu kwasababu aliumizwa?

Je, ni kwasababu Mama na baba yake walikuwa na Ndoa mbovu?

Je, anachukia wanawake kwasababu Mama yake hakuwa mwema?

Je, anaongea yote hayo ili kupata “shock value” na hivyo kupata “click”, “views” nyingi na kuongeza kipato(asilimia 99% wanasaka kipato)?

 

Nikutakie siku njema.

Baibaiiii.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao