Skip to main content

Mind your Ughaibuni business...

 Nakumbuka miaka michache nyuma nilipokuwa Twita alijitokeza Binti mmoja nakuanza kuwaambia watu wa Ughaibuni(Nchi za Ulaya na Marekani) kuachana na Siasa za Tanzania na kufurahia maisha yako "mazuri" popote walipo Ulaya(popote nje ya Afrika)....natabua kua sio kila mtu Ulaya ana maisha mazuri(inategemea sababu yako ya kuishi huko) lakini nakubaliana nae.


Wabongo wengi walimkandya/ponda kwa kudai kuwa anataka attention ya Bongo Twita sababu hakuna mtu anamfahamu, binti alijitetea na kusimamia alichokisema ambacho hakika nakubaliana nae. Watu wa Ughaibuni ambao hawaishi Tanzania  wanaguswa na Mabadiliko ya kisisa yanayoendelea Tz, hawa ni wachache sana ambao wana Biashara na pengine kumiliki ardhi(nyumba, mshamba n,k,) na wachache ambao hurudi nyumbani mara kwa mara, wengine wapo wapo tu na ndio huwa na kelele zaidi kuhusu Tanzania na Siasa zake. Unadhi utabadilisha nini  Tz na Kodi hulipi? Mind your Ughaibuni business and enjoy your High tax, cost of living and free Heathcare while it last.



Ukiachana na suala la Siasa, kula suala la ndugu tegemezi(wavivu), yaani kwa vile tu wewe upo Ulaya basi unabeba zigo la kusaidia kila mtu kwenye Ukoo, kama wewe sio Narcsist hili zigo haliwezi kukupa furaha wala amani na ku-feed ego yako ya kuwa wewe ndio Tajiri wa familia. Unadhohofika na kukonda /nenepa na kupata maradhi kwa kufanya kazi Masaa mengi zaidi kuliko inavyoruhusiwa kwa usalama wa afya yako, ili tu ukamalizie Bonge la jumba Tz, usomeshe watoto wa kaka zako na wa bibamu na dada zako na vimada wao....ukiulizwa kwanini unajitesa kwa ajili ya familia nyingine wakati una mke na watoto, unasema ni "Utamaduni wenu wa Kitanzania na Damu haipotei bure". Kama ndio hivyo basi mie sio Mtanzania kwakweli.


Ukirudi home(tz) ndugu zako wanag'aa kuliko wewe utadhani wao ndio wametoka Ulaya, unashangaa nini wakati wewe ni Serikali yao na damu(undugu) wenu ndio mchango wao mkuu wa mapato ili uwape Huduma nzuri za Afya, Elimu na Miundo mbinu(gari, makazi).


Kukitokea tatizo huko kwenu kama wewe sio wa kwanza kutoa mchango na kuwapa maelekezo ya nini wanapaswa kufanya basi uta kuwa pekee ulietoa Sehemu kubwa ya mchango, ukishangaa, shangaa unapigwa vibomu na kila mtu kwa wakati wake kwa suala/tatizo hilo hilo moja(wanakuchuna)...huezi kujua hili na hawatokuambia ukweli.


Upo Ulaya lakini unaishi kwenye jamii ya Maskini wa Kizungu, sasa kwa vile ni wazungu unajiona upo safi wakati Elimu yako na background yako na kiwango cha maisha kabla hujaenda Ulaya ni u-Surbabian.


Ungeweza kabisa kuishi hivyo(ki-surbabian) na kufurahisha Mkeo na watoto wenu kama ungedharau Ego yako na kujiweka mstari wa mbele kutaka kutatua matatizo ya kila mmoja anaekujia na shida zake na wakati huo huo kuwekeza kwenye ardhi ambayo unajua kabisa haitokuwa na faida kwako wala wanao isipokuwa Ndugu zako ambao zaidi ya kuchangia damu, hawana umuhimu kama wanao unaoishi nao Ughaibuni.


Sisemi usiwajali ndugu zako isipokuwa nakukumbusha kuwa ndugu hao wanafamilia zao walizozianzisha wao na nijukumu lao kubeba mahitaji yote muhimu. Ikitokea wanahitaji msaada once in while, sio mbaya kusaidia lakini kujiweka mbele  kama vile wewe ni Serikali, sio nzuri kwa afya yako ya akili, sio haki kwako kwa mkeo na kwa watoto wenu. Kumbuka ukiugua na hata ukijifia mapema kwasababu ya kuji-over work kwasababu ya Ndugu Tz...Mkeo na watoto ndio watakaohangaika. Piga kazi kwa kiwango cha kutosha bila kuathiri afya na ku-provide kwa ajili ya familia yako uliyoianzisha aka Legacy yako na acha kila mtu abebe  familia (Msalaba) yake.


Hao ndugu unaowasaidia ndio huwa wanaweka kikao na kukujadili, jamaa kamaa Miaka 30 Ulaya lakini hana hata tofali la choo, Kiwanja. Wanasahau kuwa kipato chote kinaishia kwao na familia zao. Kuna faida gani ya kupata sifa na kuzikwa na watu wengi kwasababu ya wema wako lakini unaacha Legacy yako inataabika Duniani? Toa msaada inapohitajika na umeguswa, kisha mind your Ughaibuni business.


Nitakuona baade...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao