Friday, 29 August 2014

Ijumaa moja Baada ya Mauaji ya MwembeChai!

Maisha haya!

Nimekumbuka 1996/97 Mauaji ya Mwembe Chai (siku mbuki vema na sitaki ku-google vilevile)!

Siku chache baada ya Mauaji yale bado kulikuwa na Maandamano ya Siri ya "Waislamu wenye Hasira".....Kile kifo cha yule Kijana pale Mwembe chai akianguka LIVE baada ya kupigwa Risasi na Polisi (FFU sijui) akiwa amevaa shati la Bluu Mpauko(light Blue) kamwe haitonitoka Kichwani! Ni kifo cha kwanza nilishuhudia live(on Tv)!!


Sasa bila kujua si tukaenda Kariakoo siku ya Ijumaa! Ile tumemaliza manunuzi si tukakutana na Waandamanaji na FFU...wakayaachia Mabomu ya "Machozi"....oh boy! Nilihisi Vita kuu ya Mwisho wa Dunia ambayo sina Uzoefu nayo ndio imefika!!!


Kimbia, huku na kule mara Tukakutana na jamaa (sijui Katibu au Mlinzi, ila alikuwa Mhindi) Wa SSC pale Msimbazi, akatufungulia Mlango kwenye Jengo la Simba....akawa anaita akina Mama na Watoto waende kupata Huduma ya kwanza....hihihihi kunawishwa Maji Usoni(wasn't a laughing matter then)!

Anyway! Baada ya hapo kukatulia, tukatolewa nje ya Jengo la SSC kwenda kupata Usafiri....kwenye Daladala! Tulikuwa tumepanda na baadhi ya Waandamanaji!

Akamuuliza Mzee mmoja na Kanzu yake...."Baba na wewe ulienda K'koo kuandamana".....Mzee akajibu "ndio mwanangu, tunapigania haki yetu"....Mdogo wangu akaulia "una watoto"...yule mzee akasema Sita na wote wapo Sekondari.

Mdogo wangu si akaanza Risala sasa? "Wee Mzee mzima badala ya kuhangaikia maisha ya wanao na kuboresha maisha yako, unaenda kupoteza muda kuandamana. Sasa kwa bahati mbaya umepigwa Risasi umekufa au Bomu umekatika Miguu nani atatimiza mahitaji ya wanao?"

Akaendelea "Wazee wengine hamfikirii, mnakuwa wabinafsi sana na Dini zenu, Pigania haki ya kupata vifaa Mashuleni, sio Dini"

Mie hapo nywiii(kimya) bado natetemeka huku nafikiria Mabomu ya Machozi yataniathiri vipi huko mbele, sikuwa na sauti wala nguvu....ujue mie ni Muoga mnoooooo linapokuja suala ya kuingiza mahewa, madawa, sumu mwilini mwangu!!

Ah! Mauaji yanayosababishwa na Dini hunisikitisha sana.


Mungu amrehemu yule Kaka alieuwawa pale Mwembe chai.

Heri ya Mwanzo wa Mwisho wa Wiki.

Bai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 26 August 2014

Kujikanganya nako!

Kuna siku nilisikilizishwa Nyimbo za Bi Rozi Mhando akizungumzia "Kunyang'anywa" Mali zao na Wageni..."Wao kuwa Wageni Nchini mwao".
Aliendelea na kuimba kuhusu kuchukua na Kunyang'anya vilivyo vyao kwa Jina la Yesu!.....Nkajiuliza Kunyang'anya(kutumia nguvu) si ni Dhambi?!!

Halafu nikakumbuka Ubunge ni Career Path kwa watu Mashuhuri ila issue nzima inayonifanya niandike hapa ni ile ya kuji-contradict!!

Isitoshe kuwa Mlokole kwa Miaka zaidi ya 20 lazma utarudi nyuma (utachoka) kumsubiri Yetu (hihihihi my ribs... Wapendwa na Watumishi habari gani?) na hivyo kuhama Kanisa, Kuanzisha Kanisa Lako au kujiingiza kwenye mambo mengine ambayo ni tofauti na Misimamo yako.

Si walokole tu wanaoji-contradict kwa kukataa "Mikorosho" lakini wakati huohuo Kumuita Yesu ni Mume wa Wajane (Wajane sio Wanawake tu kama ulikuwa hujui, kuna Wajane wanaume) kwa mfano tu!!

Kujikanganya ni kitu cha kawaida ailimradi sio kwa wakati mmoja na kumbuka kuepuka unapobishana na Mumeo/Mkeo au kwenye utetezi wako Mahakamini (siku ukishtakiwa)....!

Mwanadamu unapitia maisha tofauti na ni vema kujaribu kubadili Maisha yako au misimamo yako(ikibidi) ili uweze kufanikisha Lengo fulani ambalo ni muhimu kwako na pengine familia yako au Career si eti!

Mimi mwenyewe najikanganyaga hapa kama ifuatavyo.....unaikumbuka ile Post kuhusu SAHM (Stay At Home Mum) aka Mama wa nyumbani! Unadhani miaka 6 iliyopita ungeniambia siku moja nitakuwa Mama wa nyumbani ningekuelewa?!! Lazma tungepigana.

Ni kazi ngumu sana tu lakini inanifanya nifurahi Moyoni kuwa wanangu hawapo mikononi mwa mtu/watu wengine bali mimi mama yao ninaejua Uchungu wa kuwasukuma nje ya Mwili wangu!
Kwanini nawaita W****ge "Mikorosho"? Errr is it kwasababu Korosho imepinda au kwasababu Mikorosho inapadwa....chagua utakalo na ufaje kuwa Jawabu.Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 25 August 2014

Kizazi cha Santuri, Kaseti CD Vs MP3...

Nimekatiza mahali mtaa wa ki-Posh nikakutana na "Bei Nanini CafE" haraka haraka akilini ikaja "Price and what's not"....not exactly what they meant ni mimi tu na Utamu wa Kiswahili.....liwache hili!

Unakumbuka enzi zako ulipokuwa unakuwa miaka ya 92+ hapo ndio Tv zinaanza kuchanganya(sio Vituo) bali watu kumiliki Tv(wageni wa Jioni wakapungua nyumbani kwetu).
Kila ulichokuwa ukifanya Mzazi wako anakukatalia akisema "enzi zetu tulikuwa hivi na vile....sio nyie watoto wa siku hizi"!

Halafu unatamani kumuambia "sasa Mama enzi zako si zimeisha, hizi zetu" lakini huwezi, unaishia kununa.

Nakumbuka Baba(Marehemu) alikuwa anasema "hivi huko Madukani hakuna nguo za wakubwa, zote ni za watoto tu?" Akimaanisha zinabana au fupi!....tukamwambia "Baba hii ndio mitindo ya kileo".....alisema "vaeni mtakavyo lakini mkija Ofinisi kwangu sitaki kuona chupi ndefu" (Suruali za Kubana).

Je! Huoni kuwa na wewe umekuwa kama wazazi wako? Kutwa kufananisha enzi zako na enzi hizi....Lione vile!(Hihihihi).


Akyanani vile mie nimekuwa ka' wao....ila tofauti yangu najikumbusha mwenyewe kuwa ule ulikuwa wakati wangu na huu ni wakati wao.

Wali kizazi cha Santuri, Mie Kizazi cha Kaseti, wao Kizazi cha Mp3 wapi na wapi?!!!!.....Dinah funga Domo lako muda wako wa Kaseti?!! Kaseti kweli si nimezikuta mie! Nadhani mie ni Kizazi cha CD....(Nimesahau jinsi ya kumalizia hapo).

My 3yr boy aniambia "mummy you are useless on games, let me show you how to play"....hiki kizazi cha Code ni balaa asavali cha Mp3!!!Cheers!
Mapendo tele kwako...

Friday, 22 August 2014

Kizazi cha Miaka ya 90!

Na haraka zao!! Yaani wapo mbio-mbio tu japo mbio zao zinatofautiana.....kuna wale wa starehe(Now) na wa maisha yajayo(Future)!!

Mdogo wangu wa Mwisho anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Nilipopata habari za yeye Kuposwa nilipata hasira za ajabu!

Nikabaki nalalamika "yaani mdogo wangu mdogo hivi anaolewa"...."Vipi huyo mwanaume akienda kumtesa"? "Kwanini asisubiri kidogo jamani akue (huku nalia) bado mdogoooooooo" she's 23yrs!

Mama akaniuliza(Simuni), ningekupa taarifa kuwa anamimba au kazaa ugelia kiasi gani?!! Kabla sijajibu!! Asali wa Moyo nae akauliza swali hilo hilo(live).....nikasema but she's my little sister....can she just wait another 2yrs?!!!

Anyway, ilinichukua mwezi Mzima kukubali kuwa my baby little sister-o anaenda kuolewa!!


Sasa leo naongea nae, ananiambia "nipo site dada" Nkauliza Site ya maandalizi ya Ndoa? Akanijibu "Hapana Da Dinah, tunajenga"!!

Nkajisemea D'oh! Watoto wa 90s wanakua haraka Kiakili kuliko akina sisi the "tumuachie Mungu one day Yes"....the shenzi!!!
Tena afadhali sisi the Shenzi, kuna kile Kizazi cha 1951-1973 Oviooo yaani the Bongolala kabisa!!

Usijumuishe maelezo yangu ukapata Kiburi au ukapata hasira, sio watoto wote wa 90s wanakua haraka kiakili, inategemea na Mtu, Mazingira, Malezi n.k.Nikuache kwa sasa!
Mapendo tele kwako...

Thursday, 21 August 2014

Nimeachwa na Teknolojia...

Ah! Nimebanwa kweli siku mbili hizi....ila nafurahi kuwa nimepata muda wa kuongea na wewe kabla sijaenda kulala.....mmh! Tangu nimekuwa Mama wala hakuna kulala ni kujilaza tu.

Kuna tuwimbo tuwili twa Ali Kiba tunanikuna kweli yaani "Mwana Daslama" na "Kimaso" ingekuwa zile Kanda za enzi ninge-rewind kwa Penseli mpaka Kanda ikatike....ujue kuna Wasanii wa Bongo Flava halafu kuna Ali Kiba(I just love that Kid). Achana na hili.

Jana nikaenda Dukani kuangalia Simu....Teknolojia imenishinda au niseme tu imenipita!

Simu yangu ya mwisho ilikuwa (usicheke) Blackberry Bold 9900, ikatumbukia chooni (umama siku za mwanzo uliniCost!!!).

Siku naenda mtembeza mwanangu City center kwa mara ya kwanza si nilipanda Treni heheheheheeeeeeee mwanamke nashuka na "Pram" lenye Mwanangu obviously!!....nikaacha Hand bag kwenye Treni(walinirudishia though)!

Turudi kwenye Teknolojia ya Simu, wala siamini kama nimekaa Miaka 3 bila Simu Mpya....nilikuwa nabadilisha simu kulingana na Toleo jipya la Teknolojia kwa mwaka huo.

Baada ya kujiona "mshamba" wa Technolojia nimeamua niingojee hiyo Sa-Msang'i inayosemekana ni bora kuliko iSimu6.Nikuache kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 19 August 2014

Mtu chake...

Kwa kawaida mimi sina tabia ya kuangalia watu ninapokuwa natembea na hata kama nimekaa mahali nitakuangalia kama nimependa ulichovaa....na kuangalia kwenyewe ni kwa Sekunde chache tu.


Kuna watu wanajua kukodolea macho wenzao bila kupepesa! Yaani anakukazia macho mpaka unaona aibu kwa ajili yake!

Ukitaka ugomvi na watoto wa London wale wa Uswahilini bana wakazie Macho hivyo....anakufuata na kukuuliza "what you looking at?" huku kashikilia Kisu!

Kisu bit pale juu nimeongezea tu chumvi, ila kuna vipigo na vifo kadhaa vilitokea kutokana na mtu kumkodolea macho mwenzie.

Stori time: Sasa jana tupo mtaani tunatembea na watoto....nyie mnatoka Weekend sie twatoka J'tatu....kisa na sababu? Ili tusiwe sawa, hakuna lingine wacha kutuJAJI eeh!

Nasikia Asali wa Moyo analalamika "mijaume ya kiafrika sijui ikoje (yeye mwenye Muafrika) inamkodolea macho mke wa mtu wakati inaona kabisa yupo na Mtu wake"

Hee! Nkauliza kwani wewe umeonaje kama wananikodolea macho kama wee mwenyewe hujawakodolea?!!

Akanijibu kwa kifupi, "mtu chake"!....nkafurahi Moyoni kabla sijajiuliza maswali kadhaa kuhusiana na yeye kuwa Mwanaume wa Kiafrika!


Asali wa Moyo akampeleka Babuu kwenda kuangalia makorokocho(Toys), mie nkawa nimekaa sehemu na Kibibi(kabinti) nampatia Lishe.....Mara akaja Mkongo, akaomba direction, nkampatia kisha akasema "ningependa kukujua zaidi, nikupe namba yangu?" Nkasema akuu sina Simu mie.Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 18 August 2014

The why's!

Nilijua siku nikizaa mmoja kati ya wanangu (au wote) watakuwa waongeaji sana kama errr Mimi?!!

Well, najua kuwa napenda kuongea (labda kwa vile sinywi pombe au sina nguvu ya kupigana) lakini sio muongeaji kihiiivyo.

Nakumbuka Marehemu Baba alikuwa anawaambia watu "aah kuwa makini, binti yangu huyu anamaneno sana".

Kiukweli kabisa na admit mimi ni Mbishi sana....nope! wala sina asili na watu wa Kibondo, Kigoma! Labda kwa vile sina Nguvu za kupigana lakini wakati huohuo sipendi kuonewa, sipendi kudanganywa na siamni katika "kubali yaishe" BS na wala sio "ndio bwana"....sasa nikiwa na uhakika na ninachokisema nitakubishia mpaka kesho muda kama huu.


Turudi kwenye uongeaji ambapo ndipo Babuu(my 1st born) anapokuja sasa....Laaaa! Mwanangu anaongea jamaniiiii....akianza stori zake....halafu ana "why's" za kutosha.

Maana nilikuwa nahofia Hisabati akianza shule, sasa nina shughuli ya kujibu why's.....wakati mwingine mtu hujui hata jibu halafu huwezi kumdanganya, basi unabaki bikozi izi eh...I will google, I mean tell you when we get home!!!
Mbaya zaidi why's zake wakati mwingine ni ngumu(halafu mbele za watu)....hivi hapo ulipo bila kufikiria unaweza niambia kwanini tunapata Kwikwi (....toa jibu la Kibaiolojia kwa Kiinglishi)!

Ujue swali Why kwa Kiswahili ni gumu hivyo watoto wengi huwa waongeaji lakini huchelewa kuuliza ze "kwaniniZi"!
Mtoto anaweza kumlilia baba yake anapokwenda kazini halafu ukamwambia tu...baba kaenda kazini na atarudi jioni kesi ikaisha sio!
Huyu wangu bana lazma upate "why dad has to go to work everyday?".....na usipojibu swali litaimbwa mpaka utoe jibu lenye because....Hata sijui kwanini Asali wa Moyo anaenda kazi kila siku....eer in English that is!


Na ukitoa jibu fupi kama "dad has to work so that we can pay bills"....unapewa "why do we have to pay bills" aiiii kazi ya Ualimu nayo ni £24,000+ kwa mwaka.Nikuache kwa sasa!
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 13 August 2014

Mama wa Nyumbani...

Kwa mwaka mmoja na nusu (au tuseme miwili maana nilianza likizo ya Uzazi nikiwa na Mimba ya Miezi 5) nimekuwa Mama wa Nyumbani.


Mie kuwa Mama wa nyumbani ilikuwa choice kutokana na moja ya Misimamo yangu ya kimaisha ambayo wengi hushindwa kunielewa....kwamba miaka 3 ya mwanzo ya wanangu ni lazima niifaidi (as in kuona wanavyobadilika kila siku, kuwafunza manners n.k kabla hawajaanza shule rasmi).


Pia ile hali ya mimi kutoamini mtu mwingine kuangalia wanangu, nahisi kuwa hawatawapa huduma, upendo na attention inavyotakiwa, na wao hawataniambia kwani bado wadogo.


Hiyo ilikuja baada ya kujifungua mtoto wa Pili, yule wa kwanza bado nilikuwa na ile "lazima nirudi kazini, am financially independent working Mum" hivyo Babuu akawa Day care akiwa bado mchanga.


Back to Mama wa kunyumba! Heeeeeeee! Nawaheshimu wote, kazi yenu ni ngumu, Kuzaa is nothing compared to Mama wa Nyumbani na anashatili malipo ya juu ambayo ni zaidi ya £60,000 kwa mwaka....well sio wote bali wale ambao hawana wasaidizi (house girl/boy) na wanafanya kila kitu wao wakati Waume zao wapo Kazini.

Maana mwanamke unafanya kazi ya "domestic assistant" ambayo ni £12,000 kwa mwaka.....unafanya kazi ya Mpishi £20,0000+ kwa mwaka....unafanya kazi Dobi(laundry assistant) £15,000+ kwa mwaka.....unafanya kazi ya Nursery assistant £18,000 kwa mwaka, unafanya kazi ya Nursery Nurse 22,000+ kwa mwaka na mwisho kabisa unafanya kazi ya Muuza Ngono tena High class naa exclusive hihihihihihi nikuwekee mahesabu yake hapa?!!.


Mama wa nyumbani ni kazi ngumu kuliko kwenda Kazini (nje ya nyumbani) kila siku.....huko kazini kwako unafanya kazi ya mtu mmoja tu, Mama wa nyumbani anafanya kazi za zaidi ya watu 4 kila siku na hakuna Likizo!

Haya huyo ni Mimi Mama wa nyumbani mwenye mapenzi na Familia yangu....watoto wangu na Mume wangu, nafanya yote hayo kwa moyo mkunjufu na wenye furaha!

Vipi kuhusu wale wasaidizi ambao unawaita "mahausi gero"? Unawadharau, Unawanyanyasa kwa njia zote possible.....Unasahau au hujui thamani yao kubwa kwa wanachokifanya kwenye maisha yako na ya watoto wako kila siku!


"Am financially independent working Mum" story itakujia soon....nikikumbuka that is...hihihihi


Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 12 August 2014

Maghorofa-2

Siku nimekatiza mahali nkasikia sauti ya Kike kwa Lafudhi ya Kipemba "Bwana Dullah wee panda basi mwenzio nipo hoi".....nkajisemea eh watu na shughuli zao asubuhi-asubuhi.

Wacha mawazo machafu! Bwana Dulla alikuwa Chini ya Ghorofa akitaka Bibie amfuate kwani aogopa panda Lift-ini peke yake!

Sasa Glasgow-Scotigo kama nilivyogusia jana ni Jiji (lililozubaa) lakini linamajengo Marefu mengi kuliko Majiji mengine ndani ya UK.

Pamoja na sifa hiyo wataalam wanadai hayakujengwa vema na mbaya zaidi yana reputation mbaya ya "Komando Yoso" Vijana wakorofi na familia mbazo ni masikini(wanaotegemea Benefit).


Wananchi wakaanza kuzikimbia nyumba za Maghorofani na kukimbia maeneo ambayo kuna majengo hayo Marefu kwa kuhofia "status" zao na kuibiwa au kuuwawa.

Baada ya Muda Serikali(almashauri ya Jiji husika) wakaamua kuyabomoa yale ambayo waliona ni ghali sana kuyatengeneza na Mengine kuyagawa(kuyauza) kwa Mashirika Binafsi ya Nyumba kwa miadi kuwa watayakarabati na kufanya yavutie.


Hakika baadhi yamependeza (mie sikuwepo kabla so sijui)....kwa yale ambayo kulikuwa na Yobs(Komando Yoso) sugu, yalibomolewa na Familia zao zote kuhamishwa miji ya mbali-mbali ili kumaliza Uyoso wao.

Sasa Majengo hayo Marefu yanaanza kurudisha Hadhi yake japokuwa bado wananchi wanasita kwenda kukaa.

Jamii ya wana Architectures...wanasifia sana Mpangilio wa Majengo Marefu uliopo sasa Jijini Glasgow baada ya Baadhi kubomolewa na yaliyobaki kupewa "Cosmetic".

Baadhi ya wananchi waliokulia kwenye Majengo hayo miaka ya 50-70s wanajivunia Historia yake.Nakubaliana nao! Historia yenye vielelezo asilia na vinavyoshikika ni muhimu kwa Vizazi hata Vizazi.....na Giza likianza kuingia Skyline ya Glasgow inapendeza sana....kukicha unakutana na the Boring Glasgow hihihihihi!

Nimejifunza Mengi kuanzia u-nationality wao(wanaotaka kujitenga), Ukabila, Ubaguzi, Uvivu (eeh bana kuna wavivu kule acha)....ila la Majengo ndilo lililonivutia zaidi ndio maana nime-share na wewe.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 11 August 2014

Majengo marefu(Maghorofa)!

Kuna yale yaliyojengwa kati ya Miaka ya 40s na 70s ( I guess) Ilala, na yale pale kati ya Mnazi Mmoja na Stesheni, Posta, Kariakoo, Tandika, Keko, Upanga, Ostabei.


Halafu kuna yale ya Miaka ya 80-90 maeneo ya Tabata, Mbezi Beach.....tulia, nazungumzia Maghorofa ya NHC na ya Kampuni kubwa kama vile TTCL, PPF na kadhalika sio yake binafsi.

Ninayoyataka hapa ni yale ya 40s-70s, ambayo hayakujengwa katika mfumo mzuri wa Maji safi na Maji taka, Nyaya za umeme zimekaa kihatari-hatari na Juu ya Ghorofa ya Mwisho kuna uwazi kwa ajili ya eer "kupunga hewa" " kufurahia the view"?!!! in which kwa nchi yenye watu wenye ma-stress na ma-depression kama UK ingekuwa rahisi kujipoteza (kujirusha ili kufa).....mbona tungewa-sue NHC mpaka wangekoma.


Pamoja na hasi hizo bado majengo yale yana sifa ya kujengwa kwa kutumia Malighafi Imara ukilinganisha na Maghorofa yanayojengwa Karne hii.


Magorofa hayo yakikarabatiwa mmmh itakuwa gharama kuu na pengine kulipuliwa na yaanza kuanguka labda yapewe "cosmetic" tu....kubadili mfumo wa Maji safi na taka(choo incl) na umeme(yale manyaya bana khaaaa)!!

Majengo hayo ndio yanalifanya Jiji la Dar es Salam kupendeza na nadhani kuwa Jiji la kwanza lenye Majengo Marefu is it East Africa au Tz tu?(Hata sijui)!!....hupendeza sana mida ya Usiku (kama kuna Umeme).


Watu wanaokaa kwenye Maghorofa (Makabati hihihiihihi) hayo huwa na "status" tofauti na wale wanaokaa nyumba za Chini.....wanajidaaaaaai

Pale chini kuna Mitaro isiyorasmi inamwaga mimaji michafu na hapo pembeni kuna Mfumo wa Maji safi(what a mixture)....Karo zinafurika Vinyesi alafu watu hawana habari wala nini....full maringo! Nimekulia Maghorofani enzi zileeeeee hivyo najua ninachokizungumzia.

Kinachonisikitisha ni Maghorofa hayo kutelekezwa na ama watu Binafsi waliyoyanunua au Wamiliki kama vile NHC(kwa kisingizio wapangaji hawalipi Kodi kwa wakati).

Na pengine itafikia mahali watayabomoa na hivyo kupoteza Historia.

Kwanini nakuambia haya? Ni kutokana na uzoefu nilioupata Jijini Scotland. Kumbuka Scotigo ni wenye Majengo marefu Mengi kuliko Nchi nyingine ndani ya UK. Nitakuelezea sehemu ya pili. Very Interesting, usikose!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 7 August 2014

Reality Tv Shows....

Haiyaaaaa (Waswahili wa huku ndio wanasalimiana hivyo)....Wakishua wanasema how do yo do.....asa nani anamuda wa "hau-du-yu-du Maisha haya?!!Unakumbuka enzi Reality shoo zinaanza kulikuwa na slogan ya "Movies are boring, Reality is exciting"....well not exactly ila ili-sound hivyo bana eh!
Basi bana si Ndio akina Kadarshian* wakaanza na mimi nikiwa mmoja wa watazamaji wa mwanzo kabisa nikiamini kuwa nilichokuwa nakiona ni uhalisia wa Maisha yao....kwa miaka miwili.....mai miaka Miwili naangalia scripted "reality" Tv shoo (nalia hapa kwa aibu).
Basi bwana, nikaacha kuangalia na kuchukia Reality Tv shoo zote ikiwemo Big Brother!
Sasa nilipomimbika 2012 nilianza Likizo ya Uzazi nikiwa na Mimba ya Miezi 5.....unataka kujua kwanini? Hehehehehe aiii nilikuwa "rough" sana na kazi yangu inahitaji u-smart bana, nkaona mmh ntakosa Maternity Leave hapa, mwanamke wacha nikimbie mapemaa(natania).
2012 ndio nikaanza tena kuangalia "Real House Wives" tena marathon ili nitosheke, hee nkawa addicted (blame it on Mimba, akyanani vile halikuwa kosa langu)....nikaanza kuhisi nazidi kuwa Mjinga lakini nikashindwa kuacha mapaka nilipojifungua 2013 phewww!!Baada ya hapo nikaja gundua Mary Mary nao wana Reality Tv show, knowing wale ni Wajukuu wa Yesu nkajisemea hawawezi kukubali show yao iwe scripted(hawatokubali kucheza uongo ili kunogesha show) aiii Kitukuu cha Yesu nikaanza kuangalia.


Uzuri wa Mary-Mary ilikuwa kuimba-imba hapo wimbo wa "Go get it" ndio unazidi kunibamba....mwanamke nacheza nakuliachia tumbo langu la uzazi linarukaruka.

Mara booom! One of Mary-Mary hubby ka-cheat....sijui nini na nini...imagine hau lavi davi in jizasi nemu thei wea kwenye lishoo lao alafu sasa....mxsiii SCRIPTED!

Oh! Kijana wangu wa Miaka 3 anaimba ile wimbo ya Ali Kiba Ft Bonge la nyau "ukanifanya nilale njaa ili wewe usije kosa" mpaka nafurahi, Kiswahili kitamu.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 6 August 2014

Kupenda kusifiwa....

Ah! Kama wewe ni mzuri wa jambo fulani hakika utakuwa unajijua hivyo sio mbaya kujisifia mwenyewe.....au subiri Mpaka urudishe namba (ufariki) ndio watu wakusifie kwa Mema na hata kwa yale mabaya yako.

Mmh! Lamini ukifariki unakuwa umemaliza ya Duniani, sasa sifa za Walimwengu uliowaacha zitakusaidia nini? Kungekuwa na uhakika wa Sifa hizo kukupunguzia Madhambi uliyofanya au Ukali wa Moto siku ya Kihama, ingekuwa Poa!


Sasa, kuna Watu wameumbwa kuzitafuta Sifa kwa nguvu.....yaani mtu anatengwa, anafanyiwa maovu na mabaya yote lakini yeye yumo tu kujionyesha Mwema kwa hao Walimwengu.....wacha kujipendekeza, fanya yako....hutakiwi na huna umuhimu kwao!


Unawajua wale Jamaa wanafanyiwa mabaya, wanaharibiwa familia zao au Mradi ambao ulikuwa Tegemeo kiuchumi....Jamaa waharibifu wakirudi na kuomba Msamaha wanasamehewa na Ujamaa unarudi upya.

Mie siwezi bana, ukinitenda ama nalipiza Kisasi kwa Jamii yako Nzima au nakufuta akilini (nachukulia kuwa hau-exist) nasonga mbele.....hizi sio NYAKATI za Yesu na siamini katika "Mungu atanilipia" Bwanshee (sijui hata maana yake).


Naishi maisha mbayo hayana stress zinazosababishwa na Marafiki (ambao sina) au Jamaa (ndugu wa kuunganisha) kwasababu nimejiwekea utaratibu wa "kuengua" watu as I go....nitajaribu "kujipendekeza" mara 2....usipo-respond namie nakuwa nimemaliza!


Ukirudi baadae nitakusikiliza.....oh siku hizi nina watoto hivyo sina muda wa kusikiliza.

Nimepoteza track!.....nachojaribu kusema hapa ni kwamba usifanye mambo ukitegemea kusifiwa au kuzungumziwa vizuri kwa Watu.Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 4 August 2014

Kuwekana...

Heloooooooo there!


Mie huwa sishangai mtu akimchomekeza Jamaa yake (binamu, mtoto wa ba' mdogo).....nilishakuambia Ndugu ni wale mnaochangia Damu kwa Baba na Mama vinginevyo nyie ni jamaa tu!

Hii haina "Dinah kakaa sana Ulaya kabadilika"....tangu Mdogo mie huwa siwachukulii Jamaa kuwa Ndugu! Ndugu zangu ni wale tuliotoka Tumbo Moja au Baba na Mama Mmoja.....kama hutaki kukubali bana shauri yako!

Mambo ya kulazimisha Undugu bana ni kumaskishana (kutiana umasikini) na kuongezeana ma-stress tu.....hii ndio huwakosesha watu "bahati" ya kufanikiwa.


Bana mie ningekuwa sijui nani ni nani Serikalini halafu kuna nafasi za kazi zinapatikana unadhani nitakuajiri wewe wakati nina Mpwa wangu (Jamaa) anaelimu na ujuzi ka' wako nyumbani? Aiii nitampa nafasi yeye kwanza, akiikataa ndio wewe wa Nje utafikiriwa.


Najua sheria za kazi na kadhalika BUT Mpwa wangu sio Ndugu yangu, hatu-shei damu wala Ubini sasa undugu unatoka wapi hapo?!!!
Kuwa mkweli! Hata wewe ungefanya hivyo....kila mtu anafanya hivyo.....kama hufanyi hivyo basi wewe unaroho mbaya sana.


Nakuona hapo unataka kusema "ndio maana wenzetu Wazungu wanaendelea kwasababu hawawekani"......umeishi nao? Umewahi kufanya nao kazi Nchini mwao?


Wazungu wanawekana like nothing else, tofauti ni kama nilivyosema Binamu sio Ndugu yake.....Mtoto wa Dada yako sio Ndugu yake so hata akiwaweka kwenye "Office" hakuna anaejua "connection" ya Ujamaa.
Kumuweka Mdogo wako, Mkeo au Mwanao sasa hilo ndio Kosa!


Babai.
Mapendo tele kwako...