Tuesday, 30 June 2015

Ujidhaniavyo sivyo....

Heiyaaa.

Mara zote huwa tunaamini tupo vile ambavyo hatupo. Nitakupa mfano:-  Unapoenda kununua Foundation(matope ya kupaka Usoni kabla ya mengineyo) unachagua rangi ambayo sio yako na huwa waaaay lighter.Sio kwamba unakusudia bali hutaki kukubali ile yako ambayo pengine inaonekana ni nyeusi sana kwenye Chupa kuliko unavyoamini(kithihitisho ni Picha zako).Enzi nilikuwa na "Wifi" wa Kiarabu na kwenye familia yao kulikuwa na waliozaliwa nje ya "uarabu" kwamba mzazi mmoja alikuwa Muarabu mwingine Mweusi halafu mtoto (binti) katokea mweusiiii mwenye nywele za kiarabu.
Basi tukijikusanya tumapiga stori huyo binti alikuwa anapenda kuwasema wadada wengine kuwa ni Weusi mno kiasi kwamba hawavutii. Kwasababu mzazi wake mmoja ni Muarabu na anaishi kwenye Familia Kiarabu aliamini kuwa na yeye ni Muarabu.Hiyo pia huwatokea watoto waliochanganya na Wazungu na kuishi Uzunguni zaidi kuliko Weusini...huwa wanajidhania kuwa ni Wazungu(rangi wise).
Kingine ni uwingi wa nywele.....unajua maisha yako yote umekuwa na manywele lundo. Uwingi wa nywele hubadilika hasa baada ya kuzaa, mabadiliko ya homono na kadhalika.
Sasa kwasababu umekuwa ukijiongelea(mie)kama mtu usie na uhaba wa nywele ukweli huo hubaki kichwani na hata uhaba unapokukabili bado utaendelea kuamini kuwa wewe ni manywele person.Kuna siku nikawa nazungumzia Nyusi(ninazo za kumwaga.....well used to)....kwanini watu wanachora badala ya kujazilizia palipopungua. Kwa kujiamini(bila kujua) kabisa nikasema bora mie nina manyusi mengi..........asali wa Moyo akasema kwa upole na huruma "mbona mie sizioni hizo nyusi zako nyingi".....nikamkata jicho hilo(baadae kisirisiri nikaenda kujiangalia). Daaah! Manyusi yangu yamepururuka lini lakini? Nkajiuliza.Kipindi hicho nilikuwa nimepoteza nywele za kutosha kichwani (postnatal shedding) na sikuwa nikijiangalia kwenye kioo(nina kichanga muda nitoe wapi).Kabla hujalitoa mdomoni pata second opinion kutoka kwa mtu unaemuamini kukupa ukweli hata kama unauma. Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Monday, 29 June 2015

Magaidi wa Kiislam...


Ahsante kwa kuichagua Blog hii.....natumaini umeanza Wiki yako vama.

Post ya jana inaweza kukufanya udhanie kuwa naunga mkono Mauaji ya hao Waislamu(if you are that thick). Ukweli ni kuwa tangu 7/7 London Bombing sina Imani wala huruma na Waislam wa UK.Victoria line au Piccadilly ndio lines zangu then nateremkanpale KingX......siku hiyo ya Saba-saba niliamua kutega Kipindi cha asubuhi kilichokuwa kinaanza saa 9:30am.....ningetoka muda wangu wa kawaida labda leo nisingekuwa hapa.Nilipoona Waislamu nahofia kuwa wanaeza jilipua.....miezi michache ya 2005 baada ya 7/7 nilikuwa nahama behewa(kwenye Tube) su nasubiri the next one ikiwa kuna mkimama au mkibaba alievaa Kiislam au mwenye asili ya Waislam kama vile Wasomali, Wapakistan n.k.Mpaka leo karibu miaka 10 naishi masaa 8 driving kutoka London na Dakika 45 kwa ndege (Dar to Moshi....pata picha)bado naogopa kujimix na hao majamaa(wapo kila kona).Baada ya kilichotokea Tunisia hakika kinaongeza hofu na chuki inakua dhidi ya Waislam. Sijali kama kuna Waislam wa kweli au wa uongo au wale wenye Msimamo Mkali kama Isis. Wote ni Waislamu tu.


Tangu Waislamu "wa kweli" hamfanyi lolote kuonyesha kuwa hamkubaliani na Magaidi mie nawaweka wote kwenye kundi moja.


Kama Boris(Meya wa London)alivyosema.....hakuna kusensa Uislamu tunapozungumzia Magaidi.....kama hamtaki kujumuishwa na Waislamu Magaidi basi do something.


Tangazeni vita dhidi yao.....tokeni na muandamane kupinga vutendo vyao viovu ambavyo "vinaharibu" value ya Imani yenu ya Dini.


Nawajua Waislamu wa Kitanzania ambao kisiri huwa wanaunga mkono lolote linalofanywa na Magaidi.


Weka Siasa ya kupigania Mafuta pembeni......wanachokifanya Magaidi sio Siasa.Baba yangu alikuwa Musilamu......nimelelewa Kiislamu lakini sasa naanza kuchukia Waislam......siwaogopi tena ila naanza kujenga Chuki.

Babai.

Sunday, 28 June 2015

Usilaumu kabla hujajua kwanini

Aah kuumwa aka holiday(mpaka niumwe ndio napumzika kuwa Mama a little).......jikapata nafasi ya kusoma article moja (ndefu ka kitabu)kuhusu Wabritishi wanaojiunga na ISis.


Nimepata mwanga mpya kuhusu hao jamaa na yote wayafanyayo. Imeeleza kwa kifupi tu kuwa Kuishi Nchi za Kimagharibi kunawafanya wajihisi kuwa sio Waislam enough.Ukifuatilia hnagundua kuwa ni kweli kwasababu  Muislam wa kweli hawezi kuishi Nchi kama Uingereza.....wanaoishi humo ni wale wanaotaka kuubadilisha Uislamu ili kwenda na wakati, kwamba wanataka kuwa Waislamu wa kisasa.Vijana hao wanadai kuwa Wamekuzwa Kiislamu na Wazazo wao lakini baada ya kuwa watu wazima wamegundua kuwa Wazazi wao wamekosea kwa kuja kuishi Uingereza.Kuishi Uingereza kunamfanya Muislamu kutokuwa Muislamu kwasababu ya Mazingira, Utamaduni,Ubaguzi na kufunga Masaa 19 mwezi wa Ramadhani(nimeongezea hihihi).


Mpaka leo sielewi ni kwanini hasa Waislamu hukimbilia Nchi za Kimagharibi(za Makafiri) na kuacha Nchi za Kiislamu tulivu?Au kama wasemavyo wao kuwa Muislamu kula Mali ya Kafiri ni Halal....Nenda google kisha weka "the secret of isis brides the guardian" ukajifunze mawili-matatu.

Babai.

Saturday, 20 June 2015

Utumiaji wa Anti- wrinke....

Unashangaa Kijana wa miaka 20na anatumia Cream za mikunjo usoni kuna tofauti gani na wewe(mie) unaetumia za Mature people wakati hata hujafika miaka 40?


Za umri chini ya miaka 60 zinanipa vyunusi bana na nyingine kukausha ngozi kupita kiasi......nilipojaribu za mature people(miaka 60+) sikupata vyunusi na ngozi ikawa na afya njema.Sio mbaya kuanza mapema kuitunza ngozi yako kwasababu anti-wrinkle actually haziondoi wrinkle(mistari/mikunjo usoni) ila inachelewesha sio?Sasa kutokana na masitiresi ya maisha bana watu wanapata Mikunjo kabla ya umri. Makampuni ya utunzaji wa Ngozi nayo yanakategolaizi antirinkozi kuanzia miaka 25(well wenzetu Weupe wanakunjika mapema so yeah).
Kwa kawaida Waafrika(Weusi) huwa hatupati makunyanzi mapema na wengi wetu huwa tunaonekana wadogo kuliko Umri wetu.


Aaah! Stori time***
Siku nipo kwa Dentist akaja madada na Pram yake....anaulizwa utambulisho wake (jina na DoB) akageuka kuangalia nani anatilia maanani....akamnong'oneza tarehe akamalizia na 1995.Ukimuangalia ni mtu mzima wa miaka 40na.....hihihihihi hivi Wazungu hawajui kuwa Weusi(wa Afrika) tunaonekana wadogo kuliko umri sio wakubwa kuliko Umri.


Hata kama unapunguza (najua wengi mmepunguza) basi punguza miaka 2 hadi 5 sio 20 khaaa....huoni aibu?!

Babai.

Mwili ni Mashine....

......inayo-process Kemikali (chakula na mengineyo)....kuna wakati Machine inahitaji "huduma" ili kuendelea ku-process Chemicals ili uendelee kuwepo.


Njia pekee ya wewe kujua kuwa Mwili(Mashine) inahitaji " huduma" no mwili huo kukuambia kwa ama kuumwa au kujisikia ovyo/vibaya.Hapa sizungumzii kuumwa Magonjwa ya kuambukizwa na Mbu au Virusi (Mafua, Tetekuwanga au hata HIV)au yale ya kurithi kama Moyo, Kisukari n.k.Kuna watu ambao wanaishi wakitegemea Dawa kusaidia Mashine zao kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu.....kwamba mwili unaposema "mamaa nimechoka nahitaji kupumzika"....mwenye mwili ana pop a Chidonge au Mavidonge.Celebs wanakuambia ili ufanikiwe unatakiwa kufanya kazi bila kuchoka (wana pop pills hao).....katika hali halisi mtu huwezi kusafiri kila siku na kufanya shows usichoke!Huwezi ku-pop pills kila siku za maisha yako kwasababu unaongeza Chemicals mwilini na hivyo mwili kufanya kazi ya ziada na hivyo ku-over choka. Nachukua a year off ndio huwa inakuja hapo.


Upatikanaji wa Dawa (happy pills) hizo kwa nchi hizi za mbele umekuwa rahisi hivyo watu wa kawaida pia wanazibugia kwa ifuatavyo.Anyway.....nachotaka kukuambia ni kuwa naumwa Uchovu kuanzia Unywele kichwani mpaka Unyayoni(sina nywele unyayoni).Zisi bizinesi ofu being'i a mamu ofu tu anda faivu kidizi in yukei izinti a joki.

Babai.

Tuesday, 16 June 2015

Bahili, Mchoyo au Mbinafsi...

Heeiyaaa! Shukurani kwa uwepo wako siku ya leo.

Watu wa hivyo tunaishi nao lakini kwasababu tunawapenda(Mapenzi upofu) inakuwa ngumu kujua au kutambua.


Hawa bwana wanaweza kukufanya uishi maisha ya kiupweke kabisa na huzuni na hivyo kuondoa maana ya Umoja wenu. Sasa leo nataka ujue kiduchu tu.Wale majaa wanaotaka kujua umetumiaje Pesa na wakigundua umetumia senti kwa matumizi yako binafsi ambayo wao (wanaume) wanaamini kuwa sio muhimu wanaanza kung'aka!


Wakati mwingine unaona unaongeza mavazi ya watoto ili wapendeze lakini bado mtu anakuambia "mbona wanakila kitu"....Inafikia mahali unaanza kuhisi kama vile unasimangwa na hivyo unaamua kutumia pesa zako.


Akiona Pesa anazotoa zinatumika kwa kile anachodhani au kuamini kuwa ni "muhimu" lakini bado unapendeza na watoto wanapata vitu vipya na vizuri mara kwa mara anaacha kutoa Pesa za Matumizi.....huyu ni Bahili!Mchoyo; Mara zote akirudi nyumbani baada ya Kazi....unamuandalia chakula  anakuambia "nilipita kwa Jeff (amuuza Kuku wa Kubanika) Mke wangu...usijali" unaishia kula peke yako(wakati ulikuwa umasubiri mle wote).


Unamlalamikia kuwa ni vema akuambie kabla ili usimsubiri na pia asipoteze chakula(sio kila mtu ana Jokofu).


Haya anaacha kula kwa Jeff lakini anarudi na kifurushi cha Mishkaki au chakula chochote "fast" au cha Mataifa mengine( Chinese, British, Indian) for One!


Anakukaribisha ule akijua kabisa utakataa kwasababu hakitoshi kwa watu wazima wawili.....na tangu katoka job lazma atakuwa na njaa so yeah.


Wengine wanapitiliza mpaka kwenye Mavazi na Manukato...kila siku anajininulia yeye tu. Wewe ukienda shopping unamkumbuka.. myeye walaa!


Oh kuna zile simu za Mkataba kwa sisi wa Ughaibuni.....hihihihi yeye amachukua the latest one wewe unachukuliwa the sooo January 2015 aka 2014 smartphone.Mbinafsi; Mara zote mkienda kufabyavmanunuzi kwa mfano....mkiwa checkout anakutegea.....au anajifanya yupo busy kutafuta Kadi yake....au anaenda kulipa lakini anaweka incorrect pin hahahahha au anakuuliza (bila aibu) unalipa au nilipe?


Huyu mjamaa usipinuomba pesa za matumizi rafiki yangu utakuwa Single Mum with a hubby(napenda hii sentensi).


Wengine tunajitegemea Kiuchumi hivyo hatujazoea kuomba pesa lakini linapokuja suala la matumzi ya familia, mwenza wako hapaswi kuombwa.....anatakiwa kujua kuwa kila Siku/Wiki lazima pesa itumike so wacha Kadi au Chenji/Chenchi.


Halafu kuna wale Wazito kutekeleza....oh hii ni Post kwa siku ingine(ni kikumbuka).

Babai.

Sunday, 14 June 2015

Maisha ya sasa ni kusaidiana...

When it suits them....

Sina uhakika na wenzetu wa Nyumbani ila wengi wetu wa Ughaibuni (wanawake) tunalaliwa na Wanaume tunaoishi nao aka Wenza/Waume.Maisha ya Ughaibuni ni Magumu sana japokuwa upatikanaji wa vitu basic ni rahisi.....kwamba huwezi kuvaa nguo/viatu vilevile au kutumia Friji/Jiko/Kochi lilelile kwa miaka mitatu.Lazima kutakuwa na hitaji la kununua vipya(ni kwasababu ubora wake ni wa chini) lengo la Makampuni mengi nikuwawezesha Wananchi "wa kawaida" kumudu vitu ambavyo vinafanya maisha yao kuwa rahisi(kurahisisha maisha).Au tuseme ni "kiwango cha ubora wa maisha" kwa kila mwananchi kilichowekwa na Serikali.......sasa ukiamua kuibuka na Sumsang Fridge sababu unamudu hakika utakuwa nayo kwa miaka 10 zaidi.Turudi kwenye Kichwa cha Habari; Ughaibuni sote tunafanya kazi (mimi bado ni Temp Mama wa kunyumba)na tuna-share majukumu Kiuchumi  lakini linapokuja suala la majukumu ya kuangalia/kulea watoto tunaambia ni "jukumu la mama".Kwamba mimi baba nitacheza nao na "kuwakalipia" i mean kuwafunza lakini suala la kuhakikisha wamekula kwa wakati, wameoga na kuwa-assist back to bed wakiota majinamizi ni kazi ya Mama.Sasaaaa kama maisha ya leo ni kusaidiana iweje Mkimama akusaidie majukumu yako (Kuleta pesa nyumbani na kulipa bills) wakati wewe Mkibaba una chill tu linapokuka suala mahitaji ya watoto?Maisha ya sasa ni tofauti na yale ya bibi zetu....maana Wazazi wangu walisaidiana na baba yangu alikuwa hands on....alituogesha Uwani pale juu ya Karo sio bafuni na alitupikia kila weekends....yeah na tulikuwa na Wasaidizi x2.Natambua baadhi yetu (well mie) tunapenda kufanya kila kitu na Mume akijaribu kusaidia unahisi kama vile hafanyi kwa usahihi......si wajua kala kautaratibu ulikojiwekea na watoto wamekazoea?Lakini nikiwa nimelala na mtoto kaamka baada ya kuota anakimbizwa na Mamba  au anakiu tafadhali deal with it....usiniamshe, unless ni emergency!Kuna baadhi ya wanawake Ughaibuni ni Single Mothers with a hubby.....aii si bora ukanunue sex when you need it...kuliko kuwa na limwanaume linalotaka "kusaidiana" kwenye kulipa bills tu.

Babai.

Wednesday, 10 June 2015

Aah namjua yule....

Hello!

Ishi ujifunze au kua uyaone.....kuna wale jamaa(wake kwa waume) huwa wana uzoefu wa kila jambo linalotokea Duniani.

Au wao wanamjua kila mhusika anaepatwa na jambo lolote interesting kwa ubaya au wema. Sijui kuhusu wewe ila mie huwa wananiudhi sana!


Unaweza ibuka unazungumzia habari ya kushtusha kuhusu mtu fulani baada ya kusikia Taarifa ya Habari then "msikilizaji wako" anaanza kukupa historia nzima ya mtu huyo na matokeo yote maishani mwake.

Unamuuliza umejuaje yote hayo mwenzangu? anakuambia "aah niliwa kuishi nae mtaa mmoja" au "mama yake alikuwa mpangaji wetu" nakadhalika!

Haiwezekani umjue kila mtu kwa undani (dont you have life?)lakini inawezekana unajua habari za kila mtu au watu wengi kwasababu ya Umbea au kwasababu unafuatilia sana habari za Kidaku.

Wakati mwingine wewe sio mbea lakini marafiki zako ni wafuatiliaji wazuri wa habari za watu na kukupa "stori".....sasa wewe kujua stori za watu haona maana kuwa unawajua sema unajua habari zao.Sio mbaya kufuatilia Gossip hasa kwa sisi Wakimama lakini unapoleta "ufahamu" wako kuhusu mtu uliepata habari zake kwenye Magazetibya udaku usijifanye unamjua au uliwahi kuishi nae...mmsema tu umesoma.

Kwa mfano wale wenye "akili" huwa wanasema wamesoma wapi (site gani) au kitabu gani ili nawe uende ukapate Ilimi.


Si unawajua wale wenye "idea" ya mambo mengi tofauti ya Kijamii na hivyo kuyazungumzia kwa urahisi lakini kwa undani....intellectuals (hawa nawapenda) kwasababu najifunza kila wanapoleta Siasa.

Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Thursday, 4 June 2015

Wanawake na Usenge!

Kwanini sisi wakimama ni wepesi sana kukubali hawa jamaa?.....Hi are you well?


Usinielewe vibaya! Siwachukii wanaojibadilisha kutoka Jinsia moja kwenda nyingine(I feel sorry kwa mume/mke na watoto though). Pia sina habari na Wanaume wanaopenda kujiremba au kuvaa nguo za kike.Hakika sijali nini mwanaume na mwanaume mwenzie au mwanamke na mwanamke mwezie wanafanya chumbani kwao(keep it there).
Lakini sitoacha kujiuliza au kuuliza ni nini hasa kinafanya wanawake kuwa wepesi kuwakubali hawa jamaa kwenye Jamii? Kwanini sisi ni wa kwanza kuwachukulia poa na hata kurafikiana nao?Ni ile "huruma nature" tulioumbwa nayo au ni kwasababu Wanaume wengi ni Waoga wakidhani hali hiyo(Usenge) inaambukiza so wanakuwa wagumu au wenye Chiki/hasira wakihofia "kubadilishwa"?


Pengine wanaogopa kuwadondokea Wasenge wa Kiume hihihihihi kama unaeza mtamani wa jinsia yako akiwa Mtupu na ukawimika wewe ni Msenge tu hata kama umeoa na unawatoto.....usiogope toka Kabatini.Back to the post: Binafsi (dada mkubwa) mwenye Wadogo wa Kiume. Hakika nilikuwa napata hasira nikifikiria vipi madogo wakiwa  Wasenge? Nitawachukia? Nitawaua?


Natambua hii ni hofu ya wazazi wengi(hasa wa kiume) na can break your heart lakini kutokana na Mazigira yalivyo sasa na urahisi wa kufikia au kipatabinfomations ni vema tubadilishe namna tunakuza wenetu.


Kamwe sitokufundisha  namna ya kumlea mwanao au kukuambia lea mwanao kama nileavyo wanangu......mwenyewe najifunza daily hapa.


Nina Kijana na Binti.....je huwa namfikiria Mwanangu wa kiume kwenda kwingine na hivyo kujitahidi kumlea kama MWANAMUME? Hapana!


Nawalea wanangu kama wanangu....kila moja anajijua kuwa yeye ni a Girl na mwingine ni a boy so i go with flow.


Babuu akilia-lia au kunung'unika simuambii "boys dont cry.....au dont cry like a girl" namwambia a 4yr old...grown nursery boy dont cry like a stay home baby. Hapendi kuitwa baby na hapendi kukaa nyumbani so that works.Unapoanza kum-feed mtoto kuwa Wavulana ni  Wakakamavu, Jasiri, hawalii au kuwa emotional ni wazi kuwa unamwambia mwanao wa kiume "usiwe kama msichana" au Wasichana ni Wadhaifu.Watu wenye tabia hii ni wanaume ambao hawathamini mwanamke na nadhani wanahofu kuu kuwa watoto wao watakuwa Wasenge.....wakidhani Usenge ni kuwa mwanamke.Usenge sio Uanamke.....kupenda kuvaa mavazi ya kike au kujiremba sio Uanamke....kuwa na Matiti sio Uanamke.....kuwa mbeya sio Uanamke.Mimi kama mwanamke najiamini na kukuambia kuwa Uanamke ni zaidi ya kuwa emotinal.....unamke ni zaidi ya kulia-lia na mengine ambayo Wanaume mnaita "tabia za kike"Nimechanganya topics didn't I? 2-in 1 Blog post si ndio. Asante kwa kuichagua blog hii.

Babai.

Tuesday, 2 June 2015

Mashindano.....


Ni vema kuwa Mshindani mahali pa Kazi, Shuleni au Kimichezo, kwamba ni vema kuhakikisha unakuwa juu/mbele kuliko uwezo wako.

Unaweza kuwa umezaliwa hivyo(mshindani) au umejifunza kutokana na "kusukumwa" na Wazazi wako.


Nimewahi kuzungumzia hili lakini niliegemea zaidi ushindani kati yako na watu wengine uwaonao kwenye Sosho media au Mtaani(au was it in my head?).


Pamoja na kuwa ushindani unakusaidia kufanya vema kwenye maisha yako Kikazi, Kielimu au Kimichezo bado hali ya Ushindani au kutaka kushindana pasipo husika kunaweza kukuharibia.


Ukiiendekeza hali hiyo na kuiweka kwenye kila kitu ufanyacho inaweza kuumiza watu wako muhimu kama vile mke/mume, watoto na ndugu.


Kabla ya kufanya mapenzi hii inakuna kichwani "juzi na jana nilianzisha mie au nilikuwa juu.....leo zamu yake. Bila kusema unamsukuma au kumvuta mwenzio awe juu yako"? Huo ni ushindani na can put mkeo/mumeo off.Katika hali halisi....anaelianzisha ndio atakae so huyo huyo ndio awe mtendaji mkuu, kwamba amfanye mwenzie atake au awe tayati kuneng'enuka.Pengine sio mshindani kwenye kufanya mapenzi lakini ni mshindani kwenye masuala mengine......unarudi home na kuanza kugombania TV kwa mfano...."umeshinda nyumbani siku nzima sasa ni zamu yangu".Wengine mnapitiliza mnashindana na watoto wenu....."mmeangalia vipindi vyenu siku nzima sasa ni zamu yangu " hihihihihi well this was me nikaamua kubadilika na kuangalia Tv watoto wakilala( kama sijachoka that is).


Binafsi sio Mshindani yaani sina habari na nani kafanya nini-wapi-kwanini lakini napenda kuganya Vema na kufanikiwa hivyo naelekeza nguvu zangu kwenye Bidii zaidi ya "lazima niwe kama fulani au zaidi yake"!


Ni vema kuacha ushindani wako mahali pa Kazi au Elimu-ni na sio kuwa mshindani kwenye kila kitu na hivyo kuharibu au kuondoa maana ya Familia/Ndoa yenye furaha.

Nakupenda kwa kuitembelea Blog hii leo.

Babai.