Sio kwamba anapenda (hakuna mtu anapenda kununa)isipokuwa anatabia ya kununa(Kislani/Gubu). Kama ilivyo kwa sisi Wanawake, wenzetu pia huwa wananua ila kununa huko huwa wanakupa Jina lingine tofauti kabisa na Kisilani/Gubu ili wasihusishwe na "Uanamke"(wakiamini ni udhaifu na Mwanadamu pekee dhaifu Akilini mwao ni Sisi).
Utamsikia anang'aka na kusema hana gubu/hajanuna/hajajitenga isipokuwa "siku yangu imeharibika/imeanza vibaya", "usinisumbue nina Mawazo", "Nahitaji muda wa peke yangu kutuliza akili", "Najisikia vibaya" na ikiwa alipoteza Mzazi au Wazazi wote basi hiyo itatumika zaidi..."nimewakumbuka Wazee" nakadhalika.
Tabia hiyo inakera na inaumiza sana, inakupa wewe Mke mtu upweke wa hali ya juu. Inaweza kukupa ushawishi kwa ku-check na Ex au hata kutamani kutafuta kipoozeo. Hivyo kusababisha mtikisiko kwenye Ndoa/Uhusiano wenu ikiwa hakuna Mawasiliano au hamjuani(hamjasomana tabia, kwamba bado ni Wapenzi wapya).
Mara nyingi Mwanamke anaweza kudhani labda humpendi/jali tena, huenda kuna mtu Mpya(unatoka nje ya uhusiano) au unataka kuachana nae na hivyo unatafuta sababu.
Upweke na Maumivu kwako huongezeka pale unapogundua kuwa anazungumza na Rafiki zake na kuchekelea(onyesha anafuraha) au Watoto wenu tu lakini wewe unapata majibu ya "Ndio" na "Hapana" na Sura ya Kisilani, au wakati wa kutoka hakuagi kama kawaida yake(sisi ni Busu halafu "am off", ninyi ni nini?)....basi unapata "Am off" tena akiwa Mlangoni....ili usiisikie then akirudi umsute(lalamike) vizuri.
Wakati wa kufundwa(tuliofundwa Oyee)tulifunzwa kuwa Mume anapofanya hivyo(kununa) huwa anatafuta mahali pa kutolea yaliyoujaza Moyo wake, Wanaume wengi sio wepesi wa kuongelea "hisia" zao . Hivyo wanaamua kukununia ili ukasirike halafu mzozane na hapo apate kuyatoa mahisia yake na ionekane chanzo ni wewe wakati ni yeye.
Muhimu ni kuhakikisha yupo salama lakini muache na kununa kwake mpaka awe tayari ku-share na wewe(in 3 days max). Bila kukupotezea muda na kuongeza urefu wa Bandiko hili, nikuambie ni namna gani unaweza kukabiliana na hilo na hivyo kuepusha Ugomvi;-
Ukigundua "siku yake imeanza vibaya"(ana Gubu/Kanuna/Kajitenga hihihihi), tafuta sababu ya yeye kuwa alivyo leo na muulize kwa upendo tatizo ni nini? Jibu atakalo kupa lichukue, liheshimu na umuache alivyo. Usibishe wala kuongeza ya kwako na hivyo kumuudhi. Hilo moja.
Pili; Endelea na shughuli zako za kila Siku kama kawaida, onyesha kumjali ila usipitilize.
Tatu; Pamoja na kuwa ni ngumu kushirikiana nae Kimwili, jitahidi kumpa atakapohitaji(hasa cha asubuhi).
Nne; Ikiwa wewe ni kama mimi, kwamba unapika kama sehemu ya kuonyesha Mapenzi na umpendae kakununia unaweza kutaka kususa kumpikia ili umkomeshe. Usifanye hivyo, pamoja na ugumu wake kihisia wewe Mpikie chakula akipendacho.
Tano; Kila mnapoenda kulala, mpe kumbatio(kumhakikishia kuwa unamjali sio la kutaka Tendo).
Sita; Kama mnaishi pamoja Kununa Mwisho siku Tatu, kama mpo mbali mbali mwisho Wiki. baada ya muda huo lianzishe ili aache kununa. Usianze kwa kulalamika, isipokuwa mkumbushe umuhimu wa kuwasiliana na kuchangia matatizo ya kihisia/kiakili. Kama Wenza ni muhimu kuweka wazi issues na kuzitatua pamoja.
Atafunguka na kuomba radhi na kujielezea. Hakika utashangaa kwanini sasa asingekuambia tangu Siku ya kwanza ulipomuuliza tatizo ni nini? Kumbuka wewe na yeye ni watu wawili tofauti, sio kijinsia tu bali Malezi, Mazingira mliokulia, pengine Kabila/taifa, uwezo kiakili/kimaamuzi, ujasiri n.k.
Nathamini Muda wako, karibu hapa usome Faida za Kununa kwa Mwanamke.
Kwa leo Baibai.
Comments
Ahsante kwa ushirikiano.