Skip to main content

Jinsi ya kukabiliana na Mwanaume apendae kununa/susa/chuna...



Sio kwamba anapenda (hakuna mtu anapenda kununa)isipokuwa anatabia ya kununa(Kislani/Gubu). Kama ilivyo kwa sisi Wanawake, wenzetu pia huwa wananua ila kununa huko huwa wanakupa Jina lingine tofauti kabisa na Kisilani/Gubu ili wasihusishwe na "Uanamke"(wakiamini ni udhaifu na Mwanadamu pekee dhaifu Akilini mwao ni Sisi).


Utamsikia anang'aka na kusema hana gubu/hajanuna/hajajitenga isipokuwa "siku yangu imeharibika/imeanza vibaya", "usinisumbue nina Mawazo", "Nahitaji muda wa peke yangu kutuliza akili", "Najisikia vibaya" na ikiwa alipoteza Mzazi au Wazazi wote basi hiyo itatumika zaidi..."nimewakumbuka Wazee" nakadhalika.


Tabia hiyo inakera na inaumiza sana, inakupa wewe Mke mtu upweke wa hali ya juu. Inaweza kukupa ushawishi kwa ku-check na Ex au hata kutamani kutafuta kipoozeo. Hivyo kusababisha mtikisiko kwenye Ndoa/Uhusiano wenu ikiwa hakuna Mawasiliano au hamjuani(hamjasomana tabia, kwamba bado ni Wapenzi wapya).


Mara nyingi Mwanamke anaweza kudhani  labda humpendi/jali tena, huenda kuna mtu Mpya(unatoka nje ya uhusiano) au unataka kuachana nae na hivyo unatafuta sababu.


Upweke na Maumivu kwako huongezeka pale unapogundua kuwa anazungumza na Rafiki zake  na kuchekelea(onyesha anafuraha) au Watoto wenu tu lakini wewe unapata majibu ya "Ndio" na "Hapana" na Sura ya Kisilani, au wakati wa kutoka hakuagi kama kawaida yake(sisi ni Busu halafu "am off", ninyi ni nini?)....basi unapata "Am off" tena akiwa Mlangoni....ili usiisikie then akirudi umsute(lalamike) vizuri.



Wakati wa kufundwa(tuliofundwa Oyee)tulifunzwa kuwa Mume anapofanya hivyo(kununa) huwa anatafuta mahali pa kutolea  yaliyoujaza Moyo wake, Wanaume wengi sio wepesi wa kuongelea "hisia" zao . Hivyo wanaamua kukununia ili ukasirike halafu mzozane na hapo apate kuyatoa mahisia yake na ionekane chanzo ni wewe wakati ni yeye.


Muhimu ni kuhakikisha yupo salama lakini muache na kununa kwake mpaka awe tayari ku-share na wewe(in 3 days max). Bila kukupotezea muda na kuongeza urefu wa Bandiko hili, nikuambie ni namna gani unaweza kukabiliana na hilo na hivyo kuepusha Ugomvi;-


Ukigundua "siku yake imeanza vibaya"(ana Gubu/Kanuna/Kajitenga hihihihi), tafuta sababu ya yeye kuwa alivyo leo na muulize kwa upendo tatizo ni nini? Jibu atakalo kupa lichukue, liheshimu na umuache alivyo. Usibishe wala kuongeza ya kwako na hivyo kumuudhi. Hilo moja.


Pili; Endelea na shughuli zako za kila Siku kama kawaida, onyesha kumjali ila usipitilize.

Tatu; Pamoja na kuwa ni ngumu kushirikiana nae Kimwili, jitahidi kumpa atakapohitaji(hasa cha asubuhi).

Nne; Ikiwa wewe ni kama mimi, kwamba unapika kama sehemu ya kuonyesha Mapenzi na umpendae kakununia unaweza kutaka kususa kumpikia ili umkomeshe. Usifanye hivyo, pamoja na ugumu wake kihisia wewe Mpikie  chakula akipendacho.

Tano; Kila mnapoenda kulala, mpe kumbatio(kumhakikishia kuwa unamjali sio la kutaka Tendo).

Sita; Kama mnaishi pamoja Kununa Mwisho siku Tatu, kama mpo mbali mbali mwisho Wiki. baada ya  muda huo lianzishe ili aache kununa. Usianze kwa kulalamika, isipokuwa mkumbushe umuhimu wa kuwasiliana na kuchangia matatizo ya kihisia/kiakili. Kama Wenza ni muhimu kuweka wazi issues na kuzitatua pamoja.

Atafunguka na kuomba radhi na kujielezea. Hakika utashangaa kwanini sasa asingekuambia tangu Siku ya kwanza ulipomuuliza tatizo ni nini? Kumbuka wewe na yeye ni watu wawili tofauti, sio kijinsia tu bali Malezi, Mazingira mliokulia, pengine Kabila/taifa, uwezo kiakili/kimaamuzi, ujasiri n.k.


Nathamini Muda wako, karibu hapa usome Faida za Kununa kwa Mwanamke.

Kwa leo Baibai.

Comments

Anonymous said…
Jamani wanachosha sana hawa viumbe, mtu mpaka unashindwa ufanyeje lakini ndo ushapenda yani.
KKMie said…
Hakika! ndio maisha ndio ukubwa huo, hata sisi huwa tunawakera sema kwasababu tumekua tukiaminishwa kununa ni "uanamke" basi hatutegemei wenzentu kununa. Muhimu ni kutambua kuwa wao pia ni wanadamu na wanahisia kama sisi.

Ahsante kwa ushirikiano.

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao