Tuesday, 30 September 2014

Lugha ya Mama kwa Mtoto...

Huku (UK) watu ambao tunaongea lugha zaidi ya Moja huwa tunashauriwa kuachana na "local" Lugha na kuwafunza Watoto wetu Lugha ya "mama".....in my case Kiswahili.
Kama kawaida ya Mzungu(anajua kila kitu)....wanadai kuwa Mtoto husika atajifunza "local" Lugha (Kiingereza) akianza Shule na hii itamsaidia Mtoto huyo ku-master "Lugha ya Mama vema".
Kwenye hili kuna Mawili muhimu(Kichwani kwangu): Mosi; Wanataka mtoto wako awe nyuma Darasani, kwamba akianza shule huku hajui "local" Lugha wanaoijua (wenyewe) wataendelea mbele wakati Mwanao anapoteza muda kujifunza.
Pili; Aki-master lugha ya "mama" watamtumia vizuri (hawatoajiri Mgeni wa Lugha yenu) ili kufanya kazi ya Kutafasiri na pia atakuwa kajifunza Bure(hawakulipi kumfunza M-british Lugha yako).

Kwanini nawaza/fikiri hivi? Well....Muingereza hana Lugha nyingine zaidi ya Kiingereza, iweje akuhamasishe wewe umfunze mwanao Kilugha chenu badala ya Kiingereza, akijua wazi Shuleni hakuna "Kiswahili" bali Kiingereza?!!

Nilikuwa a bit hard kwenye Kiswahili, nilitaka wanangu wazungumze Kiswahili lakini wakiongea wanaongea Lugha ingine.....nimeamua ku-relax na niwaache wazungumze "local" Lugha.

Pamoja na kusema hivyo bado najitahidi kuwafunza wanangu Kiswahili(sijakata tamaa). Mkaka(Babuu) anaelewa ila kutamka maneno bado kunamtatizo.
Mdada nae anaiga/rudia kila neno la Kiswahili usemalo which ni dalili nzuri.
Oh Jana, nikakutana na Site yenye Methali za Kiswahili.....the excitement niliyoipata sasa! Ni kama 2002 nilipoingundua DHW/DHB(very 1st Tanzanian Forum ya Kiswanhehe)."Mwenda Tezi na Omo Marejeo ni Ngamani".

Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 29 September 2014

Nanyanyapaa au na-practice

Freedom of expressing my view? Sijui...


Alikuwa Mwanaume, akaathirika Kisaikolojia kwa kuishi kwenye Mwili wa "mwanaume" wakati yeye anajijua na kuwa ni Mwanamke.
Akaoa na kuzaa ili kuficha "tatizo" lake....akashindwa kuvumilia akawa anaibia Mavazi ya Mkewe na kujiremba mkewe akiwa hayupo nyumbani.

Anapenda urembo na kuvaa kama mwanamke, baada ya Miaka kadhaa akaomba "Shirika la Afya" ku-fund Upasuaji ili abadilishe Maumbile na Jinsia na kuwa complete au legally "Mwanamke" .

Ombili lake likapita kwa "ground" ya Kuathirika Kisaikolojia na asipofanyiwa Upasuaji(kubadilishwa Jinsia) anaweza kuji-harm.....so akanza Tiba ya Homono, baada ya Muda akabadilisha Jinsia na Documents zote zikabadilishwa kutoka Mwanaume kuwa Mwanamke.
Sasa amepata Mpenzi mpya na anampango wa kufunga nae ndoa, Mpenzi huyo ni Mwanamke.Anadai kuwa anavutiwa sana na wanawake hihihihihiihi which make him a real Man(in my head....mmh naturally)!
Wananchi wanadai Pesa zao(Kodi) zilizotumiwa na Shirika la Afya kumbadilisha Jinsia Mwanaume kuwa Mwanamke.
What a confusion Planet!!! Or I should ask, why complicate your life eiiii! Hii ikitafsiriwa nitashitakiwa kwa Unyanyapaaji dhidi ya Transgenders.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 25 September 2014

Bank Kuu Tz na Gmail account...REALLY?!!

Huenda wana account yao Official ambayo inawawepa mahali pazuri KIUSALAMA online.

Nimepokea Email kutoka Bank Kuu ya Tanzania, ikinipa tahadhari kuwa nisipobadilisha "Details" zangu via Link waliyoiweka basi sitoweza ku-Bank Online na Bank yeyote Tanzania!

Nikaenda kwa "sender" nikaona mtumaji ni "blablabla BankOfTanzani@gmail.com".....nkacheeeka halafu nikapachika tusi!

Kwanza mimi siBank na Bank yeyote Tz online, Halafu huwezi tu kuwaambia watu wabadilishe "details" zao via link, kwa sababu za Kiusalama kila mtu angepata taarifa hiyo kwenye account yake ya Online ambapo anaingia kwa kuweka "details" ambazo ni zaidi ya jina lake na Namba ya Card, yaani za "siri" na ni yeye tu ndio huwa nazo na hubadilika kila unapo BankOnline.

....aiiii naona nazungumzia System ya huku na sio ya huko Tanzania ambayo siijui.
Nachojaribu kusema ni hivi;- Kama ilivyo kwenye Kutongozwa kuna Maharage ya Mbeya na Maharage ya Kigoma....Watu tunatofautiana, kuna wale wanao-panic haraka so wataenda na kuweka "details" zao kwa hao Scams!

Halafu kuna akina sie ambao kabla ya yote tunahoji na wepesi kwenda Bank na kuwauliza kulikoni?
Najua kwa Watanzania wengi ku-bank Online ni kama "status" ya kuendelea....ni kama vile watu kukimbilia kuBank na Bank ya Nje (kwa status reasons) badala ya kubank na Local Bank.

Well hata mimi na Bank na Bank ya Marekani na Ya Honk kong sio ya UK.....nadhani bank zote za UK sio za UK, hata (niliambia wakati wa Yes/No reforandamu Kampeni) Royal Bank Of Scotland ni ya Down under.....so naezajitetea SI kwa STATUS reasons.Babai.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 24 September 2014

Misinformation za Online nazo.

Hellooooo!


Urahisi wa kuweka chochote online kwa nia ya ku-share au "kuelimisha" wengine ni mzuri sana!
Sote tunajua kuwa kwenye kila kitu kuna Faida na Hasara zake, kama Mwanadamu unatakiwa kupima na kufanya uamuzi kwa kuzingatia faida zaidi (utafaidika?).

Sio sote tuna-share yote(kila kitu) online....kwenye Blog ya D'hicious nimeshare mengi tu ila sio yote nijuayo (mengine naweka kwa ajili yangu mimi binafsi) na Binti yangu na Mwanae huko mbeleni Ntakapo kuwa Proper Bibi.


Hali kadhalika kwenye Blog nyingine Mf za Urembo, Fashion hufanya hivyo pia....tena hawa huwa hawabani some info, wanakudanganya kabsaaaaaa(wanapindisha ukweli) ili uogope au ukosee na hivyo usitokee as Mrembo kama wao wanavyoonekana au Nywele zako zisikue kama zao.


Safari yangu ya Nywele (nilishawahi kukuambia about) imenifanya nijaribu Mengi, kukosea Mengi na Kujifunza Mengi halafu nikarudi kwenye "rutini" yangu ya enzi ambayo kabla ya YouTube na Blogs za Nywele na Afya ya nywele zangu imekuwa njema.....(The new thing kuongeza Oils kwenye Conditioner).

Narudia tena, usichukue kila unachosoma online kama kilivyo, pima Faida na Hasara....kama ni Tiba(Madawa) au Afya ni vema kuangalia chanzo chenye uhakika Mf: site za Hospitali au Shirika la Afya, kwa huku nilipo NHS.com ina info nzuri sana kuhusu Magonjwa yote, yep Mpaka Ebola....sio Blogs ya mtu anaejiita Doctor(could be anybody).


Story time:Nilipoanza Kazi miaka ka' 20? Iliyopita....sikumbuki(tafanya hisabati baadae)....anyway! Niligundua kuwa ile Makala nzuri sana ya Urembo iliyokuwa inaendelea kwenye Gazeti Fulani na "mmiliki" alikuwa Mwanamke(kwa mujibu wa Picha na Jina).....kumbe MUANDISHI wake alikuwa Baba mtu mzima na hakuwa Mtanashati, alikuwa a bit rough(hajipendi)!


Sasa linapokuja suala la Afya yako au matumizi ya Madawa hakuna "Trial and Error" kama kwenye Urembo(utanawa) au Nywele(utazikata)Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 23 September 2014

Kabla ya Mobile Simu na Net....

Ulikuwa unafanya nini na muda huu unaotumia Simu yako au Mtandao eti?!!


Jinsi Teknolojia inavyozidi kukua ndivyo ambavyo maisha yanazidi kuwa busy na kuhisi muda haukutoshi (Masaa 24 yamekuwa machache).Binafsi nilichukua hatua ya kutoka Mtandao mmoja wa Jamii na Kujiunga na ambao ni latest one (Mwisho ilikuwa Twitter karibu Miaka 5 iliyopita) hivyo sikuwa kwenye Mitandao Saba ambayo ingenichukulia Muda wangu mwingi.
Kabla ya hapo hakukuwa na Mitandao ya Kijamii, kulikuwa na Forums na Chatrooms pamoja na kuwa nilikuwa na Muda mwingi bado sikujiunga na kila Forum/Chatroom iliyojitokeza.Hapa juzi nimemsikia Business Woman akisema ameamua kufuta Email address yake na baadhi ya namba za Simu za Ndugu, Jamaa na Marafiki wasio na Mpango (wasiomsaidia kwenye Biz yake) ili aweze ku-focus zaidi kwenye Uzalishaji na Uendelevu wa Kampuni yake.

Anadai kuwa Teknolojia ya Smartphone imesababisha yeye kupoteza muda mwingi kujibu Mails ambazo hazina umuhimu maishani mwake, hivyo akazuia kuzipokea, lakini akawa anapata lawama kila anapokutana na Ndugu, Jamaa na Marafiki....hiyo ikamsukuma kuifutilia mbali "account" yake.

Nimesoma hiyo Wiki mbili baada ya mimi "kupumzika" kwenye ile Blog yangu ingine ambayo husababisha mimi kupokea Mails za kila rangi ya usumbufu na Lawama kwanini sijibu mail "binafsi"(sijui hawaoni kuwa D'hicious sio blog ya kurafikiana)!

Sasa leo hii nina "kajeshi" ka' watu wa Tatu(watoto na Baba yao) ambao ni muhimu maishani mwangu. Wawili kati ya hao (watoto) wanahitaji kufunza HISABATI (nalia sana kila nikifikiria Hisabati).
Nahisi kama muda umefika wa kuifunga ile Blog. Wee unaonaje?


Babai...
Mapendo tele kwako...

Monday, 22 September 2014

Binti "akiharibika" arudishwa kwao....

...ambako hajawahi kuishi (hajakulia) huko maisha yake mapya ya "ukubwani hivyo kuwa Mgeni.

Hii tabia mie huwa inanikera sana, enzi zile nakua nilikuwa nasikia tu watu wakisema "aah fulani, kashika mimba nimemrudisha kwao" au "amelimbukia sana maisha ya mjini, nimerudisha kwao".

Unapochukua mtoto wa Mtu akiwa Mdogo kwa nia ya Kuishi nae kama "msaidizi" (which ni kinyume cha Sheria) au kukubali jukumu la kulea mtoto baada ya Wazazi wake kutangulia(Kufariki) unapaswa kuendelea kuishi nae na kumpa support/saidia ili arudi kwenye "mstari" sio kumpeleka "kwao" ambako ni Mgeni!

Pia sio haki kwa watu wa kule "kwao" kubeba "Mzigo" ambao wewe Mlezi ndio uliyesababishwa kwa maana moja au nyingine.

Unalea Binti tangu anamiaka, tuseme sita....tabia atakazokuwa nazo ni matokeo ya Malezi yako, hivyo ikitokea "kaharibika" Hatia ni yako, sio ya watu wa "kwao".

Usimwambie mtu: Wengine huwarudisha mabinti wa Watu kwao baada ya kuhusika kwenye upatikanaji wa Mimba aka KUHARIBIKIWA.....

Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 16 September 2014

Watoto wanahitaji role Model sio Model!

Ah! Nimekua busy kweli....unajua umri ukienda Majukumu yanazidi/yanaibuka kila kukicha.

Hapana sio majukumu kuhusu Watoto, Baba yao na Bills ni majukumu ya kuutunza Mwili na Uso ili kurudisha Miaka nyuma. Si nilikuambia by the time nafikisha Miaka 40 nataka kuwa kama Gabriel Union!! (Au niliota tu?).

Nataka wanangu wawe proud of my "look" nikienda wadondosha na kuwachukua Shule hihihihi....sio wakikuona tu wanakimbia kwa aibu au wanasema "that's not my mummy, she's my Shangazi/Bibi".

Eh! Nilipokuwa Msingi kuna mdada mmoja (sasa maarufu kwenye MaTv huko kwenu) alimkimbia Mama yake, tena akawa analia kabisa kuwa yule sio Mama yake....si wajua Mama wa Kinyakyusa alietoka Mbeya beak ya kwanza Shuleni hihihi hi akina Mwakaninini(naambiwa ninyi ni watani wangu upande wa Mama so usi-panic)!
Eti "Children need role model Not a Model"....wacha uvivu, hebu jipende huko.....you can be both!


By the path I AM FAR FROM a MODEL na nikijiremba sirembeki.


Babai!
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 10 September 2014

Mwanaume ka' Mwanamke na Nyumba Ndogo!

Only Mwanaume husika akifanya jambo baya, la kizembe au akionyesha "emotions"! Mfano akisema ukweli pasipotakiwa (Umbea), akilia baada ya kuumia, akizimia Msibani (Wanaume hawazimii, huwa wenda wazimu hihihihihi) n.k.

Tabia hiyo huwafanya Watoto wa Kiume kuwa na Tabia mbaya za Baba zao, kwasababu wanaogopa au hawataki kufananishwa na Wanawake.


Kwenye Jamii yetu (Tz) Baba kuwa na Kimada siku hizi imekuwa suala la kawaida, jamii imelikubali hilo na kuwapa jina zuri eti "Nyumba Ndogo" which is sooooooo annoying, Yaani ndio kukata tamaa au?!!

Sasa nyumba ndogo huwa haijengwi kwa siku moja, na mara zote Mtoto wa Kiume huwa wa kwanza kujua ikiwa Baba ana Kimada.....Vijana hujua mengi sana Mtaani/Vijiweni.

Wengi huwa wanaumia kuona kuwa Mama zao wanakuwa cheated na Baba zao lakini kwa vile wanaogopa kuitwa "Wanawake" wanaamua Kuuchubua (do you still use this word??).

Baadhi ya Vijana (watoto wa kiume) husika huamisha maumivu yao "emotionally" na kujenga Hasira na Ukaidi dhidi ya Mama zao (hawawaheshimu tena) na huwakwepa Baba zao.


Kwanini Baba anashindwa kumheshimu mama na kwenda kuwa na mtu mwingine nje ya Ndoa? Au Kwanini Mama anamuachia Baba amtende....hapo ndio inakuja sehemu ndogo ya "Wanawake sio Imara" au "Dhaifu"....

Hakuna mwanaume anataka kuwa Dhaifu! Kila mwanaume anataka kuwa Jasiri na Imara.....

Hii hubaki kichwani na wao kufanya walichofanya Baba zao, matokeo yake "Nyumba ndogo" imekuwa the new Norm!
In My Head....hii haina Uchunguzi wala Utaalam wala Uzoefu.

Babai
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 9 September 2014

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!!


Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana!

Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima.

Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu).

Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!!

Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu".

Kaongeza: "Vumilia tu mwanangu, ndio Ukubwa huo, Vaa Bra kusapoti Uzito".....anyway baada ya Wiki yakaanza kukauka na kurudi yalivyokuwa kabla sijazaa.

Sasa leo nimeamua kumuachisha Binti yangu, yaani hakuna ku-give in.....atalia, atarusha tantrums (maana ni kabingwa) walaaaa sijali.
Haya ni pale Mshauri anapoomba Ushauri....anyone?!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Friday, 5 September 2014

Mungu ni wa Afrika tu?

Umewahi kujiuliza kwanini sisi Waafrika Mataifa Mengine ambayo ni Masikini kuwa pamoja na kuamini Mungu na kusali kwetu kote bado hakuna Maendeleo?


Kwanini Mataifa hayo yanaendelea kuwa Tegemezi wa Nchi za Ulaya Magharibi na Marekani?(Wacha sababu za Kisiasa na Historia hapa sio mahali pake)....


Leo hapa (kwako itakuwa Jana) Mimi na Asali wa Moyo tulikuwa tunajadili kuhusu Ubinafsi wa sisi wanadamu, tukafikia mahali tukakubaliana (kwa kawaida huwa hatukubaliani)!


Wazungu ni Washenzi kote-kote na wengi wao hawaamini Mungu as in kusali kucha kutwa na kwenda kutoa Sadaka kanisani kila J'2 lakini linapokuja suala la kusaidia Binadamu wengine wenye Matatizo huwa mstari wa Mbele!


Huenda hilo ndilo linalowafanya waendelee kufanikiwa, kwamba hawakai(kupoteza muda) kusali na kutegemea Mungu awashushie Mahela ili wawasaidie wengine au kukesha na kuomba ili Mungu awape Makazi wakimbizi mahali palipo na Vita.


Wanafanya yote hayo kwa Vitendo.... kuna Maduka kibao ya Misaada ambapo watu hujitolea vitu ambavyo hawavihitaji tena(Mitumba) na kuuzwa ili kusaidia Masikini wa Nchi zinazoendelea, Waathirika wa Vita n.k.


Pamoja na kuwa watumishi wa juu sehemu hizo za "misaada" hupata faida bado sehemu kubwa ya mapato ya "Misaada" inakwenda kwenye "kusudio".


Pia kuna wale ambao hujitolea kwenda "umasikinini" (Nchi zinazoendelea) au Vitani kusaidia Wakimbizi.


Ndani ya Nchi husika iliyoendelea kuna "Vikundi" kibao vya kupigania Haki za watu ambao hata hawawahusu, mf; Kusaidia watu wasio na Makazi, Kusaida wanawake wenye matatizo, Kusaidia "fund" kwa ajili ya wagonjwa wa Saratani na Uchunguzi ili kupata Dawa n.k.....ndio wanapata Mishahara mizuri lakini kazi zao zinatekerezwa na Matokeo yanaonekana.


Wote hao hawakeshi na kuomba kwa Mungu, bali wanathubutu na kufanya sehemu yao kwa Akili na Nguvu zao walizopewa na Mungu(niaminivyo mimi).....Mungu anawarudishia Baraka Zaidi ndio maana wapo hapo walipo(in my head).

Angalia Ebola(kwa mfano) inavyotupelekesha Afrika, halafu tunakesha na kukemea "pepo la Ebola toka kwa Jina la Yesu" aliekuambia Ebola ni Pepo nani?.....na bado unasubiri Mzungu akuletee Dawa....Madaktari wa Afrika na Serikali zao walikuwa "Wavivu" kufanya research tangu Ebola ilipo ibuka Demokrasia ya Congo kwa mara ya kwanza?......Aiiii nimeingia kwenye Siasa sasa, wacha nifunge Simu.

Furahia Mwanzo wa Mwisho wa Wiki yako...

Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 4 September 2014

Na-admire sana watu wa Medical...

Nakupenda kwa kuichagua Blog hii...

Unajua wale wadada wakubwa inatokea unawapenda, unatamani kuwa kama wao (Kielimu) utakapokuwa Mkubwa?!!


Mie nilikuwa nawapenda sana Wadada Wanasheria, Waandishi wa Habari na Young Docs (au tuliwaita Medical assistants sababu walikuwa hawajafuzu).....sasa kuna mmoja alikuwa jirani yetu enzi hizo bado kabinti, alikuwa anasoma Russia.


Kwasababu alikuwa Mkubwa sana kwangu hatukuwa na utaratibu wa kuongea lakini tulikuwa karibu sana na alionyesha kunipenda kweli-kweli!


Kila J'Mosi alikuwa ananiita "Dinah Mdogo wangu unakazi?(Za shule)... ukimaliza naomba uje unikwangue Mba"!! Usicheke tafadhali (hihihihihihihahahahahaha)...Basi mwenyewe nafurahi naenda kumkwangua "dada MA" Mba....honestly!!!


Namkwangua, nikimaliza nampaka mafuta halafu namsuka....heee! Najua kusuka blaa tangu nina miaka 7 shukurani kwa Bibi na MSesere(Doll) wangu....nika-master Kusuka Mitindo nilipofika miaka 15 hivi....by 18 nilikuwa nasuka watu kwa Hela including Dada mMedical Assistant baibeee (Nimeanza kujitegemea kiuchumi kitambo ujue!).


Sifa kuu ni kuwa nikimsuka mtu simvuti/umizi ngozi na nywele zake hazikatiki akifumua....SISUKI watu usijedhani najitangazia Biashara bure!!


Baada ya Muda Dada akawa sijui "MD" sijui nini nini na akaolewa, akahama na kuhama....bado na admire sana Medical People, Naomba sana wanangu waje kuchagua kusoma Medicine.


Napenda Proper Degrees, sio zile useless zile sijui ninininiLogy zile....ah nimepoteza Track ya nilichokuwa nazungumzia.....Hebu nikumbushe!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 2 September 2014

Nguvu ya Mama....

Sio aliekuzaa bali uliezaa nae (Mwanaume) na wewe Mkimama mwenye mtoto au watoto.
Embu ngoja kwanza!!....Mama aliekuzaa ndio chanzo cha ninachotaka kusema hapa siku hii ya leo.
Nilibahatika kulelewa kwenye Mazingira ya Imani Kuu Mbili za Dini (Wazazi walikuwa na Imani tofauti za Dini), hali ambayo ilitufanya watoto kuwa na Dini ya Baba mpaka tulipofikisha Umri wa Miaka 18!!!

Aiii.....angalau tulikuwa na kitu cha ku-look forward to....errr 18th birthday na 1st Key for your own house au kuanza kulipa Kodi ya chumba unacholala hapo kwenu (nisikuchanganye na mambo ya Ulayani).

Kabla ya Miaka 18 sote tukahamia Dini ya Mama...Mzee akabaki peke yake na Dini yake masikini.....hapo ndio "nguvu" ya mama inapokuja sasa.

Mama akiamua watoto wasitambue baadhi ya Ndugu anaweza kufanya hivyo kirahisi kabisa na kufanikiwa.

Mama akiamua kumkufanya mtoto amchukie Baba yake anaweza kufanya hivyo like pie!
Mama akiamua kukuambia au asikuambie ukweli kuhusu Baba yako halisi anaweza kufanya hivyo pia.
Kitu muhimu ambacho wanaume hawajui au wanasahau ni kutambua kuwa unapofanya Ngono bila Kinga na Mwanamke kushika Mimba, unakuwa umempa "POWER" juu ya mtoto atakaezaliwa, Maisha yako na Bank account yako (kwa wa mbele).

Nawee mwanamke utambue kuwa unaposhika Mimba uzembe ni wako kwasababu unamamlaka na Mwili wako (wacha mambo ya Mimba yake BS) ila wakati huohuo unakuwa umepewa "POWER" juu ya Mwanao hivyo itumie vizuri kwa Manufaa ya Mwanao.


Ni watoto wachache sana ambao huegemea upande wa Baba zao na most ni kwababu ya "pesa" au Tamaa ya maisha fulani.

Nawapenda wazazi wangu wote na nilikuwa "dad's girl", ila namsikiliza na kumuamini Mama yangu zaidi. Sina hakika kama hii inauhusiano na ku-share damu na mama kwa Miezi 9?!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 1 September 2014

Raha ya Tako Kubwa kutikisika...

Sanaaa ila sio kila siku though!


Kuna siku mwanamke unahisi hitaji la "kikaza" Maungo huko nyuma katikati....maana mtikisiko unazidi kiwango cha kawaida(au ni mimi tu?!!).


Kwa wale ambao hatukujaaliwa "Choo" huwa hatuvai "kyupi" ili kuongeza "mtetemeko".....lakini waaapi bana, kitako kigumuuu ka' Jiwe.....ila angalau halipo. Sasa usiombe uwe umebebeshwa "lichoo" halafu halitikisiki!!
Au linaenda Ti------Ti-----Ti badala ya "SingidaDododoma-SingidaDodoma"

Anyway! Kama wewe huna "Litako" na ungependa mtikisiko time to time (pale unataka attention) bila kubadilisha mwendo na kuendelea kuvaa "kyupi" yako.....Hongera sana kwa kuichagua Blog hii hihihihi!

Unapotembea mbele ya "mhusika" achia sehemu ya Haja kubwa kama Vile unataka "Kushusha Mzigo".....Hakika tumbo lako liposawa maana.....!!!
And oh....unafanya hivyo ukimkaribia Mlengwa, sio Siku nzima...utajaza mahewa tumboni!!

Babai.
Mapendo tele kwako...