Sunday, 30 August 2015

Usenge + Ubunifu wa Mavazi=Skinny Models


Unaamini katika Chunguzi za Kisayansi? Mie naamini zile za Kitibabu(ambazo ni Sayansi pia.....kabla hujanijaji, tambua kuwa kuna Sayansi za aina nyingi....Viumbe,Mimea,Siasa,Kemikali n.k). Natumaini wewe ni mzima kabisa.

Kama ujuavyo suala la Waonyesha mavazi/Wanamitindo kuwa Size Sufuri ni pana na mpaka likaingizwa kwenye Siasa(likafeli). Lakini bado hawa wafanya biashara watumiao Miili yao kuonyesha mavazi(Models/Wanamitindo) wanaandamwa kutokana na wembamba wao.Baadhi ya watu "mtaani" wanadai kuwa Wabunifu wanachagua "unreal women" kwasababu wao(most of them) ni Mikorosho/Wasenge na hivyo nguo wanazobuni ni za kutosha Wavulana na sio Wanawake......Unabisha?, endelea kusoma sasa.
Kiasilia Mwanaume anaevutiwa na kupendeza kwa mwanamke atazingatia Umbile la Mwanamke, kwamba juu Mdogo halafu chini mkubwa/pana(Peasi)  au Juu mkubwa , kati mdogo halafu chini mkubwa pia(namba nane)....tuliobaki ni WAVULANA hihihihihi.
Sasa kwa Msenge ambae ni Mbunifu hakika kinachomvutia yeye ni Mwanaume mwenzie sio, na kama ilivyo kwa Wanaume wengi, wanapendezwa na "wenza" wadogo zaidi yao so hii ya Wabunifu kutengeneza Nguo za kutosha Wavulana(13-19yrs) inaleta maana.
Nimetoka kusoma Chunguzi kuhusu Wanaume wanapenda wanawake Wembamba kwasababu wanaonekana Vijana na hivyo uwezo wao wa Kuzaa(umri wako ndio Umri wa Mayai yako). Nikajifunza jambo na ndio maana nime-share nawe.


Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.

Wednesday, 26 August 2015

Kuoga Usiku Vs Asubuhi/Mchana!


Haiyaaa!

Kiangazi Kimeisha na Mvua ime-cotton fire, hii sio sababu ya wewe kuacha kuoga. Usafi wa Mwili ni muhimu kama vilivyo vitu vingine Maishani. Lakini je wewe unaoga mara ngapi kwa Siku? na je kuna ulazima wa kuoga zaidi ya mara moja kwa Siku?


Wanawake tunapewa/peana PRESHA kuoga-oga  mara nyingi na tunaambiwa tusipooga tunatoa harufu kwa sababu ya Maumbile yetu, lakini wanasahau kuwa kunakosababisha harufu sio mwili as in Ngozi, bali kwapa na kunako(Nyeti) ambazo hata wanaume wanazo na zinatema harufu pia ikiwa hazitaoshwa.


Sasa nikianzia mwisho, hakika kuna ulazima wa kuoga zaidi ya mara Moja kwa siku, Inategemea unafanya kazi gani na wapi, unatumia Usafiri gani(kubanana  kwenye daladala/train hakika unabeba wadudu) na bila kusahau hali ya hewa. Ikiwa unafanya kazi Hospitali(una deal na maambukizo), unaishi mahali penye joto sana au kazi yako inakufanya utoke jasho sana mpaka unanata basi wewe oga mara zote unazohitaji.

Kitibabu tunapaswa kuoga angalau mara Nne kwa Wiki, hii ni kuisaidia Ngozi kutunza Mafuta yake asili na hivyo kuwa na afya njema. Pia inasemekana kuwa Kuoga mara nyingi kwa siku kwa kutumia Sabuni kunaongeza uharibifu wa Ngozi kutokana na matumizi ya Sabuni(Kemikali).

Nikijibu swali la pili, Mimi naoga Mara moja kwa siku(siku saba za Wiki), na ni  Usiku tu (nitakuambia kwanini as we go along)......nimezaliwa na Kukulia Dar es Salaam hivyo kuoga mara TATU/Nne kwasiku  ilikuwa ni kawaida(baada ya Kubalehe). Kabla ya hapo nilikuwa naoga/ogeshwa Jioni tu.


Nimeamua kuoga Mara moja kwa Siku baada ya Kuwa mama(sina Muda)......unakumbuka Enzi zile(au ni mie tu) ukiamka asubuhi unasafisha Kinywa, Uso, kwapa na Sirini(kuchamba) halafu unamalizia kulowesha Miguu ili kuwezesha Mafuta ya Rays ku-apply vema? Hii ilisaidia kuokoa Muda wa Baba/Mama (hasa kama mmpo wengi) na wote mnatakiwa kutoka kwenda Shule pale Baba/Mama anapotoka kwenda Kazini au kabla.Sababu za Mimi kuoga Usiku tu(kama unajali):-

1)-Ni muhimu kuosha matatizo na vumbi/mioshi(hali ya hewa Chafu) yote ya siku nzima kabla ya kwenda kulala.

2)-Ngozi inajitengeneza/tibu vizuri ikiwa safi na unapokuwa umelala.

3)-Ni muhimu kuneng'enuka mwili ukiwa msafi/fresh(una harufu yake asilia).Mara zote mwili (weka pembeni Uso, Kwapa na Nyeti) huwa hauchafuki kama unavyofikiria, hata unapokuwa Hedhini(mwanamke) au umefanya Ngono(wake kwa waume) huitaji kuoga Mwili mzima isipokuwa unasafisha pale panapohitaji kusafishwa.Tambua nathamini ushirikiano wako, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Nikuache sasa, Babai.

Thursday, 20 August 2015

Kwa Mliojipiga/Lipua/Fuata Sheria Ughaibuni....


....yote Maisha na kila mtu anayatafuta kwa namna yake sio(usidhani nakukebehi, naelewa sana). Sasa kama ilivyokawaida ya Mie, ninapohisi kuwa nimejifunza huwa sio mchoyo ku-share. Hujambo lakini?
Unafurahia simu yakoo Mpya(smartphone) ambayo ipo loaded na ma-Apps mwengine wala hujui kazi yake(unadhani yanafanya Simu yako kufanya kazi vema) kumbe katika hali halisi sivyo. Baadhi ya Apps(zile zinazowekwa kila unapo Update Software) huwa zinawekwa na Mitandao husika ili kufuatilia Nyendo zako.
Tangu zamani wamekuwa wakifuatilia ili kuboresha Huduma za Mawasiliano, lakini kutokana na uwingi wa Uovu hasa kutoka kwa wenzetu wale Wauaji kwa jina la Dini yao takatifu, hali imekuwa mbaya linapokuja suala la "privacy".Sio Kampuni za Simu tu ndio zinatabia(banwa Kishria) bali pia Facebook, Google na Whassap wanatabia ya kutunza yote unayo-post kwa ajili ya "kuboresha" Huduma zao (wanamaanisha kutunza Data uwekazo kama Ushahidi pale  mambo yamebuna na Serikali/Polisi wanazitaka).
Umewahi kuiona Application kwenye simu yako inaitwa Computrace Agent? well pengine wala huna habari kwasababu sio mtu unaependa kujifunza nini kinafanya nini na kwanini? sasa CA inaku-monitor wewe na yote usemayo ufanyayo unapokuwa kwako au mahali popote uendako(so long unabeba simu yako).
Hii Computace Agent App haitoki hata ufanye nini? na wala usijipe Moyo kwa kusema "natumia simu hii lakini namba ya whassap sio namba ya Mtandao wa Simu hii"......muhimu ni Device sio namba ya Simu.
Haya endelea kujiachia na ndugu zako wa Kibongo waliopo Bongo huku mnabadilishana mapicha ya kihistoria(utotoni), au...au...ulienda kumtembelea Rafiki yako Bongo baada ya yeye kukualika huko (kumbe ulienda kwenu) wakati Serikali inakutambua wewe kama Msomali, Mrwanda, Mzanzibari, Mkongo, Mrundi, Mmisri au kutoka kokote kwenye Machafuko Kisiasa na huna Ndugu aliyebaki(wote waliuwawa hihihihihi).....akili kichwani mwako.
Mie binafsi nafurahia Teknolojia hii kwasababu napenda  na kujali Usalama wangu na Familia yangu (si wajua mambo ya kutekwa, kupotea, kuibiwa n.k), hii App na nyingine kama hii ni muhimu sna Maishani, Ila kwako wewe inaeza kukuletea mwisho wa kuishi Ughaibuni.


oh hey....nakupenda kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Wednesday, 19 August 2015

Pale unapokuwa Mke mwema....


....halafu unaonekana sio mwanamke "kamili", kwanini? kwasababu hulalamini-lalamiki pale mumeo anapoacha bafu chafu baada ya kuoga au pengine anachelewa kuamka na kuacha kitanda kipo shagala bagala....(hizi sio kazi za mwanamke ni usafi), huombi-ombi pesa ya manunuzi, Vipodozi wala Salon.

Inawezekana upo hivyo kutokana na Malezi/mafunzo uliyopitia au huenda umejifunza kupitia Blogs, maana Siku hizi kuna kila aina ya maelezo yanayotuelekeza namna ya kuwa  Wake(na waume) wema, mengine ni mazuri na mengine yanapotosha.....Akili kumkichwa unapoamua kuchukua na  kujaribu ulichokisoma!

Ulalamishi na kutaka jambo/kitu kifanyike pale tunapotaka  ndio  inatufanya wanawake kuwa wanawake (ni sehemu ya uanamke), sasa hayo yakikosekana inakuwa kama vile Mumeo ameoa  mwanaume mwenzie ahahahaha. I mean sawa kujitegemea kiuchumi na kuepuka ulalamishi.....lakini pia tukumbuke kuwa baadhi ya Wanaume hupenda Changamoto Ndoani (sio za kugombana na muumizana mioyo/hisia)!

Natambua kuwa unajua kuwa Changamoto kwenye Ndoa zipo za aina  nyingi na zinatofautiana, nitakupa mifano(kama kawaida) kuna zile zinamsaidia kufanya maamuzi ya Busara kwa ajili ya Familia  yenu, zipo zinazomsaidia/msukuma kuwa Msafi/kuwa na Manners, pia kuna ambazo zinamfanya ajisikie MwanaMume(ridhisha ego yake), kuna za Asili(Magonjwa) na kuna zile za kuangamizi Ndoa yenu.
Sijui utakubaliana au kutokubaliana na lipi hapa! ila kama umesoma mpaka mstari huu na umepata hisia ya kutaka kujibu/comment kwa Hasi au Chaya basi tambua kuwa umekuwa inspayadi.


babai.

Tuesday, 18 August 2015

Urijali/Uanaume Kamili/wa Kweli!


.....hapa lazma nivabe! Lakini kwasababu napenda kuchangia "knowledge" sio mbaya nikikuelezea nilichojifunza. Inawezekana kabisa hukubaliani na ninachotaka kuandika, basi angalau nipe nafasi na unisikilize(soma na share....ahsante).
Unajua pale unaanzisha Topic halafu watu wanaivamia na kuaanza Malumbano (ya busara) halafu wewe upo pembeni unafurahia huku  unachukua "Material", basi ndivyo ilivyokuwa.
Wengi tunaamini(mie mmoja wao mpaka Wiki Majuzi) kuwa Mwanume Rijal/Kamilii ni yule mwenye Uwezo wa Kusimamisha Uume kwa muda Mrefu au mwenye uwezo wa Kusimama na kufanya mapenzi na kufanikiwa kummimba mwanamke.

Baadhi hudhani kuwa Wasenge sio Marijali kwasababu hawapendi wanawake aka hawawezi kuingia ukeni sababu hawawezi kuinuka(Hanithi).....kama Kusimamisha kwa muda mrefu ni Urijali basi hawa  majamaa ni MARIJALI haswa!! Achana na hili.

Sehemu ndogo wanaamini kuwa kama Mwanaume  ni Rijali mwanamke mmoja hamtoshi....daah! Ujinga Mzigo. Hawa wanachanganya Uwezo mkubwa wa Kungonoka na Uwezo wa Kusimamisha in which vyote sio Urijali.

Urijali ni Uwezo wa Mwanaume kufanya mambo ya Kiume kwa maana ya Kiume, Mwanaume Rijali anajua Majukumu yake na anaheshimu nafasi yake kama mwanaume kwenye Familia yake, haogopi kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya watu muhimu maishani mwake(Mke na watoto), yupo tayari kufanya lolote kwa yule ampendae, sio rahisi kushawishika, anajua kuushinda Moyo/tamaa zake, anajua thamani ya mwanamke(sababu kazaliwa na mwanamke).
Sasa  Urijali sio Uwezo wa kufanya Ngono kwa Muda mrefu, Kuzaa watoto wengi kila kona ya Mtaa au kufanya Ngono mara nyingi kwa Siku na sio ile hali ya kumtamani mwanamke au kutamani utupu wake. Kumbe Urijali hauna uhusiano na Uwezo wa Kusimamisha na kutoa Manii.


Urijali ni kuwa Mwanaume Kamili/wa Kweli. Haya ndio nimejifunza kutoka kwa Wanaume Watu wazima wa Kitanzania nilipokuwa Likizo. Iwe hukubaliani au unakubaliana nao. Tambua umekuwa "Inspayadi" hivyo basi nenda kaanzishe Blog uweke Maoni yako....hah!


Ahsante kwa kuchagua Blog hii.


Babai.

Sunday, 16 August 2015

Knowledge vs Ego....


Kwa maCeleb Ego hujionyesha wazi kwenye mahojiano ya moja kwa moja. Baadhi wanadhani kuwa ni wao tu ndio wanazo hizo Ego, nitakupa mfano na pengine kukusaidia(kama hujui) kuitambua kutoka kwa Mwenza wako.

Kwa mimi na wewe Ego zetu hujitokeza zaidi pale tunapogombana. Ndoani/Mahusiano huwa tunagombana sana eti? Wakati mwingine ugomvi unakuwa hauna hata maana.


Ujue kuna ile kugombana kwasababu mmoja wenu kafanya kosa kubwa kama vile umegundua kuwa amekuwa akipeleka Pesa mahali ambapo hupajui! Kwa mfano. Sio kwanini hakupokea simu?!!


Na ikiwa mnawatoto basi mnaweza kugombana kwasababu mmoja wenu anahisi kuwa anaingiliwa kwenye kona yake ya malezi(wanaume) au mwingine(sisi wakimama) kuhisi kuwa watoto wanaonewa au mwenzio hatoi muda kuwaelewa watoto na badala yake anatanguliza kufoka (hasira) kwa watoto.


Katika hali halisi kama mmoja wenu anawakilisha linalomkwaza kwa namna ya kawaida(kukereka bila hasira/kufoka) na mwingine kusikiliza hakutokuwa na ugomvi. Inaitwa MAWASILIANO/KUWASILIANA.


Lakini kwa sababu ya Ego kubwa (kujiamini kupita kiasi/kiburi) au ndogo(kutojiamini/kujishtukia)ya wenzetu wa Jinsia ya Kiume kunasababisha issue ndogo kuwa kubwa.

Kwanini inakuwa kubwa? Kwasababu wanawake tunapenda kuongea na kuelezea kila kitu(mie), wakati wenzetu hawapendi kusikiliza na matokeo yake utaambiwa "yameisha, sitaki kusikia/ongelea hii issue tena" wakati hatujamaliza. Au anakuvuta na kukubusu au kufanya Mapenzi matamu ya ki-Ego hehehehe  ili tu usiendelee kumwaga manoleji.


Sasa kwasababu hujamaliza ni wazi kuwa issue itakuwa inaning'inia na itakukera kwa muda wa siku 3 kama sio Wiki nzima....kwanini amekukatisha?  Kwanini hataki kuimaliza issue na mfikie  mafaka? Well sababu ya Ego yake.


Kwa Weusi Ego huenda juu kupita maana ya juu kwasababu wanaume wa Kiafrika hawapendi kufunzwa au kuelekezwa na Wanawakee......ikiwa mwanamke anaelekeza basi utaambiwa huna heshima au unajifanya unajua wakati hujui kitu(kwasababu tu wewe ni mkimama).


Kisayansi, Wanawake tunakua kiakili haraka kuliko wenzetu na wepesi kujifunza na wazuri kutunza info (za maana na makorokoco)kuliko wanaume. Pia tunafunzwa au tunapata uzoefu wa kimaisha kama sehemu ya kufunzwa, tofauti na wanaume ambao huachwa wajifunze wenyewe. Hivyo ukweli ni kuwa sisi tuna knowledge kuu zaidi ya wanaume(inategemea na umri/elimu though).


Sasa unafanya nini ikitokea Ego ya mwenza wako ipo juu zaidi ya Masikio yake? Well akianza kuja juu wewe Msikilize halafu dharau. Siku akitulia ibua issue kwa upole na muimalize.


Ukijibu ni wazi mtakuwa mnajibizana na hakutokuwa na mtu anaemsikiliza mwenzie na matokeo yake mnaishia kuwa na mahasira ambayo hawasaidii.


Sasa Imagine mmoja wenu anarudisha namba(anakufa) baada ya ugomvi wa kijinga unaohusisha ego zaidi ya Uelevu? Anakufa bila muafaka......Ze hatia sasa!
Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.

Friday, 14 August 2015

Ngono ya Usiku mmoja M'ke vs M'me.......nani Malaya? Hello there.


Kwenye harakati za Mpito za Ujana ni wazi unajifunza kwa kufanya mambo mengi kwa kupatia au kukosea. Sio mara zote unakosea ili kujifunza(usifanye makosa makusudi kwa kisingizo cha kujifunza), wakati mwingine unakosea kwa Uzembe(kutokujali).

Kama ilivyo kwenye kila kipindi cha  " Mpito" mambo huwa magumu.....wakati mwingine mtu unajikuta unakata tamaa na kuamua kuwa LIWALO NA LIWE na hapo ndio maamuzi ya kizembe yanapojitokeza. Inaweza kuwa Pombe au Utumiaji wa madawa na Ngono Holela au vyote.
Inawezekana kabisa kufanya hayo ni katika hali ya kutafuta "amani" au kuondoa "msongamano wa mawazo" na pengine ku-fit in na jamii inayokuzunguuka wakati huo wa Ujana wako. Kwaharaka haraka unaweza kudhani umepata "tiba" lakini katika hali halisi unajiongezea shida/majukumu kabla ya Muda wako.
Sasa, kutokana na hali ilivyo siku hizi (Mambo ya Haki sawa sijui Usawa) inafanya mambo mengi ambayo awali yalifanywa na baadhi ya Wanaume tu sasa hufanyika kwa urahisi  kwa upande wetu wakimama ( hello Feminist).....ni vema kwenye masuala ya Kikazi, Kipato, Kielimu na Heshima. Linapokuja suala la Ngono ya USIKU MMOJA ondoa imani/msemo kuwa "kama Mwanaume anaweza hata Mwanamke anaweza".


Pamoja na Ulevu wangu  wote(mdogo) kwenye suala la Usawa, ikiwa wewe ni mwanamke huwezi kujifananisha na Mwanaume linapokuja suala la Umalaya. Huna haja ya ku-justfy Umalaya wako kwa kusema " mie mwanamke Malaya, lakini Mwanaume Player".....kama umeamua kuwa Malaya fanya hivyo kwasababu zako nyingine na sio "Usawa"!!

Unataka nikuambie kwanini? well....kwa kifupi ni kuwa Wanaume na Wanawake tumetofautiana Kimaumbile(kama ulikuwa hujui), Mwanaume hazai, wewe unazaa, mwanaume akifanya ngono na wewe akioga unakuwa umetoka mwilini mwake(kwenye ngozi ya uume wake), lakini wewe utaendelea kuwa na mwanaume huyo kwa namna mbili tofauti Moja zaidi ya Siku tatu (kama hukutumia Condom) na Pili, ni kwa kati ya mwezi mpaka miezi 3(kwa Uke wako kujirudi), ikiwa Umbile lake lilikuwa kubwa.

Nikuambie pia Kiimoshino na Kisaikolojia?....aii nafasi imejaa, hebu Kaguge.


Nisikuchoshe

Babai.

Monday, 10 August 2015

Weusi wa Ngozi sio Uchafu........ila usipokuwa muangalifu kwenye kuchagua Rangi za Mavazi/Nywele hakika utaonekana Mchafu(huvutii), hii  haina kujiamini.....nadhani ni muhimu kuchagua Rangi zinazoendana na Rangi ya Ngozi  yako.Mambo?!!
Kuna siku nipo na mishughuliko yangu ya ndani wakati Asali wa Moyo anatazama Mashindano ya Tenesi ya Wibledoni. Anapendezwa sana na wale Williams Dadaz....mmoja wao alikuwa anacheza. Mwenyewe anafurahia uchezaji wake (au kuona Tako  kila kisketi chake kinapoinuka hihihihi maana mdada mMashallah).

Sina hili wala lile nasikia mwenznagu anawasifia wadada Williams kwa kutokuwa kama Celebs wengine.....mie nkasema hao sio ma-Celeb ni Sports Stars (kwa Kiswahili ndio tunasemaje vile?) ila Media inalazimisha kuwaweka kwenye Kundi la M-aceleb kitu ambacho sio haki kwasababu wapo walipo kutokana na kazi/kujituma kwaoo na sio kuonekana kwenye Tv au kuuza Haidthi kwenye magazeti au....oh well kwa Umalaya.

Katika kufunga maelezo yangu nikamalizia na....kiukweli mie siwaelewi kwanini hawa wadada, wanamahela lakini wanaonekana kama wachafu?......Nikaambiwa na asali wamoyo tena kwa kung'aka...."Usikufuru Dinah, unadhani wao waliomba kuumbwa hivyo?"....alaa!!

Nilichogusia sio Rangi zao bali muonekano wao kwa maana ya Mitindo na Urembo.....huenda ni Rangi ya nguo wanazochagua/vaa wakiwa nje ya Michezo yao, au pengine mitindo na rangi  ya Nywele/Wings inafanya waonekana kama Wachafu.

Nikupe Mfano....kuna yule mnamuita  Super Model "legend" Fiderine Iranga halafu kuna Super Model Flaviana Matata (in my head she is Top SuperModel). Wote ni Weusi sana lakini mmoja anaonekana kama vile Mchafu.....sio kwamba haogi la hasha! bali uvaaji( Rangi za nguo/Wigs) na Urembo ndio vinafanya aonekane hivyo nilivyosema (kwenye Picha).Daaah!.,,,wiki iliyofuata si ndio Nkaumwa Tetekuwanga hihihihihi mwee. Gotta stop Jajing'i.


Babai.

Sunday, 9 August 2015

Je Unaogopa Kujaji watu(wenzio)?


Habari yako?


Nilikuwa Likizo ya Kiangazi.....katika hali halisi  nilipaswa kukujulisha lakini nikahisi kama vile nitakuwa najionyesha au napitiliza ku-share so nikapiga kimya. Anyway habari kwa ufup,  kama bado unajali ni kwamba Madoa ya Tetekuwanga(Chickenpox) yamepungua Weusi.
Ujisedhani hali ya Hewa ya UK inafanya Ngozi kutakata haraka ndugu, nilipewa Mkorogo(andikiwa dawa ya kuondoa Weusi) nitumie kwa Muda wa Wiki 8. Baada ya kugusa Wiki ya Pili nikaona Vijitundu vya ngozi(pores) vinapanuka! Aiiii nikautupilia mbali Mkorogo.Duania ya leo inamengi na kila kukicha tunaongezewa sheria za namna ya Kuishi vizuri au kuishi na watu kwenye jamii. Tunaambiwa tusiwajaji wenzetu kitu ambacho sio rahisi kwa sababu kujaji ni asili ya  mwanadamu, pia bila kujaji hakika utakuwa unafanya maamuzi mambovu na hivyo kuishi ukilalama "kwanini mimi".
Nimekwishawahi kukuambia hapa(kwenye blog hii) kuwa mie huwa najaji watu/mtu kama wewe ila tofauti yangu mimi na wewe(hello hihihihi) ni kuwa, huwa najitahidi kuelewa na kukubali kwanini wapo walivyo au kwanini wanafanya wafanyavyo nikishindwa naishia na "but why?". Sina tabia ya kumchukia mtu au kumcheka ama kumdharau kwasababu nimepitisha "jajimenti" kutokana na muonekano wake au matendo yake mabaya ya awali ama Ugonjwa/matatizo yake kiafya.Nina uhakika kabisa sio Mimi tu ambae najaji watu ama vitu na pengine vitendo vya mtu kabla sijamjua/fahamu......naamini wewe pia unajaji kabla hujafanya uamuzi wa Kurafikiana  na mtu au kununua Kiwanja au nyumba na pengine Bidhaa fulani kwa ajaili ya matumizi binafsi au ya familia.

Sasa unaposhupaa kuwaambia wenzio kuwa "msinijaji mpaka mnijue kwanza" unakosea.....kwasababu hakuna mtu ana muda wa kusubiri akujue kwanza halafu apitishe "jajimenti".....mfano mdogo ni pale Mabinti wanapogombania kuwa ma-Miss, pamoja na vigezo vinavyowekwa bado unakuwa "judged" na Jamii  kabla hawajapata nafasi ya kukujua(via magazeti ya Udaku).

Nukta ni kwamba usiogope kujaji kwasababu ni "human nature" wakati mwingine huwezi kujizuia kwasababu kuna poster zinasema "dont judge me before you know me" sijui "nenda kafanye kazi badala ya kunijaji".....wakati unajaji unakuwa njiani kwenda Job. Babai.