Thursday, 24 September 2015

Siri ya Mtoto wa Kwanza, Kati na Mwisho....Inawezekana Ndugu zako wanaokufuata au uliowakuta(inategemea umezaliwa wa ngapi) sio Damu  moja kwamba  baba na mama yenu ni mmoja. Umewahi kujiuliza kwanini mtu anaendelea kuzaa na mume/mke ambae anamtenda(tereza nje)? au Utakuta Ndoa inamatatizo lakini wanazaa tu kila mwaka....haikuhusu lakini kama Binaadam kiasilia hatuishi Kudadisi na Kujaji.

Kiasili Watoto tunadhania kuwa Mama zetu ni "Malaika" lakini bwana mwanamke akiamua kushenzika anakuwa Mshenzi zaidi ya Shetwani, tofauti ni kwamba Wanawake ni wazuri kwenye kuficha siri zao. Akitaka usijue Baba yako ni nani basi hutokaa umjue......akikuaminisha kuwa fulani ni Baba yako basi itakuwa hivyo(ukidai DNA unapewa Radhi hihihihihi).


Mtoto wa Kwanza:
Binti yupo na anaempenda lakini Wazazi hawamtaki Jamaa aoe.....wanataka aolewe na mtu wao. Binti anaolewa na mimba yake bila muoaji kujua. Pia Binti anaweza kuwa anaendelea na ampendae ili azae nae batoto atakaowapenda kama baba yao, kuliko kuzaa na limtu alililochaguliwa na Wazazi wake.


Au binti alikuwa mapepe na matokeo yake hajui Mimba ilisababishwa na nani hivyo anatoa taharifa kwa yule ambae anajua atafaidika kwa namna moja au nyingine.....jamaa akikubali ndio anakuwa baba mtoto.Pia kuna Jadi za Makabila fulani (unayajua) Baba anamfungua Binti yake kabla ya Mumewe, so akishika Mimba anamzaa Mdogo wake huku Mume mtu anajua yeye ni Dume la Nguvu....kagusa tu kitu na Box, kumbe analea Shemeji.Mtoto wa Kati:

Baada ya watoto kadhaa mama anaamua kupumzika, anaanza kufurahia maisha kama mwanamke. Majamaa wanaanza kutoa attetion ambazo mumewe hazitoi(Mume anamuona Mkewe mama wa watoto wake na sio Mpenzi tena).....mama anajiona "kumbe bado wamo". Anatereza.....mara oops baby! Mnakaribisha mtoto mpya kwenye familia yenu bila kuhoji.Mtoto wa Mwisho(hasa kama mpo zaidi ya 4):
Mara nyingi  Mtoto huyu huwa wa Hasira au kulipiza Kisasi baada ya kugundua kuwa Mumeo alizaaga kabla hamjakutana na hakukuambia au umegundua kuwa aliterezaga sometime Kitambo, kwa hasira unaamua kuneng'enuka Nje. Utu uzima unaanza kubisha Hodi, uhusiano unaanza kuwa na changamoto zilizo nje ya Uwezo wa Kibinaadamu(matatizo ya kiafya)....Mwanamke anahisi kavumilia vya kutosha na sasa anabwaga manyanga, lakini hataki uteseke hivyo anaendelea kuwa Ndoani lakini Mengi anafanya huko nje. Mara majikuta mnatarajia mtoto, bila kuhoji unajiona Dume la mbegu. Usitumie maelezo haya ukijifanya Mtaalamu, ni maoni yangu Binafsi kuhusu nafasi hizo za kuzaliwa. Naheshimu na kuthamini muda wako, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.


Babai.

Tuesday, 22 September 2015

Mtoto mwenye Utindio wa Ubongo(Tahaira).....Uzoefu wangu!


Kama mwanamke niliechelewa Kuzaa inaaminika kuwa uwezekano wa kuzaa Mtoto mwenye Utindio wa Ubongo(Downs-syndrome) ni Mkubwa. Kama kawaida nilikuwa "offered" kufanya Vipimo kuanzia Wiki ya 14 halafu tena Wiki ya 20. Mie kama mie nikakubali offer nikiamini aah mie Mwafrika bwana(Waafrika wanazaa watoto wenye afya past 50yrs, ndio itakuwa mimi wa miaka 30na?)!!


Kibibi na Babuu...


Wiki ya 14 tuliambiwa hakuna dalili yeyote kuwa mtoto anatatizo, inaonyesha anakuwa vizuri na ni active. Tulipofika Wiki ya 20 habari ikabadilika tukaambiwa Mtoto ni Mdogo kuliko Umri wa Mimba hivyo turudi baada ya Wiki Mbili. Wiki 22 hakukuwa  na Mabadiliko, so tukaambiwa turudi tena baada ya Wiki 4 wakaona "dark spot" kwenye Ubongo wa Mtoto kwa Nyuma.....Hofu ikaongezeka kati ya Madaktari na Wachunguzi.....wakaitana kufanya Mkutano.Mara wakaja na kuomba waangalie tena Mtoto(Scan)....mwanamke nikajiweka Kitandani huku namuomba Mungu wangu abadilishe wanachokiona......walipomaliza wakaenda kujadili tena. Mie naendelea kusali tu bana, wakarudi wakasema ile "dark spot" inaashiria kuwa Mtoto anaweza kuzaliwa downs-syndrome lakini ili wajue kwa uhakika  ni vema nikubali kufanyiwa Uchunguzi wa kina ili nijue kama Mtoto ni Tahaira au ni wa Kawaida.Aiii baada ya kuambiwa risks mwanamke nikawatolea nje, Pamoja na kuwatolea nje bado nilibaki kwenye HIGHEST RISK.....sasa kwani waliniacha? Nikabadilishiwa utaratibu wa Clinic, badala ya kwenda kila baada ya Wiki 4, nikawa naonwa kila Baada ya Wiki Mbili tena sio kwa  Mkunga(Midwife) bali "Specialists" (na Medical Reseach Docs) Hospitalini.Tukafika Miezi Nane na(Wiki 36), mwanamke nikawa nachukia kwenda Hospitali mara kibao halafu kila nikienda nafanyiwa Scan na wanashupalia palepale kuwa Mtoto hakui kama Umri wa Mimba, na je nina uhakika sitaki kabisa kujua kama Mtoto ana Utindio wa Ubongo.....nikawaambia nina uhakika na sibadilishi mawazo Ng'odo!Wakaanza nipa Lecture ya haw difficult kuishi na mtoto mwenye matatizo wanayodhani mwanangu anayo, nikawaambia yaani mpaka nimefika Miezi Nane bado mnataka nifanya kipimo ambacho kinaweza nipotezea mtoto?
Nikawaambia (huku nalia) sikilizeni Docs, Mimi naamini Mungu, sasa kama Mungu ametaka nizae mtoto mwenye Ulemavu wa Ubongo, hakika atanipa Nguvu na Uwezo wa Kumtunza na kumlea mwanangu. Nikaomba kuhudumiwa na Doc moja na Mtu wa Scan....sitaki Madaktari Wachunguzi. Wakanipa Kamaratazi ni Saini kuwa nimekataa katakata kufanya Vipimo zaidi.Asali wa Moyo akauliza, kama kuna chochote tunaweza kufanya ili kuongeza speed ya mtoto kukua? Docs wakasema hakuna! Nikajisemea hamnijui nyie.....kuanzia siku ile mwanamke nikaanza kula mamboga-mboga, manyama, masamaki, Mayai kwa fujo ya ajabu......Wiki ya 38 tukarudi tena, Scan ikaonyesha Mtoto anakuwa vizuri, urefu wa Mikono na Miguu upo sawia, Pua, paji la uso, macho yapo sawia, vidole vipo kamili.Scan Wiki ya 40, kila kitu kilikuwa safi na Mtoto kageuka tayari kuzaliwa lakini yeye Mtoto hakutaka kuja so wacha tusubiri.....Ujue Mimba ikifika Wiki 40 halafu huna dalili ya Uchungu uchovu unazidi? Uchungu unauma vibaya sana lakini unaulilia uje.
Binti yangu amezaliwa kwenye hallway ya Hospitali Wiki ya 41 na Siku Nne. Nakumbuka nili-share sehemu ya siku husika na uchungu-wa-kuzaa na kujizuia-usi-push. Kama kuongea sana kuliko Umri wake ni tatizo la Ubongo basi ndio kazaliwa nalo hihihihi she's just normal little girl.

Anyway, natumaini Uzoefu wangu utakusaidia  kwa namna moja au nyingine kufanya maamuzi yakinifu linapokuja suala la kukamilisha Uchunguzi za Kitibabu kuhusu  watu wa Asili yako (popote utokapo Africa) ili ku-save money. Kwasababu kutuma Madaktari Tanzania(kwa mfano)  kwa  miezi kadhaa ili kuchunguza matatizo ya watoto kabla hawajazaliwa ni Ghali mno. Sasa wakipata bahati kuna Weusi wa Kiafrika kutoka popote utakako wanachukua advantage.

Utasikiwa wanawake kutoka Nchi za Afrika Mashari wanaongoza kwa hili na lile, kumbe wamefanyia uchunguzi wanawake watatu tu waliopo UK, ze washenzi kabisa. Kuwa emotional vya kutosha na Mimba yako lakini usisahau akili yako.


Naheshimu na kuthamini muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.


Babai.

Monday, 21 September 2015

Tulionyimwa Komwe....Faida/Hasara zake!


Tufunge na kuomba kuwa na Komwe isijekuwa Fashion kama vile kuwa na Makalio Makubwa. Tutajificha wapi? wewe utakuwa unanyoa manywele yako Usoni ili uwe na Komwe?.....well mie huwa nanyoa katikati ya Nyusi (huwa zinatishia kukutana japo sio nyingi mnaita "fuzz") pia ili kutenganisha Nyusi  na "Mstari wa Nywele" huwa na Nyoa kati kati yake!

Pengine hujawahi kugundua kuwa "Hairline" yangu ipo chini hasa sehemu ya pembezoni(zoom time, usiote tu hihihihi). Umbali kutoka Nyusi kwenda kwenye Nywele ni Inchi Moja na Umbali kutoka kwenye Komwe(ambalo halipo) kwenda kwenye Nywele ni Inchi Mbili na Nusu.
Kuwa na "low hairline" kuna tofautiana kama ilivyo kwenye Makomwe, tofauti hizo zinafanya baadhi kutaka kuwa na Sura ndefu na hivyo kuondoa Nywele kwa kutumia Njia mbali mbali ili nywele zisirudi(tazama Picha).
Mie binafsi tayari ni ba Mdogo(sura ya kiume), sasa nikiachia Nyusi kuungana wajameni si nitasababisha mkanganyo even more(usicheke tafadhali)? Haya twende kwenye Faida za kunyimwa Komwe:-


 -Unatumia Bidhaa za kusafisha, Kuremba na kutunza Ngozi ya Uso kwa Muda mrefu (Uso mdogo) hivyo una-save mahela.


-Hupati Chunusi kwenye Komwe ambalo huna(Paji la Uso dogo).-Huitaji Hijabu(hahahha samahani) na ikiwa unaivaa basi inakaa vema zaidi kuliko yule mwenye Paji kuwa la Uso kubwa(Komwe).-Paji lako la Uso linaweza kuhesabika kuwa ni "la kawaida" kwa wale wanaoweka Viwango vya Uzuri wa Mwanamke(ze Washenzi)....kuwa na Komwe sio Kawaida na kuwa na Paji dogo sana huesabika kuwa sio "kawaida" aka Ulemavu(Nenda Kaguge ili ujue lako lina Inchi ngapi)!!
-Nyusi zako huwa na afya njema kwasababu zinapata Tiba yeyote ufanyayo ili Nywele zako zinawili, Deep Condition, Oiltreatment n.k.....Nani anafanya hayo kwenye Nyusi? ni Sisi tu, tena sio kwa kutaka bali inatokea tu Automatikali.


-Unapendeza zaidi ukivaa Wigs ambazo zimenyingonya(curl).
Hasara ya kutokuwa na Komwe:-

-Kila unaposafisha Uso lazima Nywele zioshwe pia, matokeo yake unakuwa na Nywele nyepesi sehemu ya mbele kwasababu zinapitiwa na chochote unachotumia kusafisha Usoni kila siku na mara zote unaposafisha uso(unatakiwa kuosha Nywele angalau mara Moja/mbili kwa Wiki).


-Unapotibu Nywele zako kwa Mafuta na ukalala nayo, mafuta hayakawii kuteremka  Usoni na matokeo yake unapata Chunusi za ghafla.


-Kunyoa kila baada ya Wiki ili kutenganisha Nyusi na Hairline.-Uvaa Wigs zilizonyooka(Straight) inaeza kuwa shughuli kutokelezea......unatokea kama vile Umevaa Hijabu yenye material ya "nywele".Babai.

Saturday, 19 September 2015

Wazungu wanajua Kupenda au wanaogopa kuonwa Wabaguzi?


Kama ulikuwa na Uzoefu mbaya na Wanaume/Wanawake wa Rangi yako hili ni Tatizo lako, na uzoefu wako mbaya haufanyi wanaume/wanawake wote wa jamii hiyo kutokujua Mapenzi/kupenda.
Linapokuja suala la kupenda kila "individual" anapenda kivyake kulingana na labda Ubora/viwango atakavyo/alivyojiwekea kutoka kwa mtu anaetaka kumpenda(well huwezi kutaka kupenda, penzi linaibukaga tu popote) na pengine ni kutaka kujaribu ili kuona wa rangi hii wapoje kama sio "attraction"(sio kila mtu anavutiwa na yeyote, wengine wanavutiwa na watu wa jamii/rangi fulani tu).


Ukiachilia mbali hayo hapo juu, pia Imani au "life situations" zinaweza kukufanya Ufunge ndoa na Mtu wa Taifa/Rangi nyingine (mostly Wazungu) ili kuboresha maisha Kiuchumi au kuapta Makazi ya Nchi fulani ambayo kutokana na Imani yako ni kuwa Utaishi maisha Bora zaidi.....au Status kama sio (hii haikuhusu wewe) kukimbia "Kacha" Maana wanawake Weusi wa Kijamaica au USA/Latino kwa DIRAMA akuuu hata mie ningeoa Mjapan(kama ningekuwa mKibaba)

Sasa unapokuwa unaishi na Mtu Mweupe kwenye Nchi ya Weupe ambapo kuna Ubaguzi dhidi ya watu wengine ambao sio Weupe, Wewe huna Uzoefu kwani umeletwa kutoka kwenye moja kati ya Nchi 54 za Afrika huko.  Mweupe wako lazima atajitahidi kutokuwa kama wenzake kwa sababu anakupenda wewe kama Mwanadamu na sio "weusi" wako.
Mweupe huyu atakuwa akiishi kwa tahadhali na kuwa makini kwa kila kitu anachokifanya au kinachofanywa na Jamii yake(Wazungu wenzake) ili usiumie. Wengine sio Wabaguzi lakini habit zao zinaweza kukufanya ujisikie kuwa unabaguliwa.

Hivyo ili kuepuka maumivu Mweupe huyu ataongeza "gestures" ambazo wewe utahisi au kudhani kuwa ni kupendwa au Mapenzi. Labda mweupe huyu anafanya mengi ili kuepuka kuonekana "mbaguzi" kwako(usijihisi Mtumwa) au Usimdhanie kuwa anaona Noma kuwa na wewe....ze puresha izi rili.

Itakuwa Ngumu kwa Mzungu wako kujadili issue zinazokugusa kwa karibu, Mfano Siasa.....utakubaliana nae au utampinga? Wengi wao wanajua kuwa Sisi Weusi ni Mabwege(well Viongozi wa Kiafrika).....ukikubaliana nae bila kumuweka sawa Utakuwa umeweka wazi Utumwa wako kwake.....Ukimpiga ni wazi malumbano yatakuwa Deeper na mwishowe utajihisi kama vile unabaguliwa.

Hebu fikiria, Mumeo/Mkeo wa Kizungu(kwa mfano) anakuambia "hebu niletee Chakula, badala ya yeye kwenda Jikoni na kujirekebishia chakula chake na Chako  na akimaliza asafishe vyombo vyote. Hakika unaenza kujihisi "Mtumwa".....lakini kama ni mweusi  hautojisikia Mtumwa wala nini, sana sana utamwambia "sema naomba"......sijui umenielewa?

Mzungu wako hawezi kukuacha ufanye kila kitu peke yako hata kama ni Mama wa nyumbani(unaangalia watoto) na yeye anafanya kazi(nje ya nyumbani), akitoka Job lazima atakusaidia kuweka watoto Kitandani n.k......hii sio kuwa anajua kupenda ila anaepuka usijione Mtumwa(in my head) hihihihihi.
Linapokuja suala la Kuneng'enuana(kuna watu wanapenda Ngono na Watumwa ujue, mambo ya kufungana kamba na kuzibana midomo, kuchapwa vibao/makofi...rafu sex eeeh.....sikuiti Mtumwa hihihihihi nachangamsha Genge  la wahuni).....Mzungu wako hapa anaweza kufanya mambo ya ajabu-ajabu wewe ukaona unapeeeeeendwa kuliko wale Weusi waliopita. Kumbe mwenzio anakuona Mtumwa....mambo yenu FANTASI.....kama hisia haziji FANTASAIZI TU.
Halafu kuna wale ambao wanapelekwa na Wazungu wao na hivyo kujikuta wanachukia kwao(wanaona aibu) wanakuwa Nazi(Ndani Weupe nje Weusi....au Kahawia?)....Anyway, nilitaka ku-blog kuhusu Mixed race kuwa "New Black", kwamba "none Mixed Black" hatuchangamki kama kizazi kipya cha " mixed race weusi" lakini nkabadili mawazo kwasababu Wasomaji wangu wengi mpo Afrika Mashariki na hamna uzoefu na kuwa "black" kwenye Nchi ya Wazungu.....so yeah!
Naheshimu Muda wako, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Tuesday, 15 September 2015

Mama wa Nyumbani kujipenda/pendeza.....Nani anakupa Ari?

Kwa sie Wafanyakazi huwa ni kawaida kushindia khanga/Pjs mwisho wa Wiki kwasababu tunatilia kila siku tuendapo kazini. Lakini je ikitokea umeamua kuwa Mama wa nyumbani kwa Muda(mie) utakuwa upo hivyo siku zote Saba za Wiki kwa Muda wote Mpaka mtoto aanze Shule?. Ni rahisi sana kujisahau na kupoteza "utambulisho" pale unapokuwa una-deal na watoto muda wote. Unafubaa, na ikiwa Nguo zako nyingi zilikuwa Office like ndio kabisaa(nani anavaa kiofisi wakati yupo nyumbani?).


Skinny Jeans nazo ni shughuli....!Hapo ndio kutafuta Ari kunajitokeza....ni vema kuwa/kupata/kupewa Ari(kuwa Ispired that is) kwa uHasi ama uChanya.....zote ni hisia na ukizipata pengine unaweza kuzitumia kufikisha ujumbe kwa watu wengine au ukaepuka na labda kujifunza kama sio kupata nafuu kuwa "aah am  not the only one then".

Mfano: Kuna Binti mmoja Maarufu ambae Kijamii anaonekana kuwa na Mwenendo mchafu na ni Mfano mbaya kwa Mabinti wengine ambao wanakuwa "ispayadi" na mambo ya kishenzi afanyayo. Binti huyo alitajwa kuwa ni Mmoja kati ya  Wananawake wanaowapa Ari mabinti wengine. Sasa wengi(mie mmoja wapo) waliona sio sahihi kwa Mtu mwenye tabia chafu kutoa Ari kwa watu wengine(hasa wadogo).....lakini tulisahau kuwa Ari inaweza kuwa Hasi au Chanya in which zote ni muhimu(hukua unalodhani litakusaidia, mengine mwachie mwenyewe).
Mtu huwezi kumtegemea mtu mwingine(sababu tu ni Kioo cha Jamii) ajibebe utakavyo wewe ili tu wanao wasijekuharibikiwa, wanao kuharibikiwa haina uhusiano na mtu mwingine bali wewe kama Mzazi na wao wenyewe kama wao. Achana na hili!
Nakumbuka enzi natwiti kuna watu walikuwa wanakerwa na watu wanaoleta Habari za Instagram, badhi walikuwa wakisema kama umekerwa au kufurahishwa sasa si ukamalizie huko huko Insta, kwanini unatuletea sisi huku kwenye Platifomu ingine? Hawa nao hawakujua/hawajui kuwa kule ni "chanzo" kama ilivyo Twitter/Facebook kwenye Taarifa ya Habari.
Anyway, mie sio Fashionista wala Stylist na sina "style".....well nilidhani-aga Staili yangu ni "Casual chic/Smart" kumbe nlikuwa najiongopea.....hata hivyo napenda kupendeza/kuvaa vizuri lakini sifuati TRENDY. Sasa wakati wa Mimba halafu tena nikawa  STHM(stay at home mum) nikajikuta mimi na Leggings(abarikiwe aliebuni hizi makitu) tunauhusiano mzuri.

Kibibi alipoacha kunyonya na mie nikaanza kulala bila kusumbuliwa n ahivyo kuanza kufurahia Maisha(hehehehe) nkasema, nahitaji kuwa na style(ambayo bado sina), sasa natakiwa kufanya nini ili kuwa Stylish Mum of 2 in her 30s  going on 40s?(ningekuwa stylish ninge-blog)....this time nilihitaji kusikia na kuona na sio kusoma hivyo nika-Ytube.Hakukuwa na 30s wala 40s.....wengi ni 40+(as in 50 mapaka 200? sijui),Curvy/Plus Size(hawa ni wengi hadi wanakera hihihihi fat peeps).....wakati nakaribia kukata tamaa nikakutana na Busbee Style Bonyeza hapa .  Pata Ari ili ujue wapi pa kuanzia. 


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blogg hii

Babai.

Sunday, 13 September 2015

Namna ya Kuondoa Mdoa(Tetekuwanga) Usoni.....


....haraka! Najua kuwa unajua napenda ku-share kile ambacho nimejifunza na kwa sehemu kubwa ni kutokana na Uzoefu. Kwabahati mbaya niliugua Tetekuwanga(ililetwa na Schooler boy wangu). Kwasababu yeye ni Mtoto haikuwa mbaya kama mie Mtu mzima.
Hii ndio nikawa naitumia Asubuhi na Usiku kama mbadala ya hiyo hapo chini

Lancome Genifique ndio Serum yangu Kitambo.


Mbaya zaidi Mapele yakajitokeza kwa Wingi Usoni( sijui kwanini hayakwenda Mapajani au Tumboni au Miguuni)....unapopata tatizo la Ngozi mahali ambapo sio rahisi kuficha inakupotezea Amani kabisa yaani.

Hakuna Dawa ya kuondoa Mdoa hayo kwa haraka(inachukua Miezi 2 mpaka Miaka kadhaa inategemea madoa yapo deep kiasi gani Ngozini). Dactor niliandikiwa dawa ya kuondoa Madoa(mie naita Mkorogo) lakini baada ya siku chache nikahisi inaharibu ngozi yangu kwa namna nyingine, kwamba inaondoa Mdoa Meusi Usoni lakini "pores" zinapanuka/zinakuwa kubwa(sijawahi kuziona pores zangu) nikaamua kuachana nayo.

Nikaamua kukubali tu kuwa naturally madoa yataondoka yenyewe, lakini sasa kutoka nje na mimadoa yangu Usoni ilikuwa inaninyima raha hivyo nikaamua kuwa navaa Matope(Foundation) kila siku. Hii ilifanya niongeze umakini wa kuitunza Ngozi yangu kwa sababu ni muhimu kuondoa "tope" usoni ili kuepusha Uharibifu wa Ngozi ambayo tayari imeharibiwa na Chickepox.

Utaratibu wangu wa kutunza Ngozi umeanza kitambo, na kama unakumbuka niliwahi kukuambia kuhusu Serum(picha ya Pili) ila sikutaka kuitaja kwasababu sikuona umuhimu wake(silipwi kutangaza) lakini leo nitakutajia kwasababu  imenisaida kwa kiasi kikubwa kuondoa Madoa Usoni.
Ila tatizo likaja kwenye Bei, Serum Genifique Mkombozi(inafanya ngozi yako kuwa Laini, kuwa sawa sawa,kuondoa mikunjo/mistari na kukupa mng'ao wa Ujana).....huo Mng'ao wa Ujana sio kwamba  niliutaka, ngozi yangu ni Mchanganyiko wa Mafuta na Ukavu hivyo nina "mng'ao asilia"  hivyo huwa naitumia Usiku tu.
Baada ya Post-Tetekuwanga si nikawa naitumia Asubuhi na Usiku, nikaona inaisha haraka, mpango wa kutumia £59 kwa Kichupa cha Seram mara Wiki kadhaa mie sina! Mkimama nikaannza kutafuta(Gugo ) Bidhaa Mbadala kutoka Kampuni Mama/Dada ya Lancome ambayo ni Loreal aiiii nikakutana na this Guy anaitwa "Youth Code" ......hapa Duniani bana kila kitu kina Mbadala wake.

Nikatumia "Kodi ya Ujana" mwaniki kwa muda wote huo well Karibu wiki Nane leo. Napenda kukuambia kuwa Wiki hii kwa mara ya Kwanza tangu June 2015 sijapaka/Vaa Tope(Foundation), Usimwambie  mtu ila "Kodi ya Ujana" inatoa matokeo yale yale ya Genifique.....jina ka' Tusi(hihihihihi) pengine better kama upo chini ya Miaka 40 lakini zaidi ya Miaka 25.
Hata hivyo Bidhaa hizi sio za kuchumbua Ngozi, isipokuwa zinaodoa rangi "ngeni" usoni....kama madoa au weusi wowote ambao sio Asilia(sio rangi yako asilia) na kufanya Ngozi yako kuwa na Rangi moja(ile uliyozaliwa nayo).


Naheshimu  na Kuthamini Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.

Thursday, 10 September 2015

Penzi la Kwanza halikufi(halifi)....

Well Penzi lolote la Kweli halifi/halifagi na penzi hili huwa halitokei kila mara, ikitokea limetokea(hilo Penzi la kweli) basi mtu unakuwa umefika.....kama ni Safari ya Reli ya Kati basi Umemaliza...upo Kibondo Kigomaaa. Pamoja na kufika kwako Kibondo( Kimapenzi) bado huwezi kusahau yule uliempenda Kweli(au kwa mara ya kwanza....sio Ngono kwa mara ya kwanza, wacha haraka).

Sasa hii ni mchanganyiko wa penzi hilo "kutokufa" au wewe kukumbuka hisia ulizozipata baada ya kuwa na huyo Mwanamke/Mwanaume ambae hana uhusiano na wewe Kidamu (sio Mama/Baba).....sote tunajua namna ya kupenda na kupendwa Wazazi wetu sio? Mwanaume wa kwanza kumpenda ni Baba yako(ikiwa wewe ni Mkimama) na Mwanamke wa kwanza kumpenda ni Mama yako(ikiwa wewe ni Mkibaba).

Hisia za kumpenda mtu baki ni nzuri na wakati mwingine zinachanganya(kuujua Ujinsia wako).....unaeza kujikuta unashindwa kutambua ni yupi hasa unampenda kiukweli(hisia hizi ni Mpya na ni tofauti na za kumpenda Babako).....ukakosa usingizi na kuanza kuwaza. Majamaa watano wanakufukuzia(nazungumzia mabinti  kwa uzoefu hapa)! Wote wanatofautiana Kimuonekano, Kimtazamo,Kiutongozaji,Kiuchumi(wazazi wao obviously)....aah unaona ya nini nawatolea wote Nje....bado mdogo mie.

Muda unafika unahisi sasa upo tayari kwa "mapambano" lakini tatizo wafuatiliaji wote wamesonga Mbele na hawana mpango na wewe, hata salamu hawakupi.....kama unabahati basi hawatokuwa wamekuzushia kuwa "aah yule Demu yule, hamna kitu, nilshamtia mara kibao" hihihihi the Low life type of  Wavulana.
Inakuja tokea tu umekutana na Mjamaa na Kemikali ikakubali, anakuheshimu, anakupenda,anakujali, hana haraka na kuneng'enuka, anakununulia zawadi, anakusaidia homework, anakufuata shuleni au anakusubiri Kituoni kwako ili tu apate Muda wa kuongea na wewe. Rahaaaa! Miaka inapita, huna uhakika kama ni Mshkaji(nyie mnaita Boyfriend)  au ni Rafiki? anyway tukatishe hadithi.....mnakuwa Wapenzi kwa mara ya kwanza. Baada ya miaka kadhaa mnajikuta mnataka vitu tofauti Maishani.....labda mmoja anataka Ndoa na Familia, Mwingine anataka Kusoma zaidi. Manaachana.

Huyo Mtu (penzi la kwanza) atabaki Moyoni kwa Muda mrefu na pengine kukufanya ushindwe kuwa na Mpenzi mwingine, si kwasababu unataka au kuombea/tarajia kuwa nae tena huko mbeleni la Hasha! ni kwamba huoni kama ni fair kuwa na mtu mwingine wakati Moyo upo kwingine(am single and happy ndio huja hapa au Shule/Kazi ndio Mpenzi wangu).
Miaka inapita, anatoka Moyoni na sasa unakuwa wazi na huru  kuruhusu mtu mwingine akae Moyoni mwako(zaidi ya Yesu, bwana apewe Sifa hihihihi), inaweza umelamba Dume au ikawa Galasha/sa hisia sio kama zile za "Penzi la kwanza" unajiengua kwake....by the time unalamba Dume  na ushakuwa Mtu mzima na unarejea tena Kibondo tena kwa Mara ya Pili, lakini hii safari ya sasa inaondoa kumbukumbu za ile ya kwanza, mazingira ya Kibondo sio yale tena, Migahawa/Maduka na Wamiliki ni tofauti, unajua Mitaa zaidi ya ile iliyo karibu na Stesheni.....nakupoteza eti? kwa kifupi Penzi hili linafunika/Zika lile la Mwanzo.

Unagundua kuwa Penzi hili ni tofauti kabisa  na lile la "kwanza" na hapa unagundua kuwa uzoefu ulioupata mwanzo ulikuwa mwanzo wa safari yako ya kujifunza kupenda nje ya kumpenda Baba na Mama na hakika hisia zile zilikuwa nzuri kwasababu Mpenzii ana-offer mambo ambayo baba/mama yako hawezi/hapaswi/nikosa kisheria/ni dhambii kukufanyia.

Pamoja na kusema hivyo bado ukimkumbuka/ukikumbuka jinsi mlivyokuwa enzi hizo(sasa ni jitu tofauti na pengine linatisha) unapata tabasamu usoni na kujisemea moyoni "aaah nilimpenda sana yule jamaa". Wakati mwingine inaeza kuwa  "nikukitana nae tena lazma nitamuonyesha how nimekuwa in er bed?"(sikutumi ukafanye hivyo, nasema tu kufurahisha Genge la Wahuni).
Hizi ni hisia ambazo sote huwa  nazo, lakini sio sahihi kudikilea kwa kila mtu kuwa "Daima nitampenda yeye "......unawajua wale "mama/baba wa wanangu, daima nitampenda".....no dear daima utamheshimu(wakati umem-cheat kwa  mfano).....huwezi kumpenda mtu wakati hutaki kuwa nae kama Mkeo/Mumeo. Duuuuh! nimehamia kwingine, ngoja nikaji-fix-ie a Cuppa!


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Tuesday, 8 September 2015

Marafiki(best) ni Milele, Wapenzi waja na kuondoka....

....kweli kabisa (kama upo chini ya miaka 29). Unapofikia umri mkubwa mambo mengi yanabadilika na unajikuta kuwa huitaji Marafiki ili kuwa na furaha(kufurahia Maisha yako). Sio hivyo tu pia unakua/badilika(nao pia) na hivyo mnakuwa hamuendani tena kama ilivyokuwa enzi zile, Matokeo yake unakuwa unafahamiana na watu na sio kurafikiana nao(best friends eeh Siwezi!).

Marafiki wanakusaidia kujifunza kuhusu Maisha (kihisia), wanakusaidia kujua namna ya kukabiliana na Drama za "maisha", wanakusaidia kujua  nini cha kudharau/kushikilia Bango, wanakusaidia kujua kuwa wewe upo tofauti nao, wanakusaidia kujuana nini cha kuchangia/kutokuchangia, wanakusaidia kujua ni wakati gani unatakiwa kuachana na jambo na kusonga mbele, wanakusaidia kuelewa jambo/somo Darasani (tunauelewa tofauti) n.k.

Hivyo ni Muhimu sana tena sana kwa Mtoto kutengeneza Marafiki ili aweze kujifunza hayo niliyoyataja hapo juu. Sio kila kitu Mtoto anajifunza kutoka kwa Wazazi, mengine anajifunza akiwa Shuleni lakini Nje ya Darasa au Michezoni anapokuwa na watu wa umri wake(si Baba na Mama/Walimu).

Mwanao pengine ana"marafiki" wengi na baadhi anawaita mabesti, baadhi yao wananakuudhi  na nisingependa arafikiane nao, lakini unajua kuwa ni muhimu kwake kuwa nao na kuwa na hisia za "u-best friend" ili ajifunze. lakini yeye kuwa na Marafiki hao sio sababu ya wewe kurafikiana na Wazazi wa hao marafiki zake.Utasema najikanganya(contradict) hapa kwa sababu mie ni Anti-Marafiki, nilishawahi kusema hapa kuwa sina marafiki(sio anti-marafiki) na sidhani kama kuwa na Marafiki ni Muhimu, halafu can be too expensive/stress you out ujue....siku za kuzaliwa, Ndoa, Ubatizo, Chrismas,kutembeleana.....aiii i love my own company....Nafahamiana na watu, sijengi urafiki/sirafikiani nao.
Nilipojifungua HV(Healthy Visitor) akajakunitembelea, akanambia kuwa inabidi nijiunge na "Mother & Baby groups" ili nitengeneze Marafiki wanaoendana na mimi (wazazi wezangu wenye watoto wa umri wa Mwanangu), maana "mabadiliko ya Homono na Kichanga vinaweza kukufanya uwe mpweke sana"....vere vere attempting ila........nkapiga mahisabati: Kukesha+Kunyonyesha+Kuogesha+Kubadilisha+Kupika+Kufua+Kunyoosha(piga pasi)+ Mimi kula(yeah it is a job)+Kusafisha nyumba+Kwenda "mother & Baby"= Sina Energy.


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, Ahsante kwa Kuichagua Blog hii,
Babai

Sunday, 6 September 2015

Kujiamini kwa Mtoto kunaanza lini?

....Watoto wa "Ulaya" wanajiamini sana, je kuna namna ya kulea mtoto ili akikua ajiamini kama wa Ulaya? Mkaka mmoja aliniuliza. Nadhani wengi wetu tumeaminishwa Mengi ya Ughaibuni ni Mazuri/Mema....lakini katika hali halisi sivyo.Kuna soko zuri sana la Vitabu/Vipindi vya TV vinavyofunza Wazazi namna ya kulea watoto wenye Kujiamini. Ni tatizo la Wazazi husika ambao walilelewa "Kimaendeleo" na hivyo kuhofia kuwa watoto wao watakuwa kama wao. Hofu hiyo inawafanya wazazi kuwa-overprotect watoto. Nahisi tu sina uhakika.

Kujiamini kunategemea zaidi na Malezi(nakubali) lakini sehemu kuwa ya Mtu/Mtoto kujiamini inatokana na yeye mwenyewe alivyoumbwa. Niliwahi kugusia Bloguni hapa kuwa kuna baadhi tumezaliwa hivyo(tunajiamini) lakini pia wapo ambao hawajiamini mpaka wafunzwe/himizwa/pewa Moyo/saidiwa kujiamini.


Naamini Watoto wa Afrika(well Tanzania wa kizazi kileeee) tunajiamini kwasababu tulitumia muda mwingi kujifunza kimwili na sio kihisia kama watoto wetu wa leo. Tulianguka kwenye Mchanga/kokoto, tulipigana, tulijikwaa kwenye Mawe na Misumali, tulianguka kutoka juu ya Miti na Milima.....yote haya yalitokea tukiwa peke yetu, hakukuwa na Mama/Baba akisisitiza...."usipande mti utaanguka".


Watotoo wa siku hizi hawapati nafasi hiyo kwa  kwasababu  nyingi tu ila kuu ni Uovu, Maendeleo/Uzungu, tunawaachia watumie(chezee) Simu/Tablets/PC/TV zaidi kuliko kucheza na "nature"  wakiwa na watoto wenzao(wajifunze bila mwalimu/Mzazi.

Watoto ambao wamekuwa/lelewa wakidekezwa kwamba Mama/Baba anawapigania ikiwa wamegombana na rafiki zao (watoto wenzao) au pengine kuonewa......badala ya kumuelekeza namana ya kujitetea na kuwa Imara ili asionewe wewe Mama/Baba unamkingia kifua.

Akiwa anacheza Park(kwa sie wa huku) basi unamfuatilia ili asianguke na kuumia, akikimbia unamwambia "kimbia taratibu usijikwae", akirukaruka na wenzie unasisitiza "kuwa mwangalifu, usijiumize/umiza wenzio".....yaani mtoto  hapati nafasi ya kuwa Mtoto na kujifunza mwenyewe.

Sasa mtoto kama huyu akiwa mtu mzima hatokuwa akijua namna ya kujitetea/pigania haki yake na hivyo atakuwa akionewa na kupoteza Kujiamini. Natambua kuwa ni ngumu(kama mzazi) lakini ni vema na ni muhimu kumuacha mtoto ajifunze(ukimfunza) kupigania haki yake ila sio kwa kutumia Nguvu/Ugomvi wa Maungoni.

Unakumbuka enzi...(well inaezekana na kwetu tu), ukienda kwa Mama/Baba kushitaki huku unalia kuwa "Mona" kakuumiza/piga au chukulia kitu chako.....Mama/Baba anakukurupusha na kukuambia nenda kamwambie "Mona" akurudishie kitu chao.....kama kakupiga basi unaambiwa "siku nyingine akikupiga, mrudishie na ukarudi hapa unalia nakuongezea(unapigwa)".
Siku zikipita hujapeleka Mashitaka, Mama/Baba anauliza wewe na Mona/rafiki zako mnacheza vizuri au bado mnagombana(hapa Mzazi anataka kujua kama unaonewa au ni mambo ya watoto), ikiwa unaonewa(wanaku-bully) then issue inahamishiwa kwa Walimu/Wazazi wa Mtoto ambae ni Muonevu.

Hiyo ni kwa Watoto wakubwa, unamfundishaje mtoto ambae ni chini ya Miaka 5 ambae yupo Shule(ya kucheza)....sikufunzi namna ya kulea mwanao lakini nitakupa uzoefu wangu since nina vitoto viwili vya umri huo.
Stori Time(sijazifanya hizi Kitambo eh): Mwanangu Babuu ni Mvulana ambae hana aibu na anapenda kujieleza(akianza kuongea hamalizi) alipoanza Shule(Vidudu) kila mtu akawa anamfurahia.....lakini kuna ile mitoto Migomvi na Mikubwa(vidudu watoto wenye  miaka Miwili na Nusu Mpaka Mitano) na wawili kati yao walikuwa wanamsumbua Mwanangu. Kila siku akirudi anashtaki kuwa mmoja wa hao wenzie wamemchokoza,

Roho ilikuwa inaniuma sana(niliapa ikitokea mtu anamuone mwanangu napigana) lakini nikamwambia tu kuwa kesho wakikuchokoza tena waambie "stop doing that, it is not nice" na wakiendelea nenda kamwambie "Mwalimu"......mashtaka yakaisha. Term nyingine ikaja na mashtaka yakaanza tena, mara hii nikaenda kuripoti kwa Mwalimu wake, so Walimu wakaanza kufuatilia na kutoa time out kwa Wachokozi. The wachokozi wamekuwa Marafiki zake....sort of.

Siku moja Toto la Kinaijeria(you know how i feel about these watu).....likaanza kumuita mwanangu(mbele yangu)....."Babuu you are so silly".....mwanangu akajibu...."no am not silly, dont call me silly".....lile toto likawa linaendelea huku linacheka(mama yake kimyaaa)....nikamwambia yule mtoto "B kasema usimuite Silly, can you stop please"! Mama yake akasema...."no he didn't call him silly"....and i was excuse me? akarudia tena.....si nikamlipukia nikianzia na "You Naigerians and lies....(kwenye kuongea hunipati, ila  sijui Kukunja Ngumi  Mzaramo mie hihihihihi).....Mama wa Kipopo ananiogopa huyo!

theeeee End,

Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Wednesday, 2 September 2015

Wanawake hatupendani....usimbee awe Jaji sasa!Sina hakika kama hii ni Imani tu au ni kweli, Naturally Wanawake hawanipendi mie binafsi(imagine ningekuwa mzuri sasa!) ila Wanaume wanananipenda(napatana zaidi na Wakibaba kuliko Wakimama). Kuna siku Mfanyakazi mwenzangu akanijia kwenye Dawati langu akanambia "dinah unajua nakuchukia".....mie nkacheka halafu nikamwambia "sio peke yako, nimezoea kuchukiwa na wanawake"....wewe ungesema is because i am Black!

Sasa, hii "wanawake hawapendani" ipo kila Nchi Duniani.....kila mtu anaibuka na sababu yake kwanini hasa hatupendani. Baadhi wanadai ni Wivu wa kike(umbile/kupendeza/mafanikio/kuwa na easylife) na wengine wanasema ni mambo ya Homono tu.

Mie sio kwamba nachukia wanawake bali sipendenzwi na tabia ya baadhi ya wanawake wanaofanya maamuzi ya Kipumbavu, kama vile kutojikinga dhidi ya Mimba, au kujitegeshea kushika Mimba ili tu waolewe au wapate sehemu ya Kipato ya Mwanaume husika. Sipendi mwanamke ajishushe ili kuonewa kirahisi.
Vilevile nachukia wanawake wanaokandamiza wanawake wenzo kutokana na masuala ya kike ili tu waonekane Imara. Unawajua wale wanaoamini kuwa Mimba sio Ugonjwa? au Mwanamke asipozaa basi sio Kamili? ama Mwanamke umeumbwa kuzaa? The shenzi kabisa.
Kutokana na Wimbi kubwa la watu kuachana, kumekuwa na Kesi nyingi kutoka kwa Wanawake wakidai Baba wa watoto wao kuwatunza wao na watoto wao. Hizi Kesi zinaweza kuwa Complicated (inategemea na chanzo cha kuachana, asili ya uhusiano, Umri wa Uhusiano na Mali mlizokusanya mlipokuwa pamoja n.k).
Lakini Majaji wengi wa Kike(Wanawake) wamekuwa wakilaumiwa kuwa na Chuki dhidi ya Wanawake wenzao kwa sababu hawaruhusu Wanaume kutoa pesa za kutosha kwa ajili ya watoto na wao(mamaz). Wanawake wanaamini kuwa kulea watoto ni kazi ngumu (nakubaliana na hili) na hivyo kama Baba hayupo "kimwili" basi Mfuko/Bank acc yake inapaswa kuchangia "ugumu" wa kule watoto wao.
Wanawake wengi wanaegemea zaidi kwenye Chuki "asilia" ya wanawake kwa wanawake. Mie nasema sio chuki bali Wanawake hao(Majaji) wanajaribu kutoa ujumbe(wengi hutoa somo mwisho wa Hukumu) unaofanana na, acha uzembe wa kutaka kutunzwa (via pesa zake) na mwanaume ambae hapati "matunzo" kutoka kwako(ni Ex) na badala yake nenda katafute pesa zako ujitunze mwenyewe.
Sawa, Watoto wana Haki ya kutunzwa/lelewa na wazazi wote wawili wenye Mapenzi sawia(au zaidi kwa one another) lakini likitokea la kutokea au in your case(sorry hihihihi) ulijitegeshea basi usitegemee kuishi kwa kutumia Kipato cha Mwanaume ambae hayupo nawe.

Majaji wengi wanawatoto na hakika walichukua muda kulea watoto wao walipokuwa wadogo kisha wakarudi  Kazini/Shuleni. Wengine walisaidiwa na Walezi kwenye Vituo vya kulelea watoto iwe Nursery au Nyumbani kwa mtu au kwa Ndugu na Jamaa. Hakika hii ni personal choice, lakini kama wao waliweza kufanya hivyo kwanini wewe ushindwe?

Weka mfano mzuri kwa kwa Watoto wako kuwa wewe  ni Mama Imara na huitaji Mwanaume ili kuishi/kujipenda/kupendeza/kuvutia/kujenga. Muonyeshe Ex wako kuwa Unaweza kuishi Maisha Bora zaidi bila yeye.


Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.