Wednesday, 30 December 2015

Ndugu anaposema "ndugu" yake fulani ni attractive....

.....ni kwamba yupo attracted nae. Yaani anavutiwa nae na uwezekano wa yeye kuwa na "wivu" wa Kimapenzi au Kumtaka kimapenzi ni mkubwa.Hawa watu wapo kwenye Jamii na nina uhakika inagusa watu wengi ikiwemo mimi mwenyewe na ndio maana Daima huwa nasema Mjomba/Binamu/Mpwa sio Ndugu wa damu kwasababu hatuchangii Damu kwa asilimia 50 au zaidi(hii haina Usayansi).
Kamakawaida nitakupa Mifano au "story" ili kukuburudisha na wakati huohuo kukusaidia unielewe ninaposimamia. Nina wajomba kama most of you, but nilikuwa na Mjomba mmoja(wa mwisho kwa kina Mama) ambae nilimpenda na tulielewana nahisi kwa sababu kiumri tuliendana, kwamba mie nilipokuwa Kidato cha Tatu, Yeye alikuwa Chuoni Mwaka wa Pili.Tulikuwa tunapatana na kwangu mie alikuwa kama "Kaka" mkubwa kabla ya Kaka yangu (wa damu)ambae ndio Kifungua Mimba wetu. Alikuwa akinifunza Hisabati (unajua mie na Hesabu tulivyo) na pia alikuwa akinisimulia Hadithi za Shida, Kuli, Thing fall a part etc(mie sikuwa nasoma hivyo Vitabu). Simulizi hizo ndizo zilizofanya nifanye vema kwenye Lugha heeey(you wonder why sijui kuandika? hihihihihi pole!).Anyway....siku Moja sasa Bibi akaitisha Kikao cha Wanawake, akasema "Mama Dinah usimuaminii sana Mdogo wako mbele ya Binti yako(mie), Mwanaume ni Mwanaume tu hata kama Binti ni Mpwa wake".  Mama akanipiga marufuku ku-hang na Mjomba.....nkalia kwa uchungu(nilikuwa sielewi kwanini). Nikalalamika nani atanifunza Hesabu na kunisimulia Kuli etc. Kwani hata alijali?!!

FastFooward: Memaliza Kidato cha Nne, sina Boyfriend wala nini (wachelewaji oyeee)....tupo kwa Bibi tukisheherekea Krismasi. Mojomba akatoa Siri kwangu....kwamba alipokuwa Kidato cha Sita alimpa Mimba Binti wa "kataja Kabila la Baba yangu ambalo ndio langu"....akasema "anaumbo kama wewe"....mie sina hili wala lile nachekaaaa! Akanipa stori yote yaani mpaka yale ya ndani ndani(weka emoji ya kushangaa).


Nkasema Hee! Mjomba unaenda mbali sasa, mie sipaswi kuyajua hayo.....nikaingia mtini. Nkaenda kumsimulia Mama, Mama akasema "Huyo ni mdogo wangu sio Ndugu yako, ni mwanaume kama wanaume wengine, kaa mbali nae". Mkimama nkaanza kujitenga.Kupunguza Urefu wa Hadithi sasa ili nisikuchoshe. Si nkaolewa bwana.....nilipoolewa kuna Wapwa pia na kuna Mpwa mmoja ambae anampenda sana Mjomba wake ambae ndio Mume wangu. Kabla ya hapo (ndoa) Mume wangu walikuwa akimzungumzia yeye tu akati ana wapwa mia na mbili hehehehe. Nkauliza jamani kwanini ni huyu tu utadhani yupo peke yake? kasema sababu anamuona yeye ni cool Ankal kuliko wengine.
Siku anaongea nae kwa kumkanya, mie Nkamwambia hebu Mwache Binti ajifunze mwenyewe, acha kumfuatilia....akasema "unajua ni binti anaevutia sana na nina hofu watu watamchezea"......akanipeleka nilikotoka. Nkajua hii inatokea kwenye Familia nyingi, lakini kwasababu watu hatujui au hatujali.....tunachukulia Poa na kuamini Mabinti zetu kwa Wajomba zao.

Sasa kwa upande wa Asali wa Moyo ilikuwa tofauti, inaelekea Mpwa alikuwa deep kwa Mjomba wake zaidi yangu kwa Mjomba wangu hehehehe. Binti Mpwa akaanza kufananisha uhusianoo wetu na wake, alipojifungua kaboom akamtumia Mjomba wake Picha ananyonyesha.....sio Titi bali titi na Chuchu(toa macho emoji). Nkashanga mnoooooooo! Nkahoji.....nkaambiwa ni "innocent" picha ya mtoto ananyonya. Nkamsamehe kwani ndio katoka Kujifungua....homono kila mahali.Nawapenda Wapwa wangu....but am a Woman na the oldest is 7 the youngest is Seven months.....Mwisho.


Ahsante kwa Kuichagua Blog hii, nathamini nakuheshimu muda wako hapa!

Babai.

Thursday, 24 December 2015

Kristmas mwaka huu ni tofauti....


Yeboyebo hihihihi bado mnatumia hili neno? Wasukuma wa Shinyanga (enzi za Usichana) walikuwa wakisema Yebaaa as in Yeah....."Wananchi Mpo?" "tupo tupo kabisa kwa Jeuri ya Chama yee yee yeebaa". Twende kwenye Krismas sasa.


Kwa kawaida mie huwa siandiki kuendana na Nyakati lakini Mwaka huu ni tofauti kwa sababu Waanangu has huyu Mkubwa kanifanya nianze kuipenda na kuifurahia Krismas tena. Miaka 3 nyuma alikuwa Mdogo so hakujali mapambo wala Santa, Mwaka huu anakaribia  miaka 5 na yupo Shule ambako wanafunzwa kama sehemu ya Utamaduni.
Babuu akaandika(makorokocho) Barua yake kwa Santa akiorodhesha zawadi aitakayo na akatengeneza na Bahasha kisha kuiweka na kumpa Baba yake akaipost(which he did, huruma kwa postman mkusanya barua hihihi). Sasa kila leo anamzungumzia Santa na kudai atakuwa extra nice na kunisaidia kusafisha(anaacha toys kila kahali) ili Santa asibadili mawazo na hivyo yeye kukosa Zawadi siku ya Krismasi.
Walipoanza kupamba Shuleni kwako akaja hima nyumbani akitaka na sisi tusimamishe Mmkrismasi(wa nailoni, tunaamini katika kutunza nature hihihihi usitujaji).....kwa maana hiyo humu ndani kuna Mapambo ya Krismasi tangu Novemba 20.....uzuri baridi sio kali sana,vinginevyo ningelalamika wanamaliza Umeme kwa kuwasha mataa 1st thing wakiamka mpaka wanapoenda kulala,....12hrs ya vimulimuli. Anyway, ukiangalia wanavyofurahia na kuhesabu siku zilizobaki kabla ya Krisimasi  kila siku inakupa furaha na kusahau "Gharama" ya Umeme.

Niliacha kusheherekea Krismasi baada ya kujua maana yake ambayo ni zaidi ya Mavazi, kula na kusaza na kisha kupewa pesa (zawadi ya xmass) na kila Mgeni aliekuja kula kwenu. Kwa kifupi ni kwamba sikuwa mtoto tena na vitu hivyo havikuwa na umuhimu tena kwangu.Ila mwaka huu ni tofauti kabisa, na itakuwa hivyo mpaka Babuu na Kibibi watakapokuwa watu wazima, may be 21yrs later?.....ntakuwa full of Botox na fillers(kutakuwa na better mbadala i guess).


Nakutakia wewe msomaji wangu na familia yako Heri ya Krismas. Furahia wakati wako na kumbuka kuwa Muangalifu kwani siku 7 kabla mwaka haujaisha ni Nyingi zaidi ya kuwa Januari nakuingojea December(sijui umenielewa?).


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Wednesday, 23 December 2015

Kupoteza Nywele baada ya Kujifungua Update (Bidhaa)....

Natumaini Post hii itakukuta ukiwa Mzima wa afya.
Kama nilivyoahidi, leo nitakuelezea utaratibu wangu uliosababisha nywele(Relaxed) zangu kurudia Afya yake baada ya kuzipoteza na kupata "upara" wa muda.
Jikoni kuna mwanga asilia, sihifadhi Bidhaa hizi Jikoni....hihihi!
Ukiachilia mbali kuongeza aina ya Mboga iitwayo Kale kwenye Mlo wangu wa kila siku na kula Mayai 2-3 kila asubuhi. Bidhaa hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa kuzuia Nywele zangu kuendelea kung'oka/anguka baada ya Kujifungua.Utaratibu wangu Rahisi.

Kila Siku: Napaka Cantu Shea Butter kila siku asubuhi na Jioni na baada ya kupaka Cantu huwa na-"seal" na Mafuta asilia ya Sweet Almond.Kila Wiki: Huosha na Deep Condition Nywele zangu mara Moja (kila Ijumaa/JumaMosi) na huwa natumia Cream of Nature shampoo. Baada ya hapo nafanya deep condition kwa kutumia Vitale Mayonaise ambayo huwa nachanganya na Hello hydration (haipo pichani) na aina 2 za Mafuta asilia ambayo ni  Nyoyo(Costor oil ) na Olive(extra virgin.). Huwa nakaa na mchanganyiko huo kwa Dakika 45-Saa Moja nikiwa kwenye Steamer.


Nasuuza kisha napaka Keracare Natural texures na Keracare normal leave ins na kisha kukausha nywele kwa kutumia Blow dryer(nitaweka Picha ya Tools kwenye post nyingine).Kila  baada ya Mwezi: Naosha(deep clense/clarify) Nywele kuondoa uchafu uliosababishwa na bidhaa nilizokuwa natumia kwa mwezi husika na hapa huwa natumia Vitale Breeze Shampoo na kutumia Mchanganyiko wa Deep conditioner nitumiao Kila Wiki.


Kila baada ya  Mwezi na nusu: Huwa nafanya "Protein treatment" kwa kutumia Aphogee step 2(fuata maelekezo kwa makini) na baada ya hapo huwa natumia Keracare Humecto ili kuepusha ukavu/ugumu kwenye nywele.
Kila baada ya Miezi 3: Huwa nahina(kupaka Hina kwenye Nywele). Hina nitumiayo ni ile asilia moja kwa moja kutoka Mtini(naagiza kutoka Tanzania). Huwa nachanganya na Chai  ya joto kiasi, kisha naiacha kwa masaa 12 then naipaka na kuiacha kwenye Nywele kwa masaa 3 hadi 5.
Baada ya hapo naosha na kupaka Keracare Humecto conditioner ili Nywele zisiwe kavu/ngumu. Hina inaongea "nguvu"  kwenye nywele kama Protein  na pia huzilainisha ila mie naitumia kwa ajili ya Rangi kwani nywele zangu si Nyeusi vya kutosha  na sipendi Weusi wa kutosha  hihihihihi so yeah kale kawekundu ka Hina kanaweka u-brown-ish Nyweleni. Hakikisha kuna nafasi ya kutosha kati ya Protein treatment na Hina Treatment. Mie huwa naweka Relaxer kila baada ya wiki 10 na Miezi  Mitatu(Wiki 12) na wiki  mbili  au Tatu baadae ndio nafanya Hina treatment.


Kama hujawahi kujifungua na kupoteza nywele au Nywele sio muhimu kwako basi huwezi kujua umuhimu wa Post hii. Back then hakukuwa na Post nyingi online, nilihangaika mno kutafuta maelezo ya nini cha kufanya na namna ya kufanya (sikuwahi kupatwa na issue hii). Naweka uzoefu wangu ili Mwanamke mwingine mwenye tatizo hili asihangaike sana kama mimi. 


Ijumaa (Christmas day) hii nitanyoosha Nywele zangu na kuchukua picha na kulinganisha na ya 2014 ili niweze uweze kuona  tofauti na "upara" wangu wa muda.....hii itakuwa kwenye Post ya Vifaa vya Umeme nitumiavyo kutibu na kuremba Nywele zangu.Nathamini na kuheshimu Muda wako hapa, ahsante sana kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Wednesday, 16 December 2015

Tumezaliwa ili tuzae....


....ndio Asali wa Moyo anaamini hivyo, which is Sad really.....but hey mepata topic!
Wazazi wako walipoamua kuanza familia nadhani ilikuwa ni maana ya Ndoa, kwamba mtafanya Tendo hilo ili kuzaliana. Nia na dhumuni la Tendo la Ngono ni kuzaliana, kama hutaki kuzaa basi tumia Kinga (usiolewe/usioe) si ndio?!!
Kwasisi wa kileo ambao tunabaki Shule kwa muda mrefu, Muda wa kufanya Tendo kwa "haki" (kuzaliana) huwa  sio muhimu, lakini pia sio wote tunaweza kuvumilia mpaka muda ufike...hivyo tunaanza Ngono kabla ya Ndoa nakujikinga "Kizungu" Dhidi ya "kuzaliana".Wazazi kutuzaa sisi ilikuwa uamuzi wao, haikuwa lazima na hakuna aliewalazimisha, sasa kwasababu tu nilizaliwa haina maana na mimi ni lazima nizae. Suala la kuzaa sio rahisi (kwa mwanamke ambae ndio anaezaa)kama ambavyo wengi wanafikiria.
Mwili wa Mwanamke ni wa ajabu in a good way, Ukiachilia mbali Athari na Mabadiliko makuu(mengine yanahatarisha uhai) kwa Mwanamke kwa ndani baada ya kuzaa bado hili suala ni nyeti sana kwa wale ambao hawana uwezo wa Kushika Mimba, kukaa na mimba mpaka ifikie mwisho nakujifungua salama au kupata Mwanaume "anaefaa".
Tunaposema kuwa "tumezaliwa ili tuzae" tunakosea kwasababu Kuzaa sio lazima bali ni Uamuzi kwa baadhi na wengine hawawezi/hawana uwezo wa Kuzaa. Imani hii ni wazi kuwa inawapa Presha Wanawake(kama vile tulizonazo hazitoshi).Ulipokuwa unakuwa Wazazi wako hawakukuandaa ili uje uzae, walikuandaa Kielimu< Kimaisha ili uweze kujitegemea na kuishi kwa furaha na pengine uwasaidie watakapokuwa Wazee. Unaona? Baba (RIP) na Mama yangu walikuwa wakisistiza kuwa hawataki "Wajukuu" hihihihi go figure!
Suala la Uzazi kwa Mwanamke ni Nyeti mno, huwezi kukurupuka tu na kuzna kusema "mwanamke umeumbwa kuzaa", "tumezaliwa ili tuzae".....vipi kama mtu hana uwezo wa kuzaa? Mwache Mwanamke(kama kajaaliwa uwezo huo) afanye uamuzi wa yeye kutaka Kuzaa, Kuzaa sio lazima, tumezaliwa ili kujifunza, tuishi na kufurahia maisha.....hatukuzaliwa ili tuzae.
Ndio! nakusikia unasema "kama wote tukiamua tusizae Dunia si takuwa tupu" well....zaa wewe uijaze Dunia, wengine ama hawana uwezo, hawapo tayari, hawajapata mtu mwema wa kuzaa nao, au simply hawataki kuzaa.Naheshimu na kuthamini  Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Tuesday, 15 December 2015

Hii ndio sababu ya mawifi/Mama wake kutuchukia?


Usinielewe vibaya, mie pia ni Wifi "mkubwa", lakini  tofauti ni...sio  kwamba nawachukia(hawajawahi kunikosea) au nawapenda(sijawahi kuishi nao).....nawachukulia kama walivyo na kuwaheshimu kama wanavyoniheshimu.

Kamwe sijawahi/siwezi kujaji lolote kuhusu wao kwasababu siwajui kama ambavyo Kaka zangu wanawajua Wake zao. Sijawahi kuhoji kwenye  kufanana kwao na watoto wao. Huwa nasema tu mnawatoto wazuri, wapwa wangu wanapendeza n.k. Ikiwa Kaka zangu hawakuwa Makini na wanalea watoto wa wenzao, hiyo ni issue yao, sio yangu.
Sasa, kuna siku nilikuwa nazungumza na Asali wa Moyo wangu kuhusu mambo ya Kijamii na tukagusia Chuki ya Wanawake kutoka Upande wa Mwanaume, akaniuliza hivi ni kwanini? Nkamwambia mie pia ni Wifi(mwanamke kutoka upande wa Kaka zangu) lakini sina Chuki na wala sifuatilii mambo yao na familia zao!Tukaenda ndani (deep)kidogo, nikagundua kuwa, chuki hii inaweza kusababishwa na moja9au yote) kati ya haya yafuatayo;-

*Mwanamke anajua kuwa yeye ni "powerful" kwenye maisha ya Mwanaume linapokuja suala la Mtoto/Watoto. Ni yeye pekee ndio anajua baba halisi wa Mtoto ni nani! Hofu ikizidi anaanza  kuhisi kutaka kutafuta "ukweli".


*Watoto alionao pengine sio wa Baba ambae sote tunajua ni Baba yake.


Kwahiyo, ikiwa mmoja kati ya Mawifi au Kiongozi(Ma'mkwe) amewahi kufanya kamchezo kachafu na hakuna anaejua ukweli wa "blending family".....hakika hatokuamini wewe. Siku zote atakuwa wa kwanza kuchunguza kucha za mtoto, rangi ya ngozi, nywele, mwendo, kuota meno n.k.
Sasa ikitokea Mumeo ndio "zao" la kamchezo kachafu ka Mama Mkwe basi utajuta hihihihihi.....unafanya DNA na Babu yake(ambae kihalisia si Baba wa mumeo) mtoto anafeli, unafungashiwa virago wewe na mwanao.....Mumeo anakuchukia Milele.
Siku ingine ikitokea Wifi/Mama mkwe anakusumbua bila sababu ya Msingi, ujue issue ni kutokuamini mtoto/watoto wako ni matunda ya Kaka/Mwana wao...... hakuna kulia na kwenda kushtaki kwa Mumeo. Mwambie  hayo mawili niliyokutajia hapo juu kwa namna yako lakini kwa upole na heshima. Utaona atakavyo kuwa Mdogo au Atakavyokuja juu na "umenikosea heshima" huku analia au kutaka kukuvamia......hapo ujue Umeshinda.
Mf: Wifi/Mama naomba tuongee kama wanawake. Mimi na wewe tunajua kuwa ni sisi pekee ambao tunajua Siri ya Baba wa watoto wetu, sasa kama ilitokea ulitereza na unajua mmoja kati ya wanao baba yake sio Kaka/Ba'mkwe kama tujuavyo, haina maana kuwa na mimi nimefanya hivyo au nitafanya hivyo. Watoto wetu wote ni damu moja(Baba na Mama mmoja).Ahsante kwa kuichagua Blog hii, naheshimu na kuthamini Muda wako hapa.

Babai.

Saturday, 12 December 2015

Kutunza Siri ni Wajibu wako.......well, inategemea na unachokifanya for a living sio! Si unajua ile Kuapa au kuweka sahihi kuwa kamwe hutotoa siri (ujuayo) ya Kampuni/Mgonjwa/Mteja n.k. isipokuwa tu ikiwa Serikali na Mahakama itahitaji. Hello, natumaini Post hii imekukuta ukiwa na afya njema.
Mie binafsi naamini kuwa kutunza "siri" ya mtu au watu ni wajibu wako. Kutokana na kile nilichokuwa nikifanya Miaka 8 iliyopita baadhi ya watu walijenga Uaminifu kwangu, kwamba walikuwa huru kuniambia mengi  kuhusu wao na maisha yao. Kwa maana hiyo nafahamu mengi ya watu wengi ambao hatufahamiani.Ile ilikuwa "kazi" ya kujitolea, sijasomea nilichokuwa n akifanua isipokuwa nilitumia uelewa wangu na uzoefu wangu(natambua unalijua hilo), hivyo sikula Kiapo na wala sikutia saini kuwa nitabaki na "siri" za watu Milele(haina maana nitazitoa).Pamoja na kuwa hakuwa "Kazi" bado nilichukulia na ninaendelea kuchukulia kuwa ni wajibu wangu kuto-share chochote kuhusu watu wote walioniandikia na hata wengine kuongea nami kwa Simu, bila kusahau wale niliobahatika kukutana nao.
Pamoja na kusema hivyo haina maana huwa nakaa na kuanza kurudia mails zao au kufikiria ninayoyajua kuhusu wao kama Wenza au kama Mwanaume/Mwanamke. Sasa ili kuondoa "mzigo" nilikuwa  na kawaida ya kufuta mails mara baada ya mhusika kurudisha feedback.
Kwa wale ambao bado naendelea kuonana nao "online" ni wazi kwamba nikiwaona nakumbuka aah huyu alikuwa na hili na lile, aah yule aliniambia ana hili na lile. Hii hunifanya nihisi kuwa pengine hawa watu wanaweza kuwa na wasiwasi kuwa siku  moja Dinah atakuja kusema niliyowahi kumuambia kuhusu mimi na fulani.
Lengo la Post hii ni kukusaidia uwe na Amani, usinikwepe(hihihihihi) sijawahi na Kamwe, KAMWE sito-share ulichowahi kunielezea. Ni wajibu wangu kuachana na uliyoniambia kama nilivyoachana na Blog iliyokufanya utake Ushauri wangu.
Sio kwamba sijawahi kutoa siri, nimewahi kutoa siri na sababu kuu ya kuitunza ilikuwa kutoonekana "wifi/shemeji" mgomvi. Lakini baada ya miaka Mingi Ndoani nikajua mengi kuhusu Jamaa niliekuwa namtunzia Siri  against Cuz yake(mume wangu), so nikaitoa.....hihihihi the man is my husband. Sina siri kwa Mume wangu ayee!Heey....naheshimu na kuthamini Muda wako mahali hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.


Babai.

Monday, 7 December 2015

Kupoteza Nywele baada ya Kujifungua....update!


Ni Mwaka na Miezi kadhaa tangu nikusimulie kuhusu Nywele zangu za kichwani ambazo ni Relaxed(bila shaka). Sasa, tangu tunamaliza Mwaka nimeona sio mbaya kama niki-share safari yangu ya kuwa na Nywele  tena zenye urefu wa kutosha kutengeneza mitindo na pia zenye afya.
Halafu sio mbaya kama nikikutajia/nikionyesha Bidhaa ambazo zimenisaidia kufika hapa nilipofikia. Vilevile nitakuambia ni Bidhaa gani natumia lini na kwa nini(kwenye post nyingine) na nitaambatanisha Picha.

Pamoja na kusema hayo ni vema utambue kuwa Bidhaa hizi hazikuhakikishii matokeo kama yangu, inaweza kuwa bora zaidi yangu au usione mabadiliko yeyote.

Baadhi ya Bidhaa hizi nilikuwa natumia kitambo, baada ya kuhangaika na kujaribu aina nyingine na kutofanikiwa nikaamua kurudi kwenye bidhaa kutoka Vitale, Nikaamua kutumia "Steamer" na "Blow dryer". Awali nilikuwa situmii Heat kabisa kama nilivyoshauriwa na Gurus.


Baadae nikagundua kuwa Nywele zangu zinapenda Heat so nikarudia utaratibu wangu wa kitambo wa ku-steam kama sehemu ya deep conditioning na baadae ku-blow dry.

Bidhaa mpya  ambazo natumia kila siku,  kila Wiki, kila mwezi, kila baada ya Wiki 6 na kila baada ya Miezi 3 ni Cantu Shea butter, Keracare, Olive oil,  Almond oil, Cream of Nature, Aphogee,Jamaican Costor oil,  HH essense, Dr Miracle oil Gro, Henna.


Natengeneza  na "Kutibu" Nywele zangu mwenyewe. Utaratibu wangu ni wa kawaida ni rahisi. Ni utaratibu niliokuwa nikiufanya pre-Children. Kilichobadilika ni umakini na  kuongeza bidhaa mpya (sikuwahi kuzitumia kabla)nilizozitaja.


Je ulipoteza Nywele baada ya kujifungua kutokana na Mabadilkko ya Homono? Ikiwa umefanikiwa kurudisha afya ya Nywele zako.... je ulichukua hatua gani?

Naheshimu na kuthamini muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua blog hii.
Babai.

Thursday, 3 December 2015

Single Mum/Loner Parent, Mzazi Mmoja=no HelpHi!


Sitojifanya mjuaji kwenye hili, tangu sijawahi kuwa "single mother" iwe kwa kutaka (wale wanaoamua kushika Mimba bila kuwa na hitaji la mwanaume husika) au kwa bahati mbaya, kwamba kutofautiana kwenu kumefanya mmoja wenu abaki na mtoto/Watoto(hapa siwazungumzii Wajane au wale waliobakwa, hii ni issue nyingine).


Ninaowagusia hapa ni wale ambao kuwa "single mother" ni Mtindo wa Maisha,Sifa, chanzo cha kuonekana Imara/Unaweza! Wengi hapa ni wale Wasichana waliokulia miaka ya 90s na wale wa early 2000s. Ule msukumo wa kutaka kujitegemea ukikuwa na "impact" kubwa kwetu kiasi cha kuhisi hatuhitaji Wanaume ili kuwa na Familia.Tuliamini kuwa tunaweza kufanya yetu kama Wanawake na tunaweza kufanya ya Wanaume pia, "ikiwa mwanaume anaweza hata mimi naweza" sort of Imani....hakika hakuna afanyacho Mwanaume ambachoo sisi hatuwezi kufanya, lakini kuna mambo ambayo hatuwezi kuyafanya kama Wanawake kwenye malezi ya Mtoto au watoto(hasa wa Kiume).


Nakumbuka mimi mwenyewe niliwahi kusema kwenye Moja ya Forums kuwa, sitaki Mume na ikifikia mahali nahisi kutaka Familia basi "nitabaka" Mwanaume aka kujilengesha ili nishike Mimba, na nikifanikiwa basi sitomwambia huyo jamaa na hivyo kunirahisishia mimi kumlea "mwanangu" bila Baba yake. Nilikuwa young and stupid early 20s girl, sikufikiria hisia za Mtoto na kiukweli sikuwa nawaza kuwa siku moja nitakuwa mama so ilikuwa "chat" tu....lakini kwa wakati ule nilimaanisha.
Ni vema tutambue kuwa, Mungu ametubariki(sileti ulokole hapa usikimbie hihihihi) kwa namna tofauti, Mwanamke kabarikiwa kivingine na Mwanaume kabarikiwa kivingine (hatufanani) lakini sote tupo sawa in a different way na tunahitajika sawa sawa kwenye Maisha ya Mtoto/Watoto. Usawa huo hauna maana mmoja wetu anaweza kuufanya kwa kuchukua nafasi ya mwenzie.
Mfumuko huo wa "loner parents", wengi wakiwa Wanawake....umeondoa thamani ya Maisha ya Familia, kwamba watu hawajali kuwa Familia na badala yake wanajali zaidi kuonekana kuwa wao ni "single parents" na wanataka kutambulika na kusifiwa kuwa ni "Imara na Jasiri" kwa kuchukua Jukumu la Baba wa mtoto. Fuatilia "Fathers Day" uone wamama wanavyoingilia hii siku kwa kutaka "kutambuliwa" kwa kuchukua/fanya majukumu ya Baba. Huwa najiuliza, Majukumu ya Baba ni yapi hasa?

Jukumu la Baba ni yeye kuwepo kwenye Maisha ya mtoto/Watoto, kutumia muda wake na wanae/mwanae, kumfunza kama Baba(kumbuka Mungu ametupa Baraka tofauti kijinsia, hatufanani kiakili so mafunzo yetu kwa watoto ni tofauti pia). Sasa kama Baba hayupo kwenye Maisha ya Mtoto kwasababu zozote zile, bado hufanyi Jukumu la Baba wa Mtoto/watoto husika.

Natambua kuwa Mzazi ni kazi ngumu, haijalishi kama wewe ni "Single Parent" au "Couple Parents". sasa ni wapi hasa unapaswa kujiita "single Parent"? well Kama unafanya kila kitu mwenyewe bila Pesa za Matunzo ya Mtoto kutoka kwa baba yake, Msaada kwa ndugu, jamaa, marafiki, Walimu n.k. kwenye kumfunza na kumuangalia mwanao wakati upo kazini....basi wewe ni SINGLE/LONER Parent(Mother/Father).Vinginevyo, wewe ni Mama wa Mtoto/Watoto ulionao.....Kuwa single sio Ushujaa, kuwa Single sio sifa. Hakikisha unapata msaada kutoka kwa watu wengine unaowaamini, hata kama kati ya watu hao Baba mtoto/watoto hausiki. Inasikitisha sana kwa Watoto wetu kukua wakiona Mama anafanya kila kitu, hii inawaharibu na huenda ikawapa shida huko mbele kwenye maisha yao ya Kisosho na pengine wakati wa ku-date nakadhalika.
Natambua kuwa kuna Vijana wengi sana ambao walilelewa na Mama tu, lakini kwa wakati ule bado kulikuwa na "father figure"....Wajomba, Baba wadogo/wakubwa(waume wa...) , Babu na hata pengine Kaka kutoka kwa Mama wakubwa n.k. Ila, kutokana na maisha ya leo(sio kwa Ughaibuni tu) wengi tunaishi mbali na watu hao(niliotaja hapo juu) kwa sababu ya kazi au Masomo, hivyo watoto (hasa wa jinsia tofauti na Mzazi anaewalea) hukosa kujua upande wa Pili wa Mzazi wake au hata "wasaidizi" ambao ni watu wa karibu (sio wale unaoajiri).Kuwa Mzazi sio ushujaa, ni Jukumu lako kwasababu ni wewe ndio uliamua kuleta Maisha ya watu wengien Duniani, sasa kama umeamua kwenda mwenyewe au imetokea kwa bahati mbaya mwenzio kakimbia majukumu yake, hupaswi kujiona Shujaa au kudai Sifa za upande wa pili(wa mzazi) kwa sababu unadhani kufanya majukumu yako kwa mwanao/wanao ni kufanya yako na ya baba yake. Kila mtu ana nafasi yake kwenye maisha ya Mtoto/watoto.
Kuna ule Usemi wangu maarufu (in my head) kuwa una Mume lakini bado ni Single mother.....kwamba unafanya kila kitu na Mumeo amekaa tu au anakuwa "mwanao", unamfanyia kila kitu mpaka kumfunza manners!....Kujitegemea kunapitiliza unaishia kuwa "single parent" japo una Mume/Baba wa watoto wao. Sijui umenielewa.....(mwenyewe sielewi)!


Nili-protect maandishi yangu, mesahau neno la siri ili ku-unprotect na sikuwa na muda wa kuandika upya, so yeah....Sorry!
Nashukuru na kuthamini muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua blog hii.

Babai.

Tuesday, 1 December 2015

Kukosoa na Kumcheka mtu ni "interest" yako?

Nakuona!

Wengi huamini kuwa ukiwa na tabia ya kukosoa au kucheka watu wengine basi wewe utakuwa na Matatizo kwenye Maisha yako, maisha yakoo hayana furaha na yamejawa na Huzuni na hivyo kukosoa na kucheka watu ndio njia pekee ya kujipatia "furaha".Nakubali kwa kiasi fulani, kwa baadhi kuwa Hasi kwenye kila kitu  ni tatizo na linaathiri maisha yao ya kila siku. wengine huamua kuwa Hasi kama sehemu ya kupata "attetion" au "Trafic" na "Views" popote walipo kwenye Sosho Midia.
Kwa wale wa Ughaibuni, Maisha mitaa hii yanaweza kuwa ya Upweke sana na hivyo kumfanya mtu kutumia muda wake mwingi kwenye kutafuta "furaha" kwa kuwa Negative towards watu wengine. Upweke wa huku unatokana na utofauti wa Kitamaduni, Utaratibu wa kazi za "shift",  Majira ya Mwaka(Kiza kuingia mapema) vilevile kutumia muda mwingi kusafiri to na from work....by the time unafika nyumbani upo hoi, tayari ni Giza hivyo  hakuna muda wa kutoka au kukaribisha watu kwako as kesho unatakiwa Kazini.
Nilipokuwa Teen nilijulikana kwa baadhi ya wanafunzi wenzangu kuwa "Dinah siku zote huwa na sababu ya kukosoa", nilikuwa na tabia ya kuchea watu, haijalishi  mtu kafanya nini jema lazma nitapata/ona Kasoro na kukosoa....by doing that wenzangu walikuwa wanacheka balaa!Sasa, Darasa letu lilikuwa juu (Ghorofani) na hivyo tulikuwa na tabia ya "kuwachora" Wanafunzi na Wageni waliokuwa wanakatiza maeneo ya Nje ya Gate ay ndani ya Gate. Wakati mwingine nilikuwa busy na mambo mengine, lakini bado wataniita ili nione kasoro ya watu au mtu na hivyo wao kupata Burudani.Ilifikia mahali nikachukulia kuwa kucheka watu ni "interest" yangu, kiukweli napenda kucheka na huwa najicheka mwenyewe.....lakini kucheka watu haikuwa sahihi. Mwaka 2010 ndio nikaamua kubadilika. Ni baada ya kushika Mimba.....Mimba ikanibadilisha. Nikatambua kuwa unapokosoa mtu ama watu kama sehemu ya "burudani" ni wazi kuwa unatatizo, sikuwa na sababu ya kukosoa na kucheka watu.Unapomkosoa mtu kila siku hata kwa yale mema au yale yasiyohitaji "maoni" yako huko kunakuwa sio kukosoa tena bali ni kumchukia mtu huyo. Kwanini umchukie mwenzio/wenzio? wamekukosea nini? Pamoja na tabia hiyo  ya ajabu bado sikuwahi kucheka Walemavu, Wenye matatizo au Masikini zaidi yangu.
Era ya Sosho Media imewarahisishia wale watu ambao wapo kama nilivyokuwa mimi huko nyuma. Tofauti ni kuwa mimi nilikuwa nafanya hivyo bila kuwagusa wahusika moja kwa moja. So walikuwa hawajui nawakosoa kuhusu nini. Siku hizi mtu anakufuata live kwenye "profile" na kuanza kukukosoa.....anakuwa na utaratibu huo kila siku.Mwaka 2013 niliugua PD(stori yake itakuja siku ingine)....baada ya kupona nikajifunza kuwa "Chanya" kwa Msaada wa Daktari. Hapa ndio nilipojifunza kuwa mambo mengi yanatokea kwenye Maisha ya mtu, huwa kuna sababu. Mpaka uijue sababu ya yeye kufanya alicho/anachokifanya ndio umkosoe. Kama hujui basi muache kama alivyo.
Kukosoa ni tofauti na Kujaji......bado najaji (siwezi kujizuia), pamoja na kuwa nitakujaji  bado sitokucheka. Heeey, ahsante kwa kuichagua Blog hii. Tambua nathamini na kuheshimu muda wako hapa.


Babai.