Skip to main content

Posts

Miaka 20-na vs Arobaini-na kwa Mwanamke...

Heri ya mwaka Mpya! Sasa umegonga zaidi ya 40 unajisikiaje? Nakumbuka nilipokuwa in my 20s Ma-Celeb walikuwa wanasema wanajisikia kama walivyokuwa in their 20s....wakaibua msemo wa 40s in new 20s. Kwangu binanafsi nakuhakikishia sio kweli kwa asilimia Mia moja, kwasababu nilipokuwa na umri nusu wa nilionao sasa, sikuwa najiamini kwenye kufanya maamuzi Kiuchumi, Kimwili na Kimahusiano(ndugu, marafiki, mpenzi) na kijamii kwa ujumla. Kama ulichelewa kuwa na watoto basi ujue utapoteza umuhimu wa baadhi ya mahusiano na watu wengine sababu watoto wako ni muhimu zaidi kwa sasa kuliko hao watu wengine, sio hivyo tu wanao wanakupa sense ya ukamilifu na kuridhika na maisha uliyonayo na hutaki kupoteza muda kufanya mambo nje ya familia yako ulioitengeneza na Mumeo/Mkeo. Kwa wale waliokuwa na watoto ktk umri mdogo, wanaweza kuikuta wapweke sababu watoto wamekua na wanajitegemea hivyo ktk umri wa miaka 40na unaweza kujikuta unatamani kujenga mahusiano na watu wengine nje ya Mwenza wako ...

Ndoa ni Social construct, haina umuhimu...

....vipi kuhusu Elimu, Dini na Familia? Aah Elimu ni kwa ajili ya masikini kwani haina faida, sababu watoto wa vigogo wanainunua. But tunahitaji wajuzi wa afya ya Ubongo, Mwili na viungo vyake, Mifupa n.k kuanzia tupo tumboni mpaka tunafika miaka 120(yep tunafika huko as hii ni karne ya 21 sio 11).   Wajuzi wa mazingira,vyakula, sumu, Madawa, Nishati, Shetia na utaratibu wa kulinda na kupata Haki yako maka mtendwa au mtendewa jambo kinyume cha sheria n.k. Vipi kuhusu Imani ya Dini? Nayo tumeaminishwa tu na Wazungu na Waarabu ili watutawale si ndio? Vipi Waarabu na Wazungu huko makwao ambao bado wanafuata, kuamini na kusimamia Imani hizo za Dini, wanafanya hayo ili kujitawala? Aaah ili kunyanyasa Wanawake na watoto....Achana na Uislamu/Ukristo, vipi Imani za Dini/Miungu ya kimila na Desturi?  Bado unaamini haikuwa sehemu nzuri ya kuifanya jamii husika kuwa na structure na hivyo kufanya maisha yawe rahisi kumudu hasa linpokuja suala la stress, shida na matukio mengine ambay...

Wazazi wa Teenager leo ni...

...wale wa Miaka 30-39, isipokuwa mimi ambae naelekea miaka 50 na wanangu wala hawajafika miaka 16. Hawa teen ndio wanaoendesha Social media huku kaka/dada zao in their 20s wanasakama watoto wangu(kizazi kipya aka kizazi cha mwanzo). Nilienda kuchukua mwanangu wa Sekondari nakutana na wamama watu wazima...mie pia ni mtu mzima ila naona kama vile wenzangu wazee zaidi yangu kwa muonekano, makunyanzi na mvi...oh bila kusahau fashion. Talking about fashion, siku moja kabla ya Covid19 my Std 5 kid akanambia "kwanini unapenda kuvaa same dark colors "clothes"  nikamwambia navaa different colors but Winter coats ndio the same dull colors....halafu ikawa March 2020(deleted memories).  Anyways, turudi kwenye malezi ya watoto wenu wanaosumbua mitaa ya social media na real life. Picha kutoka comment-ini. Wengi ambao wapo in their 30s(kwa mujibu wa hiyo comment) bado ni Wanawake wa nguvu na waliamua kuwa na watoto bila Baba kwasababu wanaweza kufanya kila kitu...

Jinsi ya kulea watoto ktk Kacha mbili...

Wazazi wengi wanalea watoto wao kimagharibi bila kuishi Magharibi kwasababu Umagharibi unavutia au ni kwasababu inakufanya ujione bora, tofauti au upo juu zaidi ya wenzako ambao wanalea watoto wao kibongo-bongo ndani ya Tanzania? Usijisikie vibaya sababu hata mimi nalea wanangu kibongo-bongo wakati hawajahi kuishi Bongo kwa zaidi ya miezi kadhaa ndani ya miaka yote ya umri wao.  Humu ndani hatuwezi kutumia "kumbuka ulikotoka" au "usisahau nyumbani" sababu nyumbani kwao ni England na ndio walikotoka na walipo.... Sasa unafanyaje kuhakikisha wanao wanakuwa kibongo-bongo as well as ki-kwao(walipozaliwa)?  Picha kutoka gugo. 1: Hakikisha wanapata values na principals ulizokuwa nazo kama mbogo. Unafanikisha hili kwa kuwapa simulizi za ukweli kuyokana na uzoefu wako wa Mila na Desturi, pia kutokana na uzoefu wako wa huko mlipo na unavyoijua Kacha hiyo hakikisha una-up date inapohitajika. Mf:-  Bongo: Heshimu wakubwa wako. Ngambo: Heshimu anaekuheshimu bila kuj...

Siri ku-bounce back baada ya Kuzaa...

Mambo? Aah mie pia nimekukumbuka ndio maana nimeamua ku-blog kila siku kwa siku 5* kama zawadi yako ya  Christmas. Tegemea michapio kadhaa, nita-edit baada ya Xmas.   Now that is out of the way....njoo kwenye Somo la leo ila kama umekuja kujua namna ya kurudia mwili wako baada ya kuzaa, Pole ila usiondoke nataka nikupe siri yake ili ukome kutaka ku-bounce back haraka haraka, sio tu kwamba ni Kacha ya kimagharibi bali pia ni aina ya unyanyasaji wa jinsia kutoka kwa Mumeo. Maisha yangu yote nilikuwa chikonda aka skinny hivyo nilijizoea hivyo na nilijipenda nilivyokuwa. Baada ya kushika Mimba kwa mara ya kwanza nilinenepa na nilipojifungua mwili ukarudia wembamba wake ila nikawa  "shapely", kwamba nikawa na umbile la kike(vitu vikajitenga, nikatokelezea)zaidi. Hiyo ilichukua wiki 2, Mimba ya pili nikanenepa tena na mwili ukarudi ulipokuwa ndani ya miezi 2...baada ya hapo mambo mengi yakatokea kwenye huu mwili(story ndefu na sina muda) then akaja mtoto mwingine, tufanye ...

You know you are the oldest...

....when Viongozi wote ni umri wako au wadogo kwako, Unakumbuka May 2, 1997 Tony Blair alikuwa Waziri Mkuu mdogo  UK? Alikuwa kundi moja kiumri na Mama yangu ila sawa na Dingi. Hapa nilipo najihisi kama mama alivyojihisi mwaka huo(well I was not her then so I don't really know how she felt).   Awali, binafsi nilihisi nipo nyuma ki-career kwasababu nilichukua time off kulea wanangu badala ya kuachia Childcare industry, sio hivyo tu kufanya kazi halafu mshahara wote unaishia kwa Walezi wa watoto wako ni dhambi. Yaani unabaki masikini halafu wakati huohuo huwajui wanao na wao hawakutambui kwasababu hujawahi kuwalea. Mbaya zaidi wakikua wanakuchukia na kumpenda Miss Amanda, kumsikiliza Mr Cook and  kumuheshimu Mrs Mcmun huku wewe ukishangaa na kujiuliza kwani nimekosea wapi? Kwanini tabia  haziendani na Values zenu(baba na mama).  Mara pap! Nikakumbuka, Wakati wenzangu akina Macron, Jacinda wa NZ (alikuwa mdogo zaidi ila kazi ilimshida), Sanna Marin wa Ufini, Georgi...

Diaspora Wives...

...the long suffering ones wa US, UK and Canada nyie wa Scandinavia, Spain, Italy, Germany, etc hamuolewagi...wait, huwa hamuolewi na Waafrika wenzenu na wengi ni Mama wa nyumbani (natania). Dayaspora wives work several  shifts in the cold and spend the  money to support their husband's  business ventures in Africa. Them ones who want something back home, they want to become somebody somewhere kule kwa Motherland.  Mnakubaliana vema tu kuwa mara 4 kwa mwaka yeye atakuwa anaenda Tanzania au Kenya(depends on their origin) na kukaa huko kwa wiki 2 mpaka mwezi "kusimamia" Mradi/Biashara,  hiyo ni kila baada ya miezi 3.                                       picha kutoka gazeti la The Telegraph*? Kwasababu ya yeye kurudi kwao/kwenu mara kwa mara ni wazi kuwa haingizi kipato cha kutosha na hivyo yeye sio breadwinner isipokuwa wewe mkewe. Unajitolea mhanga ukiamini...

Enzi tulitongozwa uchochoroni...

Miaka 10 iliyopita mlitongozana kwa texts au kwa sauti baada ya kuona picha, nasikia siku hizi wala hamtongozwi kabisa au nyie ndio mmekuwa watongozaji. Wanawake wamekua wawindaji, watafutaji, wapiganaji....wanaume wanafanya nini?  Basi sie "Mid Gen X" a.k.a Xennials a.k.a MillenX (tulizaliwa 1975-85) tulikuwa tunakimbiliwa huku tunaitwa " oyaa mrembo" au "oyaa dada'ke (weka jina la kaka yako)" au hey Binti (weka jina la Baba yako), kama jamaa humtaki/hakuvutii unakimbia kama athletes au unaingia kwenye nyumba yeyote unatulia mpaka jamaa apitilize au ageuze na kurudi kijiweni, then unaendelea na safari zako au inatokea mtu kwenye nyumba hiyo anakisindikiza so unakuwa pretected. Kama jamaa unamkubali basi unapunguza mwendo so anakufikia haraka.  Mnatembea huku anakuuliza maswali kisha mnafika kichochoroni(hakuna watu wengi) then anashusha mistari yake...unadengua-dengua pale na kujiringisha(hiba ya kike) huku unachora chini au unatafuna kucha...unamuang...

Asking for money, mmepoteza aibu online?

Majuzi nilikuwa nakatiza mitaa ya YouTube  nikitafuta best  Female TV talk show Bongo Tanzania baada ya kukumbuka enzi nikiwa msichana kulikuwa na kipichi cha wanawake, siku mbuki jina wala Host wake ila Jaquline Ntuyabaliwe (sasa Mrs Mengi) alikuwa mshiriki, ilidumu kama episodes 3 hivi(kila Ijumaa/Jumamosi)..unfortunately sikupata nilichokuwa natafuta ila  nikakutana na podcast/Youtube Channel ya Salama, nikawa nasikiliza mazungumzo na mgeni wake, which was quite interesting then kwa chini I saw there were kijibango anaomba "kuchangiwa" as in donate to the channel/podcast, I thought these people have no mshipa wa aibu.  Am used to other youtubers asking for money or as they demand "cash Up me:, "donate first ndio nitaanza kuongea", "join my channel  for elfu 3(£1) kwa mwezi to get exclusive"...but Dada si Muajiliwa kule Sekta ya private which they pay better than Serikalini...No? au mazungumzo yake na Mastar ni side haso?  Huwa najiuliza, I (you) su...

Endelea mtongoza Wife...

Ni kawaida kwako Mume (na jamii kwa ujumla) kutegemea mkeo afanye kila awezalo kuifanya ndoa kusimama utasema kajioa mwenyewe. Kuna siku nikaamua kugugo matatizo ya Ndoani, kila maelezo niliyoyapata kwa Kiswahili na Kiingereza, mzigo wa kuweka mambo sawa wenye Muungano huo alibebeshwa mke.   Hakukua na maelezo ya kutosha ambayo yanamsaidia Mume kutatatua matatizo ya ndoa zaidi ya nini afanye akishindwa kusimamisha, Mke na Mama nani nimpende? au nini cha kufanya ikiwa anamaliza haraka? Vipi kuhusu nini cha kufanya ikiwa umemuudhi mkeo? Nini mbadala wa kumnunia/fokea/ignore mke wangu, kitu gani nifanye kukabiliana na mzunguuko wa hedhi wa mke wangu baada ya kupevusha pale anapokaribia Siku zake(sio za kufa bali Hedhi) n.k.? Kuna mengi kwenye ndoa zaidi ya Ego, Mama yako na Uume wako.     Kwenye blog hii tutakumbushana mengi tu ambayo hayahitaji uekisipati wa jinsia bali ni uelewa wa kawaida tu wa kusomana kwa pande zote mbili. Nakumbuka enzi nilipokuwa Twitter kuna wakaka w...

Saikolojia ni Sayansi rahisi, you need to heal...

...huwa wanamaanisha nini? ku-heal ndio kukoje wakati huna matatizo ya kiafya(kimwili)?  Kuna maneno watu wa mitandaoni wanapenda kuyatumia ili kuonekana wajuzi au wana upeo ama wana akili/wasomi(kila mtu anataka kuonekana hivyo), unakuta mtu anajieleeeeeza halafu hakuna anachoelezea, anajazia tu maneno ambayo yana-sound vizuri au kisomi ama yale "clinical" yanayotumiwa zaidi ya Wanasaikolojia(wale wenye Leseni ya kutoa Huduma hiyo baada ya kumaliza masomo na kufuzu kwa kiwango cha phD) au Madaktari wa Akili Sisi tuliosoma "Social Science" kama sehemu ya Kozi nyingine hatupaswi ku-act kama vile ni Wanasaikolojia, ni kama Sheria kuna sehemu unaijua na unaweza kuizungumzia lakini wewe sio mwanasheria, uliisoma tu kama sehemu ya Kozi yako na sio Kuisomea. Huezi amini leo ndio nimeelewa kwanini Wanasheria wa Bongo huitana "Mwanasheria Msomi". Juzi hapa nilikuwa nasikiliza PodCast(yeah them ones) kuhusu malezi ya watoto kutoka kwa "wataalamu", kukawa ...

Tangu umefunga ndoa, ume-improve...

 ..Mchezo au upo vile vile? Kwamba ya nini ni-showcase  au ujiboreshe wakati  umeshampata, ni wako mpaka kifo? Sio sasa ni wangu wacha ni practise nae zaidi na time to time ni showcase niliyofuzu? nayo hapana? Ndoa ikibuma je utaanza kujifunza upya?  hehehehe hawa wa siku hizi hawajui kusubiri, yaani hata muda wa ku-show off maujuzi hupewi.....ukitoka na hujalipia  meal, umeachwa(wakati haukuwa na uhusiano nae)....hii kwa wote, wewe na mkeo/mmeo.  Natambua kuna kubadilika au tuseme kukua(inategemea na umri mliofunga ndoa)....uboreshaji  wa tabia au mtindo wa maisha ni jambo muhimu, maana huwezi kuishi kama kijana/binti wa miaka 32 wakati sasa una miaka 47...Wataalamu wanasema kuwa Uhusiano haubadiliki bali wenza ndio hubadilika, mimi nabisha kwasababu ninyi mkibadilika/kua ni wazi kuwa mahitaji yenu yanabadilika na hivyo uhusiano mzima kubadilika.  Mfano; Uhusiano wenu ulivyokuwa kabla ya kufunga ndoa ni tofauti na sasa mmefunga ndoa, na uhusiano ...

Imani ya Dini ni Msingi mzuri kulea watoto....

  Pamoja na kusema hivyo haina maana kuwa Dini ndio kimbilio kwasababu ukizidisha huko Dinini pia unaweza kuongeza viungo kwenye matatizo yako ya akili au kuongezea mengine. Unapokuwa unafuata Imani ya Dini (Traditional Churches na Uislamu, hao matawi ya ukristo wa kisasa aka MATAPELI mie siwatambui) inakusaidia kuishi kwa heshima na kufuata princimples zake, unajua nini chakufanya(unamkimbilia Mungu) unapopata matatizo   mfano kupoteza kazi, migogoro kwenye urafiki, wazazi, ndoa, ndugu au hata pale unapoyumba kiimani.   Sio tu kwamba unakuwa na kimbilio (Mungu) bali pia unakuwa na Community kutokana na Asilia yako(Kabila) ambayo kwa kiasi kikubwa mnakuwa mnajadili masuala mbali mbali ya kimaisha na mnakuwa na activities hata kama ni mara moja kwa Mwaka, mnakuwa karibu kwavile mnamisingi inayofanana, mnaiheshimu na hivyo inakuwa rahisi kuepuka “Drama” ambazo ni chachu ya matatizo ya Akili.     Kutokana na muibuko wa social media, kumekuwa na watu wakipea...

Jinsi ya kurudisha Furaha Ndoani 2...

  Yafuatayo yatakusaidia kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu ikiwa mtashirikiana na kuyafanyia kazi. Yote haya mmeishawahi kuyaishi hivyo hakuna ugumu/jipya, sema tu mmezeoana so mnayachukulia kawaida, kwamba hayana "maana/umuhimu" kwa sasa.   -Wote; Acha yaliyopita huko huko yalikopita, kamwe usiayarudishe tena kwasabau tu unataka kushinda mabishano au unataka kumkumbusha mwenzio ni kiasi gani umemsamehe au namna gani alikuwa bwege hapo zamani za kale ili kumshusha na kumuumiza hisia zake(huo ni utoto).   -Wote; Unakumbuka enzi zile kabla hamjawa wazazi? Mlikuwa lovers, natambua hii inaweza kuwa ngumu hasa kwa sisi wanawake(wake)kwasababu katika haki halisi tumebadilika kiakili, kimwili na kiafya. Uzazi ni kujitolea mhanga, uzazi unakuja na trauma sio kimwili tu bali kiakili, Uzazi unabadilisha namna unamuona mumeo sio kwamba anapoteza umuhimu bali unahisi hakuhitaji tena kwasababu kuna kichanga.   Waume zetu mpo vile vile kimwili kwasababu hamkubeba mimb...

Twitter ya Elon na heka heka zake...

Ni mwaka na wiki kadhaa tangu Elon Musk alazimishwe na "Mahakama" aichukue Twitter  baada ya kutishia kuinunua 2021(for attention) na ni Mwaka  Mmoja na Wiki Sita tangu nami niachane na Twitter(nisome  kama unajali  ). Maisha bila twita yamekua ya kwaida na sijawahi kuhisi kutamani kuchungulia na kusalimia watu wangu ambao huwa  nawakumbuka mara kwa mara na kutabasamu kutokana na vichekesho au jinsi tulivyokuwa tunaelewana, kupishana na kushangaa pamoja. Hey I miss you on twita too. Sasa juzi hapa nikaona habari kwamba Elon anataka kubadilisha Kindenge na kuwa Eksi(huenda tayari imekuwa hivyo), nikaudhika na kuombea Twita ikufe kabisa na kubaki kumbukumbu, maana ni aibu hata kusema niliwahi kuwa Twita tangu mwanzo miaka 17 iliyopita. Ilikuwa jamii nzuri sana na kamwe sitoisahau kama ilivyokuwa DHB(Dar Hot Board)/DHW(Dar hot Wire), JamiiForum na Facebook. Nimesikia kuna mabadiliko mengi ambayo nilijua yatatokea kutokana na jinsi Elon anajibeba. Elon n...

Jinsi ya kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu!

Kumbuka sababu kuu ya ninyi kuwa pamoja ni mapenzi na sababu ya kufunga Ndoa ni kwavile mnapendana na mnataka kuishi pamoja kwa furaha. Ulipenda na ukataka kupendwa na kufurahia Muungano wenu. Sasa kama hiyo ndio sababu kuu, kuna umuhimu gani wa kuendelea kuishi Maisha ya ndoa wakati hakuna furaha? Utasema Mapenzi, kwasababu mapenzi hayaishi obviously, jinsi mnavyozidi kuishi pamoja ndivyo ambavyo unapata sababu nyingine nyingi kwanini unapenda Mume/Mkeo.   Kuna wakati unaweza usipendezwe na mumeo/mkeo kutokana na matendo yake au kutokana na jinsi alivyokujibu/ongea nawe au kafanya jambo Fulani hukubaliani nalo, hii hali hutoweka mara akiomba radhi au wewe ukiamua kudharau. Hali hiyo haiondoi mapenzi yako kwa mume/mkeo.   Ule msemo wa watu wa social media kuwa “my happiness comes first” au “I choose me” ni kwa wale ambao hawana Imani (hawamuogopi Mungu) ni single au wapo kwenye Ndoa mbaya za unyanyaswaji, vipigo, mateso na masimamngo. Sie wengine ambao wenza wetu wamebad...

Kufananisha/linganisha relationship...

 ,,,au yaliyopita si ndwele tugange ya jayo? Ikiwa umetoka Kimataifa (mbali sio nchi za jirani) halafu baadae ukajaribu nyumbani na kubaki huko kimapenzi ili kuepuka kufuta Race ya watu weusi unakuwa na uzoefu tofauti au tuseme kacha ya kupendwa na kujaaliwa na akupendae tofauti kabisa. Ni kama vile mategemeo yako(maisha uliyozoeshwa) yanakuwa hayana nafasi, sometimes unaeza  jaribu kuyafanya wewe badala ya ku-receive ukitegemea mweza atakusoma ili akupe upatiacho? unatoka bila. Mwanzoni kabisa unaeza usijali sana kwasababu penzi ni upofu obviously, ila jinsi mahusiano yanavyozidi kukua nakuota mizizi unaanza kugundua kuwa watu wa nchi za mbali wanajali zaidi na wanaonyesha mapenzi zaidi kuliko wa nyumbani(inawezekana wanaogopa kuonekana wabahuzi). Kwa kawaida unaambiwa usifananishe/linganishe ila kama ulikotoka huko Mataifa ya mbali kulikuwa ni furaha  na "kula bata" zaidi ya maumivu kihisia na huzuni...unajikita tu unarudi na kuanza kukumbukia(hulinganishi bali unakumbu...