Skip to main content

Posts

Showing posts from 2023

Diaspora Wives...

...the long suffering ones wa US, UK and Canada nyie wa Scandinavia, Spain, Italy, Germany, etc hamuolewagi...wait, huwa hamuolewi na Waafrika wenzenu na wengi ni Mama wa nyumbani (natania). Dayaspora wives work several  shifts in the cold and spend the  money to support their husband's  business ventures in Africa. Them ones who want something back home, they want to become somebody somewhere kule kwa Motherland.  Mnakubaliana vema tu kuwa mara 4 kwa mwaka yeye atakuwa anaenda Tanzania au Kenya(depends on their origin) na kukaa huko kwa wiki 2 mpaka mwezi "kusimamia" Mradi/Biashara,  hiyo ni kila baada ya miezi 3.                                       picha kutoka gazeti la The Telegraph*? Kwasababu ya yeye kurudi kwao/kwenu mara kwa mara ni wazi kuwa haingizi kipato cha kutosha na hivyo yeye sio breadwinner isipokuwa wewe mkewe. Unajitolea mhanga ukiamini...

Enzi tulitongozwa uchochoroni...

Miaka 10 iliyopita mlitongozana kwa texts au kwa sauti baada ya kuona picha, nasikia siku hizi wala hamtongozwi kabisa au nyie ndio mmekuwa watongozaji. Wanawake wamekua wawindaji, watafutaji, wapiganaji....wanaume wanafanya nini?  Basi sie "Mid Gen X" a.k.a Xennials a.k.a MillenX (tulizaliwa 1975-85) tulikuwa tunakimbiliwa huku tunaitwa " oyaa mrembo" au "oyaa dada'ke (weka jina la kaka yako)" au hey Binti (weka jina la Baba yako), kama jamaa humtaki/hakuvutii unakimbia kama athletes au unaingia kwenye nyumba yeyote unatulia mpaka jamaa apitilize au ageuze na kurudi kijiweni, then unaendelea na safari zako au inatokea mtu kwenye nyumba hiyo anakisindikiza so unakuwa pretected. Kama jamaa unamkubali basi unapunguza mwendo so anakufikia haraka.  Mnatembea huku anakuuliza maswali kisha mnafika kichochoroni(hakuna watu wengi) then anashusha mistari yake...unadengua-dengua pale na kujiringisha(hiba ya kike) huku unachora chini au unatafuna kucha...unamuang...

Asking for money, mmepoteza aibu online?

Majuzi nilikuwa nakatiza mitaa ya YouTube  nikitafuta best  Female TV talk show Bongo Tanzania baada ya kukumbuka enzi nikiwa msichana kulikuwa na kipichi cha wanawake, siku mbuki jina wala Host wake ila Jaquline Ntuyabaliwe (sasa Mrs Mengi) alikuwa mshiriki, ilidumu kama episodes 3 hivi(kila Ijumaa/Jumamosi)..unfortunately sikupata nilichokuwa natafuta ila  nikakutana na podcast/Youtube Channel ya Salama, nikawa nasikiliza mazungumzo na mgeni wake, which was quite interesting then kwa chini I saw there were kijibango anaomba "kuchangiwa" as in donate to the channel/podcast, I thought these people have no mshipa wa aibu.  Am used to other youtubers asking for money or as they demand "cash Up me:, "donate first ndio nitaanza kuongea", "join my channel  for elfu 3(£1) kwa mwezi to get exclusive"...but Dada si Muajiliwa kule Sekta ya private which they pay better than Serikalini...No? au mazungumzo yake na Mastar ni side haso?  Huwa najiuliza, I (you) su...

Endelea mtongoza Wife...

Ni kawaida kwako Mume (na jamii kwa ujumla) kutegemea mkeo afanye kila awezalo kuifanya ndoa kusimama utasema kajioa mwenyewe. Kuna siku nikaamua kugugo matatizo ya Ndoani, kila maelezo niliyoyapata kwa Kiswahili na Kiingereza, mzigo wa kuweka mambo sawa wenye Muungano huo alibebeshwa mke.   Hakukua na maelezo ya kutosha ambayo yanamsaidia Mume kutatatua matatizo ya ndoa zaidi ya nini afanye akishindwa kusimamisha, Mke na Mama nani nimpende? au nini cha kufanya ikiwa anamaliza haraka? Vipi kuhusu nini cha kufanya ikiwa umemuudhi mkeo? Nini mbadala wa kumnunia/fokea/ignore mke wangu, kitu gani nifanye kukabiliana na mzunguuko wa hedhi wa mke wangu baada ya kupevusha pale anapokaribia Siku zake(sio za kufa bali Hedhi) n.k.? Kuna mengi kwenye ndoa zaidi ya Ego, Mama yako na Uume wako.     Kwenye blog hii tutakumbushana mengi tu ambayo hayahitaji uekisipati wa jinsia bali ni uelewa wa kawaida tu wa kusomana kwa pande zote mbili. Nakumbuka enzi nilipokuwa Twitter kuna wakaka w...

Saikolojia ni Sayansi rahisi, you need to heal...

...huwa wanamaanisha nini? ku-heal ndio kukoje wakati huna matatizo ya kiafya(kimwili)?  Kuna maneno watu wa mitandaoni wanapenda kuyatumia ili kuonekana wajuzi au wana upeo ama wana akili/wasomi(kila mtu anataka kuonekana hivyo), unakuta mtu anajieleeeeeza halafu hakuna anachoelezea, anajazia tu maneno ambayo yana-sound vizuri au kisomi ama yale "clinical" yanayotumiwa zaidi ya Wanasaikolojia(wale wenye Leseni ya kutoa Huduma hiyo baada ya kumaliza masomo na kufuzu kwa kiwango cha phD) au Madaktari wa Akili Sisi tuliosoma "Social Science" kama sehemu ya Kozi nyingine hatupaswi ku-act kama vile ni Wanasaikolojia, ni kama Sheria kuna sehemu unaijua na unaweza kuizungumzia lakini wewe sio mwanasheria, uliisoma tu kama sehemu ya Kozi yako na sio Kuisomea. Huezi amini leo ndio nimeelewa kwanini Wanasheria wa Bongo huitana "Mwanasheria Msomi". Juzi hapa nilikuwa nasikiliza PodCast(yeah them ones) kuhusu malezi ya watoto kutoka kwa "wataalamu", kukawa ...

Tangu umefunga ndoa, ume-improve...

 ..Mchezo au upo vile vile? Kwamba ya nini ni-showcase  au ujiboreshe wakati  umeshampata, ni wako mpaka kifo? Sio sasa ni wangu wacha ni practise nae zaidi na time to time ni showcase niliyofuzu? nayo hapana? Ndoa ikibuma je utaanza kujifunza upya?  hehehehe hawa wa siku hizi hawajui kusubiri, yaani hata muda wa ku-show off maujuzi hupewi.....ukitoka na hujalipia  meal, umeachwa(wakati haukuwa na uhusiano nae)....hii kwa wote, wewe na mkeo/mmeo.  Natambua kuna kubadilika au tuseme kukua(inategemea na umri mliofunga ndoa)....uboreshaji  wa tabia au mtindo wa maisha ni jambo muhimu, maana huwezi kuishi kama kijana/binti wa miaka 32 wakati sasa una miaka 47...Wataalamu wanasema kuwa Uhusiano haubadiliki bali wenza ndio hubadilika, mimi nabisha kwasababu ninyi mkibadilika/kua ni wazi kuwa mahitaji yenu yanabadilika na hivyo uhusiano mzima kubadilika.  Mfano; Uhusiano wenu ulivyokuwa kabla ya kufunga ndoa ni tofauti na sasa mmefunga ndoa, na uhusiano ...

Imani ya Dini ni Msingi mzuri kulea watoto....

  Pamoja na kusema hivyo haina maana kuwa Dini ndio kimbilio kwasababu ukizidisha huko Dinini pia unaweza kuongeza viungo kwenye matatizo yako ya akili au kuongezea mengine. Unapokuwa unafuata Imani ya Dini (Traditional Churches na Uislamu, hao matawi ya ukristo wa kisasa aka MATAPELI mie siwatambui) inakusaidia kuishi kwa heshima na kufuata princimples zake, unajua nini chakufanya(unamkimbilia Mungu) unapopata matatizo   mfano kupoteza kazi, migogoro kwenye urafiki, wazazi, ndoa, ndugu au hata pale unapoyumba kiimani.   Sio tu kwamba unakuwa na kimbilio (Mungu) bali pia unakuwa na Community kutokana na Asilia yako(Kabila) ambayo kwa kiasi kikubwa mnakuwa mnajadili masuala mbali mbali ya kimaisha na mnakuwa na activities hata kama ni mara moja kwa Mwaka, mnakuwa karibu kwavile mnamisingi inayofanana, mnaiheshimu na hivyo inakuwa rahisi kuepuka “Drama” ambazo ni chachu ya matatizo ya Akili.     Kutokana na muibuko wa social media, kumekuwa na watu wakipea...

Jinsi ya kurudisha Furaha Ndoani 2...

  Yafuatayo yatakusaidia kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu ikiwa mtashirikiana na kuyafanyia kazi. Yote haya mmeishawahi kuyaishi hivyo hakuna ugumu/jipya, sema tu mmezeoana so mnayachukulia kawaida, kwamba hayana "maana/umuhimu" kwa sasa.   -Wote; Acha yaliyopita huko huko yalikopita, kamwe usiayarudishe tena kwasabau tu unataka kushinda mabishano au unataka kumkumbusha mwenzio ni kiasi gani umemsamehe au namna gani alikuwa bwege hapo zamani za kale ili kumshusha na kumuumiza hisia zake(huo ni utoto).   -Wote; Unakumbuka enzi zile kabla hamjawa wazazi? Mlikuwa lovers, natambua hii inaweza kuwa ngumu hasa kwa sisi wanawake(wake)kwasababu katika haki halisi tumebadilika kiakili, kimwili na kiafya. Uzazi ni kujitolea mhanga, uzazi unakuja na trauma sio kimwili tu bali kiakili, Uzazi unabadilisha namna unamuona mumeo sio kwamba anapoteza umuhimu bali unahisi hakuhitaji tena kwasababu kuna kichanga.   Waume zetu mpo vile vile kimwili kwasababu hamkubeba mimb...

Twitter ya Elon na heka heka zake...

Ni mwaka na wiki kadhaa tangu Elon Musk alazimishwe na "Mahakama" aichukue Twitter  baada ya kutishia kuinunua 2021(for attention) na ni Mwaka  Mmoja na Wiki Sita tangu nami niachane na Twitter(nisome  kama unajali  ). Maisha bila twita yamekua ya kwaida na sijawahi kuhisi kutamani kuchungulia na kusalimia watu wangu ambao huwa  nawakumbuka mara kwa mara na kutabasamu kutokana na vichekesho au jinsi tulivyokuwa tunaelewana, kupishana na kushangaa pamoja. Hey I miss you on twita too. Sasa juzi hapa nikaona habari kwamba Elon anataka kubadilisha Kindenge na kuwa Eksi(huenda tayari imekuwa hivyo), nikaudhika na kuombea Twita ikufe kabisa na kubaki kumbukumbu, maana ni aibu hata kusema niliwahi kuwa Twita tangu mwanzo miaka 17 iliyopita. Ilikuwa jamii nzuri sana na kamwe sitoisahau kama ilivyokuwa DHB(Dar Hot Board)/DHW(Dar hot Wire), JamiiForum na Facebook. Nimesikia kuna mabadiliko mengi ambayo nilijua yatatokea kutokana na jinsi Elon anajibeba. Elon n...

Jinsi ya kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu!

Kumbuka sababu kuu ya ninyi kuwa pamoja ni mapenzi na sababu ya kufunga Ndoa ni kwavile mnapendana na mnataka kuishi pamoja kwa furaha. Ulipenda na ukataka kupendwa na kufurahia Muungano wenu. Sasa kama hiyo ndio sababu kuu, kuna umuhimu gani wa kuendelea kuishi Maisha ya ndoa wakati hakuna furaha? Utasema Mapenzi, kwasababu mapenzi hayaishi obviously, jinsi mnavyozidi kuishi pamoja ndivyo ambavyo unapata sababu nyingine nyingi kwanini unapenda Mume/Mkeo.   Kuna wakati unaweza usipendezwe na mumeo/mkeo kutokana na matendo yake au kutokana na jinsi alivyokujibu/ongea nawe au kafanya jambo Fulani hukubaliani nalo, hii hali hutoweka mara akiomba radhi au wewe ukiamua kudharau. Hali hiyo haiondoi mapenzi yako kwa mume/mkeo.   Ule msemo wa watu wa social media kuwa “my happiness comes first” au “I choose me” ni kwa wale ambao hawana Imani (hawamuogopi Mungu) ni single au wapo kwenye Ndoa mbaya za unyanyaswaji, vipigo, mateso na masimamngo. Sie wengine ambao wenza wetu wamebad...

Kufananisha/linganisha relationship...

 ,,,au yaliyopita si ndwele tugange ya jayo? Ikiwa umetoka Kimataifa (mbali sio nchi za jirani) halafu baadae ukajaribu nyumbani na kubaki huko kimapenzi ili kuepuka kufuta Race ya watu weusi unakuwa na uzoefu tofauti au tuseme kacha ya kupendwa na kujaaliwa na akupendae tofauti kabisa. Ni kama vile mategemeo yako(maisha uliyozoeshwa) yanakuwa hayana nafasi, sometimes unaeza  jaribu kuyafanya wewe badala ya ku-receive ukitegemea mweza atakusoma ili akupe upatiacho? unatoka bila. Mwanzoni kabisa unaeza usijali sana kwasababu penzi ni upofu obviously, ila jinsi mahusiano yanavyozidi kukua nakuota mizizi unaanza kugundua kuwa watu wa nchi za mbali wanajali zaidi na wanaonyesha mapenzi zaidi kuliko wa nyumbani(inawezekana wanaogopa kuonekana wabahuzi). Kwa kawaida unaambiwa usifananishe/linganishe ila kama ulikotoka huko Mataifa ya mbali kulikuwa ni furaha  na "kula bata" zaidi ya maumivu kihisia na huzuni...unajikita tu unarudi na kuanza kukumbukia(hulinganishi bali unakumbu...

Mama/Baba wa mtoto wa kwanza, sio wewe wa sasa!

  Unatambua kuwa ulivyo sasa kama mzazi ni tofauti na ulivyokuwa ulipoanza kuwa Mama/Baba? hasa kama watoto wako wamepishana kiasi fulani kiumri, sio tu ni kwasababu wewe na mumeo/mkeo mmkua bali pia uzoefu wenu kama wazazi unabadilika kuendana na umri wa watoto wenu. Sasa hivi unaongea na mwanao wakubwa kama watu "mzima" wenzako kwa kuwasikiliza, kuwaheshimu na wakati huo huo kuwafunza na kuwakumbusha  kuwa wao bado  ni watoto na wewe ni mzazi mwenye urafiki ila sio rafiki yao na bila kusahau kuwakumbushia uliyowafunza awali. Kwa wadogo zao ambao tuseme labda ndio toddlers, hutowalea kama ulivyowalea hao ndugu zake waliozaliwa kabla yake, kwa sababu sasa wewe ni Mjuzi wa malezi, unafanya mambo bila kuomba ushauri wala kuuliza kwa Mama au Dada au vitabu. Hakuna kinachokushangaza kwasababu yote umepitia na kwa jinsia zote mbili, unajiamini balaa. Wiki iliyopita nilipata muda wa kufikiria(surpriiiise I can actully think) jinsi nilivyobadilika tangu nilipokuwa mama kwa mara ...

Chochote ukijuacho/ulichopitia make money out of it...

 ...uza uzoefu wako iwe wa mapenzi, magonjwa, uzazi, matatizo ya familia au hata disoders na matatizo ya akili! Mie sikujua kama kuwa home body(which I am) ina jina lake na kuna watu wanatoa "courses" kuwafunza wenzao ambao nao ni introverts(hawapendi watu wala kujichanganya nao kwa zaidi ya lisaa limoja) namna ya kuondokana na hali hiyo. Hakuna mtu anaweza kubadilisha vile ambavyo umeumbwa....kuwa mwenye aibu, mapole, mkali, mtembezi, mpenda ku-party, usiopenda ku-party n.k. binadamu tunatofautiana na that is okay. Sio sahihi kutumia "kipaji" ambacho honestly huna na hata kama unacho sio muhimu na hakina faida kwa yeynote Duniani halafu ukaanzisha Kozi ili uweze kuwa tajiri, kwanza kwanini unataka kuwa tajiri? na ikiwa kuwa tajiri ni rahisi hivyo kwanini wengi wetu sio matajiri? Kuna ubaya gani kuingiza kiasi cha kutosha kuendesha maisha na kufurahia Holiday na kumaliza matizo yako ya kifedha mwenyewe bila kuwa tajiri? you know, kufanya kazi na biashara pembeni kih...

Mind your Ughaibuni business...

 Nakumbuka miaka michache nyuma nilipokuwa Twita alijitokeza Binti mmoja nakuanza kuwaambia watu wa Ughaibuni(Nchi za Ulaya na Marekani) kuachana na Siasa za Tanzania na kufurahia maisha yako "mazuri" popote walipo Ulaya(popote nje ya Afrika)....natabua kua sio kila mtu Ulaya ana maisha mazuri(inategemea sababu yako ya kuishi huko) lakini nakubaliana nae. Wabongo wengi walimkandya/ponda kwa kudai kuwa anataka attention ya Bongo Twita sababu hakuna mtu anamfahamu, binti alijitetea na kusimamia alichokisema ambacho hakika nakubaliana nae. Watu wa Ughaibuni ambao hawaishi Tanzania  wanaguswa na Mabadiliko ya kisisa yanayoendelea Tz, hawa ni wachache sana ambao wana Biashara na pengine kumiliki ardhi(nyumba, mshamba n,k,) na wachache ambao hurudi nyumbani mara kwa mara, wengine wapo wapo tu na ndio huwa na kelele zaidi kuhusu Tanzania na Siasa zake. Unadhi utabadilisha nini  Tz na Kodi hulipi? Mind your Ughaibuni business and enjoy your High tax, cost of living and free Heath...

Kila Familia/Ukoo ina mtu huyu...

  ...Kikao cha familia, hakianzi mpaka Dada/Kaka aje... Kwenye kila familia (hasa kama mpo wengi) huwa kunakuwa na ndugu mmoja ambae anajipa cheo na anataka abaki pale kwa njia na namna yeyote ile. Achana na wale ndugu wakubwa ambao automatically wanapewa "uongozi" na Wazazi...kuna yule mmoja wenu huibuka tu na kuanza kujiona ndio mwenye akili, ndio fashionable, Mfuata maadi, anajua kila kitu maishani, anafahamiana na watu wenye Majina(maarufu/viongozi), Msomi n.k, mara nyingi huwa mtoto wa Tatu mpaka Tano hivi kuzaliwa. Huyu mtu huangalia mapungufu kwenye familia halafu ana pursue kitu ambacho kitamfanya awe tofauti na ninyi wote. Kama ni Elimu basi atasoma kwa bidii na juhudi zote ili awapite wote, kama  ni mafanikio kiuchumi atakuwa juu zaidi ya wote humo familiani(hii itampa nguvu ki-social hasa kwenye mikutano ya familia), likija suala la marafiki, yeye atakuwa ni rafiki zaidi kwa marafiki zenu wote ila rafiki zake ni wake peke yake...kwenye suala la wanawake/wanaume...

Mtoto wa kambo...part 2.

Mtoto wa kambo...part 2. Ukiachana na misukosuko ya txt na simu za mama mtoto, kuna suala la kufanya mapenzi ambalo wengi huwa hawalizungumzii sababu wanaogopa kuambiwa hawajiamini. Unless wewe una-elements za kichawi au zile za ukimada ndio utaweza kuwa na a very good sex life on the daily (kila anapowasiliana na mkimama wake wa awali kabla yako, unapata mhamko).   Vinginevyo bana the thought of dudu kuingia kwa mwanamke mwingine bila kinga itakuondolea hamu na ile desire kwa mpenzi wako inatoweka, unaanza kujiambia “omg nimekosea kuchagua”, kama umeshawi humuona ex unaanza kujiuliza kama jamaa ana type na wewe umefanana na Ex wake, unapata kinyaa…unawaza “niingie mitini nini?”, unaendelea kuwaza “yaani ndio nimejitolea mhanga maisha yangu yote yatakuwa kupambana na drama za ex”, “si bora niwe single and happy” …yaani akili haitulii. Na kama ujuavyo bila akili kutulia, hakuna ushirikiano na bila ushirikiano tendo hakuna, ukifanya linakuwa doro.     Kwa uzoefu wangu...