Monday, 30 June 2014

Uelewa na kumbukumbu ya Mtoto.

Nilipotobolewa Masikio nilikuwa na Miezi Sita (kwa Mujibu wa Mama), alienitoboa ni Mama wa Kimasai na aliekuwa kanibeba/shika ni Bibi yake Mama.
Sikumbuki maumivu, lakini nakumbuka nililia sana nilipomuona Mama wa Kimasai na Shanga zake na Masikio yakiwa marefu "kwenda chini".

Siku niliyomsimulia Mama kuhusu hiyo siku ya tukio (nilikuwa teen na bado naikumbuka)...alinishangaa na kusema kuwa lazima nilisikia akisimulia watu, mtoto wa miezi Sita hawezi kukumbuka.
Nilipokuwa na miaka 3 au zaidi, tulikuwa Mjini Mbeya....Mama, Mimi, Mjomba na watu wengine tulikuwa tunapita pembezoni mwa Mto. Mjomba wangu alinibeba na kutishia kunirusha kwenye Maji(Mto)....Nadhani ndio maana naogopa Maji....Safari zangu ni za Anga, Reli na Barabara, mie Meli sijui Boti sipandi....Mtumbwi? Bora uniue.
The point is, Mtoto anauwezo wa kutunza kumbukumbu kuanzia umri mdogo sana kuliko tunavyoaminishwa na "Mzungu" the Shenzi.
Sio unafanya mambo ukidhania kuwa "aah bado mtoto, hajui kitu"....heee utakuja kukumbushwa mambo wewe ubaki uduwae(is that word?).
Mzungu (as usual, anatulazimisha/aminisha) anasema mtoto anaanza kuelewa na kutunza kumbukumbua akiwa na Miaka mitatu.
Inawezekana kweli, maana Babuu (my 1st born ni 3yrs) juzi kamwambia Mdogo wake "Mummy will go to hospital again and bring a baby".....SINA MIMBA, nimemaliza kuzaa mie!
.....ila Mdogo wake alipokuwa anazaliwa (sikujali nani yupo anafanya nini...KIFO hakichezewi) alikuwepo na alikuwa na miaka 2 na ushehe! out of topic kimtindo ila umenielewa.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 26 June 2014

Kaja for a reason....

Wacha kujipa Moyo.....hakuna mtu anajiijia tu maishani mwako isipokuwa wewe unaruhusu awe/aingie Maishani mwako.


Ukisema umefanya maamuzi mabaya ya kuruhusu huyo particular mtu maishani mwako nitakuelewa.


Kumbuka wewe ndio responsible kwa kila kinachotokea maishani mwako iwe ni maamuzi mazuri au mabaya.....beba mzigo na ujipange upya, sio kujipa-jipa moyo...eti sababu Mzungu anakuaminisha kuwa "people come in your life for a reason".

Kuna watu wanaishi ili kuharibu maisha ya watu, ndio furaha yao. Wengine walikosa mapenzi na malezi bora kutoka kwa Wazazi/Walezi matokeo yake wanayatafuta waliyoyakosa kwa kuharibu maisha ya wenzao.....nakadhalika.

Sasa ni juu yako kumsoma yeyote anaekuja maishani mwako na kumruhusu aingine kama Rafiki, Mpenzi, Jamaa ( wale mliooa/olewa Ukoo Mmoja), ukigundua tu kuwa umekosea basi haraka muepuke kabla hajaharibu zaidi.


Nikupe mfano?....I looooooooooove mifano hihihihihi(watu tunauelewa tofauti, bila mifano wengine tunatoka kapa).

Unaishi maisha Mzuri tu na Dada/Kaka yako, mnapendana, manashirikiana, saidiana na kushauriana.....Mtu pembeni anapenda maisha mnayoishi kama ndugu au familia. Yeye hana au hakuwahi kuwa karibu hivyo na Ndugu.


Anapiga mahesabu na kugundua kuwa njia pekee ni kuanzisha urafiki na Dada mtu, ili ampate kaka mtu kama Mpenzi kisha avuruge "undugu" wao kwa kuwa Mpenzi wa Kaka yako na hiyo inatakuwa furaha yake.


Mf wa Pili; Wale Wake/Waume wenza....kwamba mmeolewa Ukoo/Familia moja (hatari sana).....kwa vile wewe umeoa/olewa mwisho (kabla yao) kwenye Ukoo/Familia husika kwa kawaida unapata attention Mingi kuliko wale "wazee" hata kama Wadogo kwako bado walikuwepo kabla yako kwenye Ukoo/Familia hiyo.


Ili kuua attention au upendo unaoupata kutokana na Upya wako, wanaaza kuvuruga kwa kutumia njia zote zilizopo Chini ya Mbingu.

Mf wa Tatu na wa Mwisho; Mpenzi....baada ya safari zako zote unahisi hapo sasa ndio umefika mwisho wa Reli Kasuluuuuuu(is it?) Anyway! Yaani umependa.

Mpenzi anabadilika kutoka Mpenzi na kuwa Mtawala.....need I say more? Aiiiii Kimbia.

Hakuna ajae maishani mwako ili kukufunza au kukusijui nini na nini....wote unawaruhusu mwenyewe kwa Upumbavu au Ujinga wako au kutokuwa makini(unafanya maamuzi mabaya).

Hakuna mtu aliepita kwenye maisha yangu ambae kanifunza kitu, nikigundua wee ni "mzigo" aiii nakugaya....naanza Upya.....actually nafanya hivyo kila mwaka....maisha haya nani anataka mizigo ya stress?!!


Ya leo ndefu eti?

Pole....na babai.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 25 June 2014

Mali ya Familia...

Kuna baadhi yetu tunatabia/kasumba ya kuita Mali za watu kuwa zetu na pengine kuanzisha fujo na kupelekea Vita kubwa ili kila mmoja apate "mgao" wake.


Kwasababu tu Mali ni za Baba/Mama yako au Kaka/Dada yako haikupi haki ya wewe kupata Mgao....wacha papara za kutaka kunijibu, nitakupa mfano ili unielewe vema.

Baba na Mama wameachana wakiwa hawana kitu, Baba kaanzisha uhusiano mwingine na kupata familia "mpya"....mambo yakaenda vema wakawa na Mali za kutosha....wewe uliezaliwa na Mama wa kwanza unadhani una unahaki na Mgao sawa kama watoto waliomo kwenye "familia Mpya"?


Upatikanaji wa Mali za Baba yako na familia yake Mpya unamchango Mkubwa wa Mama yao (familia Mpya) na sio Mama yako (alieachana na Baba yako akiwa hana kitu)....sehemu ya mali utakayoipata ni ndogo sana, tena kama Mke atakubali upatiwe. Mf; wa kwanza.

Mf wa Pili: Dada/Kaka kajipinda na kujituma yeye na Mume/Mkewe na sasa wanamiliki Mali nzito, inakuaje wakubwa/wadogo watu mhesabu kuwa hizo ni Mali za Familia wakati hakuna mchango wenu wala wa Baba na Mama yenu (Wazazi wenu)?


Hata kama umeajiriwa kwenye Kampuni ya Dada/Kaka bado Mali sio ya Familia....usifanye kazi bure ukitegemea kurithi Kampuni....dai Malipo(Mshahara) ili uweze kutengeneza Mali zako. Ukimfanyia ndugu yako tajiri kazi bure ni kwamba anakutumia....kwenye Maendeleo(kutafuta Pesa) hakuna Undugu, dai Malipo.

Wenzetu Wachaga (well naijua familia Moja tu hihihihi)hutumia "Chanzo" kimoja kupeana njia ya Maendeleo Mf: Bwana Shoo ana Duka, analeta mdogo wake....baada ya Miezi kadhaa nae anafungua Duka lake....analetwa mwingine, nae anatoka kivyake kupitia pale pale kwa Kaka....hakuna kungoja Mgao(Urithi).

Mali ya familia ni ile iliyotengenezwa na Mzazi wenu kisha kurithishwa kwa wengine ama waiendeleze kizazi hata kizazi au waiue(kila mtu apate chake afanya yake).


Wacha ku-relax ukiamini siku Dada/Kaka wakienda nitapata Mgao wangu...."Baba/Mama akienda nitapata Mgao wangu".


Jitume kwa jasho lako utengeneze zako, wacha kutegemea Urithi(Uzembe)....I say!

Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 24 June 2014

Weusi mzuri...

If you have to tell us then it isn't....Mambo vipi?Weusi wa Afrika tuna issues zetu ambazo zinasababishwa na Watawala wetu(Siasa)....ila Weusi wa Wamarekani wana issues vichwani mwao kuhusu Weusi wao, yaani wapo ka' Mikorosho vile.

Ujue kunatofauti ya kujivunia ulivyo na kulazimisha watu wajue kuwa unajivunia ulivyo.

Mf: Kuna ulazima gani wa kusema "mimi ni mweusi na ninajivunia" wakati tunakuona wewe ni mweusi, unajipenda, unapendeza na unafanya mambo yako kama watu wengine. Kwanini utulazimishe kutambua kuwa "unajivunia"?

Mf wa pili; Kitu gani kinakufanya uweke "kichwa cha habari" cha video/picha na kusema "beautiful black baby"....kwani ukiandika "baby" au "beautiful baby" haileti maana au hakuna watoto weusi na wazuri isipokuwa huyo wako?

Unatulazimisha kutambua kuwa unajivunia Weusi wako alright, lakini picha/video "unazipausha" ili zionekane na karangi ambako sio kako(weupe).....tukiuliza, unasema "mianga" ya taa za Studio!
Kama unajivunia jambo, iwe Ujinsia (hello Mikorosho, how are you doing? Hihihihihi) au Rangi....huitaji kulazimisha watu kutambua kuwa unajivunia bana....wewe jivunie tu kimoyomoyo.I am fat, black and beautiful......oh oh kuna wale "I am educated, Black Woman and proud".....wee vipi?
Au "I am Black, Jew, Gay and proud"....Thubutuuuuu, hapa lazma ujivunie kimoyomoyo tu!


Heri ya J'Nne.

Babai!
Mapendo tele kwako...

Thursday, 19 June 2014

Kumbukumbu...

Nimekaa hapa nakumbuka watu wote niliosoma nao Msingi na Sekondari kwa Majina yao yote Mawili(la mwanzo na la Mwisho).....nimeambulia kusisinzia.
Darasa Moja tulikuwa. Wanafunzi 200na! Tuligawanywa katika Mikondo 5 yaani A-B-C-D-E-F....shule kubwa ka' Kijiji....hiyo Msingi. Sekondari hatukuwa wengi sana Mikondo ilikuwa Minne.

Sasa mwanamke nkasema ngoja nipime uwezo wa akili yangu sehemu ya kutunza kumbukumbu....nimefeli yaani nimepoteza kumbukumbu hata Miaka 40 sijafika!.

Nikajipa Moyo; labda niagize picha za enzi za shule ili nikiona sura zao niwakumbuke vema, lakini hata hivyo sikupiga picha na kila mtu niliesoma nae kwahiyo haitosaidia. Yaani ndio basi tena.
Nimejisikia vibaya sana....yaani kupoteza kumbukumbu ya sehemu ya Maisha yako ndio inauma hivi?!!!Kama ulisoma na mimi na unanikumbuka eeh! Drop me a line.

Babai...
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 18 June 2014

Msingi/Malezi bora...

Habari gani?

Kuna watu walikosa Malezi(Msingi) bora utotoni, malezi bora sio kula vizuri, kuvaa vizuri na kusoma shule nzuri bali kulelewa katika Mazingira ya Heshima na Adabu (kwako na kwa watu wengine), Staa/Stara, Uvumilivu, Kuridhika, Kutokata tamaa, Utu na Haiba.

Hivi majuzi nimekutana na mtu akaanza nipa stori za mambo na vitu Ghali anayomfanyia Ex wake....nadhani alitaka kufikisha ujumbe kuwa yeye ni mtu wa kujali sana na kutumia Mahela kwakwe sio tatizo.

Kwa bahati mbaya alikuwa hajui kuwa mimi ni Mwanamke (a bit tofauti) sibabaiki na Mahela ya watu kwani naamini ninauwezo wa kutafuta na kupata zangu.....pamoja na kusema hivyo zawadi napokea hihihihihi!

Stori zikaendelea huku nami (kama kawaida) nikiuliza maswali...."Kwanini unamhudumia Ex wakati una mwanamke mpya?"...."Kuna kitu unataka au unapata kutoka kwa Ex"..."Je, Ex ana siri zako nzito unaogopa atazitoa"? n.m(na mengineyo).

Kabla hatujaagana chini ya Ardhi ili kila mtu achukue "tube" ya huko aendako! Jamaa akanambia...."Kwani Di hujamchoka tu mumeo mpaka leo?" Nikamwambia sidhani kama kuna siku nitamchoka....akasema "well siku ikitokea basi kumbuka mie nipo".
Umeona alipotokea? Khafiri Mkubwa kabisa aliekosa malezi (Msingi) bora wa Maisha kutoka kwa Mama yake Mlezi/Mzazi.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 17 June 2014

Phd...

Naitaka sana yaani, sitaki kuzeeka bila kuipata....shughuli inakuja ni lini hasa nitarudi "shule"?Baada ya kupiga mahisabati nadhani by the time nagonga Miaka 50 Mwenye enzi Mungu akibariki mwanangu wa Pili (mwisho) atakuwa kwenye Teen kati hivi na huo ndio utakuwa muda mzuri.
Nia sio kupanda Cheo au kugombea Uwaziri(Ubunge) la hasha! Ni kutimiza Malengo niliyojiwekea kuwa kabla sijazeeka niwe na kaelimu katika levo ya "Udaktari" Dk Dinah blablabla.
Sasa angalau mie nilisomaga (si ndio nkachelewa kuzaa!Nilitaka kula life kabla ya Majukumu).....Mambo ya kutoka Binti wa_____ to Mke na Mama wa_____ in my early 20s haikunivutia....Ningeishi Mimi kama mimi lini sasa eti?!!!
Anyway, kwa wale "baadhi" walioamua kuanza na Mke na Mama wa_____ hu kurudi "shule" baada ya watoto kukua which ni kitu kizuri ila unakuwa "hujayafaidi" maisha ya Usichanani....ule uhuru wa kutokuwa na Majukumu au kufikiria watoto na Mumeo kwenye kila maamuzi ufanyayo.
Baada ya kumaliza malezi ya watoto na kurudi "Darasani", Mwanamke (Wake) huongeza ile hali ya kujiamini kitu ambacho huwa kinawakera sana Wanaume (Waume) na kuwapotezea hali ya kujiamini.
Unakaa Darasani na Vijana eeh....(Wanaovutiwa na Wamama wenye uzoefu hihihihihihi).....Mwanamke unaaza kujisikia na kujiona bado wamo....mara Gym inaanza, Mara routine za Skin care ambazo hujawahi kuzifanya(ulikuwa busy na malezi ya watoto)....mara mavazi na ulaji vinabadilika!

Sio kwamba mwanamke unataka kutoka na Dogo-dogo la hasha! na si kweli kuwa umebadilika bali umemaliza "kulea" na huu ndio wakati wako wa kufurahia "uanamke" wako japo umegonga miaka 50na.
Sasa mie bana, nishafanya yote hayo nilipokuwa in my 20s....well ukitoa hizo routine za kujali Ngozi (nazifanya sasa).....hata nikirudi "shule" nitaendelea tu kutupia Magauni ya Khanga na Vitenge kwa heshima ya Wanangu na Baba yao na Taifa kwa ujumla!.....natania hapo kwenye Vazi.


Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 16 June 2014

Pale Mwenza aongea kwa Code na rafiki zake....

Alafu mkifika nyumbani anaku-de-code-a yote....hapo sasa ama utadanganywa kabisa au utapewa robo ya ukweli(utadanganywa kwa robo tatu).

Unajua upokwenda kutembelea watu mnaofahamiana au unapokuwa kwenye shughuli kwa kawaida inayojumuisha watu mbalimbali baadhi yetu tunaofahamiana/juana sana huongea kwa "Code" au unavutwa pembeni kisha unaambiwa jambo au kuombwa Msaada.

Nia na madhumuni ni ili watu wengine wasielewe, wanasahau kuwa watu tunaupeo tofauti, baadhi "tunadikodi" hapo hapo......wengine ndio mpaka wasubiri "wadikodiwe" na Wenza wao watakapofika nyumbani.

Natumai unaendelea vema, mimi leo bana sijielewi-elewi, yaani ka' nimepigwa au nimefanya kazi ngumu sana ningekuwa kwetu(KissWay) ningesema "nililimishwa" Usiku wa kuamkia leo.


Heri ya Wiki Mpya!

Babai.
Mapendo tele kwako...

Monday, 9 June 2014

Ugumu wa Masomo...

Hisabati....Hisabati....Hisabati!


Sikufanya Mtihani wa Mwisho kwasababu nilijua nitapata LieFu.....sikulitaka Li-F kwenye Cheti changu.

Nikapiga Mahesabu ya namna ya kuepuka F kwenye Cheti changu cha Fom Foo....nikapata jibu deshi-deshi, ila mie nilitaka Deshi moja tu so siku ya Mtihani sikutokea.....nikajipatia Mathematics-!! Nilifurahiiiiiii.

Nazipenda Hesabu (kuhesabu hela na Pea za viatu tu) ila kama somo hapana, sio kwamba nilikuwa siziwezi la hasha! Nilikumbuka Kanuni zote, nilifuata na kupatia njia ili kupata jibu.

Tatizo lilikuja Muda napoteza muda mwingi kuhakiki jawabu matokeo yake najikuta nimefanya Maswali 5 out of 25=Efu...SIPENDI Somo la Hisabati sababu speed ya akili yangu ni a bit slow.

Hakuna kitu kinachoniudhi kama kuishiwa Muda wakati wa Mtihani......Baba (Merehemu) alikuwa ananiambia "ukitaka akili yako iwe "sharp" na kuongeza uwezo wa ku-focus kwenye hesabu, fanya Mzoezi ya Hesabu mahali ambapo kuna kelele nyingi".....nilijaribu na nilifanikiwa nje ya Chumba cha Mtihani tu!


Hofu niliyonayo hivi sasa ni Watoto wangu na Hisabati.....wakihitaji kufundishwa na mimi....hehehehe na hivi nitakuwa Mzee, akili itakuwa on slow motion ya slow motion mode!
Pengine by then kutakuwa na Transplant ya Ubongo. Kama unapenda Hisabati...Power to ya!

Babai...
Mapendo tele kwako...

Friday, 6 June 2014

Michezo ya Utotoni 90s

Jambo!


Msita (Mdako), Dama, Marede, "Amina sasa naomba, turudiane...hayo yamekwisha kipenzi changu" yaani kuruka Kamba....don't you miss them au wewe ulikuwa wa Kishua unashinda kubebelea ma VHS ya akina Comando Kipensi....??

Usiseme ulikuwa unacheza Game, enzi hizo Bongo hakukuwa na Games za Tv achilia mbali PCs....Tv zenyewe zimechanganya 1994.

Nilikuwa mzuri sana kwenye Marede na Mdako(Msita kwa wale wa pande za Shinyanga na Mwanza). Nikikamata Jiwe kwenye Mdako sikosei....kwenye Marede kila Timu ilinitaka mimi (niligombaniwa).Marede ya kujaza Chupa kwa mchanga niliipenda lakini sikuruhusiwa kuicheza kwasababu ya vumbi(Nilikuwa na Pumu). Ila nilikuwa naibia....kisha narudi ndani nimebanwa....kupumua siwezi....jicho limetoka ka' Ndula(unazijua Ndula weyeeeee)....hehehe.
Naishia kuonewa huruma na kupewa na kupewa ile Inhaler, kisha nakuwa nimerudishiwa Uhai.....Nashukuru Imeisha (sijabanwa Tangu nilipofikisha miaka 21).Let's do a get together tucheze Marede eti?!!! Nikutakie MMWMWW(Mwanzo Mzuri wa Mwisho wa Wiki)....


Wiki ijayo takuwa over busy. Usiponiona tambua nimeshikwa.

Babai...
Mapendo tele kwako...

Thursday, 5 June 2014

Heshima kwa Maiti...

Imepotelea wapi? Au ndio kwenda na Wakati?Juzi kati nimekutana na Picha ya Maiti ya Mpendwa wangu....pamoja na familia kufanya kazi ya ziada kuzuia upigaji Picha wa shughuli nzima ya Mazishi achilia mbali Mwili wa Marehemu wa mpendwa wetu zaidi ya alieajiriwa kwa ajili ya kazi hiyo....bado kuna jitu likapiga picha na ku-share online.

Kwasababu hana Uhai tena haina maana kapoteza Haki zake kama Mwanadamu mpaka atakapozikwa(Fukiwa).

Maiti ingeweza ingejisitiri na kupozi ili apendeza au kutokea vizuri zaidi....pia angechagua ni Picha gani itumike kutangaza Tukio lilipolekea Mauti kumfika.

Unapata faida gani ku-publish au ku-share picha ya Maiti?.....kwanini unataka tumkumbuke Marehemu kama Maiti na sio alivyokuwa Hai na mwenye furaha?!!

Unaweza kusema naegemea kwa Waingislishi kwa vile naishi huku na wao hawana utaratibu wa kuonyesha Maiti au kuiaga zaidi ya Jeneza na Picha ya Marehemu alipokuwa hai....nia ni kubaki na kumbukumbu ya yeye na sio Maiti yake.

Maiti inaagwa/angaliwa na wanafamilia au ndugu na jamaa wa karibu (kama watapenda, sio lazima). Lakini hukuti picha za Maiti ya Mpendwa husika kila kona ya Blogs na Magazeti.
Pia wenzetu Waislamu huwa hawatazami/aga Maiti sasa kwanini tusiheshimu Imani yao na kutopiga Picha Maiti zao na kuzisambaza Mitandaoni?.

Kwanza kitu gani kinakufanya uende kwenye Msiba wa watu na Lisimu lako, au Litablet au Likamera?....upo msibani kufariji na kuwapa ushirikiano Wafiwa lakini badala yake...wewe upo busy kuchukua picha na kushare na kuchat online.
Unaenda kwenye tukio(eneo alipofikwa na Mauti), badala ya kutoa ushirikiano upo busy kuchukua picha ya Maiti hatua kwa hatua kisha mbio mwenye liblog/lisite lako.
Hata kama ni Mwandishi wa Habari, hupaswi kutumia Picha za Maiti ya Mtu kwenye Gazeti, TV wala Site....kuwa na Utu hulipii Kodi!
Nasikitishwa sana na hii tabia ya Wabongo ya ku-publish Maiti za watu online na kwenye Magazeti.


Babai...
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 3 June 2014

Radio za Dini

Hiyaaaaa!


Umewahi kuzungumzia Sheria za Dini ya Kiislam dhidi ya Wanawake kwa Binti wa "kisasa" wa Kiislamu ukasikia anavyojitetea!....Hadi huruma.
Kuna siku mmoja aliniambia Uislamu hauna budi kubadilika baadhi ya Sheria na kwenda na wakati.....sizungumzii wale Waislamu wa Mwezi wa Ramadhani to Ramadhani....la hasha!

Nazungumzia wale Mabinti ambao wanaipenda na kuifuata Imani yako kwa Dhati lakini wanahisi kuna mambo kwenye Sheria ya Dini yao zinawakandamiza.

Nimekuwa nasikiliza sana Radio za "Kiislam" (za Kikristo miyeyusho,kazi kuomba Michango tu).....napendezwa sana na Mafundisho yao ya Maisha, kitu pekee kinachonikwaza ni pale wanapozungumzia Wanawake....Mwanamke kwenye Imani ya Kiislam bana....daaah!(Naachia hapa).

Radio za Kikristo nazo zimejaa Ushuhuda wa kipuuzi tu yaani....alafu wanaomba Michango kuliko kufundisha wasikilizake wake namna ya kuishi Kikristo.....Maombi ya Michango ya pesa 90%....Shuhuda 7% na 3% Nyimbo....(Usipanic, nimekisia tu hizo asilimia...hihihihi).Nafaidika na Imani zote kwa kiasi cha kutosha.....


Babai...
Mapendo tele kwako...

Monday, 2 June 2014

Kuchapia...

Ni Sunna....Relax!


Enyi Wakaguzi wa Lugha Fasihi sijui Fasaha Mtandaoni mnahitaji kwenda kunywa dawa zenu....(Lazima mna some sort of Mental Disorder).

Ailimradi unaelewa kinachozungumziwa au kilichokusudiwa unapaswa kurekebisha kichwani mwako kisha endelea na mambo mengine...
Wengine tunachapa/ongea haraka na muda wa kuanza kuhariri hatuna....Mimi binafsi ni Bingwa wa kuchapia....mara nyingi nikisoma (kesho yake) nagundua kuwa nimechapia lakini bado naeleweka.
Huwa nachapia hata nikiongea na watu japo sio sana, labda maneno mawili kwa siku....aiiii hebu ngoja kwanza....sasa nina watoto which means naongea zaidi....usikute nachapia zaidi ya maneno 10 kwa siku!

Haulipii kusoma na alieandika halipii Kodi kuandika....tulia na furahia uwepo wako Online.Kumcheka mtu kwa vile nimekosea/chapia is bullying/Trolling.....hihihihihi!


Happy new Week!

Babai...
Mapendo tele kwako...