Friday, 30 October 2015

Kufutiwa Matokeo Kidato cha 2.....Miaka 20 Tangu Secondary!


Ni Ijumaa nyingine tena ambapo tunaendelea na "Series" yetu. Unakumbuka nilikuambia kuwa pale Shuleni kwangu kwa zamani kulikuwa na Watoto wa watu Wazito na wale wa Mabalozi wa Tz Nje(waliokuwa wanasubiri kupewa Ofisi).....Tulipokuwa Kidato cha Pili kikaja kimtoto kina miaka Nane kilikuwa kinatokea Nchi gani sijui huko. Kilikuwa kinashuka mahisabati kwa Kiingereza hicho hihihihihihi. Aliondoka baada ya Wiki 6. anyway.

Kusoma na watoto wa watu wazito ni raha, unapata kujua mambo mengi sana kuhusu maisha yao na(sio muhimu kivile lakini ndio hivyo), unakula maCandy na Majuisi ya Ulaya bana.....hasara yake inakuja kwenye Mitihani, sio siku ya Mitihani bali kwenye Matokeo.

Kama unakumbuka mwaka wetu(piga mahisabati mwenyewe) baada ya Matokeo kufutwa(sote tukafaulu) ndio Mtihani wa Taifa wa Kidato cha pili ukafutwa, sababu zilikuwa nyingi kwanini hakukuwa  na umuhimu wa Kukaa Mtihani wa Kidato cha Pili.
Nakumbuka siku tunaenda kuangalia Matokeo(ilikuwa siku ya shule) wanafunzi wengi hawakuona Majina yao pale kwenye Karatasi za Matokeo, watu wakaanza kulia eeh bana(nani anataka kurudia Kidato?)....hao kwa mwalimu Mkuu. Mwalimu akaanza kupiga simu huku na kule.

Baada ya siku tatu Majibu yakaja na wote ambao hawakuona majina yao kwenye Karatazi za Matokeo, wakawekwa kwenye karatasi mpya, lakini wote wakawa wamefeli! Vita si ikaanza bwana, wazazi wakaja juu hawakubali kuwa Watoto wao wamefeli. waliamini kuwa Wamefelishwa ili Watoto wa Wazito wafaulu.
Ile mbinu ya kawaida ya Walimu wa Shule ya Msingi kwamba  Mtoto wa Mwalimu akifeli  basi  Mtihani lazima urudiwe!  ilishindikana kwasababu Mtihani uliandaliwa Kitaifa. Wakaona isiwe tabu basi wote mmefaulu na hakutakuwa na Mtihani wa Kidato cha Pili....hihihihihi. Nadhani waliurudisha baada ya Mwaka au miaka miwili baadae.Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua blog hii.

babai.

Thursday, 29 October 2015

Sababu Kuu ya Kumchukia Ex wake...


.....wengi hudhani kuwa ni Wivu au Hofu kwamba Mwanaume anaweza kurudi alikotoka au kukuacha kama alivyomuacha yule ila tofauti ni kuwa anakwenda kwa Ex wake sio Mwanamke mpya. Yote ni  sababu common lakini ile kuu ambayo wanawake wengi hutusumbua na hata kujenga dislike(nikisema hate inakuwa too strong) huenda ni hii hapa chini.
Umewahi kutaka kumjua kama Mpenzi wako ana type? na pengine kwenda ndani na kutaka kumuona Ex wa Mpenzi wako kabla yako na hata kutaka kukutana nae? sio ili muwe marafiki bali ni kutaka kuona kama alikuwa Hot au Not....(hihihihihihi).

Ikiwa Mpenzi wako ana type na aliempitia kabla yako alikuwa Hot basi unafurahi kuwa na wewe ni hot (pengine wala sio that hot) na kwabahati mbaya kama ex alikuwa Not basi hapo ndio hasira huja. Kila ukimfikiria/kumbuka yule Ex alivyo unamchukia vibaya sana hehehehehe huku unajisemea "am not that ugly" na kujiuliza "am I that ugly?". Yaani sio kwamba unachukia alivyo (kuwa ugly is okay but....) bali unachukia kwasababu unahisi au kudhani kuwa unafanana nae kwa namna moja au nyingine.

Kuna wadada hufurahia sana kuambiwa na wapenzi wako kuwa Umefanna sana  na Ex wangu(yep nawafahamu wengi tu) kwasababu tu Exs walikuwa Hot......inasikitisha lakini ndio ukweli kwa baadhi ya sisi Wanawake.
Wengine hudhani kuwa wanawake huwachukia Ex wa wapenzi wao kwasababu waliwatangulia na hivyo wao kula Makombo.....hii sababu ni invalid kwasababu Kimaumbile mwanaume haachiwi uchafu na kukaa nao kwa muda mrefu(unless alipata Gonjwa) pia Mwanaume  hazai na hivyo hata kama alizaa na Ex wake bado huyo mwanaume sio Makombo.
Ex wake kwa next mpenzi ndio atakuwa anakula  makombo hasa kama ex(mwanamke) huyo ameachana na mtu wake chini ya Miezi 3 au  alizaa nae, alipoingia akaacha Uchafu wake kisha ukatoka kama Mtoto na yeye ndio anaenda hapo hapo(rejea Topic ya Usiku Mmoja).....samahani hii haina Mfumo Dume hivyo usiingize U-Feminis hapat...... ni Fact of Life.Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Tuesday, 27 October 2015

Presha ya kuweka/toa info zako vs Ukarimu....


...enzi za DHB, Yahoo/MSN chatrooms (heeey Maajuza wenzangu hihihihi) ilikuwa ni kawaida kuulizawa upo wapi na unafanya nini au umefikaje huko uliko, wengine wanapitiliza mpaka kwenye unakuja lini Bongo n.k. Kwa baadhi yetu ilikuwa sio big deal kwasababu info hazikuwa muhimu kivile(kabla ya Google haijatufanya Kijiji) kuorodhesha Nasoma, mwaka wa pili  na huwa narudi Home kila Christmas.
Jisni siku zilivyozidi kwenda na Maendeleo kuongezeka  na watu wengi kuwa na wasaa wa kufikia Mitandao na hivyo kuweka mengi kuliko wanavyohitajika. Siku hizi imefikia mahali wewe mwenyewe kwa hiyari yako unahisi kusema/share kila kitu, ikitokea mtu kauliza basi unajimwaga kwa uhuru kabisa, which is okay maana info ni zako bwana. Tatizo  ni kwamba wengi mnatoa mengi kuliko mnavyohitajika na matokeo yake baada ya muda wale wale mliowaambia wanatumia hayo kukuumiza au kukudharau.

Hakika kila mtu ana haki ya kusema atakacho kuhusu maisha yake Halisi  au ya Kimtandaoni  ili tu awemo anapotaka kuwemo,,...hali ambayo inaweza kukupa Presha ku-keep up au ku-maintain Mtindo huo wa Maisha uliojitengenezea Online au ule ulioaminisha watu. Hali inayoweza kukusababishia dharau ikiwa  wale "uliowaaminisha" wakukute unaishi vinginevyo(wapate  kujua ukweli).

Pamoja na kuwa ni uamuzi wako na  ni haki yako kusema/share kila jambo lako, kumbuka kuwa sio lazima. hulazimiki by Law kufanya hivyo, kwahiyo zingatia nini hasa unataka kuweka wazi na nini kibaki kwa ajili ya watu wako wa Karibu na Marafiki(kama unao) waaminifu.
Kwasababu tu wengi ulionao kwenye maisha yako ya Mtandaoni(kwenye Sosho Midia) hasa maCeleb wanaweka kila kitu(wapo kazini na wanalipwa kufanya wafanyavyo) haina maana na wewe pia ufanye hivyo.
Ku-share kupita kiasi huenda mpaka nje ya Mitandao/Sosho Midia. Mfano baadhi yetu huwa na tabia ya Ukarimu eeh Watanzania sie ni ndugu. Jamaa kutoka Serikalini anakuja Ughaibuni kwa mfano, anataka kutunza Pesa alizopewa kwa ajili ya Hotel.....anatafuta connection ya mtu mwenye nyumba kubwa ampe Chumba ili a-save anunulie familia ya Mazawadi ya UK au akajenge huko Bongo baada ya Semina.

Unapomkaribisha mtu kwako(akae bure au achangie sehemu ya Bill) na kuishi nae kwa muda wa siku 3 au zaidi hakika atakuwa amekusanya Info za kutosha bila wewe kukusudia kuzitoa na matokeo yake anazitumia hizo kujumuisha Watanzania waishio Nje na hapo ndio Dharau inapoanza.
Kuanzia sasa Muache kukaribisha Wabongo kwa kisingizio cha Ukarimu/sisi Ndugu majumbani mwenu wanapokuja kwa ajili ya Semina, waacheni wakakae Hotelini huko. Hao mnaowafanyia Wema ndio hao hao wanaokwenda kuwaumiza na matokeo yake wote tunaonekana tunaishi maisha ya Kishenzi mnayoishi nyie......duh! hii sijui imetoka wapi.Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Friday, 23 October 2015

Scandals: Binti ajiua kisa B'friend+...Miaka 20 Tangu Secondary!

Hello tena, karibu  tuendelee na "series" sehemu ya maisha yangu ya Shule.


Baada ya Muda si watu wakaanza ku-date bana.....unasikia tu gossip kuwa fulani anatoka na fulani, tulipotoka wao walienda kujibanza kwenye ma-bin na kufanya yao. Unaangalia Darasani(wa Asubuhi na Mchana) huoni hata Kijana wa kutoka nae(hakuna anaekuvutia(well mie nilikuwa mdogo Sec, 1st Bf alikuja nilipomaliza Kidatoo cha Nne huko mbele....Team Wasiona haraka. Achana na hili!

Kanisa la Mtakatifu Joseph
Wanafunzi wa nyuma yangu walikuwa Mapepe sana, na wengi walitokea palepale (Forodhani Msingi) hivyo walikuwa na Mahusiano na Wakaka wa Vidato vya juu  na mmoja wao aliekuwa akipiganisha Wadada wa kila Shule pale Mjini. Aliitwa JJ (sitasema alipokuwa akiishi wala alivyofanana)....alikuwa Mbele yangu Kidato. Huyu jamaa alikuwa napiganisha sana Mabinti wa Msingi na Wale wa Secondari(si unajua kuwa Foronda kuna Msingi na Sekondari eeh). Mwaka wao hawa akina JJ kulikuwa na wakaka "fresh" kweli(Watanashati/Ma-handsome).


Basi siku tumeingia Getini tunasikia watu wanalia, kulikoni? kuna taarifa Binti wa Kidato cha Pili amefariki(amejiua) kwasababu Mpenzi wake kamkataa.....Mpenzi wake ni nani? JJ....aiii Mie kama mie nikamuona yule Binti Bwege kweli, huyo JJ mwenyewe sio m-hot kiviiile(enzi hizo hatukuwa tunatumia neno Hot hihihihi).

Polisi wakaja wakamkusanya JJ "for protection" na hatukumuona tena mpaka baada ya Wiki 2.....huku nyuma bwana kama kawaida watu tukaanza kuchangishwa Senti za Rambirambi na baadae kurudishwa Nyumbani....yeah Ulaya Mwanafuzi mwenzenu akifa mnapewa "Kanselazi" wawasaidie kupokea Msiba Kisaikolijia , sie tukarudishwa tu nyumbani na mimachozi na mawazo na uoga wetu dhidi ya "mtu kujiua".
Kesho yake, Shule ikaendelea kama kawaida halafu siku ya Kuzika ikafika....likaletwa Couch(yale ya Sarafi ndefu yale Mazuriiii, watu walikuwa na mbwembwe)  la kutupeleka Mazikoni tukiwa Ndani ya Sare za Shule kama kawaida(mie sikwenda though).
Msiba wa Binti huyo ulinisumbua sana akili kwasababu nilikuwa sielewi kwanini hasa mtu ajiue kwa sababu ya Mvulana! Mvulana anakupa nini mpaka ukimkosa unaamua kuishi basi eh? Anyway Mungu aendelee kumrehemu yule Binti(sijamtaja kwa sababu ya Kuheshimu Familia yake).
Scandals zilikuwanyingi sana pale Shuleni, Kuna Mwalimu na rafiki ya Baba yangu(Mungu akurehemu Dingi) aah Mwalimu Marehemu "D"mkali wa Hisabati(halafu sijui Hesabu wala nini), maskini alifariki siku chache kabla ya kufunga Ndoa na Mwalimu mwenzie(mkimama wa Kihaya alikuwa muzuriiiii na anamadoido utafikiri hachutami kukamua Kimba) ambe ilisemekana alikuwa na "gundu".....kila anaemchumbia hufa siku chache kabla ya Ndoa.
Scandal nyingine ilikuwa ya Binti Mmoja wa Kizungu(alizushiwa kafa kwa Ngoma)....alikuwa Mwaka wa akina JJ....alikuwa Kiwembe huyo hihihihi....huyu alitoweka ghafla tu.Kuna Scandal ya Jamaa moja hivi ambalo lilikuwa linachukia Wanawake lakini wanawake walimpenda so alikuwa akiwakubali na akienda nao huko anakowapeleka anawafanyia "dharau" ili wasimsumbue tena.....hihihihihi ningekutajia ila wacha nmstahi tu(atakuwa kazeeka sana sasa maana alikuwa wale repeat-ers).....unapiga Darasa la Saba mara zote mpaka Ufaulu.Pia kuna yule Binti wa Kizungu alikuwa Kiwembeee, akazushiwa kuwa na HIV,,,,,,akatoweka ghafla. Miaka 3 baadae watu wakasema amefariki.


Kulikuwa na Watoto wa Pembeni(nje) wa wakubwa wa Inji yenu pale shuleni kwetu, kuna Mdada alikuwa Bingwa wa kupata Mitihani kabla haijafanywa hehehehe, kila Mtihani yeye anatuacha Mita 200....halafu alikuwa Mnoko na Msongo(hacheki ovyo-ovyo) balaa huyo Mdada.

Mwaka 2005 (sikumbuki vema) nikakutana nae ndani ya Ndege ya Ethipia....nkamsemesha, akajifanya hanijui hihihihi. Nkamwambia well tulisoma wote....so unafanya nini UK? akasema anasoma....Nkaongeza wee baba yakoWaziri sasa kwanini unapanda Ndege ya walala hoi? akasema ndio flight pekee iliyopatikana haraka.....kumbe mie sikujua Baba'ke alikuwa na Scandal ya Ufisadi sijui nini na nini na yeye alikuwa anarudi kimya-kimya ili kuua "uzushi".....hihihihi. Oh yeye alikuwa Mtoto wa Mkufunzi sio wa pembeni enzi hizo tupo Shule.....nimechomekea hadithi(mambo ya Live Tv haya nayo hehehehe).

Enhee yule Mwalimu wetu yule Mkali wa Physics(nimemsahau, nili-drop PCB nkaenda Biashara), alikuwa fashionable sana pia ufundishaji wake ni wake- naughty-naughty hivi hihihihi alikuwa anatengeneza Pesa nzuri, maana alifundisha Madarasa ya Ziada Mapaka Usiku....huyu nae alikuwa kiWembe mpaka Mkewe (mwalimu pia) akahamia Forodhani kulinda mali zake.

Talking about kuchukua Biashara, kulikuwa na Limjamaa (Mwalimu wa Bookkeeping) abuser kweli....Wanafunzi wa mbele yetu walikuwa wanasema kwamba Jamaa akikutaka na ukamkataa basi atakuwa anakuchapa Daily bila sababu.....by the time nafika Kidato cha Tatu Maombi yangu kwa Mungu baba yalikuwa Mwalimu huyo sijenitaka mimi. Kwa bahati nzuri au mbaya kukawa na Mgomo wa Walimu wa Secondari na yeye akaacha kufundisha akaenda Kutangaza Radio(ile ya Kanisani palepale Forodhani).Hizi ndio Scandals nilizozikumbuka siku hii ya leo. Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa.ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Wednesday, 21 October 2015

Kijinyama/Ngozi kutoka K-ini...


...pengine hujawahi kuambiwa kuhusu hili la "kijinyama", "Kijingozi" lakini lipo na huwatokea wanawake wengi tu, tatizo ni kuwa wengi hawapendi kulizungumzia.....Uanake ni zaidi ya Makeup, Matiti na Kuvaa Magauni na Blauzi.
Umewahi kujiswafi na ukakutana na kitu cha ajabu ukaanza kuogopa n a kudhani Kizazi kimetoka(hahahaha) au Mimba imeharibika bilakujua kama ulikuwa  nayo au ukadhani Umelogwa ili upate Hedhi ya Manyama badala ya Damu?
Mara nyingi hii hutokea mara tu baada ya Kumaliza Hedhi na kufanya Mapenzi, au pengine umefanya Mapenzi na Mwenza akaenda "mbali" na baada ya kumaliza ukaona Damu na baada ya kujiswafi ukatoa "kijinyama" ambacho hakiterezi kama Ute Mzito au Damu nzito......usiogope hasa kama Umeruka Hedhi.


Mfumo wa Uzazi wa MwanamkeUkuta wa Mji wa Uzazi(Uterus/Womb) hujijenga kila baada ya siku 23 na baada ya hapo  hung'oka na kuteremka sambamba na Damu pale unapokuwa Hedhini....sasa ikiwa umepitiliza au kuruka Hedhi moja au mbili, Ukuta ule ambao  ni ngozi/kijinyama huwa mnene zaidi na hivyo kugoma/kwamba wakati una-Hedhi-ka kile kijingozi hakiteremki  moja kwa moja Ukeni(Vagina) na matokeo yake hubaki ndani  pale pembeni mwa  Mlango wa Uzazi (Cervix).

Wakati mwingine huwa imeng'ang'ania na hivyo baada ya Uume kuingia na kufanya Uume ufanyavyo  "best" kile kijinyama hujiachia  na hivyo kuwa tayari kutoka kwa msaada wa kidole chako na Maji. Kama huna utaratibu wa Kujiswafi Ukeni ni wazi kuwa kitakaa huko na baadae kusababisha maambukizo au kutoa "ute" wa rangi ya ajabu (kahawia) na harufu mbaya.
Huenda hujawahi kutwa na hili hasa kama Mzunguuko wako sio wa Kuruka(unaenda Kila Mwezi) na haujawahi Kuzaa na Kunyonyesha.  Kama nilivyogusia hapo juu, kuwa kila baada ya Hedhi Ukuta wa Mji wa Mimba hujijenga na hung'oka baada ya muda ikiwa hakuna Yai lililorutubishwa na "ukuta" huo kuteremka sambamba na Damu yako ya Hedhi(Mie sio Daktari usiniulize Maswali).Sasa ukizaa na ukawa unanyonyesha mara nyingi unapoteza Hedhi(hupati Hedhi mpaka umalize Kunyonyesha sio!), mpaka Hedhi bin Homono vinakuja kutulia baada ya kunyonyesha  ni wazi kuwa utakuwa unaruka-ruka na hivyo "ukuta" wa Mji wa Uzazi wako kuwa Mnene na hivyo kutoka kama nilivyoelezea hapo awali.Pamoja na kuwa nimekutoa hofu bado ni Muhimu kwako kwenda Kumuona Daktari wa Magonjwa ya Kike na umuelezee hali halisi, jitahidi kuweka kumbukumbu ya Tarehe na aina/ukubwa/udogo wa "kijinyama" hicho ili Daktari aweze kukuelewa zaidi nahivyo kufanyiwa Vipimo yakinifu kuangalia kama Mfumo wako wa Uzazi upo na afya njema.


Naheshimu na kuthamini muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Monday, 19 October 2015

Mke anafanyiwa mapenzi, sio the other way around!


Umewahi kusikia au kusoma mahali Wanaume wakisimulia namna wanavyowafanyia Wake zao na kuapia kuwa Mwanamke nahaitaji kufanyiwa mapenzi zaidi kuliko wao Wanaume, halafu uka-wish kimoyo-moyo Mumeo aje mahali hapo asome na ajifunze?!!
Kama ilivyokuwa Dinahicious Blog, kwamba kuna baadhi ya Wanaume walikuwa wakitaka Wake zao wasome Baadhi ya Makala zangu ili wajifunze. Nakumbuka wapo walioniandikia wakisema huwa wanaacha Blog wazi kwenye Simu/Laptops kwa Makusudi tu ili Mke/Mpenzi apitie.
Ni muhimu kumfanya Mumeo/Mpenzi wako ajihisi  kuwa ni Mfalme hapo nyumbani kwenu na unaweza kufanya ajisikie hivyo kwa namna nyingine  nyingi na sio kwenye Kufanya mapenzi kila anapokuhitaji/mnapohitajiana/unapomhitaji(siku hazifanani si unajua Homono nini  na nini).....Mwanamke huwezi kufanya yote, mengine mwachie na yeye!
Imekuwa ni kawaida kwetu sisi wakimama kutafuta Mbinu za kumfurahisha Mwanaume Kingono zaidi kuliko wao.....wao wakibaba ni kama vile wametulia tu yaani wanasubiri kupakuliwa(sio wote). Mbaya zaidi kuna hata maneno kwenye Nyimbo zilizoimbwa na Wanawake zinakubaliana na kusisitiza kuwa Mwanamke "mambo" au "kujituma" au "kujua wajibu wako" Kitandani.
Lakini kihalisia Mwanaume ndio anapaswa kumfanyia  Mapenzi Mkewe/Mwanamke wake, sio tu kwasababu  "kuneng'enuka" kwetu kunahitaji akili kutulia (hatuna mawazo wala hofu) bali pia mwanamke anahitaji kuhisi kuwa anapendwa na kutakwa na wewe(mwanaume) ili afurahie Safari ya Kuneng'enuka.
Kwenu ninyi wanaume Ngono ni Ngono tu, unachohitaji ni mtu kukubali kufanya.....mfano Mwaname akisema "nataka unifanye" unakuwa tayari....au unaeza kuona upindo wa Chupi ukawa umefika(hihihihihi). Wanawake pia huwa tayari ila sio kila siku(inategemea na Mahesabu ya Mzunguuko).
Kuna siku za Mzunguuko unahitaji kupendwa zaidi ya siku nyingine, kuna siku unahitaji kuguswa Bega au kiuno na ukawa "tayari", siku nyingine unahitaji kupendwa na kufanya Malkia kwa Dakika 45(duh hizi nyingi.....tufanye Dakika 20 hivi).Siku nikipata Muda(nikikumbuka that is) nitakuletea "hisia" za Mwanamke kulingana na Mzunguuko wake wa Hedhi (siku 28 ndio nina uzoefu nayo) ili ikusaidie kujua kuwa Leo akitaka  kuwa in control na ku-make love to you haina maana itakuwa hivyo siku zote za Mwezi. Inaeza tokea mara moja au Mbili tu.....usizoee!


Ili uwe Mfalme ni wazi kuwa unahita Malkia.......ila kumbuka Malkia hawezi kuwepo bila ya kuwa na Mfalme kwanza. Mwanamke kwanza!


Naheshimu na kuthamini Muda wako wapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Saturday, 17 October 2015

Siku ya kwanza Kidatoni...Miaka 20 tangu Secondary!


Mwaka huu November inatimia Miaka 20, sasa sio mbaya kama nikiweka kumbukumbu zangu za safari yangu ya Shule kuanzia Msingi mpaka Secondari(intro hiyo hihihihi).Siku ya kwanza naingia kama Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza ili kuwa ngumu maana hakukuwa na mtu nilietoka nae Msingi. Wengi walikuwa wanajigawa kwa makundi kwasababu wanajuana kwa kutoka shule moja ya msingi ama shule zao zilikuwa jirani. Kulikuwa na Wanafunzi kibao kutoka Mlimani Shule ya Msingi, Olympio na Upanga(wajuajiii, mabishoo, Kiingereza kingii).

Ikabidi nitafute namna ya kujiunga nao, maana kati yao watakuwa na mimi Darasa moja.....nikaanza kutumia Tiketi ya Kuiba (naongea Kiingereza kwa Nyimbo hihihihihi). Nilikuwa najua nyimbo nyingi ahsante  "Double Compact something Cassete Music system".....unaweka Compact yako halafu unasimamisha ili kuandika mstari wa Wimbo husika. Nilikuwa na "book" full of nyimbo za RnB.
Baba(Mungu amrehemu) alikuwa anatununulia hizo eti tujifunze Kiingereza(hahahahaha) wengine mpaka leo hatujui Kiingereza na tunaishi na kufanya kazi Uingereza daah! achana na hili.....Basi nikaaa pembeni na Miatu yangu Mieupe ambayo 2002 ni Wazee tu ndio walikuwa wanavaa.(imerudi kwenye fashion though) nikaanza kuwa busy kuimba TLC's baby baby baby.


Viatu vyangu vilikuwa exctly like this....nilikwa na Nyeusi na Nyeupe


Mara Kengere ya Mstarini ikagongwa....zikaanza Risala za kutukaribisha nini na nini. halafu kupangwa Madarasani nakujitambulisha. Kwenye kujitambulisha nikatupia Tiketi nyingine ya " iaemu zionli pyupu to pass to zisi schooli fromu mai skuli" excactly like that.....nikapigiwa Makofi. Sasa kuimba na kuja Foronda peke yangu kati ya watoto Mia Sita waliofaulu Shuleni kwetu aii nikawa popular.

"Dinah unaweza kuimba wimbo huu.....Dinah nani ali-produce wimbo huu?".... zikawa nyingi hihihihihi. Nikaona hizi toto za "wakubwa" sio Level yangu....nikaanza kujichanganya na kila mtu. Kila siku nabadilisha Group....Darasa zima wakawa "marafiki" zangu. So hii sina "Best friend" imeanza kitambo sana bila mimi kujua.


Naheshimu na Kuthamini muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Thursday, 15 October 2015

Wale wasema "Watanzania" Wavivu/Wazembe/Waoga...


Binafsi naamini kuwa sio sahihi kumuita mtu majina ambayo unauhakika ukiitwa wewe hutofurahia iwe ni kweli upo hivyo au la! Mfano unapomuita Mwenzio Malaya unapaswa kuwa na Uhakika kuwa  Baba ni Baba yako kweli (una DNA bila rushwa).


Utamponda huyu hajitumi au Utaiponda Ofisi yake?


Sasa kwa sababu tu wewe umezaliwa au kubahatika kuwa na shughuli ya kufanya huna haki ya kuwalaumu na kuwaita majina mabaya kama vile Tegemezi, wanapenda kuomba-omba Wavivu, Wazembe, Waoga, Masikini wa Fikra n.k.Pia wewe wa Ughaibuni, kwavile tu wewe unaishi huko ulipo na kuona Maisha ya baadhi ya "wenye Nchi" mazuri na ukapendezwa na labda utaratibu wa Serikali na kudhani Utaratibu huo umewekwa na "wananchi" hao kwa sababu sio Wavivu/Wazembe au majina yeyote machafu unayowaita Watanzania wenzako basi tambua kuwa unakosea.
Kabla ya kuanza kumlaumu na kumshutumu Mtanzania  mwenzio kuwa matizo yake yanasababishwa na yeye kuwa mvivu au kutopenda kujituma au kufanya kazi kwa bidii (wakati hakuna Kazi).....unahitaji kujua Chanzo kinachosababisha yeye kuwa hivyo unavyodhani alivyo.Chanzo cha Matatizo ya Mtanzania au Umasikini wake na mengine yote unayomuita ni Utaratibu wa Serikali yake! sasa kama unataka kumsaidia Mtanzania huyu unapaswa kupigana ili "system" ibadilike na kusababisha mabadiliko ya "Kacha" ya Uvivu, Uzembe, Kuomba-omba n.k."Kacha" inatengenezwa na hivyo inaweza kubadilishwa.....kabla hujaanza kubisha unapaswa kujua Tofauti ya Utamaduni aka "Kacha" na Desturi. Desturi haibadiliki, lakini Utamaduni unaweza kubadilika kwa sababu ya Maendeleo au Mabadiliko.
Utamaduni hubadilishwa haraka kwenye Nchi husika kulazimisha Jamii kuishi kwa namna fulani, namna hiyo inaweza kuwa ya Kifukara, Kati au Juu. sasa ili Wananchi wabadilike nakuicha "kacha" ya kuomba-omba au Uvuvu ni wazi kuna Ulazima wa "system" kubadilika na kuweka sheria Mpya zinazotekerezeka.....kuondoa Mgawanyo mkubwa kati ya Masikini na tajiri.
Kwasababu Umeishi Ughaibuni na kuona  kuwa Wazungu ni watu wenye Bidii na Kujituma which is kweli kabisa lakini sio wote. Unadhani kwanini wanabidii na kujituma? Kwasababu kisheria wanapaswa kulipa Bills zao kwa wakati na wakikosa wanalipishwa "riba" sio tu kwenye Wanavyomiliki bali pia Bank inawalipisha kwa kutokuwa na pesa kwa wakati husika ambao ulijua unapaswa kulipa Bills zako.Kuna utaratibu wa kusaidia wasio na Kazi(Benefit), Utaratibu huu ulifanya wananchi hao unaoamini kuwa wanajituma na wana bidii ya kazi (Wazungu) kuwa Wavivu nakutegemea "kukinga mikono", hii ikawa "kacha" na hivyo watu wengi wakaamua kuacha kujituma na badala yake kukaa Home na kutukana wenzao via Sosho Midia, kuangalia Tv na kucheza Games kwenye PC."Kacha" hiyo ikaharibu Uchumi wa Nchi kwasababu Serikali ilikuwa inatumia Pesa zaidi kuliko kuingiza  na Matokeo yake wakaamua kubadilisha utaratibu na hivyo kubana Kipato cha "Benefit" ili watu warudi Makazini.....umeona sasa?!!Watanzania wanajituma sana tu (angalia Machinga na Mama Ntilie, Wauza Sokoni,Wlanguzi n.k), sema  Utaratibu wa Serikali yao unawaangusha. Naamini Vijana wanauweza na nguvu ya kufanya kazi na wanania ya kujituma......lakini sasa utajituma kwenye nini wakati hakuna Kazi?Serikali ikibuni Ajira na kuweka "thamani" ya ajira kwa kuwa na kiwango cha malipo na kisheria lazima wafanya kazi walipwe hivyo au zaidi na sio chini ya Kiwango husika. Pia kuondoa "kacha" ya kila kazi kuhitaji "Kiwango cha Elimu ya Digrii kwa kazi ya Uratibu Ofisi".....Karatasi pembeni waangalie nia ya mtu na Uwezo wake wa kufanya Kazi husika(kutokana na Mahojiano), kuwe na utaratibu wa kufundisha kazi with Malipo then "Kacha" ya kusubiri kusiaidiwa au kukinga mikono, Uvivu na Uzembe itaondoka/isha.
Kama huna uwezo wa kubadilisha chanzo cha Watanzania wenzako unaowaita Wavivu/Wazembe, hawajitumi au pengine huijui Siasa wala  System ya Nchi yako hakika  kaa pembeni na uwaachie wenyewe. Bora  nisome Makala/Twiti kutoka kwa Muandishi(sio lazima awe Habari bali muandikaji mzuri na anaejua Siasa kwa mbali) kuliko kuambiwa na Celeb au Star kuwa Watanzania ni Wavivu/Hawajitumi, wanapenda kungojea wasaidiwe.
Wewe ni Celeb wa uhakika au Uchwara, una Mikataba na Projects zaidi ya tatu kwa Wiki moja, ni rahisi kwako kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwasababu kuna "kazi" na umesaini kuzifanya na usipozifanya hakika utakosa Kipato(na mialiko itakauka) na utashtakiwa/Daiwa....sijui naeleweka!


Kwa kawaida sifanyi Siasa(siku hizi) lakini here we are! Nathamini na kuheshimu Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Tuesday, 13 October 2015

Wale akina Wanangu Come First....


Hakika! wao kwanza kabla ya watu wengine baba yao included(hello Asali wa Moyo hihihihi). Hata mie nimewahi kusema/kuwaambia watu kuwa Wanangu kwanza halafu wengine na mengine ndio yanafuta.
Nakumbuka nilikuwa na mwambia Mama, "nikija kuwa na mtoto, sitoruhusu mtu amshike....hata baba yake" hapo nilikuwa sijui Uchungu wa Mtoto wala Emotional connection na Bond kati ya Mimba/Mtoto na Mama. Nilihisi kuwa mtoto yupo Salama zaidi akiwa na Mama(nadhani ni Nature tu).
Baada ya kuwa Mama hakika Wanangu waka wa kwanza kabla ya lolote kubwa au dogo. Maisha yangu yakazunguukwa na Wanangu na kila kitu kinachowahusu. Ikafikia mahali nikaanza kuhisi sifurahii hii "biashara" sijui "kazi" ya kuwa Mama. Ikawa too much mpaka nikasahau mimi ni nani.
Nikasoma mahali (ukinipa mtihani wa Mimba, Kuzaa na kukabiliana na shida/mabadiliko ya kuwa  Mama early days baaya ya kuzaa nafaulu zaidi ya Kufaulu), maana sijawahi kusoma in my life kama nilivyosoma/ninavyosoma kabla ya Mimba ya Babuu mapaka leo.....bila shaka nitaendelea kusoma ili kujifunza zaidi kutokana na uzoefu wa watu wengine. Achana na hili.
Nilipomaliza kusoma nikajifunza kuwa Mama mwenye furaha anasababisha furaha ya Familia yake na hivyo watoto kukua Vema Kiakili, Kimwili, Kihisia na Ki-sosho. Sasa je utakuwaje Mama mwenye furaha?
Niliamini kuwa hakuna tatizo kwenye Uhusiano(ndoa yetu) so i was(still am) actually happy na kila kitu, isipokuwa hii "biashara" ya My kids first inaniondolea furaha kwa kuchoka Kimwili n a Kiakili, so wanangu ndio Tatizo? Hapana....Tatizo lilikuwa ni Mimi kuwaweka wao Mbele na kujisahau/kutokujua kuwa Mimi ndio Nguzo na hivyo napaswa kuwa Imara.
Mimi ndio nilitakiwa kuwa Mbele, Mimi ndio nilitakiwa kuwa wa Kwanza kabla yao ili niweze kuwaangalia na kuwatunza kwa Umakini bila kuwa na Mzigo wa Uchovu na Mawazo ya "nimepoteza Utambulisho" wangu!


Haya ndio yaliyonifanya nianze kufurahia tena Maisha kama Mama;-

1-Nalala na Kuamka Muda ule ule kila siku(kuepuka mwili kuwa comfused).


2-Naamka mapema....nusu saa kabla ya watoto na kujiandaa/pendezesha(huwa naoga Usiku tu so time saved),


3-Nafungua Madirisha


4-Watoto wanaamka Saa Moja na Nusu (sijui huwa wanaamshana hehehe)....nawaandaa wote kwa pamoja.


5-Tunafungua Kinywa Pamoja


6-By Saa 8:40am tunatoka kwenda Mdondosha Babuu Shule.

7-Narudi na kuendelea na Mipango Mingine ya Siku husika.


Nafanya Mzoezi Mara 3 kwa Wiki (Nyumbani sina pesa wala Muda wa Gym), nafanya Mazoezi Jioni kwasababu Naoga Usiku/Jioni tu. Kufanya yote hayo kwa Mpangilio huwa kunanifanya ni "look forward" kwa siku inayofuata.Kuhitimisha: Wanangu wanakuja  baada ya Mimi. Hivyo  mimi kwanza, Watoto pili, Baba yao tatu, familia yangu(wadogo zangu na Mama).... halafu mengine na wengine hufuata.Je wewe Mama mwenye watoto wadogo, huwa unafanya nini au unafuata mpangilio gani ili kufurahia Umama wako bila kuhisi kuwa "umepotea".....sio Dinah tena bali MamaBI au Mke wa DK(mie).


Naheshimu na Kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Friday, 9 October 2015

My Stori: Miaka 20 Tangu Nimalize Sekondari


Hi.

Mwaka huu (November) inatimia Miaka 20 tangu nimemaliza Elimu ya Secondari Pale katikati ya Jiji la Dar es Salam....well sio katikati bali pembezoni mwa Bahari ya Hindi Jijini Dar. Dah kweli nimezeeka!
Nimeona sio Mbaya kama kila Ijumaa(najipa Presha hapa) nikawa na-share kumbukumbu zangu  zote nikumbukazo kuhusu Safari yangu ya Elimu kutoka Msingi Mpaka Kidato cha Nne(sikwenda Kidato cha sita....nilienda Chuo na kupoteza Mwaka mmoja kufanya ile "Foundation"  hii ni hadithi ingine).


Kwenye Kona ya  Samora Machael Avenue and Julius Nyerere Way, Harare, Zimbabwe
Kutoka Shuleni kwangu nilikuwa Mwanafunzi pekee kwenda Shule ya "Wasafi/Mabishoo/Watoto wa mama" basi nilijulikana Wilaya Nzima (natania) kwasababu nilikuwa navaa Sare kama ya Shule ya Msingi wakati nipo Seko. Anyway....kusoma shule hiyo nilipata bahati ya kusoma na watoto wa Vigogo(wa enzi zile), watoto wa Mabalozi wa Nje na Ndani ya Tz....na watu wakubwa wakubwa tu Serikalini.

Shule yetu ilikuwa ni ya pekee ku-offer great Breakfast (Chai ya Maziwa, mikate ya Asia na Siagi na Jam) na Lunch(Wali maharage na Mchicha/Kabeji kila siku ila J'5 na Ijumaa ni Nyama ya Ng'ombe) na Matunda, basi Wanafunzi kutoka Tambaza, Azania (hasa tambaza aka wababe)....walikuwa wanakuja Shuleni kwetu kwa ajili ya Kula.


Wanafunzi wengi pale kwetu walikuwa hawali Chakula cha Shule (mie mmoja wapo), sio kwasababu wengi walikuwa "matajiri", bali waoga kuchafuliwa......hihihihi. Mie binafsi sio mpenzi wa kula nje ya nyumbani (nilikuwa naumwa tumbo)....Mpaka leo hii  napata shida kidogo kula chakula kilichopikwa kwa ajili ya watu wengi(nadhani ni Kinyaa issue au Saikoloji? hata sijui).

Maisha yangu ya Shule yalikuwa Mzuri, nakumbuka most of wanafunzi wenzangu (most sio kwa majina though), nakumbuka sura zao kwa wakati ule(watakuwa wamebadilika sana). Kuna Dada mmoja nilisoma nae Msingi then akahamia tukiwa Kidato cha Pili (wengi walikuwa wanafanya hivyo kwasababu ilikuwa vigumu Kufaulu kwenda Foronda).

tukucha twa Kibibi tuchafu!
Siku nimekaa ki-balcon level ya Pili huku nimening'iniza Mikono yangu napiga stori(ilikuwa Mapumziko).....nikasikia mtu ananiita "Dinah" kuangalia kwa juu namuona yeye. Nikamuuliza umejuaje kama ni mimi? akasema nimeona Mikono yako? nkauliza Mikono yangu ikoje kwani? akasema imezeeka hahahahahahaha, yeah i laughed so hard!(poor me)!
Mikono haikuwa muhimu kwangu kipindi kile(nilikuwa mdogo sio), muhimu ilikuwa kuchukua PCM au PCB kama Baba yangu alivyo Wish. Anyway Mikono yangu ni moja ya sehemu ya Mwili wangu ambayo inaniudhi(ila naitunza vema)....hey Girl who is Old now? eeh-eeh?!!(natania).Naheshimu na kuthamini muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Thursday, 8 October 2015

Eating Clean: Kifungua Kinywa kwa busy mums

Kama wewe ni busy Mum wa watoto wawili chini ya Miaka Mitano bila Msaidizi kama mimi,  hakika utakuwa unatafuta Kifungua kinywa kitakachokaa tumboni muda mrefu. Chakula kitakachokuchukua kuanzia saa Moja asubuhi mpaka saa Kumi na Moja Jioni(au muda wako unaokula Chakula cha jioni/usiku). Hapo katikati unaweza kutafuna chochote na kunywa maji (ya kutosha) ili kujiongezea nguvu na kukata Kiu ila hutopata hisia ya kutaka kula chakila kizito.Baada ya kujifungua mtoto wa pili nilikuwa nakula Lunch asubuhi na nilifanikiwa kupunguza Mwili wa "Mimba".....then nikagundua Mayai na Kale(mboga jamii ya Kabeji).Nadhani ni kama Spinach(sio Mchicha kama Wanavyoita wa UK na US), unazijua zile Spinachi tulikuwa tunapanda kwenye Bustani za Shuleni(kama ulisoma Shule za Msondo aka non Academy? Radha yake na Muonekano wake ni tofauti lakini nahisi kuwa ni Jamii hiyo.Kwa kawaida nakula Mayai 3(kiafya unajitaji 2 kwa siku)....huwa nachanganya na Kale  kisha naweka kwenye Microwave kwa dk 3. Halafu nanyunyizia chumvi na pilipili Manga. Nakula na tunda Moja.Huwa nabadilisha matunda kati ya Apple na Ndizi Mbivu au Embe Mbivu. Siku nyingine nabadilisha "upishi"......badala ya kuMicrowave huwa nakaanga kwa kiasi kiduvhu cha Olive oil na kisha naongeza Jibini kwa juu(kabla Yai halijapoa).....kama picha inavyoonyesha.Mwili wako unahitaji Protein kama mwanamke kwa ajili yakujenga Misuli(kama unazoezika) na Kale ina Vitamins na Mineral muhimu na inasaidia Nywele na kucha zako kuwa na afya njema na kukua haraka kuliko kawaida yake.


Mabadiliko ya mwanamke baada ya kuzaa ni mengi higyo ni vema kuwa muangalifu na unachokiweka au kukiondoa mwilini. Mlo huu haukinai (mwaka wa pili na nusu nakula hivyo kila Asubuhi) na haunenepeshi so long unakula mlo huu mara moja Kwa siku. Na usile mlo mwingine uliopikwa kwa kutumia Mayai.

Naheshumu na kuthamini muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua blog hii.

Babai.

Tuesday, 6 October 2015

Kipindi cha Baridi ndio unahisi kuwa Stylish....

Jambo!


Nimeamua kuipenda Autum/Winter sasa, sio tu kuwa Kipindi hiki ndio najihisi kuwa stailishi bali pia napata nafasi ya kutumia(vaa) kila aina ya nguo niliyonayo kwa Kujiamini zaidi kwasababu hakuna  ile "presha" ya Kunyoa Kwapa wala Miguu na Mikono.....(well naficha chini ya Tights, Jaketi au Koti). Halafu Majira haya ni Marefu kuliko hizo siku 3 za Kiangazi. September Mpaka June ni total Baridi.


mekosa Pic ya Mweusi ambae ana-stayle kama yangu (ubaguzi kando)Halafu pia Wivu wa hali ya hewa unakuwa hauumi sana kwa walio  Nchi za joto, unajua kuna muda unaangalia Fashinblogs za Tz halafu unapata Wivu wa hali ya hewa.....wanavalia nguo nyepesi na wanafurahia Kiangazi kwa Muda mrefu zaidi yako.
Kipindi cha Kiangazi huku kinadumu kwa Mwezi mmoja, tena sio Mwezi Mzima mnapata Jua la maana bali mara mbili au tatu kwa Wiki ndani ya Miezi 3! Sasa kuna ulazima gani ya kuipenda Summer(Kiangazi)?
Halafu huku tulikohamia Mwaka huu Kiangazi kilijitokeza kwa Siku 3 tu, yaani kuanzia Mwezi wa Sita Mpaka wa Tarehe 23 Mwezi wa Tisa ambapo Kipupwe (si ndio Fall/Autum?). Unaangalia hali ya hewa unaona South East wapo 32C hala nyie North mpo 5C.....mxsii.
Sasa sio mimi tu ambae najiona stylish kipindi hiki, naona kila Mama pale kwenye Geti la Shule la Babuu ameanza kuwa  stylish kuliko alivyokuwa June-September. Kila mama kapigilia  Nice Boots, Hand bag, scaf, kajiremba, Hereni nini na nini......nilipofika nkadhani kuna kasherehe ambako mie sijaalikwa hihihihihi kumbe ni watu kuipenda Autum /Winter.
Well kipindi hiki huwa a bit depressing sasa kwanini mtu usijichie-up kwa kujivalisha  na kupendeza ili ufurahi Moyoni? Inachukua Muda (hasa kama unawatoto)  lakini unapata faraja na siku yako inakuwa Njema sana. Nitajitahidi(finger crossed) kuwa na-share "inspo" kwa wale akina Mama going on 40 kama mimi.


Nathamini na kuheshimu Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Monday, 5 October 2015

Dawa za Kuzuia Mimba.....Ukweli uliofichwa!


Haiyaaa! Kitambo eti?

Leo tuzungumzie Dawa za Kuzuia Mimba, pengine unajua Mengi kuhusu hili zaidi yangu kwa sababu mie sijawahi kuyatumiaga haya Makorokocho bana. Sababu kuu haikuwa kwamba niliogopa Saratani (zote zinaongeza Uwezekano wa kupata Cancer), au Kunenepa(inategemea na Mlo wako) au kukonda bali sikutaka kuwa "mchafu"......Napenda Ngono sana tu ila sina Mpango wa Kuolewa na Wewe wala kuzaa na Wewe sasa kwanini unikojolee(achie uchafu wako, wakati wangu unauosha in sekunde).

Mara nyingi huwa nakuwa Mkali ikiwa Binti(well mdogo wangu) ananijia na kuniomba ushauri wa kutumia Dawa za kuzuia Mimba wakati hana mpango wa kuolewa na huyo Bf wake.....nkauliza utakojolewa na wangapi in your life wajameni??!! Pia huwa naudhika ninaposikia Wanaume wanasema kuwa ni kazi ngumu sana kumalizia Nje na Condom inapunguza "utamu" na hivyo kuwasukuma/Lazimisha Wanawake kwenda na kutumia Vidonge/Sindano au kufanyiwa "upasuaji mdogo" ili kuwekewa ile "Y" aka Coil.
Madhara(side effects) za Dawa hizi(ondoa Condoms kwenye Pic hapo juu) zipo nyingi na zinazojulika ni zile ambazo ni za Kitibabu. Zile za kihisia huwa zinafichwa.....well wanasema unaweza kuwa Depressed  in which inaweza kufanya Uhusiano/Ndoa kuwa na matatizo sasa hilo sio ninalotaka kukuambia hapa.

Wanaume hawa hawa wanaowalazimisha Wanawake kwenda kuongeza Mahomono wasiyoyahitaji, huwa wanashangaa kwanini  Wake/Wapenzi wao hawawapendi/tamani tena, unakuta Mkimama anavutiwa na aina nyingine kabisa ya Wanaume na sio alie nae tena(anakuwa sio type yake)......mara zote utasikia "tangu Mke wangu kazaa, amebadilika sana, hanipendi tena".....well si ulikataa kutumia Condom na kumlazimisha atumie Dawa za Kuzuia Mimba.
Sasa kwa huku Ughaibuni kila Dawa unayopewa inaelezea faida na hasara zake(sio kupewa kama zawadi na Mhudumu wa Dula la Dawa Baridi), lakini badiliko ya Mwanamke kutompenda Mwenza wake anymore huwa hawaiweki wazi(nadhani kwa sababu za kibiashra), lakini inasemekana kuwa, Mmwanamke anaeanza kutumia Dawa za Kuzuia Mimba baada ya kukutana na Mwenza wake(mwanaume) hubadilika na kutokumpenda tena mwanaume huyo.

Na wale ambao wanapenda Wanaume wakati tayari wanatumia Dawa za Kuzuia Mimba hubadilika na kuwachukia/kutowapenda waume zao pale wanapoacha kutumia Dawa hizo......ndio maana wakimama wakishika Mimba huwa na Mahasira  kwa waume wao eeeh? Homono...homono....HOMONOO!
Stori Time: Kuna mjamaa na Mkewe, wamependana kwa Miaka kibao na kujaaliwa watoto kadhaa. Life happened(matatizo) wakatengana sio kwa hiyari bali kwa sababu za "kisheria", jamaa Kaswekwa kwa Miaka 2 na hawakupewa ile "haki" ya kupata Ngono mara moja kwa Mwezi so Mkimama(mkewe) akaona aiii ya nini kuendelea kutumia Midawa ya kuzuia Mimba wakati Mtiaji Mimba yupo Jela, Mkimama aka-withdraw.
Mara akaacha kwenda kumtembelea Mumewe Jela, akienda ni kwasababu watoto wamelazimisha. Mkimama akaanza Kupendezwa na "type" nyingine ya Wanaume.....unaijua ile hisia ya "nimevaba na nimepoteza Muda wangu  na nimekuwa used na limtu ambalo hata sio type yangu" ile....yeah? kama vile unakutana na Ex  halafu huamini kama ulilala nae na kujiuliza hivi nilikuwa nimelewa au? yaani huyu ndip angekuwa mke/mume/  Mama/Baba wa wangu YAACK!! au ni mimi tu?! hihihihihihi.

Basi Baada ya Miaka yake Mitatu (Miezi 18) jamaa huyu hapa, Mkewa walaaa hana habari. Mumewe anaanza kushangaa kulikoni Mke wake anatereza nje nini? hakukuwa na Ushahidi wala nini. Mke msafi, alikuwa nasubiri Mumewe atoke ndio aombe Talaka maana tangu kaacha kutumia Dawa za Kuzia Mimba amejikuta hampendi wala kumtamani Mumewe tena.
Jamaa akaanza kulia, hajui ataishi vipi bila Mkewe.....watoto wanabembeleza Mama aendelee kubaki na Baba yao, lakini Mama anasema hawezi kwa sababu Baba yao sio Mtu ambae anampenda au angempenda kama asingekuwa "chini" ya Madawa ya Kuzia Mimba.....amevaba!!


Hii haina Mikutano ya Familia, wala Saikolojisti wala Kansela wa Mmahusiano na Ndoa Kanisani kwenu.....Kuvaba hakuna Dawa wala Therapy na Yesu hausiki. Ziiiii Endi.


Naheshimu na kuthamini Muda wako, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Sunday, 4 October 2015

Maharage Mabichi kutoka Tz yauzwa ASDA-UKUnajua ile furaha unayipata unapokula kitu kutoka kwenu ambacho hujawahi kukila ulipokuwa kwenu? Kwamba unakula kwasababu tu unahisi unampa sapoti Mkulima wa kwenu.

Hii ni mara ya tatu nanunua bidhaa hii  kutoka Asda kwasababu kuu mbili. Moja ni ya kijani(sababu za kiafya na kutunza mwili) na pili ni kwasababu yanatoka Bongo.

Jinsi ninavyotengeneza: (kama upo interested)...
Kula na/kwa Wali kama mboga: Nayachemsha kwa sekunde kiasi kisha namimina Tui la nazi (well unga wa nazi uliochanganywa na maji ya moto). Ongezea utamu kwa mlo wako kwa kuweka Embe mbivu au Ndizi mbivu.Kula na Samaki bila Wanga: Nayachemsha 
pamoja ya "maua ya coli" na "brocoli" kisha  nanyunyizia pilipili Manga na Chumvi kisha namwagia "Fish sauce" kama uonavyo picha na tuvipande twa  Samaki.

Kama ni mpenzi wa Rost pia zinakwenda vema hakikisha una Gravy. Unaweza kuchanganya hizo na Kisamvu (kuungwa na Karanga)au Majani ya Kunde au Mchicha kisha unga kwa kitunguu na Tui la Nazi.Sijawahi kula hizi makitu kabla ya kuja huku ....sijui yanapikwaje kibongo bongo (niamini mimi ni mpishi mzuri sana tu hihihihi) nimejaribu kupika kwa namna nklizokutajia na zinalika vema sana.....sasa wewe unayapikaje?Ahsante kwa kuichagua blog hii.

Babai.