Heri ya J'Nne,
Kama nilivyokuahidi Wiki (mbili na Siku Moja) iliyopita (bonyeza hapa kama ulipitwa) kuwa nitakuja nikukumbushe tu ni kwa namna gani Imani yako ya Dini inaweza kuyumbisha Ndoa au Uhusiano wako.
Kwa kawaida wengi hudhani kuwa mtu anapokuwa Mumini Mzuri wa Dini au "anamuogopa" Mungu ndio atakuwa muaminifu, atampenda kwa dhati, atakuwa mkweli, hatomuumiza na mengineyo mazuri mazuri.
Ukweli ni kuwa Mtu wenye Dini mara nyingi huwa mwepesi kutenda "dhambi" au yale ambayo hayaruhusiwi na Dini zao akijua kuwa atasamehewa, sio tu na Mungu bali wewe Mwenza wake unapaswa kumsamehe. "Ikiwa Mungu aliemuumba anatuambia tusamehe iweje wewe ushindwe kunisamehe".
Mazoea hayo ya kutegemea kusamehewa kila unapofanya makosa ya makusudi hupelekea upande mmoja kuhisi upweke na kuondoa Amani na Furaha kwenye Uhusiano /Ndoa. Hii inaweza kupelekea kujitenga na pengine kutafuta furaha Nje ya Muungano wenu. Hilo moja.
Pili, Imani yako ya Dini inakuzuia kufurahia Tendo vilivyo kwa kuwa "Freak" unapokuwa faragha na Mumeo au mnakuwa waoga kujaribu vijimambo vingine ili kufurahia uumbaji wake Mungu. Unahisi kuwa Mungu hatopendezwa kwa sababu wanaofanya hayo ni "Malaya".
Sasa kwa baadhi, wakikosa "u freak" kutoka kwa wenza wao, huamua kujaribu nje....ukimuona Mama wa Mchungaji/Mtumishi anavyojiheshimu huwezi amini anayoyafanya kwa Kiongozi wa Kwaya. Ukimuona Sheikh huwezi kuamini anayofanyiwa Mwalimu wa Madrasa(hihihihihi), kabla hujakasirika, hebu malizia aya ya mwisho.
Nnacho jaribu kusema hapa ni kuwa Imani yako ya Dini isiwe Kikwazo cha wewe kushindwa kumunysha Mwenza wako Ujuzi, Utundu, wehu wako n.k mnapokuwa Faragha. Natambua mmeambiwa maneno yafananayo na "Mume huna mamlaka juu na Mwili wako bali Mkeo na Mke huna Mamlaka juu ya Mwili wako bali Mumeo"....hii haina maana kufanya Tendo kwa namna ile ile kila siku, bali kuwa huru kuufanyia chochote (kizuri) Mwili wa mwenza wako ili kumpa Raha(well this is my logic).
Nisikuchoshe, nathamini Muda wako hapa.
Mapka wiki Ijayo....kwasasa, bai!
Comments
Dini inaweza kuyumbisha uhusiano/ndoa yako kama hauifahamu vizuri wala haujapata na kuyaelewa mafundisho yake. Strong values zinazojenga uhusiano imara zinafundishwa vizuri sana kwenye dini.