Wednesday, 30 April 2014

Celebs

Hii jamii ina power ya ku-normalize kila kitu, hata vile ambavyo ni normal lakini jamii nyingine hawavifanyi, wao hu-normalize.Mfano ni "attachment parenting" ambapo mama analala na mtoto wake na kumnyonyesha for as long as possible.Hiyo "attachment parenting" si ni kitu cha kawaida kwenye jamii ya Kitanzania(na Afrika kwa ujulma)....nimezaa mwanangu wa kwanza nikapigwa marufuku kulala nae ili kuepusha cot death.
Nikakumbuka Mama alipozaa wadogo zangu 3 wa mwisho, wote alikuwa analala nao kitanda kimoja na hakuna aliepoteza maisha....Aii....nikawa na lala na mwanangu ka' ifuatavyo na amenyonya mpaka mwaka na miezi 3. Siku hizi analala chumbani kwake lakini akiota ndoto mbaya anakimbilia kwetu so tunalala wote wanne.Huyu wa pili bado analala na sisi na bado ananyonya (mwaka na miezi 3) tena huyu ni king'ang'anizi kuliko kaka yake ambae hakujali kulala peke yake au kulala na sisi..Kingine ni Kuzaa kwa kupasuliwa, hee kila mtu si akawa anataka kuzaa kwa kuchagua upasuaji (selective C-section)....siku hizi Celeb wanadhani ni sifa kuzaa kiasilia.Don't you get annoyed when liCelebu linasema uchungu wasn't that bad(wakati alidungwa Epidural sijui ganzi)....
Alafu kukuhakikishia anaweka lividio lake ana-push huku anacheka......the shenzi kabisa.Mwisho kabisa ni kuzuia watoto wasitumie Gadgets, wasitazame TV na badala yake wacheze nje, wajifunze nature, wapande miti, wacheze na wadudu n.kThat is how we've been doing for years in Afrika, yaani kwetu hatuna hizo mavitu, tunacheza na Nature tena sio ya kutengeneza ni ile necha ya necha (isipokuwa kama wewe ni wa Kishua, umeishi kizungu).Naenda kuwanunulia wanandu Kilo 3 za Mchanga ili wachezee huko gadenini....how sad!


Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 29 April 2014

Uswahili Mzigo...

Halo, haloooo....Halo ya Mbuzi meeeeee!


Kuna tofauti kati ya Uswahili way of life which ni kitu cha kujivunia, ni kama "culture"....alafu kuna Uswahili "ile hali ya kutokuwa Mstaarabu" na Uswahili simply kwavile wewe ni mwafrika(Muafirika).


Wenzetu wa Kishua hawapendi Uswahili kabisa yaani! Wao wanaishi Kizungu zaidi....usiniulize kwanini wengi wao wakifika Uzunguni (Ulaya, Marekani, Down Under etc) wanakuwa Waswahili kupita wale Waswahili wa Mtaani kwetu pale KissWay(Kisarawe).


"Unaedha" dhani kuwa wamebadilika, hapana hawajabadilika bali kuishi "Kizungu" Ulaya inabidi uwe Posh....U-posh waenda sambamba na Pochi(mahela).....sasa inawezekana kabisa tuhela twako + rangi yako, Elimu na ulikotoka inakuwa ngumu kidogo kuishi "kizungu" kwa Wazungu.....sijui umenielewa?!!!


Sasa unaishia kuishi na Waswahili wenzako "wa Kizungu" ambao awali hukujua tofauti yao kati ya Middle class, Working class, Chav n.k


Kama tunavyojitenga Tanzania kuwa kuna Uswahilini na Ushuani....Uzunguni nako kupo hivyo, na most of us huwa tunaishia "Uswahilini" kwasababu "rank" yetu kiuchumi na ki"class" haituwezeshi kuishi "uzunguni" kwa Wazungu.


Uswahili ninaojaribu kuuzungumzia hapa ni "hali ya kutokuwa Mstaarab"....Jirani yangu kapangisha nyumba yake Waswahili wa Kizungu....mbona tunakoma!!Unasikia "Dean honey can you get me my Channel bag please?...oh don't forget my D&G trainers"(fake ones)

Wakiwa wanatoka utajua, wakirudi utajua....full makelele, gossiping tena kwa sauti na Vicheko juu.....Gari lao sijui wameliwekea nini (sio mtaalam mie) basi latoa muungurumo mkubwaa....aaaaah Uswahili Mzigo.


Yote hayo ni kutaka watu wajue kuwa wao wanavaa "dizaina" na wakitoka au kurudi lazima mjue sababu "they run the street" Muungurumo wa Gari ni sooooo cool(I mean so annoying)!


Mkiwa mnatoka/rudi nyumbani, wote wanatoka Nje kuwaangalia....awali nilidhani hawajawahi kuona Familia ya Weusi....then nkagundua wanataka urafiki.

Aiii Sababu kwetu Kisarawe haina maana mimi ni Mswahili....na Ulaya haijanibadilisha,

Nipo vilevile(kitabia).....vingine? Hehehehehe total kutepeta!

Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Monday, 28 April 2014

Baba zetu nao...

Wiki Mpya oyee!

Nimeacha kujivunia Tanzania kama Taifa(Kisiasa) miaka kadhaa iliyopita, najivunia Tanzania kama Nchi na baadhi ya Tamaduni zake, kama vile kuvaa Vibwaya (vile vifupi, kuachia tumbo na kufunika Matiti), Ngoma na nyingine nzuri nzuri.
Kuna unataratibu wa baadhi ya wanaume kudai kuwa mwanamke yeyote atakaelala nae ni Mama yako na mtoto yeyote atakaezaliwa na mwanamke ambae sio Mama yako ni Ndugu yako. Sina uhakika kama ni Utamaduni,Tabia au pure______!
Mama yako ni yule aliekuzaa au "kisasa" aliekulea tangu ukiwa na umri wa masaa au siku chache.....sio random women aliolala nao Baba yako.Pia ndugu yako ni yule mliotoka tumbo Moja, wengine ni Jamaa (tena ukiamua kuendeleza ujamaa huo kwani sio lazima).
Tabia ya Baba kulazimisha watoto wao kuwaita wanawake wengine Mama au watoto waliozaliwa huko (kabla au baada ya Ndoa) wadogo/kubwa zao sio haki na sio sahihi kwa mtoto/watoto husika.Huyo ni Mkeo na hao ni watoto wako wewe na huyo Mkeo na hao watoto ndio ndugu,
Ku-share Baba haina maana ninyi ni ndugu wa Damu kwani asilimia kubwa ya Damu yako/yake ni kutoka upande wa Mama sio baba......(In my head).
Kwani Mbegu za Mwanaume huwa na Damu? Lile yai la mwanamke ni Damu na jinsi Mimba inavyokuwa Mama na Mtoto wana-share Damu.....sasa Damu ya Baba (in my head) haina uzito linapokuja suala la "undugu wa Damu" kutoka upande wa Baba bali Mama si eti?.
Nukta hapa ni kwamba, Baba wa Kibongo acheni ku-bully watoto wenu na kulazimisha undugu au "ufamilia"....ili kufurahisha Ego zenu(nina wake/watoto wengi)." Mimi Yakhe? Ninao kumi na Tano na mwingine anakuja hivi karibuni hehehehe familia kubwa sana hii Yakhe, mama zao wapo 7"....hapo hata Tofali la choo huna.Usichukue au kutumia maelezo haya kama kielelezo cha Kitaalamu mie sio Mjuzi, nimesema tu kilichonijia kumkichwa.


Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Friday, 25 April 2014

Mkorogo...

Habari...


Mkorogo ni kutumia bidhaa "illegal" au "home made skin lightening" na "kujiton" ni kutumia bidhaa zilizothibitishwa na Jamaa wa Ubora wa Viwango eti?.....wote nia yao Moja.
Waafrika kwa Waafrika kwa ubaguzi wa rangi zetu hatujambo....tofauti ya Ubaguzi wetu sisi Watanzania ni kuwa hatutengani au kuuana kwa sababu baadhi yetu ni weusi sana au weupe sana.
Well, isipokuwa kama wewe ni Mweusi tii alafu huna nywele laini na unaishi Somalia au Sudani Kaskazini.....oh au Chotara ndani ya South Africa.
Ila Machotara ndio huwa wabaguzi zaidi kwa Weusi kuliko sisi wenyewe kwa wenyewe....Usiombe ukutane na Chotara wa Kizungu aliekubaliwa kwenye jamii ya Kizungu ayeee!!
Anyway, nukta hapa ni kuwa tofauti ya weusi wetu wa ngozi ndio hutufanya tuwatanie wenzetu na kuwaita majina....Mf: Cheusi dawa, Mpingo,Cha usiku n.k
Huu utani huwafanya baadhi(hasa wanawake) wajisikie wanyonge, hawavutii....inafikia mahali wanataka kufanya ngozi ing'ae kidogo wenyewe wanaita "kujiton".
Wao kufanya hivyo haina maana wanataka kuwa Wazungu au Waarabu, nadhani wanataka kujisikia vema kwani hakuna kosa "kuboresha" kitu ulichonacho au ulichopewa na kukifanya kiwe vile utakavyo.
Hakuna haja ya kuwasakama na kuwacheka wapaka Mkorogo na badala yake waelimishwe.
Kama ilivyo kwenye Masuala mengine ya Afya, watu waelimishwe kuhusu Matumizi ya "Sun creams", Elimu kuhusu "ingredient" za bidhaa wanazotumia ili wajue Chemikali hatari ni zipi na salama ni zipi wajue.
Miili yao ni mali yao, wanafanya watakacho...kama ni Saratani ya Ngozi au kuaa Figo ni juu yao (Dawa za Kuzuia mimba pia zinasababisha Saratani, Sigara je? Vipi Pombe? Uzinzi?.....)Kama wee umezima ka' Ms. Lupita Nyongo, unajipenda na kujivunia weusi tii wako Power to you.Haina "kujiamini" hapa hata mie ningekuwa nimezima ka' Umeme wa Tanesco aiii "ningejiton".... bahati mbaya Babu mzaa Bibi alikuwa Chotara (hivi nilikuambia.....hihihihi)


Takuona J'3.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 24 April 2014

Usinijaji....

....relax is a human nature!


Tangu u-single mother umekuwa "fashion" vijana karibu wote wa late 20s na early 30s walishazaa huko nyuma, hivyo ni ngumu kweli kukutana na mtu ambae ni "m-clean" ka' wewe (hana mtoto/watoto).
Shughuli inakuja kwa sie tuliozaa(Oa/Olewa) na Wanawake/Wanaume ambao washalizaaga "ujanani" huwa tunajajiwa sana yaani.
Unaonekana "Mwizi" kwenye jamii na familia, hata mtoto aliezaliwa kabla wewe hujakutana na Baba/Mama yake uhisi kuwa wewe ndio sababu ya Baba/Mama yake kula Buti la pua ( I know how it feels cause I was a kid once).
Unaenda mahali na Mumeo/Mkeo na tutoto twenu (bila yule wa kabla) watu wanawasonta-sonta (Shinganya Oyee!! Kusonta ni kukunyooshea kidole kama ulikuwa hujui)....anyway!
Wengine bila haya wanaanza kuuliza "nanilihu na Mama/Baba yake hawajambo" mbele yako just to piss you off....Mindugu mingine Mikosi kweli!!?
Inafikia mahali unajistukia na kuhisi kutaka kujieleza ili kuweka mambo sawa, "Ndugu jamaa na Marafiki mimi sio Mwizi, nimekutana na huyu mutu miaka 5 baadaye. Wezi ni hao walipita hapo kati kabla yangu".
Alafu unakumbuka....aiii kwani mnanisaidia kulipa Bills? Unasonga mbele kama ifuatavyo.....Ni muhimu kuhakikisha mkibaba/Mkimama aliachana na Mkimama/Mkibaba aliezaa nae angalau miaka 2-3 kabla yako.....ili kuwe na wengine kati wamepita/pitiwa kabla yako.
*whispering* Ukiweza epuka kuoa/olewa na aliekwisha zaa kabla, unless you want to stick with an Ex for the rest of your remaining years na kujajiwa....!


I hate EXes....oh! Kumbe na mimi ni Ex wa mtu?....I hate me too.


Kwaheri kwa sasa....
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 23 April 2014

Kufananishwa/Linganishwa....

Jambo!


"Baba yangu alikuwa bla bla bla kwanini wewe usi bla bla bla kama yeye" kaolewe na Baba'ko sasa (this apply to wakibaba pia, kaoe Mama yako sasa eti)....
Kama tulivyozaliwa Nyakati, Siku na Dakika tofauti ndivyo ambavyo tunapaswa kuishi tofauti(na wazazi wetu).
Utaishije maisha waliyoishi wazazi wako wakati wewe ni mtu tofauti na unaishi kwenye Nyakati tofauti na wao?
Kuna zile "manners" nzuri ambazo ni muhimu maishani na kila familia inapaswa kuwafunza watoto, mfano Kusalimia, Kuomba, Ukarimu, Heshima, Kushukuru, Msamaha....
Kama utafananisha hizo hakunaga mashida, mengine yaliyobaki yaache yabaki huko huko yanako stahili.
Ungependa kuwa au kuishi na mtu kama Baba/Mama yako? You need to go out a bit more rafiki.....by out I mean OUT OF YOUR COUNTRY!!!


Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 22 April 2014

Kujipendekeza Kipaji....

Helloooooo!


Napenda kuandika mambo ambayo watu huogopa kuyasema lakini yanawakera...kwanini? Sababu sinywi Pombe hehehehe...!
....Kwa kawaida Ndugu wa mume hupaswa kuwa karibu na wewe (hata kwa ku-pretend) ili ujisikie umekaribishwa kwenye Ukoo eti...kwa Kacha yetu ya Kitanzania.
Mwenyewe unajitahidi kuweka mawasiliano ya karibu....wao walaa(mpaka uwatafute)!
Unajipa moyo labda wanashughuli nyingi na muda hawana, unasubiri siku mbili-miezi mitatu still Jiiiii....hee unaanza kujistukia, unataka kumuambia Mumeo lakini unaona noma.Maana wengine hawachelewi kukuambia "unataka kutugombanisha, we mwanamke tu....wale ndugu zangu"....so unaugulia Moyoni.
Kujipendekeza mwisho mara 3(in my head), unajaribu kwa Mwaka mzima wao hawajitumi kukutafuta hata XMas to Xmas!
Sina marafiki kwa ajili hiyo(sijui kujipendekeza, najaribu....usipoweka effort nafunga Ukurasa na songa mbele.....
Unajiuliza nani atanizika "nikikufa" maana sina Ndugu wala marafiki? Aiiii mie mtoto wa Serikali babu....haitoniacha nitoeze!
Kuna Local Newspaper hapa Kijijini, hutangaza Misiba ya watu wasio na Ndugu, so kama utaguswa na ungependa kwenda kumzika Mhusika asie na ndugu wala rafiki.Hata wakija kwenye Msiba hawapunguzi madhambi yako...Ulaya bana, raha sana....Inabidi Serikali ya Tz itoe huduma kama hii...well ipo...unafukiwa na Almashauri ya Jiji ka' takataka.


Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 17 April 2014

Kazi za watu...

Maoni ya Mhariri...siku hizi sote tunatoa Maoni on particular or similar issues....Teknolojia na Uhuru wa kujieleza/Changia utakacho au ulichokiona/shuhudia unaharibu kazi za watu.
Mfano, kazi ya Uandishi wa Habari wa Magazeti na Radio....imeingiliwa na Blogs, Online Radios, Social Media na YouTube(is YouTube sosho Media pia?).Jamaa wanatumia Sosho Midia kama "chanzo cha uhakika" na wale Waandishi wavivu wa kukopi na kupesti ndio wamerahisishiwa kazi.Habari zenye Uzito ni zile za Uchunguzi....labda na mahojiano magumu ya Wanasiasa!Jana nipo YouTube (napenda Fashion Haul na beauty review....how sad!!?) nikakutana na Matangazo kutoka Kampuni moja kubwa ya Urembo....alietumiwa ni Vlogger na sio Model/Celeb kama nilivyozoea.Nkajisemea eeh Teknolojia imeharibu na kazi za Celebs na Model pia.....sio haki kabisa!
....Hebu ngoja kwanza! Hawa Vlogger ni real people wanatumia bidhaa na kuzi-review hivyo wao kutangaza bidhaa husika wanaaminika kuliko kutumia Celeb au Model ambae hatumii, anatangaza kwasababu yeye ni "Brand"(in my head).
Oh hey....Shukurani za dhati kwako wewe unaepitia Blog hii. Natumaini huwa unapata kucheka au kutabasamu kutokana na uandishi wangu.Inawezekana kuchapia ndio kunakuchekesha....na pengine unajisemea "hili nalo" vyovyote vile mie nashukuru.


Mungu akijaalia, nitakuona J'4. Pasaka Njema.

Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 16 April 2014

Diet...

Hiya....

Utaratibu wa kula kwa kila mtu ni Asubuhi, Mchana na Jioni. Baadhi yetu tunaongeza Mlo in between na wengine hatumudu Milo miwili kwa siku.Sijawahi kujinyima ili kupungua au kukonda, nimekuwa chembamba maisha yangu yote ya Usichana mara boom nikafikia size 12(Mimba hizo).Nikajiambia, ah nikijifungua nitakuwa nakwenda Gym ili nirudie kamwili kangu ka enzi....aiii muda si ukagoma kutokea. Nikaamua tu kupiga mazoezi yangu mwenyewe nyumbani.Sikuweza ku-keep up na mazoezi kutokana na Uchovu (mother of two kids under 5 baibeee isn't as easy as Celebs looove to lie on our faces)....
Nkapiga mahesabu, mmh am on my 30s nikishangaa hapa nitakuwa na kitambi for life....nifanye nini sasa wajameni?
Nikapata jibu...relax Dinah Relax.....wacha Kichanga afikishe miezi 9 (atakuwa anajitegemea...kukaa peke yake na kulala vema usiku) alafu ndio uanze mambo yako.
Kusubiri mpaka afikishe miezi 9, mbali alafu sio guarantee atakuwa "anajitegemea" au kulala vizuri. Back to my hesabu!Anhaaa!! Nitakuwa nakula Dinner (Wali/Viazi/Ndizi/Ugali + Mboga yeyote) asubuhi na Breakfast Jioni (Uji, Ndizi 1 + Chai au Mkate na Yai + Chai).
Well, sina hakika "diet" yangu imesaidia mimi kupungua au ni kunyonyesha + Mazoezi.....lakini najua kuwa imechangia kwa namna moja au nyingine.
Sijawahi kuwa Mnene hivyo kugonga size 12 hakika nilikuwa Kibonge (in my head) na hata wadogo zangu waliokuwa wakiniita "Chikonda" mara wakawa wananiita "Chibonge"....Mambo ya kufuata Diet za so called wataalam au Watu Mashuhuri/Maarufu zinabadilika ka' software na zinaongeza stress tu....


Kula pale unapohisi njaa na kula kiasi....

Siku njema.
Mapendo tele kwako...

Monday, 14 April 2014

Nywele zako ni 2a au 4z?

Wenzetu ambao wamezaliwa na Mzazi mmoja Mwenye asili ya "Nywele kunyooka" wanapenda kutupeleka mbio sana sisi wenye kipilipili.
Hata kama Bibi yake Bibi wa Baba yake ndio alikuwa "nywele kunyooka" na mweupe bado mtu ana-claim yeye ni asili hiyo which is Okay ila msitupeleke mbio sasa eti!
Juzi nimesoma mahali, Binti mmoja anasema anamshukuru Baba yake kwa kutokuoa Mwafrika mwenzie maana angezaliwa mbaya na mwenye nywele mbaya za 4b....anampenda sana mama yake ambae ni Mzungu.
Nkakimbilia ku-google ili nijue maana ya hizi namba na herufi "Nyweleni"....well nilitaka kujua namba ya Nywele zangu, aiiii nadhani ni 5z...the higher the number the Mbayest the hair.
Tunanyoosha nywele sio kwasababu hatuzipendi tulizozaliwa nazo au tunataka kufanana na nyie bali ni kutaka kuzi-manage kiurahisi...Ni kipilipili cha haja lakini kuna wakati kilikua na kufika katikati ya Mgongo....HAPANA!! am not that short...am 5'4 nadhani Babu mzaa Bibi alikuwa Chotara....hihihihihi!


Kwaheri kwa sasa!
Mapendo tele kwako...

Saturday, 12 April 2014

Ugomvi wa Ndugu...

Sie tuliozaliwa wengi (zaidi ya wawili) huwa hatuoni umuhimu wa attention ya wazazi wetu....labda kwavile hatukupewa au tulipokuwa tukihitaji kwa vile kulikuwa na Kichanga. Tuliihsia kuambiwa "acha kudeka" na kofi juu.
Na baadhi yetu tuliishia kulea wadogo zetu ambao walihitaji attention zaidi yetu wakati Mama na Baba wako busy na mambo yao mengine kama sio kutengeneza mtoto mwingine.
Tunapenda kuwamwagia sifa kutokana na malezi yao mema kwetu na kutangaza ni namna gani tunawapenda na baadhi hudai wazazi wao ni mifano mizuri kwao (good role model)!
Wakati mwingine ni kweli ni "good role model" lakini mara nyingi ni Hatia moyoni inakufanya udhani kuwa walikuwa wazazi bora na wanafaa kuigwa....si unajua the "bila wao nisingezaliwa au kusomeshwa" sort of guilt.....
Well (1)-Uamuzi wao kukuzaa (hukuomba kuzaliwa) + (2)- ;ukumu lao kuhakikisha unaishi vizuri na unapata Elimu hivyo wacha kuhisi hatia.

Kuna mahali wazazi wetu walikosea....kwasababu kutoa "attention" ya kutosha kwa kila mtoto kati ya 3 au zaidi sio rahisi (I struggle with my 2)....!!
Watoto waliozaliwa wengi huwa wanajumuishwa linapokuja suala la "attention"....pamoja na kuwa wazazi wanaupendo wa dhati bado upungufu wa attention unaweza kusababisha matatizo ya Ukubwani.
Umewahi kujiuliza kwanini kwenye kila familia yenye watoto zaidi ya wawili (wengi) huwa kuna ugomvi kati ya siblings?!!
Inatokea Dada au Kaka anakuchukia bila sababu ya msingi.....likija suala la Mirathi ndio watu wanatoana roho kabisa....chanzo? Revisit enzi za utoto.....
Wazazi wakienda(fariki) wanaachia "hisia" zao huru....issue sio Pesa wala tamaa ni kukosea kwa wazazi wakati mkiwa wadogo.....Kuna wakati unajiuliza hivi sisi ni baba mmoja mama mmoja kweli?!!
Usichukue na kutumia maelezo haya kama ushahidi, mie sio Mtaalam nisema tu kilichonijia kichwani asubuhi ya leo....


Kuwa na Mwisho Mzuri wa Wiki.
Mapendo tele kwako...

Friday, 11 April 2014

Pale 40something anaposhindana na 20something....

Kwa hamu nasubiri siku nitakayofikia miaka 40(God willing) ili namie nijisikie kama wanavyojisikia waliogonga hiyo namba.Natumaini Botox itakuwa imeshuka bei by then, maana Viganja kwa nyuma vinamakunyanzi ka' Bibi yangu wa miaka 90.Wengi huamini kuwa miaka 40 ndio Uzee ila nadhani Tz mwanamke akifikisha miaka 30 huitwa Mzee.....Mtukome....Mzee Mama yako (hii imetoka mchicha ka tusi eti?) Well, namaanisha mwanamke aliekuzaa ndio Mzee.
Celebs waliofika Umri huo wa miaka 40 hujisifia kuwa wanajisikia kama walivyokuwa kwenye umri wa miaka 20s ila tofauti ni kwamba sasa wanajijua, wanajiamini, wanajua watakacho nakadhalika.........well inawezekana kabisa sio kweli ila ni mikakati ya kutaka kuendelea "kuonwa" kijana.
Hakuna haja ya kuendelea kufanya uliyoshindwa kuyafanya enzi zako za Yahoo na Hotmail, relax na uwaache watoto wa 20something wafurahie Era yao.
Tunafanikiwa sana kuficha au kudanganya Umri lakini sura siku zote haiongopi mara boom "inasema" kwenye Vurugu za Mwembe Chai ulikuwa in your 20s....!


Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 10 April 2014

Tunapenda kufanana...

Heri ya Alhamisi....

Katika kupitia Vlogs (nilikuwa nanfanya uchunguzi kuhusu nywele) nikagundua kila chumba au Vanity room (where they film) vinafanana....Nikatafuta ukweli kwanini wote wanafanya hivyo? Nikagundua chanzo ni Kadashianzi.Mara nikakumbuka watu wa kawaida tu kwenye jamii pia hupenda kuigana kuanzia Nyusi, Fashion mpaka mapambo ya nyumba/ndani....Blogs na Sauti (bwahahahaha)Najua kwa baadhi ya watu ni muhimu kufuata "trends" na hivyo kufanya kama wanavyofanya wengine.....kama inakupa furaha maishani why not eti?Dressing table yangu ni ile ya kizamani, kabati upande mmoja, chini na juu droo katikati kioo chenye kijisehemu cha kuweka Manukato, Wanja n.k!...Vanity/Dressing Room? Aii only in Amerika na Kanada (majumba yao makubwa) or Mamilionea wa Bongo na Ulaya....
Tangu nilipokuwa Mdogo nilikuwa sipendi kufanana na watu wengine, si unajua midosho nini na nini....Dar combine...hihihihihi.Ndani kwangu hakuna Picha ukutani kuna siku mgeni mmoja akasema humu ndani "doesn't feel like home, there is no family photos" nkamwambia "we are the ones who live here, why would we want to look at ourselves on the wall"?Well, ndani kwetu kupo kama shule ya Chekechea(Toys kila kona)....hihihihihihi!

Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Wednesday, 9 April 2014

Changudoa...

Kwa kawaida jamii hushupalia ikiwa mhusika au wahusika ni Wanawake. Tena wanawake wenyewe ndio wanaongoza kuwakandamiza Machangudoa.
Katika hali halisi Machagudoa hasa kwenye maisha ya Chuoni ni kitu cha kawaida, haina maana mimi nimewahi kufanya hivyo bali kuna wake kwa waume niliosoma nao walikuwa wakifanya kazi hiyo ili kujimudu.
Siungi mkono kazi yao na wala sipingi kwasababu sijui ni circumstances gani(ukitoa tamaa ya high life) zimepelekea wao kufanya uamuzi huo huko Nchi za watu....
Tambua tu kuwa wanaume pia wanafanya Uchangudoa Nchi za nje na sio Wanawake pekee.
UK ya leo sio ile ya Tony Blair na kama UK maisha magumu huko kwingine si ndio basi tena (in my head).Kwenda "Majuu" is not as cool as it used to be....ndio maana watoto wa Vigogo siku hizi hawaendi Nje (hawaishi Nje), wanafungua mabiashara makubwa au wanakuwa Wanasiasa.....Uanasiasa na kumiliki Biashara yenye mafanikio is new Cool.


Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Tuesday, 8 April 2014

Uchungu wa Kuzaa + Kujizuia usi-Push = Near Death

Mimba ya mwanangu ya Pili Iman haikuwa enjoyable + alipitiliza. Mkunga kanaipangia siku ya kuwa "induced" ili nipate Uchungu.Binafsi sipendi vitu ambavyo sio asili kwenye mwili wangu na hakika sio Uchungu, pia ni Mpinzani wa kuzaa kwa. C-section.Kwabahati nzuri (Mungu alijibu maombi) Asubuhi ya kuwa induced "chupa" imepasuka, nikawapigia simu wakunga wakasema wanajiandaa kunipokea wakati wowote.Mimi being mimi, nikasema nitavumilia mpaka maumivu yachanganye ili nikifika tu Hospitali nijifungue....maana kwa Barack ushamba/kutokujua tulienda Hospitali mapema....uchungu ukachanganya Saa saba....Lol!Anyway, nikapata uzoefu mpya sasa....kama unadhani Uchungu wa Kuzaa ni kamambe!!....Usiombe Kuumwa uchungu huo + juhudi za kuzuia mtoto asitoke.
Mambo yakaenda vizuri, Uchungu unakuja unarudi....ikafika saa Kumi na mbili Jioni, mara booom! Mtoto namhisi huyu hapa....naita baba mtu, kusanya Barack....hao garini.
Najisemea "Mungu nisaidie mtoto asitoke" nikawa naumwa huku nazuia kusukuma....Tumefika Hospitali Mume wangu akawapigia simu kuwa tupo Chini na sijiwezi, wakasema wanakuja na Wheelchair....Aaaah ile nawaona tu kwenye Korido na mavifaa ya kuzalishia mwanamke nikajiachia....wananiambia "breath-breath aaah" nikawaambia "Iman is here".Katikati ya Korido, mbele ya Mgahawa wa Hospitali Madaktari wanapata Dinner....Wakunga wakanilaza chini, madaktari wakaacha Dinner wakaja mbio kusaidia na kuweka "uwigo" for my privacy....one push Iman huyu hapa.
Wakakaweka kifuani then nikaletewa Machela (is it) anyway...wakakachukua na kwenda kukapa "first checks" in which kakafaulu 10/10.
Tukapelekwa kwenye Suite yangu ambayo ndio nilipaswa kujifungulia....Lol!
Misukosuko during my pregnancy....Iman is very special girl kwangu. Mwaka umepita, kananipa tantrums za kutosha.....naangalia nyuma....nacheka tu.


Kwaheri kwa sasa.....
Mapendo tele kwako...

Monday, 7 April 2014

Nywele....

Baada ya kujifungua Barack na kupoteza nywele za kutosha, nikavumilia mpaka nilipomaliza kunyonyesha.Niliposhika Mimba ya Iman nikaamua kukata nywele hivyo nimekuwa na nywele fupi kwa miaka 2.Siku moja nika-google kujua "Tiba" ya nywele zangu "kumwagika" kutokana na kunyonyesha(mabadiliko ya Homono). Nikakutana na Vlogs za hair journey bana...hee!Nikagundua mafuta yanaitwa Castor (mafuta ya Nyonyo) mwanamke si nikakurupuka....nikawa naosha nywele kila siku na kupaka Mafuta ya nyoyo + leave in + hair cream za kutosha,Wacha nywele ziendelee kukatika mpaka nikawa kipara hihihihihi (I was crying actually).Nikaendelea kufanya Uchunguzi kwa kusoma na kusikiliza Shuhuda za watu nikagundua kuwa nakosea na nywele zangu zilikuwa zinalainika zaidi(too much moisture) bila kupata nguvu kutoka kwenye Protein (nywele zinahitaji balance ya vyote).Ndio nikakutana na wadada wakitoa shuhuda kuhusu Aphoghee Step 2 treatment ambayo unatumia kila baada ya wiki Sita.Magic!!....hivi naongea tunywele twangu tumefikia masikioni nikatu-relax sasa hivi tunakaribia shingoni....


Ningegundua hizo Bidhaa kabla nywele zangu zingekuwa ndefu mno.

Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Matumizi ya Tablets kwa watoto....


Mambo!

Nitakuwa naandika chochote kinachonijia kichwani kwa wakati huo.....kuanzia malezi ya wanangu, habari itakayogusa Mtima wangu (usijali sio habari za Tz) na siku husika kwa ujumla.


Hali ya hewa leo ni ya Unyevu na Mvua kwa mbali,

Wataalam na wachunguzi wa huku wanalalama kuwa watoto wasitumie Tablets kwa vile zinawafanya wasiweze kutumia mikono kuandika au kuchora kama ilivyokua kwetu enzi zile.


Lakini Enzi zetu si zimepita? hizi enzi zao waacheni ila tuwe responsible na wanachokifanya kwenye Tables, Fundisha mwanao....usitegemee mtu mwingine (Yaya/Mwalimu) akufundishie just because you pay them to do so.

kwaheri kwa sasa.