Thursday, 30 April 2015

Miaka 30 ndio mwisho wa kutaja Umri wako...

Kwa mwanamke.....habari za Masiku tele? Ahsante kwa kuichagua Blog hii.


Nilipojuja Nchi hii miaka zaidi ya 10 nilikuwa kwenye my early 20s na nilikuwa nasafiri kama mtoto....sio nilifoji la hasha! Wakata Tiketi waligoma kukubali umri wangu na wakasema mie ni binti wa miaka 15yrs.


Nilinilikuwa nakaa Kijijini halafu nasoma London) na Kiingilishi changu cha kudandia akuu mkidada wala sikubisha so nikakata Kibali cha Usafiri kama mwanafunzi wa Kimataifa wa Miaka 15 ambacho ni Chee.Enzi hizo (2000s) hakukuwa na mambo ya kufuatiliana kwenye Passport.FAST FOWARD....nikawa na Mume ambae anakunywa Pombe, nikienda nunua Pombe wanagoma kuniuzia eti mpaka niwe na Miaka 25 hihihihi.Nikiwaambia mie ni mama wa watoto 2 na nipo in my 30s wananicheka na kunambia a 23yr old woman can have a child too so wanaomba  niwaonyeshe kithibitisho cha umri(Driving License) nawaonyesha.....misamaha mingi ikijumuishwa na hongera kwa kuluku so yang'i.Au kwa maana nyingine am a 23yr old who look like a 30something woman....hiihihihi got it? Wadada wa 20s wa sass wanaonekana watu wazima.Mama yangu alimzaa mdogo wangu wa mwisho akiwa na miaka 35.....hakika nakumbuka mama alivyokuwa so yeah. Hapana that isnt my age! Nakaribia 40 ndio my age(nimevuka 35).


Kuna kijisheria kisicho rasmi cha wanawake kutotaja miaka yao baada ya 25.....hawa huwa na hatari ya kuishi wakiamini bado wanaonekana in their 20s na pengine kushindana na 20s girls hass kwenye ulimwengu wa Sosho midia.


Mie nimeacha kutaja umri wangu baada ya miaka 30. Yaani ukigonga miaka 31 vitu vilivyokua muhimu in 20s havileti maana tena(i wonder why a 40yr  old anadai kuwa anahisi kama a 27yr).I hope I wont go back to my 20s when i hit 40......nataka kubaki hapa hapa kwenye 30s kihisia na kadhalika.

Babai.

Monday, 27 April 2015

Usafi na Kinyaa....

Ni vitu mbili tofauti....Natumai umeamka/shinda salama.


Mtu kuwa msafi haina maana ana kinyaa na mwenye Kinyaa sio kwamba ni msafi pia....japokuwa wapo wasafi na wanakinyaa pia(mie).....hivi ni kinyaa au uoga wa kupata maambukizo?Nakumbuka nilipokuwa nakwenda Hospitali kwa matibabu au kumtembelea Mgonjwa....nilikuwa naumwa kichwa balaa. Nikitoka tu maeneo ya Hospitali napona.


Natabia ya kubana Mkojo kwa muda mrefu(usijaribu hii ila kama ni mtu wa Kuendiketa poa) ili nisitumie vyoo vya wote(public)....Haja kubwa (sorry 4 TMI)huwa haiji nikiwa kwa watu au nje ya kwangu/kwetu.....hii sasa ni Saikoloji issue.Jana nimetoa siri yangu kwa Asali wa Moyo kuwa tukienda kwa watu(ndugu zake incl) huwa siogi wala kutumia vifaa vyao vya kujisafishia.Nitafungua Shower vema tu au kujaza Ndoo maji(inategemea nipo wapi) na kuacha shower iendelee au kumwaga maji as if naoga kumbe nanawa miguu...hihihihi.Badala ya kucheka akabaki kaduwaa hehehehehe well sina siri tena maana hata wewe msomaji umejua.


Huwa natembea na kila kitu changu (wipes zinachukua nafasi ya maji) najiswafi juu kwa juu halafu tukirudi Hotelini au kwetu(kwa mama yangu) au kwetu tunapoishi ndio nafanya ile kuoga na kujisugua.


Halafu kuna ile kugusana gusana kwenye Tube au Mabasi....wakati nasoma nilikuwa na tabia ya kuzunguuka na Daladala kwamba nalipanda Stesheni kisha narudi nalo Posta then nyumbani so nalipa nauli ya Mtu mzima x 2.Nilikuwa radhi nikashuke kituo cha mwisho na kutembea kuliko kile kilicho karibu na nyumbani so that nisigusane na watu.Linapokuja suala ma mahusiano na mapenzi....nafanya mengi ambayo wewe unadhani ni kinyaa but sio siku ya kwanza au miezi 2 ya mwanzo.....hii ni anaza mata kwa anaza day.Sooooo kama upo kama mie...wewe sio wa ajabu na hii sio issue ya Kisaikolojia ni kawaida kabisa.

Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Friday, 24 April 2015

Kiswahili Kigumu....spesho Post kwako!

Heyaaa.
Ahsante kwa kuichagua Blog hii.


Naona Idadi inaogezeka kila siku. Hi wa USA...How do you do wa hapa nilipo....jambo Afrika Mashariki.....Hello wengine wote popote mlipo Ughaibuni.Tambua kuwa ninathamini ugeni na ukazi wako wa muda mfupi au mrefu(unaposoma).....natumaini naweka makunyazi usoni kwako ama kwa kutabasamu au kwa kukunja sura.

Umewahi kuamishwa(na Gugo) kutoka Kiinglishi kwenda Kiswahili halafu ukashindwa kuelewa....yaani unachanganyikiwa na hujui nini kina maanisha nini?Kwasababu ninablog kwa Kiswahili mara nyingi Gugo wananijaribu kutumia Blogger kwa Kiswahili ambayo siielewi.
Mara chache nasoma Blog za Kiswahili kama vile http//www.tech255.com , www.bwaya.blogspot.com (simu haniruhusu kuweka link so yeah copy and paste uone waandikacho)na nyingine za Kuelimisha.Huko pia huwa nachanganyikiwa na kutokuelewa baadhi ya maneno ambayo nadhani ni mapya. Ila tofauti ni kuwa yapo kwenye sentensi hivyo inanirahisishia kuelewa Mwandishi alimaanisha au anamaanisha nini?Oh by the path....tumebakiza siku 14 tupige Kura....najizuia mno kuweka Siasa hapa(well hata nikizungumzia haikusaidii).....naingojea hiyo May 7 kwa hamu kuu.

Babai.

Thursday, 23 April 2015

Vita ya Vibonge(plus size) kwenye Umodo!


Uchibonge aka Undimbo aka minyama uzembe....hello! Habari ya JumaSita?

Jana nilikuwa naangalia kipindi cha Plus size War. Ambapo walizungumzia mengi kuhusiana na mwanamke kuwa mnene.


Walianza na kuwasifia Bloggers wa Fashion ambao ni wanene halafu wakaenda ni nani hasa anapaswa kuwakilisha Plus sized women kwenye Umodo wa Mavazi to changamoto za wabunifu na waendesha maduka yanayouza nguo kubwa.Ila kilichonivutia zaidi ambacho nakiunga mkono kwa sababu nilikuwa najiuliza siku nyingi. Kwanini a size 14-16 anamodo kama Plus size?Well labda ni plus kwasababu UK size ndogo ya mtu mzima inayopatikana madukani ni 6 so ukiidabo au plus unapata 12 so year mie pia ni Plus size hihihihihihi. Mungu nisamehe.Binafsi nadhani Mawakala wa Plus size wanakosea.....japokiwa kwenye Documentary hii wamejielezea kwamba Soko walilonalo na demand wapatayo sio plus size tuitakayo watu wa kawaida kwamba ni size 20 to 34 au zaidi.Wanene hawana option linapokuja suala la fashion na Trend kwasababu madukani wanatambua plus size ni kuanzia 14-18....kama ni size 20 au zaidi inakubidi uende kwenye Vibonge Speshalisti shopu.


Angalia hii ucheke au u uwe inspayadi.... https://youtu.be/My8jVUxvd7s

Halafu Gugo
Chanel4oD kisha tafuta Plus size War kama upo interested.....unaweza kipata idea ya Biashara kama ni smart enough.

Babai.

Monday, 20 April 2015

Elimisha mwanaume asibake(Rape) mwanamke....

....sio kufundisha Mwanamke jinsi ya kuzuia asibakwe!

Habari ya wewe? Nasema ahsante kwa kuichagua Blog hii.


Unategemea Nchi iliyoendelea kama UK kwamba huwezi kusikia suala la kuelimisha Wanaume kuhusu Ngono ili wasibake Wanawake via Media eti!


Wapo wachache walioelimika na wenye kumthamini Mwanamke na kumheshimu na kutomjaji kutokana na Mavazi yake. Pia Hukumu kali dhidi ya Ubakaji inasaidia kwa mbali.Lakini bado kuna Wanawake na Wanaume ambao wanadhani kuwa Mwanamke kubakwa ni Kosa lake na hivyo kufundisha Wanawake namna ya kuzuia Kubakwa as in wasivae Mavazi yanayovutia Wanawame n.k.


Mwanamke Habaki.....sasa kwanini yeye awe responsible kuji-limit kwa ajili ya Mwanaume?


Kwanini Mwanaume asifunzwe kuji-control na kutomuona Mwanamke kama object ya kumalizia haja zake za Kimwili?Kanini Mwanaume asifunzwe kuwa ili kufurahia Tendo ni lazima au ni vema upande wa pili ukubali kutoa ushirikiano na sio kulazimishwa?


Kwanini Mwanaume asionywe kuwa Kubaka ni Kosa? (Natambua wapo wanaosingiziwa na wapo wanawake wanaobaka Watoto ni issue inayojitegemea siku ingine).Kwanini kwenye kila Jambo baya linalomtokea Mwanamke kwenye Maisha yake hasa ya kimahusiano na Ngono ni kosa lake....(well isipokuwa Mimba, ni kosa lako sababu ni wewe ndio unaruhusu mtu akuwekee mananilihu yake).


Kwanini baadhi ya wanawake wanapend kuwatetea wanaume kwenye suala la Kubaka sababu ya aina fulani ya Mavazi ya Mwanamke?Usilete suala la "sio Asili yetu....Utamaduni wetu" kwa wewe unaenisoma kutoka Pande za Afrika(Wasomaji wangu wanatoka Kenya...Burundi...Rwanda)....Mavazi ya aina zote sio Utamaduni wala Asili yetu.....tuliletewa kama tulivyoletewa Imani za Dini.Sisi zetu zilikuwa ni Majani na Magome ya Miti....Vibwaya ambavyo vilikuwa vifupi.....na vijikamba ili kushikilia Jani la mbele lisianguke na kuonyesha Nyeti.Mzungu(well na Mchina) huyo huyo ameamua kuboresha mavazi ya Asili yetu na sasa tunavalia "flori" sketi ambazo zimechanua na  zina-move kama vibwaya.....nisizisahau Thongs ambazo ni kama vila walizovaa mabibi zetu miaka 9000 iliyopita (sina uhakika na namba hizo hihihihi but you get the idea).Fundisheni Wanaume namna ya kuheshimu wanawake na chochote ambacho mwanamke anaamua kufanya juu ya Mwili wake....ni mwili wake hivyo anahaki na Mamlaka yakufanya chochote atakacho.Mwanaume huna Mamlaka juu ya mwili wa Mwanamke.....unless ni mkeo in which nae pia atakuwa na Mamlaka juu ya mwili wako  kama Mumewe.

Babai.

Sunday, 19 April 2015

Pale Gugo inapokuomba kutunza kila kitu chako...


Kuanzia Picha, Emails, Work Docs na bila kusahau details za kubanki Online.

Habari ya J'pili na ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Kwa ubize wa maisha hakika utamshukuru Gugo kwa kukurahisishia......na yeye anakuukiza unataka nikumbuke pin au password yako fo yo konviniensi....na wewe unabonyeza Ok kwa hiyari kabisa.Tena inakuambia pia ni rahisi kufanya manunuzi online ukiseti Gugo loko(mahali ulipo)......na wewe unakenua na kukubali settings hehehehehe you are done Mwananchi.


Baada ya miaka kupita utaanza kulalamika kwanini unaibiwa pesa au kwanini kila mtu anajua unapoishi.Ikitokea umefanya Jinai ndio utaijua Google na vitongoji vyake....siku itokee unautaka Ubunge sijui Uwaziri watu wanavuta Gugo na kupata kila kitu.Aiii nafurahia urahisi wa ku-shop online na kujua nini kinapatikana wapi lakini hayo mengine natunza na kukumbuka mwenyewe. Asante nashukuru Google.Well wanajua kila kitu cha yeyote anaewatumia isipokuwa hawawezi kuweka wazi details zako zipatikane kwa sababu hujawaruhusu kwa kusema Ok kwenye ombi lao.Lakini "mtu" akiziomba ili kusaudia Uchunguzi Kisheria wanazitoa bila idhini yako......scary stuff.

Babai.

Friday, 17 April 2015

Faida ya kumchukia mtu usiemjua....

Ni nini hasa?

Unajua kuna watu maisha yao ni ya huzuni sana bila wao kujijua. Anakaa kabisa na kutulia kisha anaanza kurusha maneno makali. Unawezaje kum-attack mtu kwa matusi wakati humjui?


Hupendi anachokiandika au kukisema fair enough....sasa kitu gani kinakupeleka kwenye Ukurasa wake wa FB au Twitter au Blog na Sites?


Binafsi kama sipendezwi na Blog fulani basi sitoitembelea tena.....muda wa kuendelea kufuatilia anachokiandika ambacho mimi sikipendi sina.


Heri nitumie muda huo kupeleka Wanangu Park wakacheze au nikoshe nywele zangu au kutengeneza Kucha au kwenda kufanya manunuzi at the end nifurahi moyoni......there are so much more in life than being a Troll.


Unakosa usingizi ukifikiria nini cha kwenda kumuambia mtu in an attack way kwenye Site au Page yake.....unapata faida gani?


Mimi Dinah kuacha kublog Dinahicious is nothing to do with January Makamba au mabadiliko ya Sheria Tz ni uamuzi binafsi.Ngoja nikusaidie kuelewa: Google walipokuja na mabadiliko ya Sheria Mwezi wa Kwanza nikapata nguvu as in excuse ya kuachana na Blog bila lawama za Wapenzi wa Blog husika.Google imeifanya Dunia kuwa Kijiji (biggest search engine)na inafanya kazi kwa karibu na Serikali zote Duniani ili ku-protect watoto dhidi ya Ngono (na masuala mengine ya Kiulinzi ofcoz)na hivyo kila Nchi kufanya iwezavyo kuzuia upatikanaji wa Ngono kirahisi via Mitandao.Baada ya Bloggers wa Ngono wa Muda mrefu kulalamikia kuwa google wanakuwa unfair....Google waka-withdraw uamuzi wao kuzifanya Blogs za Ngono kuwa private  au kuzifuts na ndio maana bado unaweza kuiona Dinahicious na Blog nyingine za Ngono isipokuwa ni lazima uingie ukiwa na miaka 18.I blog from the UK.....I don't follow Bongo's Politics for nearly 3 years  sasa hivyo I know nothing about Sheria zenu.


I thought  I should help you to know the above. I didnt really have to do that....but here we are.


Try to have peace in your heart and improve your life Mwana wa Tanzania. Remain blessed.

Babai.

Thursday, 16 April 2015

Namba ya Simu imekuwa too personal....

Heyaaa!

Unawajua wale watu wanagawa namba yako ya Simu kwa watu wengine bila idhini yako.

Tangu enzi mie nachukulia namba yangu ya simu ambayo haihusiani na "Kazi" ni personal na hakuna mtu anapaswa kuwa nayo isipokuwa wale ambao nadhani ni muhimu maishani mwangu kama sio leo basi huko baadae.

Sasa kutokana na Maendeleo ya Kitekinolojia Simu si ndio zimezidi kuwa PERSONAL kuliko namba? Halafu unashangaa kwanini watu wanaweka Passwords au PIN ku access simu zao.

Nilipopata simu yangu Mpya (kumbuka nimekuwa nyuma na  Teknolojia ya  Simu kwa Miaka 3.5)....so niliponunua ze latest simu si ndio ikanishtua.

Ile mambo ya urahisi wa kupokea na kutuma Emails mdio ikanitisha kabsaaa. Nime add Email address nikaletewa the whole thing.....kumbuka sijagusa emails via desktop kwa miaka sasa nilipoona mafolda yaliyokontaini barua za wapita njia na some picha zao dated back in 1999 to 2005 si nikapata Mini heart attack! Nikabonyeza futa daima milele.

Zaidi ya hizo kuna zile unasubiri mtu akuchokoze halafu jmkumbushie kwa ushahidi wa Email iihihihihihi cant wait. Hizi jimeziacha kwenye sever ya Yahoo.

Hakuna mtu anataka mapasti yake yaonwe na watu Kazini au mahali popote utakapoisahau Simu yako. Pia sio vema watu wajue kama jana wewe na mumeo mligombana via whassap.

So yeah hata mimi Mpinga PIN na Password ku access simu nimebadili Msimamo.......ila siziamini Pin na Password hivyo naingia simuni mwangu kwa alama za Vidole.

Babai

Jaribio.....jaribio la Picha!

Tatizo...kila nikiambatanisha Picha Post inagoma ku-publish. Nimapunguza ukubwa....nimebadilisha settings lakini Ola! 

Nimeambatanisha picha kwenye post ya jana lakini haionekani....kwenye hii pia nimeweka picha.

Heeeelp tafadhali.

Ahsante.

Wednesday, 15 April 2015

The other woman kwa Kiswahili ni Kimada?

Jana nilikuwa masoma Magazine moja hivi nikakutana na stori ya mdada Mashuhuri kiasi cha kutosha Uingereza.


Alikuwa akizungumzia suala la kuwa Kimada ukitumaini au kuomba kama sio kusubiri Mwanaume unaemuiba amuache mkewe na watoto wake ili mwanaume huyo awe na wewe full time.Akaongeza....Mume wa mtu alipomtokea kabla hajajua kuwa ni mume wa mtu alimkubali then Jamaa akamwambia ameachana na Mkewe na Talaka itachukua muda  kiasi hivyo sio mbaya kama wakilianzisha.Mkimama akagoma na kumwambia watatoka soon baada ya Talaka kukamilishwa kwasababu hataki kuwa sababu ya kuharibu Maisha ya Mkewe na Watoto wake.Akagusia kwa kusema....wanaume  Wazinzi huanza kukuvuta kingono via mitandao ya kijamii na kuomba uwaambie utawafanyia nini ikiwa utapata nafasi ya kuwa nao.Kisha huenda na kuponda maisha yao ya kingono na Wake zao kwako.....halafu wakiona upo interested wanaongeza "i wish my wife angekuwa open minded kama wewe"(wakati uliyomwambia ni masuala ya kawaida tu ambayo kila mwanamke anayafanya.).Umeingia mtegoni ukidhani mjamaa kafika kwako kwani utampa mambo ADIMUUU. Siku ya siku inafika anakuambia "hatuhitaji Condom....nitatolea nje"....unakubali mara kabuumu Mwanaharamu katunga hihihihi samahani Kiswahili kitamu bana na hakina huruma....love child? No ya wazungu waachie Wazungu thank you....ni MWANAHARAMU.


Miaka mitatu imepita yule Jamaa bado yupo na Mkewe na wameongeza Mtoto wa tatu kwenye familia yao.Nikamkumbuka Binti mmoja aliomba ushauri kwangu ili nimsaidie arudiane na Mpenzi wake ambae ni Mume wa mtu kwani anampenda sana Mume huyo wa mwenzie na hajawahi kumtenda wala kuingilia Ndoa yake.


Got it? Mpenzi wake ni Mume wa mtu lakini hajawahi kuingilia Ndoa yake.

Babai.

Monday, 13 April 2015

Sio wote Ughaibuni tulifika kwa Ndege....

Mabaharia.....I see ya!

Mambo vipi lakini(i sound like a male)? Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Ujue huku nje ya Tanzania kila mtu anauchungu wa maisha kivyake kutokana na sababu zilizomleta....sio mnatujaji kwa kutujumuisha bana.Kuna wale walikuja kuongeza Elimu ili wakirudi waitumie ilimu yao ya kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi yao Tukufu Tanzania.


Halafu wapo waliochukia maisha yao yalivyokuwa Bongo na kwa hasira kutaka kwenda kujaribu au kuanza upya huko kwingine.....hawa kurudi sio chee(as in rahisi).Wengine walipelekwa na Wazazi wao baada ya kuanza tabia mbaya na zenye kutia aibu Wadhifu....sasa ili Wazazi waendelee ku-keep Status.....er ya Uchungaji wa Kanisa, Ukuu wa Jeshi au Uwaziri n.k so unapelekwa Nje ukafanye Umalaya wako kwa nafasi.Pia kuna akina sie tulioletwa huku kama Mtaji au Urithi.....kwamba Wazazi wanatumia Akiba ya familia ili ukasome na ukimaliza na kuanza kazi ama ulipe Deni na Riba au uwasaidie Nduguzo ambao technically umetumia Mgao wao wa Urithi ili upate Elimu ya Nje.Nisiwasahau wale walioamua kuingia Mtini baada ya Kualikwa kwa ajili ya Sherehe au walikuja kimichezo mfano Michezo ya Jumuiya ya Madola na wale waliowafuata wake au waume au wapenzi wao.Halafu kuna Mabaharia.....hawa bana wamefika Uingereza kwa mfano....kwa kutumia Boti sijui Mtumbwi,Basi au Treni....kivipi? Piga mahesabu mwenyewe.Wote tunaishi Ughaibuni lakini hasira za Maisha na bidii ya utafutaji ni tofauti sana.


Babai.

Come to terms with your Uchibonge....

Hello!

Naweka viraka mbinguni ujue(mekuwa busy namna hiyo).


Mwisho wa wiki nilipata wasaa wa kupekua pekuwa YouTube na huko nikakutana na "how to gain weight".....nikabofya na kuanza kusikiliza hadithi moja baada ya nyingine kuhusu Wanawake wanaotaka sana kunenepa.


Unajua unapomsikiliza mtu au kusoma hadithi yake na kuhisi kuwa anakysemea au kukuwakilisha wewe? Yaani anakugusa kumtima.Nikakumbuka jinsi nilivyokuwa Chikonda (skinny)enzi zile nakua(nimeacha kukua nilipofikisha miaka 25 nadhani).Story Time: Nilikuwa mwembamba kiasi kwamba baadhi ya watu walidhani nina Ugonjwa. Mmoja wa Binamu zangu alikuwa akiniambia "mtu mwenyewe maiti wewe.....umebaki mifupa tu".Nilipofika late teen baadhi ya watu Familiani wakawa wanasema ninatoa mimba sana wakati sikuwa namjua mwanaume sasa sijui Mimba ziliingia kwa Roho mtakatifu!


Wengine walisema naiga Uingilishi figa na hivyo kutumia madawa ya kujikondesha.Nilichoka kusakamwa kwa uchikonda wangu ambao sikuuomba. Nikaanza kunywa Uji wa Ulezi na kula Mayai na kunywa Maziwa kila leo. Kaka yangu akanifundisha mazoezi ya kukuza misuli ili nionekane mnene so nikaanza mazoezi ya kienyeji (kuchutama ili miguu na mapaja  yanenepe, kunyanyua Nondo za 5kg ili ninenepe aka jazia mikono).Matokeo yake nikawa nanenepa sehemu ya chini kwa nyuma pale kati ya mwili.....so nikawa naonekana mwembamaaa halafu  nimebinuka aka chikonda mwenye tako lililojitokeza.....kikaambiwa naTigoliwa.....Wanadamu bwana daaaah!


Ikafikia mahali nikakubali tu kuwa mimi ni mwembamba so nikawa nafanya mazoezi kwa ajili ya kiafya na sio kunenepa tena.


Nikaambiwa nikizaa nitanenepa na kweli nilinenepa in which sikupenda Unene ule kwasababu sikuzoea kuwa Mnene so nikajitahidi na kurudia size yangu ya awali mara tu baada ya kujifungua.


Baada ya mtoto wa pili naona mwili hautaki kurudi pale 8-10.....nimefanya yote sahihi kwa Miaka miwili ili nirudie size yangu lakini wapi.


Sasa nimekubali AGAIN kuwa mimi ni chibonge sio kiviiile bali size 10-12. Will try and keep this sitaki kurudi size 14....*Size zote ni za UK.


Mimi mkimama wa kawaida (sio Celeb) nilitaka kupungua kwa sababu sikuzoea kuwa "mkubwa" sio kwasababu nilitaka niwe kama one of the Celebs.


Pamoja na kusema hivyo ni vema kuzoezeka na kula kwa juzingatia afya....sio kula makorokocho na Chips.

Babai.

Tuesday, 7 April 2015

Wale akina bila "mimi" usingekuwa hapo!

Unawajua?
Kwanza haujambo? Anhsante sana kwa kuichagua Blog hii.Kwa sie wa Ughaibuni (tuishio nje ya Tanzania)au wale tulioitwa Mjini kusoma au kufanya Kazi pia sisi wa Mtaani tuliamua kujaribu Fani na tukaipatia na tumefanikiwa kimtindo ndio huwa tunabeba hili limzigo.
Sawa pengine bila wewe kweli asingekuwa hapo lakini ulifanyanini hasa kwenye mafanikio yake aliyonayo hivi sasa......zaidi ya kuwa njia tu ya yeye kufika hapo na actually ukajaribu kuharibu bila mafanikio?
Kwa kawaida sisi wa Ughaibuni tukikaa sawa huwa tunapenda kusaidia wengine waje kujaribu maisha huku.
Wanafikia kwako na unawasaidia kutafuta Kazi  na baada ya hapo nauli kwa miezi kadhaa halafu wanaanza kujitegemea.
Kutokana na Ughali wa Maisha Ughaibuni well UK + "kikacha" unapaswa kuchangia sehemu ya Bills.....hakuna cha bure na hakuna "nakaa kwa Anti hapa" lipa bill dadaaa au nakutimua.....hapa sio Tanzania.
Anyway.....maisha yanakuwa magumu kwa upande wako so unaongeza bidii kwenye kusoma na kufanya kazi 3 ili uweze kumudu Ada ya Chuo cha Uhakika(sio kile cha Kinaijeria alichokuombea  Dada yako) £12,000 kwa mwaka sio lelemama.....unajigawa vipi.....utajijua mwenyewe.
Mpaka hapo aliekuleta hana mchango kwenye kuhama Chuo wala Ada bali wewe mwenyewe.....isitoshe kaisha kufukuza kwake na amegoma kukupa Udhamini (wa Maandishi) baada ya kuona umekuwa "kitisho" kwamba unampiku (ujanja wa kusaka mahela)......
.......wenye Nchi nao wanagoma kukuongozea Kibali kwasababu "Mdhamini" aliekuleta amegoma kukudhamini kwa Maandishi ili uendelee kusoma na hivyo kulazimika kurudi kwenu Tanzania. Na huu ndio mwisho wa "bila mimi usingekuwa hapo" kwani techically umerudi Bongo.

Haya.....unapiga mahesabu urudi kwenu mahesabu hayaleti Jawabu. Umebakiza Mwaka uvute Degirii ya Muingereza halafu upate replacement ambayo itakusaidia kupata ajira ya Kudumu(ukifanya vema).

Unachukua Risk na unabaki Nchini kwa watu bila Kibali ili umalizie Masomo.....unaishi kwa hofu na wasiwasi. Kila ukiona au kukutana na Askari unahisi wanajua huna Karatasi....mtu akibisha hodi unakimbilia auvunguni......ukiona mtu kaja kazini na amevaa kiofisa unaenda jificha Chooni....basi ni karaa tu.

Mungu anabariki unapata replacement baada ya Muda unamaliza Shule halafu KABOOM Kampuni uliyofanya nayo replacement inakudhamini na kukuombea Kibali kama Mfanya kazi wao.

Siku unarudi Tanzania baada ya miaka Tano. Hakuna anaejua uliyopitia huko utokako na kwanini hukutudi likizo.....wanakupa siku tatu uzoee halafu kila mtu anakuja na tatizo lake.....wanakuona Mkombozi....usipotoa msada kwa kiwango watakacho basi unakumbushwa "bila nanilihu usingekuwa hapo".Najua nimekugusa au nimekusaidia uelewe upande wa pili wa Hadithi ya "bila mimi usingekuwa hapo"......

Babai.

Friday, 3 April 2015

Kumfulia nguo sio wajibu ni msaada.

Heri ya Ijumaa!

Najua umewahi kukutana au kusikia watu wakisema wanataka kufunga ndoa ili wapate watu wa kuwafulia nguo na kuwapikia er futari?


Pia umewahi kuona wanaume wakimsifia mwanamke kwasababu akienda kwake lazima atamfulia nguo na hivyo mwanamke huyo anafaa kuwa mke au bado?Unakuta mtu anakasirika kabisa kwasababu nguo zake hazijafuliwa na kunyooshwa tayari kwa ajili yake akidhani kuwa hiyo shughuli ni wajibu au kazi ya Mpenzi wake(wanasahau kuwa kuna Dobi kila Mtaa).Kwa wale wanaofanya kazi nyumbani(mama wa nyumbani) kazi zao ni nyingi kuliko kazi yako nje ya nyumbani hivyo anapokufulia nguo ni msaada.....kwamba anakusaidia so usizoee ukadhani kuwa ni wajibu wake kukufuli.Kunyoosha Nguo aka kupiga Pasi huku Ughaibuni inachukuliwa kama kazi ngumu kwamba inaweka presha kwenye Miguu na uti wa Mgogo sasa imagine mkimama anaefua(kwa kuinamisha mgogo pia).....!Nina sifa nyingi kama mwanamke kwenye "shughuli" za nyumbani lakini sifa kuu ni kunyoosha Mashati na Suruali.....Mzee wangu alisaidia sana kwenye hili kila J'2 lazma aniite na kunionyesha namna ya kunyoosha nguo zake.Pia alikuwa anapenda mimi nimpikie Dagaa wale wa Kigoma na Ugali....nimeanza kupika nikiwa na Miaka 8 hivi. Wachana na hili......Stori taimu: Enzi nimeanza kutoka na Asali wa Moyo nilianza tabia ya mbaya ya kumfulia na kumnyooshea nguo (nilipogundua kuwa ni keeper bana angekuwa mpita njia wala nisingefua) na alikuwa way too busy na kazi so ili asipoteze muda kwenye usafi wa nguo na hivyo nipate muda nae nikawa namsaidia.
Basi siku moja tunaongea Simuni akanambia kuwa kanikumbuka kweli (nyumbani kwake)na alichokikumbuka zaidi ni mimi kumfulia Nguo.....aiiiii si ndio ukawa mwisho wa mimi kumfulia.Umenona hata wa Ughaihuni wenye Mashine za kufulia bado wanaona kufua nguo ni Kazi ngumu.Kuna tofauti kubwa sana kati ya Msaada na Wajibu au Kazi ni Msaada.

Babai.