Skip to main content

Posts

Showing posts from 2022

Namna ya Kumshukuru Mumeo bila kusema "Ahsante".

Ukiachilia mbali(naipenda hii msemo) kuwa Ahsante ni "common" kitu ambacho kinaondoa uzito na maana yake, pia neno hilo ni rahisi na kila mtu anaweza kuambiwa bila kumaanisha. Mumeo sio mmoja ya hao watu, Mumeo ana umuhimu na uzito tofauti na watu wengine wote Maishani mwako(ukute ni mimi tu ndio nahisi hivyo).   Sasa kuanzia leo acha kukimbilia Ahsante kwenye kila jambo analokufanyia kama Mkewe na mlezi wa Familia(watoto wenu) yake.  Moja, Wakati mwingine mpikie/andalie chakula/kinywaji anachokipenda. Mpokee kama vile wanao wanavyompokea(bila kusema babaaa)....hiyo Pili. Shikamaneni hivi ktk Ndoa. Tatu, akikuudhi au ukiudhika na mambo mengine(unakaribia Hedhi) usimfanye alipe, hasa pale anapofika Nyumbani kutoka Kazini. Jaribu kumjulia hali, kumuacha apumzike na kisha ongea nae vizuri na kwa upendo/heshima. Nne, Ilinde Ndoa yenu pale ambapo mambo yqmegona kuendi vema, mfano Kapoteza Kazi/Tenda/Biashara imabuma, badala ya kumpa Moyo, Matumaini na Ushirikiano....we...

Kwaheri Social Media(Twita)...

...hivi YouTube inahesabika kama Sosho Midia?  Kama sio basi Platform pekee naiaga kwa sasa ni Twitter. Sijawahi "kujiunga" na Instagram, Snapchat wala Tiktok. Kwanini? Ukiachilia mbali kuwa Muda unabadilisha watu(wanakua), vilevile vitu na mitazamo hubadilika kulingana na Tabia Uchumi/Nchi/Utamaduni....nadhani Twita imejaa wafanya Biashara kwa kupitia Ajenda binafsi/Harakati, Biashara ndogo ndogo na Biashara Utapeli (ulipie waliojifunza YouTube  bure), Biashara ya Miili(intimate picha/vid) oh bila kusahau Biashara ya "kuomba omba". Baada ya miaka kadhaa, nimegundua kuwa Twita hainifaidishi kwasababu sina Biashara(sikuzi Brand), hivyo sihitaji kuwa active na ku-engage na followers every few hours on daily. Kabla ya hapo nilikuwa Active sana kwenye Masuala ya Kisiasa(Naunga Mkono Upinzani Tz), baada ya Muda nikajitoa, uamuzi uliopelekea  "kurukia" zaidi issues rahisi rahisi ambazo zimejaa chuki/vita ya Wanawake vs Wanaume, hasira, kutokujiamini,...

Kama Mke, Umejitosheleza?

Kila Mwanamke ni Imara hiyo inajilikana na wala huitaji kujitanganza(kuwa chini ya Kundi fulani kuthibitisha hilo), pamoja nakusema hivyo  wewe kama Mke bado ni Dhaifu/laini(Kimwili) na hakuna kosa mkimama kuwa mlaini(jivunie  udhaifu wako). Kazi yako kubwa Duniani ni kuwa msaidizi wa Mumeo, kuleta uhai(kubeba Mimba na Kuzaa), kulea, kufundisha na kutunza Familia. Ili uweze kufanya hayo(niliyoyatajabhapo juu) unatakiwa kuwa  umejitolesha kwenye nyanja nyingine ili kurahisisha Maisha yako kama Wewe, Mama na Mke. Unapaswa kuwa na uwezo  wa kufanya baadhi ya vitu haraka na kwa ukamilifu bila uwepo wa mtu wa pili iwe Mumeo au Muuza Huduma. Je ni nyanja gani hizo? Dharura; Unaweza kujituliza, kutafakari kwa haraka na kufanya uamuzi kwa faida yako na familia badala ya kusubiri mpaka Mumeo apokee Simu/arudi. Uchumi; kuwa na Akiba ya Senti kwa mahitaji madogo madogo(ya ghafla) nje ya Bajeti ya Familia(kutoka kwenye zile anazokupa Mumeo), sio kila akikupa Pesa u...

Dayaspora na Uraia Pacha...

Natumai unamalizia vema Mwezi huu wa 3(na Dayaspora). Suala la Uraia pacha ni zuri sana na lina faida nyingi kwa pande zote Mbili za Watanzania(Ndani na Nje), na Taifa lenyewe kwa ujumla(hasa kwenye Michezo Kimataifa, Uchumi, Afya na Elimu). Uwekezaji? Sio sana kwasababu kama Mtanzania utataka "kupendelewa" au "kupunguziwa" Masharti kutokana na Uraia wa Taifa hilo la Uzawa wako na hivyo Serikali kupoteza Mapato(Visa ya Uwekezaji na gharama nyingine) kutoka kwa Wawekezaji wa Kigeni.  Dayaspora wengi wanadhani kuwa Serikali inakwepa suala la Uraia Pacha kwa sababu ya Wivu, Chuki au Uoga wa "kupitwa" Kimapato, Ujuzi na Uzoefu. Kwaharaka haraka(uvivu wa kufikiri) inawezekana kweli ni Roho ya "kwanini wao", lakini ukiamua kutulia na kwenda ndani, utagundua kuwa  Taifa(Serikali) itapa Hasara zaidi kuliko mnavyorembesha Faida za Uraia Pacha. Hasara za Uraia Pacha zipo nyingi ila mie ninazo Nne tu. Tangu kupata Uraia wa Tanzania ni rahisi(kwa sababu ya M...

Dayaspora vs Wazawa "groundini"...

Enzi Watqnzania "waishio" Twita walikuwa wakiwasimanga Diaspora kwa kujifanya wanajua kila kitu, mie nikaandika hii  kaisome tafadhali. Imekua kawaida kwa Wabongo wa Tz na wale wa Nje ya Tz kupishana mara kwa mara, huenda ni kwa Utani uliojificha kwenye yalioujaa Moyo ambayo ni ukweli au kuchangamsha Genge. Kuna wakati huwa naona "point" ya wale wa Bongo kuachwa wajadili na kuishi naisha yao na Siasa zao, lakini wakati huo huo naelewa kwanini Dayaspora wanapata hitaji la kutaka kutoa maoni/mawazo yao kuhusu Bongo kwasababu (wana Miradi, Ndugu na Jamaa...ni Kwao pia) wanaguswa kama unavyoguswa wewe. Kitu kingine ambacho Wabongo wa "Graundini" wanapaswa kujua au kujifunza kukubali kuwa,  "Dayaspora" wana-options tofauti kulingana na Muda gani ameishi huko aliko. Mtaani, Chuoni na Kazini yupo na watu wale wale wanaongea masuala tofauti kuhusu Nchi tofauti ambayo katika hali halisi ha-relate(inategemea kaishi huko nuda gani). Akija Mtandaoni anakutan...

"Dayaspora" na Kuzikwa "Nyumbani"...

Mtu aliehamia Nchi nyingine kwa Kupenda(uamuzi wake binafsi) nae ni "Diaspora" au ni  "Migrant" au yote mawili kwa pamoja? kwasababu tunatumia neno "dayaspora" wacha niende nalo ili kurahisi mambo. Wewe umeishi zaidi ya miaka 10 nje ya Tanzania, umejenga Marafiki(ndugu) wapya, umeanzisha Familia(ambayo haina uzoefu na Nyumbani kwa Wazazi/Mzazi mmoja) na kuwekeza kwenye "Property(ies)" na Biashara nyingine.  Lakini ukifariki "watu" wanalazimisha uzikwe kwenu(sio kwako kwenye Familia uliyotengeneza ambako ndiko ulikofia) na Marafiki wa Ukubwani. Sio tu ni ubinafsi wa Jamii hiyo "nyumbani" bali pia ni kujipa Majukumu na Gharama ambazo sio zao(hata kama wanachangisha) bila kusahau kuwanyima Watoto na Mkeo/Mmeo Haki ya kutembelea Kaburi lako wanapohitaji kufanya hivyo. Familia yako kutumia Milioni kadhaa kuja "Nyumbani" kila mara wanapotaka kuongea na Mzazi/Mwenza wao ulielala Kaburini ni ghali. Ukiachilia hil...

Jinsi ya kuheshimu Mkeo...

 Kwa kawaida huwezi kutana na Wanawake(Mkeo) akidai kuheshimiwa mpaka labda Mume utoke nje ya Ndoa ambapo uwezekano wa yeye kubaki Ndoani huwa ni  0.01%(that's me)....Hiyo haina maana kuwa Mkeo haitaji Heshima. Jaribu yafautayo kudhihilisha kuwa unaheshimu mkeo vile anavyo/utakavyo akueshimu wewe. Usimuudhi/Umize: Msome Mkeo ili ujue nini anapenda/hapendi Uwanjani na nje ya Uwanja na ujitahidi kutekeleza/kuacha vitu hivyo. Usimfokee/Karipia: Mkeo sio Mwanao/Mdogo wako bali ni mtu mzima mwenzio hata kama umemzidi miaka kadhaa, ongea nae kwa adabu kama Mwenza wako na sio mtu alie chini yako. Msikilize: Pamoja na kua wewe ni Kichwa na Kiongozi wa Familia haina maana kuwa Mkeo hana Sauti humo ndani.  Mkeo ni Mwanadamu na m-treat kama mwanadamu mwenzio ila  sio kwa Usawa (kama Mwanaume mwenzio) na sio kwa kiwango cha chini kama vile hana thamani ya Utu. Usilazimishe Itikadi(mf Ushirikina, Imani, Siasa n.k):   Usijione kuwa wewe  ndio mwenye ku...

Amina wa Ali Kiba adai Talaka Mahakamani na Kiba(2)....

Soma Mosi na Pili hapa .... Tatu, Mtoto anamuhitaji Mama yake full time kwa Miaka 5 ya mwanzo ya Maisha yake baada ya hapo PT sio mbaya. Malezi ni Kazi  kama kazi nyingine na inachosha Akili na Mwili, tofauti ni kwamba hakuna Likizo na huwezi kuacha/badilisha na pia kwa  Tz Mke (Mama wa Mtoto) huwa halipwi na hiyo inafanya kuwa "Kazi" hiyo kuonekana kuwa ni rahisi. Mkeo anapoamua au mnapokubaliana kuwa yeye abaki Nyumbani kulea watoto ni jambo zuri na la kuheshimika kwa Ulimwengu wa sasa. Mkeo akigoma kufanya Kazi ya Kulea na kuamua kwenda kufanya kazi/biashara nje ya nyumbani ni wazi kuwa mtahitaji "Mlezi" wa watoto wenu wa hapo nyumbani na yule wa "shule", na atalipwa kwa "rate" nzuri tu kulingana na Kipato/aina ya Maisha mnayoendesha. Wengi kwenye Mitandao wamelichukulia suala la Amina na Kiba kwa kuangalia Kona ya maisha waliyonayo wao kwa sasa, na sio Maisha ya Star Mkubwa mwenye Thamani ya Dollar  Millioni 5(11,570,000,000). Pi...

Talaka ya Amina kwa Ali Kiba...

Mimi na wewe hatujui kwa Undani ni kitu gani hasa kilichopelekea wawili hao kufunga Ndoa 2018. Lakini kutokana na Maelezo ya Amina kwenye Hati ya Madai tunajua kuwa Kiba alikuwa Mtesi/Mnyanyasaji kwa Mkewe (Kiakili, Kimwili, na Kisaikolojia)baada ya Miezi 6 ya Ndoa. Kwa maelezo hayo inaonyesha kuwa Amina hakuwa "kipenzi" cha Familia ya Mumewe na hivyo kuhisi kuwa mahali walipo watu hao sio Salama kwake na kwa Watoto na hivyo kurudi kwao Mombasa*. Pia Amina ameongeza kuwa Mumewe(Kiba)ni Muasherati na hakuiheshimu yeye(Amina) wala Ndoa yao(alimdhalili adharani). Amina amedai kiasi cha Laki mbili kwa mwezi(Ksh) kwa ajili ya Matunzo yake na watoto. Madai ambayo yamesababisha Watanzania wa Twita kuhoji... Tu(na)jigunza nini kwenye tukio hilo. Moja, Kwa Msanii mkubwa kama Ali Kiba ambae ana Thamani ya Dollar Millioni 5(568,500,000Ksh) Laki mbili kwa mwezi kwa mahitaji ya Mtoto sio pesa nyingi, pengine haitoshi tukiongeza Ulinzi, Usafiri na Bima ya Afya.  Unalipa Matunzo...

Hebu tuone Past life yako: Kuachwa/Telekezwa(2)...

Jambo, ni furaha iliyoje kukutana nawe na ahsante kws kuwa nami leo. Naendelea kukumbusha Maisha uliyopitia ulipokua angali mtoto ili kuona jinsi gani yana athiri Maisha yako hasa kwenye Mahusiano na watu wengine. Kuachwa ni jambo ambalo limezoeleka sana kwenye Jamii(hata za Ulaya ya hapa), kwamba utaachwa, utalia weeee kisha utanyamaza halafu Mzazi akirudi hautokumbuka tena(asiporudi tena baada ya miezi 2? Miaka 3?). Imani hiyo hufanya Wazazi wengi kufanya maamuzi yanayo umiza mtoto(hukumbuka ila hawajui ku-express hisia zao) bila kujua(kwa sababu hata wao walifanyiwa hivyo na they turned out just fine hivyo its okay). Kuachwa/Telekezwa na Mzazi kunafananaje? Mama ambae anamnyima mtoto Nyoyo kwasababu nyingine hana tofauti na Baba ambae hajihusishi (hayupo)kwenye maisha ya mtoto.  Mzazi aliefariki wakati kabla  hujazaliwa/angali ukiwa Mdogo....athari ni zilezile. Na je ni Matendo gani yanaashiria kuwa uliachwa/telekezwa na Mama/Baba na umeathiri? 1-Unapenda "attentuon" na ku...

Hebu tuone Past life yako: Kutelekezwa/Achwa...

Umekuwa na mama yako kwa Miezi 9 mpaka 11 kama ulikuwa na bahati, wengine ni miezi 6 na wengine karibu Mwaka(Miezi 12). Ni mtu pekee unaemfahamu, na unahisi kuwa upo salama na unapendwa, sababu Mtu huyu sio tu amehatarisha maisha yake ili kukubeba na kukuleta Duniani. Mtu huyu ataendelea "kuteseka" sababu unataka ule x4 usiku wa manane, ataendelea kukupenda, kukulinda, kukufunza na kukujali.  Hayo yote hutokea kwa Miezi 3 ya mwanzo, baada ya hapo unamuona mtu huyo Nusu siku, kila unapoachwa unalia sana. Siku zinavyozidi kwenda ukaribu wako na mtu huyo unapungua na kilio chako kinapungua. Kitendo cha Mtu huyo ambae sasa unamtambua kama Mama(au Anty, Dada wa Kazi ndio Mama yako) kukutelekeza/kukuacha huwa kinaumiza sana. Sasa umekua na unajitegemea kwenye mambo mengi kama vile kucheza peke yako, kujivisha viatu/nguo nk. Lakini bado ni Mtoto na bado unamuhitaji Mama yako. Jana la leo Mama amekua nyumbani siku zima, unahisi furaha, upendo na kujaaliwa.....Mama anaamua kutaka kuto...

Heri kwa Mwaka 2022, hebu tuone Past life yako...

Ni kawaida kuamini kuwa ulipigwa, tishwa, telekezwa/achwa kwa masaa kadhaa au miaka na Mama/Baba na umekua vema tu, huna shida yeyote Kisaikolojia/Kimwili/Kihisia. Unaendelea kuwapenda Wazazi wako despite the mateso walikupatia ilipokuwa kichanga, Mdogo na Kijana. Unaamini kuwa walichokifanya wazazi wako ndio kimesaidia kukufanya wewe uwe hivyo ulivyo sasa. Hakika bila wazazi wako kukulea walivyokulea usingekuwa hivi ulivyo ambavyo wewe unadhani ni "kawaida". Kukubali kuwa uliteswa/na kutengwa(rejea kipengele cha kwanza) na kuwa malezo hayo yamefabya uwe ulivyo sasa lakini una kutaa kuwa huna tatizo, tayari ni tatizo.  Nikukumbushe....Kupigwa, Kutelekezwa/achwa na kutishwa kwa awamu tofauti. Kupigwa : Ikiwa Mama/Baba kukupa maumivu ya mwili ambayo uliyachukia na kuogopa kwanini unatumia mbinu hiyo hiyo kuumiza mtoto wako? Mtoto anapofanya kosa(bado anajifunza), kwanini huchukui hatua na kumfunza/elewesha na kisha kumpa adhabu kulingana na umli wake ambayo sio kipigo.  Kwanini...