Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2014

Dave na Jamaly

Hawa walikuwa "my best friends" wangu yaani walifanya lolote kwa ajili yangu....baadhi ya watu walidhani jamaa walikuwa wapenzi wangu. Naelewana vema na Wanaume kuliko Wanawake, naturally, wanawake hawanipendi (I think like man most of the time) hihihihihi natania, I just don't click kirahisi na watu wa jinsia yangu. Jamaly nilisoma nae Msingi na wote tukafaulu yeye akaenda Tambaza na mie nikaenda shule moja hivi pale Mjini kati.....Bado urafiki wetu uliendelea Mpaka Chuo. Tulikuwa tunakaa Dawati Moja (yeah nilikuwa nakaa na Wavulana), tulikuwa tunapishana nafasi ya kuongoza darasa. Tulikuwa tukisoma pamoja lakini hatukuwa tukikaa pamoja kwenye Mitihani sio wajua ile kupangwa kwa herufi.....still tulikuwa tukibishana ni maswali gani yatatoka kwenye Mtihani usika. Urafiki na Dave ulianza Kidato cha Pili, na ukaendelea Mpaka naondoka Tanzania karibu miaka 17 iliyopita. Tulikuwa tukisoma pamoja kila tunapotarajia Mitihani japoku

Addicted to Dini....

Jiadhari, inaua! Wataalamu wanaamini kuwa kila Mwanadamu anaumwa Akili(anaugonjwa fulani wa Akili) na huwa triggered na aina ya Maisha anayoishi mhusika. Sasa kuna wale watu wako so dedicated na Imani zao mpaka unahisi akili zao hazipo sawa....hizo mtu zipo Addicted (Dini imetriga Gonjwa la Akili). Kama zilivyo addictions nyingine Imani ya Dini inaharibu Mahusiano, Inasababisha Mfarakano kati ya familia na familia na hatimae kupoteza Maisha au kumfanya Muathirika kuishi Maisha yale yale wakati Mkuu wa Dini (Zungu) anafurahia the High life + attention ya Jamii. Nakumbuka enzi, Mtu (kwenye familia yangu) alikuwa yupo radhi kupeleke "fungu la Kumi" kanisani kila Mwezi kuliko kuwanunua watoto wake mahitaji muhimu. Ilifikia mahali anasomesha watoto wa Waumini wengine wakati Elimu ya watoto wake haieleweki. Addiction ilinoga akaamua kuacha kazi ili "afanye kazi ya Bwana"....akawa anaamka asubuhi kwenda Kanisani na kurud

Nafurahia kuwa Mama...

Lazima umeisikia hii kwa Wanawake wengi wa kileo....Mimi sifurahii kuwa Mama (way too hard) ila najivunia kuwa Mama kwa wanangu. Kuna wale wanawake ambao wakikua tu wanatamani kuwa Mama (kuzaa) yaani kuwa mama ni muhimu kwenye "list" ya mambo wayatakayo Maishani. Mimi sikuwa hivyo, yaani kuzaa haikuwemo kabisa akilini mwangu....nilijua siku moja nitazaa, lakini sikuwa na haraka au niseme urge/desire ya kuwa na Mtoto. Hata nilipojifungua Wanangu sikupata ile hisia wanazopata wanawake wote(wengi waongo hehehehe) "falling in love like never before" au "falling in love all over again"....nilijipa "hi5" in my head nikafurahi na kuwa-proud huku nikujiuliza "kapitapitaje pale"? Haina maana siwapendi Wanangu la hasha! Nawapenda sana na siwezi kuishi bila uwepo wao....hata kwa masaa machache yaani SIWEZI. Ila Mapenzi kwa wanangu hayakuhitaji mimi ku-fall in love na Mapenzi kwa Mtu baki ndio huita

Nafurahia kuwa Mama...

Lazima umeisikia hii kwa Wanawake wengi wa kileo....Mimi sifurahii kuwa Mama (way too hard) ila najivunia kuwa Mama kwa wanangu. Kuna wale wanawake ambao wakikua tu wanatamani kuwa Mama (kuzaa) yaani kuwa mama ni muhimu kwenye "list" ya mambo wayatakayo Maishani. Mimi sikuwa hivyo, yaani kuzaa haikuwemo kabisa akilini mwangu....nilijua siku moja nitazaa, lakini sikuwa na haraka au niseme urge/desire ya kuwa na Mtoto. Hata nilipojifungua Wanagu sikupata ile hisia wanazopata wanawake wote(wengi waogo hehehehe) "falling in love like never before" au "falling in love all over again"....nilijipa "hi5" in my head nikafurahi na kuwa-proud huku nikujiuliza "kapitapitaje pale"? Haina maana siwapendi Wanangu la hasha! Nawapenda sana na siwezi kuishi bila uwepo wao....hata kwa masaa machache yaani SIWEZI. Ila Mapenzi kwa wanangu hayakuhitaji mimi ku-fall in love na Mapenzi kwa Mtu baki ndio huitaji

Rafiki wa kweli...

Haitaji kuku-support kwenye kila jambo hata kama ni baya! Kama ukikosea atakuambia ukweli hata kama unauma....akiku-support kwenye kila kitu ujue ni MNAFIKI. Ndio maana Mimi sina Rafiki bali nafahamiana na watu....oh wait! Actually ninarafiki Mfamasia nilikuwa nae Chuo in olden days....labda kwavile ni Mghana so tofauti ya Kacha imefanya Urafiki Udumu. Sijui wenzangu mlilelewa vipi lakini kukosolewa ni muhimu kama kusifiwa. Ilikuwa unakosolewa kwa kinachokosoleka (ujinga/upuuzi ulioufanya) mbele ya wenzio so that usirudie tena upuuzi wako. Usiogope kuitwa "double standard" akienda ovyo mpe cheupe ajirekebishe. Babai... Mapendo tele kwako...

Kujiremba....

Kipajiiii....heri ya Alhamisi! Nilipokuwa Msichana 10-17 sikuwa najali mambo ya kujiremba....Mama hakuturuhusu kupaka Rangi ya Kucha Ijumaa kisha tuondoe J'pili jioni. Eti tulikuwa tunaharibu Rangi zake... Basi tukawa tunapaka Wino mwekundu(Pen nyekundu) au ukitaka Rangi "clear" au kucha zing'ae basi unachukua Marumaru au Vipande vya China (sahani, vikombe n.k vilivyovunjika) unasugua kwenye Sakafu ya Sementi kisha ile vumbi yake unaisugua kuchani. Nilipofikia Miaka 18 nikaanza kupaka Wanja na Lip gloss. Nimeanza kujipangusa Poda usoni, kutinda Nyusi na kupaka Mascara nilipokuwa na miaka 28....anyways! Baada ya kuwa addicted na Beauty Vlogger nikaamua kujitutumua kwenye kujiremba bana....basi siku ambayo najua sitoki nje mwenyewe napanga nitakavyo vyaa the next day na Vipodozi gani vya kujipaka....(Ninavyo kibao kwani kila Birthday napewa zawadi ya Vipodozi....watu wachokozi)! Naamka mapema, nafanya shughuli zangu za ndan

Mti/Ua Shamba....

Yenye viwango na Uchunguzi wake umefanywa kisasa.....(Wataalam wa Sayansi) sio wale wa "Maono"....The wezi. Oh! Heri ya Juma Nne....Hongera na ahsante kwa kuichagua Blog hii. Ile Nywele issue (bado ninayo) bana inanifanya nijifunze mengi kuhusiana na vitu asilia ambavyo vinamanufaa mazuri kwa mwili wa Binadamu ikiwa ni pamoja na nywele. Kunywa maji ni muhimu kwa ajili ya ngozi, nywele na kupunguza Mafuta Mwilini kwani inakuzuia kula chakula kingi/kupita kiasi.....ila ukiwa ulibeba mtu mbili Tumboni eh bwana lazima uwe mwangalifu na maji unywayo. Unakunywa "Fundo" ndogo mbili na sio kumimina robo/nusu Lita kwa wakati mmoja....unaeza pata Mimba atifisho a.k.a Kitambi....(Hata sijui kwanini nakuambia hili)! Oooh! Back to Miti shamba, ninayotaka kuizungumzia hapa ni Chai.....huyoo ulidhani mizizi na Magome? Hehehehe....Chai ya Kijani na ile ya Maua aina ya Chamomile. Come to think of it, Mizizi na Magome hutumiwa kama

Mabadiliko ya Ngozi

Naamini au niseme kuwa nadhani nina ngozi nzuri, kwamba si nyeusi na si nyeupe. Ila tatizo linakuja kwenye mabadiliko yake kutokana na Hali ya hewa inavyobadilika. Awali wakati naishi Tanzania ngozi yangu ilikuwa inachukia Mafuta Mazito, hivyo nikawa napaka mafuta ya "maji" ya asilia ambayo ni ya Nazi. Baadae nikagundua aina fulani ya "Lotion" nikawa nachanganya Mafuta ya Nazi na kupaka mwilini (usoni incl). Kipindi chote hicho sikuwa naona mabadiliko ya Rangi ya Ngozi yangu kama ninavyoiona huku Ulayani. Yaani wakati wa Baridi na kipupwe Ngozi yangu inakuwa Nyeupe (napauka)....alafu wakati wa Kiangazi naiva (Rangi inakolea).... Nikadhani labda macho yangu yanaumizwa kutokana na Mwanga wa jua wakati wa Kiangazi ndio maana najiona "nimeiva). Siku nikaenda kwa Daktari kumueleza tatizo langu hehehehehe I know(am so stupid....not really mie muoga wa Magonjwa bana)....nilidhani labda ni dalili ya Ugonjwa wa Michael Jac

1st time Mothers....

Za mida hii....? Enzi zile za Usichana(shuleni) kulikuwa na kipindi cha watoto "chuchuchu" kilikuwa kikiendeshwa na Marehemu Amina Chifupa(Pumzika kwa Amani). Alipojifungua basi kila wakati ilikuwa "nani huu hivi, nanihu vile" yaani ali-share excitement ya kuwa mama kwa mara ya kwanza. Mimi na wanafunzi wengine, tulikuwa tunakereka kweli na hiyo "mwanangu hivi, vile".....tukawa tunasema "Amina nae ka' yeye ndio wa kwanza kujifungua, Ulimbukeni tu!! Kumbe bana tulikuwa wadogo, hatukujua hisia anazozipata mwanamke baada ya kujifungua kwa mara ya kwanza. Niulize mimi nilipojifungua mara ya kwanza hehehehehe nilikera watu kwa picha na vijimaandishi vya kuwakilisha vitendo au pose yake kwenye Picha. Hakika niliwakera watu sana tu. Namkumbuka Marco Mwenda (nae ni marehemu alifariki kwa ajari ya Gari mwaka Jana, apumzike kwa Amani)....aliwahi kuniambia " Da' Dinah nawe unachosha, utadhani wewe ndio mama wa kwanza hapa Duniani"...

Kesi za Kubaka za Miaka ya 70s-80s....

Bari gani? Hizi Kesi na Hukumu zinazotolewa huku dhidi ya "vibabu" waliobaka au ku-abuse wasichana wadogo miaka 40 iliyopita zinaudhi eti! Unaeza sema "masikini vibabu vya watu vinafungwa bure kwa makosa ya miaka ile".....au ukajiuliza "hao wanawake walikuwa wapi tangu enzi zile kupeleka Mashtaka yao". Well! Huwezi kuelewa mpaka uwe umepitia huko au wewe ni mwanamke na unakuwa targeted kwasababu tu una Matiti na Uke. Sipendi kulinganisha lakini linapokuja suala la ku-abuse wanawake kingono hasa sehemu za kazi Tz, mimi ni mmoja kati ya wengi ambao tulitishiwa kufukuzwa (kunyimwa ajira ya Kudumu) kama tutakataa kujitoa kimwili. Wenzangu sijui, lakini mie na misimamo yangu nikamwambia "unikome ka' ziwa la mama yako na sina shida na Kazi yako".....nikatoka, mefika nyumbani nikaenda kumshitaki kwa Mama na Baba (hihihihi hapo nilikuwa Binti wa miaka 25). Sijui sheria ya Unyanyaswaji wa Kijinsia na Ubaka

Comments kwenye Gazeti la "kushika"

Jambo jambo? Sijasoma Gazeti la kushika kitambo kweli, asa nipo Trenini nasoma Gazeti la asubuhi, baada ya kusoma sinkawa natafuta "comments" ili nisome maoni ya watu....ikabidi nijicheke! Wiki ijayo kuna Uchaguzi wa Wawakilishi wa Ulaya, Hakuna chama kinachonifurahisha mpaka sasa. Nikieka majina ya Vyama hapa nitaanza kufuatiliwa kwa karibu na siku nikitereza tu narudishwa Kisarawe, so wacha wabaki "kapuni". Sijui umuhimu wa Umoja wa Ulaya kwangu binafsi zaidi ya kushikilia Bango Haki za Binadamu, hivyo nitapiga kura ili tubaki kwenye umoja huo kwa maana hiyo sitochagua yeyote anaetaka tutoke kwenye Umoja wa Ulaya. Siasa inagusa Maisha yangu, napenda Siasa ila nimeacha kufuatilia zile za Nyumbani kwani hunipa hasira alafu hazinifaidishi. Za huku zinaeza kukupa hasira (kama umekatiwa msaada wa senti hihihihi) lakini angalau unapewa nafasi ya kumtumia Mbunge wako kwa issues ambazo labda hazikutiliwa maanani na wajinga

Kila Kidume(secretly) hupenda kidume Maishani....

Hapana sio "Mikorosho" bali kupata/zalishiwa mtoto wa Kiume......Heri ya Wiki Mpya kwako! Umewahi kutana na wanaume ambao watoto wao wa kwanza ni wa Kike, na ukasikia wanavyotetea Binti zao na kuponda watoto wa kiume au hata kujifanya "hawajali" mtoto gani anazaliwa. Wengi hudai "Bora Binti Malaya kuliko Kidume Shoga"....ukielewa Sentesi hiyo kwa undani utagundua kuwa Msemaji hapendi watoto wa kike na kesha Muita Malaya kabla hata hajakua masikini. Hawana mtoto wa Kiume hivyo "ushoga" hausiki (hauna nguvu) hapo lakini tayari wamuita Binti Malaya....haa! Kisiri-siri wanatamani sana na pengine waliombea kupata mtoto wa kiume lakini haikuwa hivyo..... Wengine husema "Mheshimu Mkeo kwani kakuzalia kidume muendeleza jina la Ukoo" Mimi binafsi SIKUTAKA kabisa kuzaa mtoto wa Kike kama 1st born kitambo kabla hata sijajua kama ipo siku nitazaa. Nadhali ilitokana na hali ya kujisikia "safe" na kuheshimiwa (ogopwa) kwa vile nilikuwa na m

Marehemu....

Mungu aendelee kuwapa Mwanga wa Milele, Amina......hebu ngoja kwanza!! Wameenda wakiwa "wamelala" sasa mwanga wanini wakati wamelala? Ile kasumba ambayo mimi naona ni ubinafsi au kutafuta/taka kuonewa "huruma".....yaani marehebu baba blablabla....Marehemu sijui nani blablabla. Marehemu Baba wa Taifa anatuangalia na kugalauka Kaburini......yaani aache kufanya yaliyomuhimu huko aliko abaki kutuangalia sisi huku na kugalauka kutokana na ujinga au makosa na shida zetu! Sidhani kama hao marehemu huwa hata wanatuombe tulio hai tuendelee kupata "kiza" cha milele ili tusiamke na kukabiliana na shida za Dunia. Mtu akienda, ameenda na huna budi kukubali kuwa kaenda na anaendelea na maisha mengine bila wewe....dizaini ukifa unasahau all bout Dunia na watu wake.....Mambo ya new start...new life. Si wanasema unakuwa "declared dead only" kama Ubonko (Ubongo) haufanyi kazi, sasa kama Ubonko haufanyi kazi kumbukumbu za ya Duniani watazitoa wapi? (In my

Fashenista....

Za jioni? Kabinti kanakua basi sijui ni homono au au kitu gani?!! Khaaaaaaa! Hakajui kuongea basi kila kitu ni "this...this" huku kanasonta (nyooshea kidole) anachokitaka. Unamvalisha Viatu, anaenda kubeba Viatu vingine anataka umvishe juu ya vile ulivyomvisha mwanzo.....Uanamke shughuli, tena kumbe shughuli huanza mapema hivi! Aiiiii.... Ujue...kunatofauti kati ya Kupenda Fashion na Kujua Fashion. Mimi napenda sana tena sana ila sifuati sheria zake(well sizijui na sina muda), navaa ninavyotaka au kujisikia. Sasa kwavile tu napenda Fashion hainipi ruhusa au Mamlaka ya kukuambia uvae nini na wakati gani wakati vaa yangu tu inaashiria nahitaji kuambiwa ninayowaambia wengine. Tangu nimegundua Vlog ayeee nimekuwa addicted, sadly wengi wao ni 20s, which is annoying. Few days ago....oh kiswanhehee....siku chache zilizopita nikakutana na Vloggers ambao wapo 30s aiii nkajiSubie (subscribe). Sasa najifunza kuwa stylist.....natania, una

Kilugha kinakera!

Morning/Noon! Lugha za Tanzania zinaingiliana hivyo hazikeri alafu lazima utaambulia maana kwa mbali hasa kama unatetwa. Kuna Mtangazaji "Tiger beibiiii" wa Ebony ya Iringa huwa ananikosha sana akitumbukizia/nogesha kwa kilugha chake, sio Watangazaji wa Dar wamejaa "you know what I mean" "waraaaap" nyiingi....hiyo sio nukta, nimegusia tu. Lugha za Nchi hii bana ayee! Kichina, Kinigeria, Kipolishi, Kizairwaa, Kisomali, Kirusi na nyingine nyingi....zinakera sana (kwasababu sing'amui kitu). Asa ombea umepanda Basi Moja na Mnaija, Mkongo na Mchina, alafu wapigiwe simu kwa wakati mmoja....Utadhani wamekodisha basi kwa ajili yao tu. Sikuhizi nawaelewa sana Wainglishi wanapoonyesha kukerwa unapoongea Kilugha chako....(Sehemu ni wivu as hawajui lugha nyingine hihihihihi). Huwa siongei Kiswahili ninapokuwa kwenye kadamnasi ya watu ambao najua hawaelewi na kama mazungumzo ni nyeti (lazima kilugha ili wengine was

Daktari na Dawa wanazotupa....

Jambo weye? Umewahi kwenda kwa Daktari ili kuongezewa Dawa unazotumia (repeat prescription) Daktari akakubadilishia Dawa akikuambia "hii ni bora zaidi" kuliko hiyo?!!! Unahofia "side effects" lakini Daktari anakuhakikishia kuwa hakuna baya litakalotokea (niligundua kuwa dawa mpya ni Ghali zaidi kuliko ile ya awali). Jana natazama Documentary (yeah am that boring) nkajifunza kuwa hawa Madaktari tunaowaamini wakati mwingine wanatupa Dawa kama majaribio bila sisi kujua. Na wakati mwingine wanakula Deals na Makapuni ya kutengeneza Dawa ili kufanya Dawa husika kuwa popular au kama sehemu ya Uchunguzi. Ile "kama utapata tatizo lolote tafadhali nipigie simu haraka" hiyo ni report muhimu sana kutoka kwako kuhusu dawa husika. Ushindani wa kuuza Dawa kwenye Makampuni hayo ni mkubwa sana, imefikia mahali Madaktari wana-creat "Disorders" na kula Deals na Wafamasia ili kutengeneza Dawa "kutibu/tuliza Disorders&

Wanyumbani na Wanje....

Heri ya Wiki Mpya! Siku hizi wa Nyumbani na wa Nje zimekuwa "jamii" mbili tofauti wakati zamani tulikuwa kitu kimoja ailimradi tu sote tunatoka Nchi mmoja iitwayo Tanzania. Kuna kama kaushindani au kaubaguzi ka chini kwa chini hivi....well, nilishakuambia kuja Nje siku hizi sio deal labda ndio maana wa nje tunadharauliwa hihihihihi. Alafu tunajifanya tunajua sana utatuzi wa matatizo yanayojiri nyumbani wakati wengine hatujagusa huko mwaka wa Tano huu....kazi kufananisha tu "Kwa mfano huku blablabla" sort of people. Pia kuna wale ambao wapo Nyumbani kazi yao kulinganisha pia....wale akina "when I was in London" kind of people...."Hata wenzetu wa Ulaya blablabla" wakati hujawahi kuishi huko au ulikaa si zaidi ya tumiaka 3. Wote hamna tofauti linapokuja suala la kujifanya mnajua utatuzi wa matatizo yanayojiri Tanzania (hasa kijamii, kisiasa na kiuchumi). Sie wenye watoto wadogo haturudi moja kwa moja

Hoarders....

Hello! Mambo! Wadogo zangu wa Kike enzi zile walikuwa wakiniita....wacha ni seme tu bana....najulikana kwetu kama "mchafu" sio kwamba siogi, sishafishi nyumba au kutandika kitanda la hasha! Nilikuwa nafanya hayo yote in my own time....sio ukiamka tu unakimbilia kuosha vyombo(which I hate) au kupiga deki na kupangusa vumbi incase wageni watakuja.... So nilikuwa na-swap kazi hizo na yeyote mwenye zamu ya Kufua au kunyoosha....nazipenda kwavile zinafanywa baadae....pia napenda kusafisha choo/bafu (huwa nasafisha usiku)....hihihihi. Asa siku moja mume wa mimi na mimi tulikuwa tunaangalia kipindi kuhusu Hoarders....hee, mkibaba akaniambia wee mwenyewe ni "hoarder" aiiii niliumiaaaa mpaka nikakaribia kulia! Wacha nianze kubisha(vere mbishi nikiwa na uhakika, tabisha mpaka kesho yake) na kuthibitisha maana ya Hoarders....nikisisitiza kuwa ni Ugonjwa wa Akili. Kesho yake nikaenda "store" nikakutana na Masanduku na M

Lete Ushahidi wa unachoongelea...

Hello DHB/DHW member....year 2003 lazima umezaaka hihihihi maana mie tu niliekua katoto mekuwa kibibi(no, not princess, ni kibibi as in Mzee).....drop me a line please!! Enzi hizo bana, kulikuwa na malimbukeni wa Elimu ya juu kibawoo au niseme Wasongo....ukisema kitu online lazima wakuambie uwape/utoe vielelezo au statistics. Yaani walitufanya sie wa Elimu ya Chini going on to Elimu ya Juu(enzi hizo) tujione "hamna kitu" kabisa, tulinyimwa haki ya Msingi ya kusema tulichojisikia au tulichotaka au kukijua . Ukiongelea kitu bila kuwapa "ushahidi" wanakuambia unaongelea mambo ambayo "unadhani" unayajua, lazima mtu uwe na ushahidi wa kuthibitika kuwa unachozungumzia "umesomea" au unakisoma. Siku hizi aiii unapewa kielelezo cha picha inayotembea na sauti kabisa tena bila kuomba....shukurani kwa Teknolojia na urahisi wa ku-share yale tutakayo/ujisikiayo. Kwaheri kwa sasa. Mapendo tele kwako...