Skip to main content

Posts

Showing posts from 2014

2014....what a Year!

Ulitegemea nitaorodhesha matukio yote ya mwaka huu? Hehehehe pole. Napenda kuwa tofauti. Ahsante kwa kuichagua Blog hii siku ya leo ambayo ni ya Mwisho kabisa mwaka huu wa 2014, Ubarikiwe sana. Wiki mbili zilizopita zilikuwa hectic kweli, si unajua Christmas inavyokuwa ukiwa na Watoto? Hasa mmoja ambae sasa yupo "Shule" na huko anafundishwa zaidi kuhusu "Santa na Presents" kuliko Kuzaliwa kwa Yesu...Achana na hili. Sasa tangu nimekuwa Mama nimejikuta nasoma sana Forums zenye reviews mbalimbali kutoka kwa "real people" from Vipodozi to Kampuni za Umeme. Nikawa kwenye Forum moja ya masuala ya Wazazi, Malezi, Mimba n.k. Nikawa nasoma review za aina ya Dawa ya Kuzuia Mimba (Uzazi wa Mpango)....mwanamke sijawahi kugusa hayo mavitu. Kama kawaida hukosi maswali ya mabinti wadongo ambao wanataka kutumia Madawa hayo, nikisema wdogo kwa huku ninamaanisha 16 kushuka chini(inatisha, najua)! Binti mmoja akas

Je wee ni Muafrika Halisi?

Kwamba vizazi 9 vya pande zote mbili (baba/ yako, Babu/Bibi yako, Baba/Mama wa Babu/Bibi yako, Baba/Mama yake Babu/Bibi wa Baba/Mama yako na whoever kabla ya wote hao) vilivyopita kabla yako ni Waafrika Weusi asilia bila tone la Uarabu, Ujerumani, Ureno na Uingereza? Baada ya Obama wale Mchanganyiko wakaonyesha "rangi" yao, hasa wa huku....walikuwa wanaongea kwa uchungu na hasira kuwa wao sio Weusi bali ni Mixed, hawataki kutambuliwa kama Weusi bali Weusi na____!....Which was/is fair ila kwanini msubiri Mpaka wakati wa Obama?!!! Huwa nakerwa na tabia ya baadhi ya watu (hasa Mixed ambao U-mixed wao hauonekani bali Weusi wao) wanaopenda kusema "mie ni robo Mhindi,Nusu na robo Muingereza halafu Nusu Muafrika". Vita ya Ubaguzi kati ya Weusi Mixed na Real Weusi bado ipo na inaendelea kukua hasa baada ya "mapinduzi" ya Natura hair kwa African american aka Black peeps. Wale Real ndio wanahisi wanahitaji pongezi

Mwanamke Kujitegemea Kiuchumi....

Ndio kukoje? Unakumbuka enzi nipo Shule ya Msingi(just imagine...) enzi akina Taji Lihundi, Deo Mshigeni, Ramkim Ramadhani(RIP), Sunday Shomari....kabla ya akina JD hawajaja mjini....ndio walikuwa "the coolest"....Educated (well that is what I (myself) thought) watu kuwasikiliza na kuchukua "maushauri yao"....waliyokuwa wakiyasoma Ebony Magazine (sina hakika nimesema tu). Taji Lihundi zake zilikuwa "I want a girl who can speak at lest 3 languages, independent, have a job and beautiful" by 3 languages hakumaanisha Kinyamwezi, Kihehe na Kizaramo....alitaka Malugha ya mbele huko. Sasa huyu Baba(alikuwa mKaka then) ali-influence sana kwa akina sisi (Teenagers) enzi hizo bana, tulipofika miaka 20na na kuanza shughuli za kupenzika tukaanza kukimbia Vijana wanaoonyesha wapo sawa "kiuchumi" ili tusionekane "tegemezi". Sasa kutokana na "muonekano" wako wa Independent....unapendeza, unavaa vitu vikali nini na nini....wanaonyesha interes

Wema hadumu....

Now I have your attention, kaa chini.....Wema hawadumu (hufa mapema) ndio namaanisha. Hivi hujawahi kujishtukia na kupunguza wema ili usije ukaenda mapema? Mwanamke I have! Wema mtu anazaliwa nao (nadhani) lakini pia unaweza kujifunza kuwa mwema....sasa kupunguza wema sio kwamba unakuwa na roho mbaya bali unapunguza "misaada" iwe ni Pesa, Vitu au Muda wako kwa watu wengine. Kitendo chako hicho kinafanya wale "watu wengine" wakuone unaroho mbaya au sio mwema kiviiiiile na hivyo kuanza kukujungua na kukudongoa(kukusema vibaya) na hapo siku zako Duniani zinaongezeka (in my head)! Hayati Bibi aliwahi kusema watu wanapokusema vibaya na hata kukutakia/ombea kifo ni vizuri kwani wanakutakia kinyume chake....Unaona my NUKTA sasa! Muone mzito kumkichwa ka' m-Irish. Usije anza kumuombea mtu wako mpendwa anaeumwa afe ukitegemea itakuwa kinyume hehehehe lwako. Furahia Mwanzo wa Mwisho wa Wiki yako. Babai. Mapendo t

Akina sie on Budget...

Ili kuifanya itoke vizuri huwa tunajiita "the simple life" women....well U-simple unatofautiana nadhani unalijua hilo. Mfano hapa hunikuti na hautonikuta nazungumzia Manunuzi ya Wiki au Mwezi huko High end (Designers) pamoja na hilo pia hunikuti nazungumzia Maduka ambayo ni Lowest End.....mie nipo kati. Napenda Ubora, Mfano Bag lazma iwe Real/Genuine Leather kwani ndio my Kitu sio Trends. Sasa si nilipita kwenye Charity Shop maeneo wanayoishi Mastaa Jumamosi iliyopita, nikakuta watu Kibao kwa nje....nkauliza kwani kuna Star humo ndani? Wakasema hapana ila kuna "new stock" by new wanamaanisha Stars wame-donate Ma-used-designer Gear jana yake. Aii! Mwanamke sijawahi kumiliki Designer Bag Genuine....wee! Mie huyu ninunue Hand Bag kwa £2,340 wakati hata Tofali la Choo (sio Jimmy Choo, Choo as in Toilet eeh) sina.....hata Fake ones sina. Nikaweka u-simple pembeni....nkaunga foleni....nkajipatia "Chloe Python Paraty Tot

Happy December.....nimekuwa huru!

Nikajikuta nashindwa kusoma maandishi au kutambua Sura ya mtu kwenye Tv au popote pale ambapo ni umbali wa hatua 4, sasa naona (Navaa Miwaani baada ya kuikwepa kwa Miaka zaidi ya 15). Halafu Binti kaacha kunyonya full-time (haombi na wala hadai) hooray...whoop!...whoop! Sasa siku moja nipo Bafuni najilola(najiangalia) nikaona pale nyuma kati pamekuwa a bit "firm" and more Duara(maana ukizaa matako yanashuka/tepeta kidogo ujue)....nkasema wohooo mazoezi yangu yanalipa! Kuja kuhamaki....kumbe nimenenepa hihihihihihi(nlijipima kitu kutoka 32inch to 46). Side effects za kuacha kunyonyesha nazo, mxsiii (kama unataka kuzijua zote nitafute nikumwagie mauzoefu). Na mwisho kabisa Asali wa Moyo anaumwa "Flu"(Homa, body ache, Kikohozi na Mafua).......si unajua wanaume wakiumwa "Flu"...full kudeka hehehehe I mean "hoi" imagine wangekuwa wanazaa the Puuzi kabisa! Babai. Mapendo tele kwako...

Wale "naenda Africa", Natoka Africa....

Unawajua? Huwa hawasemi Nchi zao.....mf: unauliza (kwa kizungu) unatoka wapi? Wanasema "Africa"....where about in Afrika...."East Africa"....yes...where exactly? Sasa tangu Ebola ime-"cotton fire" Afrika inaitwa the Land of Ebola....hihihihihi watu hawasemi tena wanatoka Afrika bali Tanzania au nchi yeyote ambayo sio Magharibi ya Afrika (au karibu)! Kuna jamaa enzi akiwahi kusema (na wakamuamini) kuwa yeye anatoka Afrika, akaulizwa Afrika wapi....akasema "a small Country inside Tanzania called Tabata" na Baba yake ni King of Tabata! Mie siipendi Tanzania Kisiasa(sipendezwi na Siasa za Tanzania), lakini naipenda kama Nchi niliyozaliwa, na ndio maana sina (nimekataa) Ganda Jekundu kwa makusudi kabisa....(Kwa faida ya Wanangu)! Nilivyojihami hapo juu! Babai. Mapendo tele kwako...

Vyombo vya Wageni....!

Vinakaa Kwenye kabati KUUUUUUUbwa sebuleni (I used to hate that thing)....ila nilikuwa naelewa kwanini wengi wao (nilikuwa mtoto so simo) huwa na Kabati la vyombo (vitumiwavyo only wageni wakija) Sebuleni. Nyumba nyingi za kupanga ama Mna-share jiko au kila mtu anapika Sebuleni kwake kama sio nje ya mlango wake pale Koridoni/kwa nje, hivyo kuwa na Kabati la vyombo Sebuleni inaleta maana(Wapangaji sita, wote muweke makabati yenu jikoni? Hapatatosha). Achana na hilo...turudi kwenye "vyombo vya wageni"....mpaka leo (well mwaka juzi niliponunua Gold China Dinning Set and Tea Set*) ndio nimeelewa umuhimu wake. Kuwa sahihi naweza kusema nimejua umuhimu wa viatu vingi baada ya kuwa "Temp house wife", vitu kama vile kusafisha nyumba mara kadhaa kwa siku (nlikuwa nasafisha once a week, ile deep cleaning). Sasa nikienda madukani, lazima nikasalimie kwa akina "Home Departments"....yaani hadi nimeanza kuwaza mambo ya kuwa &

Kuchamba or Kutokuchamba (kwa Maji)

Wewe una prefer ipi? Kabla ya Waarabu (Wachamba kwa Maji) na Wazungu(Wachamba kwa Karatasi)....Watu walikuwa wakitumia Majani au Mchanga kujiswafi baada ya kushundi(Kutoa haja kubwa). Tulikuwa (utotoni) tunatumia "karatasi" (toilet tissues) siku maji yakikatika. Maji na Mkono ni sehemu ya "utamaduni" (ambao tuliletewa na Waarabu) na baadhi ni Usafi. Hii haina Uzungu bana, ila mambo ya kushika mavi yako moja kwa moja mie hata sipendezwi nayo!....angalau ukitumia "tissue" huyashiki mavi moja kwa moja pale mahala. Baadhi ya watu hudai kuwa wasipotumia maji hujihisi "sio wasafi" huenda ni kutokana na Mazoea au....well nenda karudie kuchamba tena kwani ni wazi umeacha mabaki. Ukitumia muda wako vizuri baada ya kushughulika utakuwa msafi(usisahau kuosha mikono kwa kutumia Sabuni hataka kama hujagusa Shundi lako). Kwanini nakuambia hivi? Well ni kwasababu ya Wanangu...najiuliza niwafunze kutu
Inapendeza sana na unapata hisia maalum za kipekee unapokutana na "High End" new publication wanazugumzia kitu ambacho wewe(Mimi) "nisiejulikana End" nimekizungumzia Mawiki na Mawiki yaliyopita! Unakumbuka Feminisim?hiyo ilikuwa Wiki iliyopita so achana nayo!....unakumbuka "kujilinganisha/fananisha"?.....aaah Dinah naona mbali sana ujue, nafaa kuwa Rais wa KissWay?!!! (*nimeacha kuchapa nacheka kwanza*). Pengine bila kujua unachapisha maelezo ya siku yako ilivyokuwa "njema" au unaweka picha au unaweza tu ku-share ulichonunua wiki hii kwa ajili ya wanao au mwenyewe n.k.....ni sehemu ya maisha yako hivyo unadhani ni poa tu uki-share na watu wanaofuatilia "kurasa" yako popote ulipo kwenye Social Media. Kuna mahali unafikia unakuwa karibu sana na watu hao ambao huwajui(mnakuwa connected), sometimes mna-miss-iana.....Jinsia tofauti hapa lazma "lust" au hata "love" hujitokeza....duh! Niliku

Zawadi kutoka kwa Mwenza!

Kwa siee wa Ulayani huwa tunapenda sana zawadi kutoka Nyumbani, zawadi (Radha ya Nyumbani) kama vile Ubuyu, Mahindi Mabichi*, Matembele ya Kukausha, Dagaa wa Kigoma, Viuongo vizima vya Pilau, Maembe Dodo au Embe Tanga bila kusahau Embe Ngong'a(unazijua?!!), Maharage ya Mbeya au yale ya Njano, Njugu Mawe n.k. Mimi binafsi huwa napata hizo mavitu moja kwa moja kutoka kwa Mama, lakini kwa wale wenye Wenza wanaopenda kwenda Bongo Mara kwa Mara huwa wanavipata moja kwa moja kutoka kwa Wenza wao. Tatizo ni kuwa Mwenza anapokuletea zawadi wakati mwingine inakuwa imetoka kwa Mme/Mke mwenzio bila wewe kujua. Inasemekana wenzetu walioungana na "rangi" tofauti huwa wana-miss sana "rangi" yao hivyo wanaporudi Nyumbani huwa rahisi kupata wanawake/wanaume ambao huwapatia kile wanachokikosa kutoka kwa wenza wao Weupe....Maisha yaha....namaanisha Haya!!! Halafu kuna wale ambao wanapenda tu kulala hovyo(Malaya)....Ujue! Ili uendelee k

Kuaga au kutokuaga Marehemu!

Hiyaaaa! Leo si Halloween bana, wacha nami niungane nao kwa kuzungumzia Wafu. Jana tulikuwa (Mimi na Asali wa Moyo) tunaangalia Tv, mara Tangazo la Documentary ya Ebola (Ebola crisis) hilooo! Nkasema mie sipendi kuona/onyeshwa miili ya wafu hata kama imefunikwa(hifadhiwa vizuri), kama wameenda wameenda tu hata mkituonyesha haifanyi Ebola kuwa Hatari zaidi ya ilivyo! Mwenzangu akasema, "mie sielewi kwanini watu hupenda kwenda kutoa "Heshima" za mwisho wakitegemea kumuona Marehemu kwa mara ya Mwisho, marehemu ambae hawakuwa nae karibu kama Ndugu(wa Damu). Kwanini utake kumuona Mtu akiwa Maiti? Nikakumbuka Msiba wa Marehemu Kanumba(Mungu akuongezee heri huko uliko, Ameen), ambao sasa umekuwa (in my head) kama "model" ya Misiba ya MaCeleb wa Bongo kwa Uwingi wa watu....*whispering* nasikia MaCeleb wa Kibongo wanaombea nao wajekuzikwa na watu wengi kama huyo nliyemtaja! Walioshiriki walilalamika na wengine kukasirika kwanini hawakupewa nafasi ya "kumuona"

Wacha kuzungumzia Wanao, unatukwaza!

....ambao hatuna watoto! Kabla sijawa na Watoto sikuwahi kukwazika ikiwa mtu anazungumzia mtoto au watoto wake. Niliona ama chukulia kuwa ni sehemu muhimu ya maisha yao. Wakati huo nilikuwa nazungumzia mambo ambayo hayahusishi "wazazi" hivyo ni wazi mimi pia nilikuwa nawakwaza wenye watoto (in my head). Maisha tunayoishi siku hizi "Ulayani" au Ulaya ya hapa nilipo yametawaliwa na "hofu" ya ku-offend (kukwanza) wengine.....imefikia mahali mpaka Sikukuu ya Krismasi inakwaza wasiohusika (mostly Waislamu). Yaani ule uhuru wa kuzungumza na mtu kisha kuulizia kama anawatoto haupo tena. Ila mie huwa nauliza kwanza kabla sijaanza habari za akina B-I(initials za majina ya wanagu).....wakisema hawana watoto then siwazungumzii wanangu, wakisema wanao hapo inakuwa sherehe. Suala la watoto linatetewa kwasababu lina umiza hisia za baadhi ya watu ambao kwasababu mbalimbali hawana watoto. Well, binafsi nimeacha k

Feminism....

Na ugomvi wao wa nani ni "real Feminist", yupi ni "fake Feminist" anatumia U-feminist kama "PR" na yule sio "feminist enough". Women....WOMEN!! Majuzi yaleee, well Wiki iliyopita)....nilipokuwa naandika post ya maJuzi yalee nikajihisi nakuwa Feminist! Then nkakumbuka....Nimeitwa majina mengi sana mabaya, machafu na makali tangu nimeanza kujihusisha na "maisha " ya online mwaka 1999, yote huwa hayaniumi kwasababu najua mimi sio hayo majina wanayoniita (wote hawanijui zaidi ya maandishi/text). Ila walipoanza kuniita "Dinah ni Feminist" kiasi cha kutosha, nikaanza kuchukia na kutamani kubishana au kujibu...."acha Uswahili" inakuja kichwani, nadharau na kupoteza Comments husika! Binafsi sipendi kuitwa Feminist pamoja na kuwa baadhi ya "views" zangu za kimaisha zinaweza kukufanya udhanie kuwa mimi ni Feminist. Sababu nyingine inayonifanya nichukie kuitwa "

Vita dhidi ya Ebola imeSiasa-iwa!

Kila mtu anakuja na lake, mara Wazungu wametengeneza Ebola ili "kumaliza" Kizazi cha Weusi(Waafrika)...huyu ni Mwafrika/Mweusi aweza kuwa Manasiasa au Mtaalam(daktari) n.k. Mzungu wa kawaida (mtaani) anahoji Kwanini mnahaha na Ebola iliyoua watu Chini ya Elfu Kumi wakati Malaria inaua Mamilioni ya Waafrika kwa siku? Vipi kuhusu HIV na Umasikini ambavyo vinaondoa mamilioni ya Watu....TB je? Karibu Miezi Nane tangu mlipuko "mpya" wa Ebola kuibuka(according to my kumbukumbu) Wamagharibi walielekeza nguvu zao Ukraine na Iraqi ambako kuna faida zaidi ya kuokoa Maisha ya Muafrika, Afrika.....mara boom wanapigana zaidi kuliko wenye Tatizo (waafrika)?!! Mwenyewe jana nikajiuliza, kwanini US, EU na Cuba (is Cuba....never mind) wanapeleka "jeshi" la Wataalam kupigana na Ebola which ni more expensive kuliko kupeleke Vifaa na Wataalam wachache wa kutoa mafunzo kwa Locals (Waafrika). Nikapata jibu kuwa, labda Wazungu wanajua w

Kwanini Mtoto awa wa Baba?!!

Nimekaa hapa nikafikiria(sio kweli)....limenijia tu kichwani. Kwanini tunaaminishwa kuwa Mtoto akizaliwa ni wababa, Jina lake la ukoo lazima liwe la Upande wa Baba. Ukimpa mtoto jina lingine la mwisho....baba anakuwa Mkali au anahoji kama kuna "mwenzie"! Kutokana na Mfumo Dume, nahisi(in my head) kuwa wali/na lazimisha hivyo kwasababu walijua/wanajua kuwa Baba ana sehemu ndogo sana kwenye Uumbwaji wa Mtoto. Baada ya zile Dakika Tatu (if you are lucky that is) kazi yake (baba) imeisha, isitoshe Mbegu hazina Damu so mtoto kuwa na Damu ya Baba yake ni kama 0.5% hihihihihi (lazma mnipige mkinikamata wababa). Hebu angalia suala hili kwa undani kwenye jamii bila kuhusisha Sayansi wala Dini! Kwanini hasa Babaz au ndugu Upande wa Mwanaume ndio huwa na viherehere vya kuendeleza Undugu kama sio kujishtukia kuwa hawana undugu (wanalazimisha). Stori time: Kuna siku nipo shereheni, mkaka mmoja akaanza kutambulisha ndugu wa Mama mbali-mbali l

"Ngoja nitakupigia" = Stop calling me....

Za milimo? Unawatambua wale watu ukiwapigia simu hawakawii kukuaga utafikiri wao ndio wamepiga....mnasalimiana vizuri, mara baada ya salamu...enhe nipe stori au "mamo mengine vipi?" Upande wa pili wa Simu(uliempigia) anaanzisha stori, unamsikiliza ukingonjea kwa hamu zamu yako ije ili uongezee kwenye stori husika (uongee).....yeye anakuambia " eh bwana eh, ngoja nitakupigia" halafu kimyaa. Baada ya Wiki kadhaa unampigia tena na kabla stori hazijachanganya yeye yulee "nitakupigia baada ya dk 20"....ndio imetoka hiyo mpaka umtafute tena. Mtu hutakiwi lakini hukomi mpaka mtu akuambie "sitaki Urafiki/Ujamaa/kujuana na wewe"....baadhi ya watu wanakupa "ujumbe" ili "muachane" vizuri bila kusutana, ukikimbiwa once na "nitakupigia baadae"....subiri mpaka akupigie (obviously hatokupigia). Unajua kuna watu wanapenda kuwa tegemezi kifikra.....hata sijui kama inaleta maana kwenye nili

Kutoboa Mtoto Masikio(Kutoga)

Ni umri gani hasa unapaswa kumtoga Binti yako Masikio? Na je yeye kutoga masikio na kuvaa Hereni ni muhimu kwake au kwako wewe Mzazi? Mie nilitogwa nikiwa mchanga (Miezi Sita) na nilichelewa, kutokana na Imani sijui Desturi ya mmoja wa Wazazi wangu ni lazima Binti wa kwanza atogwe na kuvalishwa Dhahabu. Binti yetu alipofikisha Miezi 3 Baba yake akasema tumpeleke akatobolewe(Togwa) Masikio, mie nikapinga na ku-suggest kuwa tumuache na akikua ataamua mwenyewe kutoga au kutokutoga. Nikaongeza, tena atakuwa na kitu cha ku-look forward to, mf: "nikifikisha miaka 15 natoboa Masikio".....kuliko tumalize kila kitu akiwa Mchanga halafu akikua tu tunaletewa Bf au Mjukuu kabisa sababu kila kitu tumekifanya akiwa bado mtoto. Isitoshe (in my head) tunatoboa watoto masikio kwa ajili yetu wenyewe Wazazi, yeye mtoto wala hajali kama anavaa Hereni ama hana "kitobo" cha kuweka Hereni. Baadhi ya Wazazi huku Ulayani wanachukulia kumtoga m

How to be Mum, Wife, HomeMaker and Blogger...

Mimi sijui! Hihihihihihi huyooo unapenda kutafutiwa kisha wee unameza tu (copy and paste)!! Mwanamke mwenye maisha kama yangu (not exactly ila kwa mbaaaali) unawezaje ku-keep up na Blog updates kila siku? Sio blog kama hii ambapo sihitaji kufikiri bali natiririka tu. Zile ambazo unatumia akili kimtindo kwa kuvuta kumbu-kumbu (Uzoefu) na kufikiri.......aiiiii Imenishinda! Basi nimefika nyumbani siku hivi, nawakilisha nilichoambiwa na Walimu wa Babuu.....Baba mtu wacha aanze kung'aka....."Mimi sifuati wanachotaka wao kwenye nyumba zao za Kizungu, nafundisha mwanangu nijuavyo mimi". Nikajiuliza kwa hasira bila kutoa sauti....hihihihi "sasa ni kwanini tunampeleka mtoto shule ikiwa hatutaki kuwa kitu kimoja na Walimu wake?". Nikasema....Asali wa Moyo, shuleni kuna Mihula (mipya imeanza August) na ili watoto waimalize vizuri, kuelewa na kwa wakati ni lazima Wazazi wa-work together na Walimu, vinginevyo mtoto atakuwa

Blogger wapya!

Hellooooo*clear throat*....hi! Kuna kipindi wana-blog (wapya) walikuwa wanasemwa sana, "kila mtu anaanzisha blog" baadhi ya Blogger wakaacha (mie nakaribia kuicha ile ingine maana.....takuambia siku ingine) hivyo naangukia kwenye "newbes" si ndio!!! Kipindi naanza ku-blog 2005(kabla sijawa serious 2007), hao hao walikuwa wakilalama kuwa Watu (Wabongo) wapo nyumba, hawa-blog kama wenzao wa MBELE(hasa Wahabari na Watu mashuhuri). Mara haooooo wote wakawa na Blogs(well baadhi).....kinachoKERA ni kuwa na habari zilezile bila kusema chanzo/Kielelezo. Mambo ya Beauty, Lifestyle, Fashion and News(kila mtu). Aaah! Who cares....maisha ya kila mmoja wetu yapo tofauti na interesting in a way hivyo sio mbaya kuongea mwenyewe via Blog kwa matumaini kuwa mtu mmoja atasoma na kucheka au kujifunza.....asa uta-Copy vipi na Ku-paste mtindo wa Maisha na Uzoefu binafsi ya Mtu? Hihihihihihi lione! Hata hivyo....Mbio zimepungua ila mizung

Lugha ya Mama kwa Mtoto...

Huku (UK) watu ambao tunaongea lugha zaidi ya Moja huwa tunashauriwa kuachana na "local" Lugha na kuwafunza Watoto wetu Lugha ya "mama".....in my case Kiswahili. Kama kawaida ya Mzungu(anajua kila kitu)....wanadai kuwa Mtoto husika atajifunza "local" Lugha (Kiingereza) akianza Shule na hii itamsaidia Mtoto huyo ku-master "Lugha ya Mama vema". Kwenye hili kuna Mawili muhimu(Kichwani kwangu): Mosi; Wanataka mtoto wako awe nyuma Darasani, kwamba akianza shule huku hajui "local" Lugha wanaoijua (wenyewe) wataendelea mbele wakati Mwanao anapoteza muda kujifunza. Pili; Aki-master lugha ya "mama" watamtumia vizuri (hawatoajiri Mgeni wa Lugha yenu) ili kufanya kazi ya Kutafasiri na pia atakuwa kajifunza Bure(hawakulipi kumfunza M-british Lugha yako). Kwanini nawaza/fikiri hivi? Well....Muingereza hana Lugha nyingine zaidi ya Kiingereza, iweje akuhamasishe wewe umfunze mwanao Kilugha chenu badala y

Nanyanyapaa au na-practice

Freedom of expressing my view? Sijui... Alikuwa Mwanaume, akaathirika Kisaikolojia kwa kuishi kwenye Mwili wa "mwanaume" wakati yeye anajijua na kuwa ni Mwanamke. Akaoa na kuzaa ili kuficha "tatizo" lake....akashindwa kuvumilia akawa anaibia Mavazi ya Mkewe na kujiremba mkewe akiwa hayupo nyumbani. Anapenda urembo na kuvaa kama mwanamke, baada ya Miaka kadhaa akaomba "Shirika la Afya" ku-fund Upasuaji ili abadilishe Maumbile na Jinsia na kuwa complete au legally "Mwanamke" . Ombili lake likapita kwa "ground" ya Kuathirika Kisaikolojia na asipofanyiwa Upasuaji(kubadilishwa Jinsia) anaweza kuji-harm.....so akanza Tiba ya Homono, baada ya Muda akabadilisha Jinsia na Documents zote zikabadilishwa kutoka Mwanaume kuwa Mwanamke. Sasa amepata Mpenzi mpya na anampango wa kufunga nae ndoa, Mpenzi huyo ni Mwanamke. Anadai kuwa anavutiwa sana na wanawake hihihihihiihi which make him a real Man(in

Bank Kuu Tz na Gmail account...REALLY?!!

Huenda wana account yao Official ambayo inawawepa mahali pazuri KIUSALAMA online. Nimepokea Email kutoka Bank Kuu ya Tanzania, ikinipa tahadhari kuwa nisipobadilisha "Details" zangu via Link waliyoiweka basi sitoweza ku-Bank Online na Bank yeyote Tanzania! Nikaenda kwa "sender" nikaona mtumaji ni "blablabla BankOfTanzani@gmail.com ".....nkacheeeka halafu nikapachika tusi! Kwanza mimi siBank na Bank yeyote Tz online, Halafu huwezi tu kuwaambia watu wabadilishe "details" zao via link, kwa sababu za Kiusalama kila mtu angepata taarifa hiyo kwenye account yake ya Online ambapo anaingia kwa kuweka "details" ambazo ni zaidi ya jina lake na Namba ya Card, yaani za "siri" na ni yeye tu ndio huwa nazo na hubadilika kila unapo BankOnline. ....aiiii naona nazungumzia System ya huku na sio ya huko Tanzania ambayo siijui. Nachojaribu kusema ni hivi;- Kama ilivyo kwenye Kutongozwa kuna Ma

Misinformation za Online nazo.

Hellooooo! Urahisi wa kuweka chochote online kwa nia ya ku-share au "kuelimisha" wengine ni mzuri sana! Sote tunajua kuwa kwenye kila kitu kuna Faida na Hasara zake, kama Mwanadamu unatakiwa kupima na kufanya uamuzi kwa kuzingatia faida zaidi (utafaidika?). Sio sote tuna-share yote(kila kitu) online....kwenye Blog ya D'hicious nimeshare mengi tu ila sio yote nijuayo (mengine naweka kwa ajili yangu mimi binafsi) na Binti yangu na Mwanae huko mbeleni Ntakapo kuwa Proper Bibi. Hali kadhalika kwenye Blog nyingine Mf za Urembo, Fashion hufanya hivyo pia....tena hawa huwa hawabani some info, wanakudanganya kabsaaaaaa(wanapindisha ukweli) ili uogope au ukosee na hivyo usitokee as Mrembo kama wao wanavyoonekana au Nywele zako zisikue kama zao. Safari yangu ya Nywele (nilishawahi kukuambia about) imenifanya nijaribu Mengi, kukosea Mengi na Kujifunza Mengi halafu nikarudi kwenye "rutini" yangu ya enzi ambayo kabla ya YouT

Kabla ya Mobile Simu na Net....

Ulikuwa unafanya nini na muda huu unaotumia Simu yako au Mtandao eti?!! Jinsi Teknolojia inavyozidi kukua ndivyo ambavyo maisha yanazidi kuwa busy na kuhisi muda haukutoshi (Masaa 24 yamekuwa machache). Binafsi nilichukua hatua ya kutoka Mtandao mmoja wa Jamii na Kujiunga na ambao ni latest one (Mwisho ilikuwa Twitter karibu Miaka 5 iliyopita) hivyo sikuwa kwenye Mitandao Saba ambayo ingenichukulia Muda wangu mwingi. Kabla ya hapo hakukuwa na Mitandao ya Kijamii, kulikuwa na Forums na Chatrooms pamoja na kuwa nilikuwa na Muda mwingi bado sikujiunga na kila Forum/Chatroom iliyojitokeza. Hapa juzi nimemsikia Business Woman akisema ameamua kufuta Email address yake na baadhi ya namba za Simu za Ndugu, Jamaa na Marafiki wasio na Mpango (wasiomsaidia kwenye Biz yake) ili aweze ku-focus zaidi kwenye Uzalishaji na Uendelevu wa Kampuni yake. Anadai kuwa Teknolojia ya Smartphone imesababisha yeye kupoteza muda mwingi kujibu Mails ambazo hazina umuhimu mais

Binti "akiharibika" arudishwa kwao....

...ambako hajawahi kuishi (hajakulia) huko maisha yake mapya ya "ukubwani hivyo kuwa Mgeni. Hii tabia mie huwa inanikera sana, enzi zile nakua nilikuwa nasikia tu watu wakisema "aah fulani, kashika mimba nimemrudisha kwao" au "amelimbukia sana maisha ya mjini, nimerudisha kwao". Unapochukua mtoto wa Mtu akiwa Mdogo kwa nia ya Kuishi nae kama "msaidizi" (which ni kinyume cha Sheria) au kukubali jukumu la kulea mtoto baada ya Wazazi wake kutangulia(Kufariki) unapaswa kuendelea kuishi nae na kumpa support/saidia ili arudi kwenye "mstari" sio kumpeleka "kwao" ambako ni Mgeni! Pia sio haki kwa watu wa kule "kwao" kubeba "Mzigo" ambao wewe Mlezi ndio uliyesababishwa kwa maana moja au nyingine. Unalea Binti tangu anamiaka, tuseme sita....tabia atakazokuwa nazo ni matokeo ya Malezi yako, hivyo ikitokea "kaharibika" Hatia ni yako, sio ya watu wa "kwao".

Watoto wanahitaji role Model sio Model!

Ah! Nimekua busy kweli....unajua umri ukienda Majukumu yanazidi/yanaibuka kila kukicha. Hapana sio majukumu kuhusu Watoto, Baba yao na Bills ni majukumu ya kuutunza Mwili na Uso ili kurudisha Miaka nyuma. Si nilikuambia by the time nafikisha Miaka 40 nataka kuwa kama Gabriel Union!! (Au niliota tu?). Nataka wanangu wawe proud of my "look" nikienda wadondosha na kuwachukua Shule hihihihi....sio wakikuona tu wanakimbia kwa aibu au wanasema "that's not my mummy, she's my Shangazi/Bibi". Eh! Nilipokuwa Msingi kuna mdada mmoja (sasa maarufu kwenye MaTv huko kwenu) alimkimbia Mama yake, tena akawa analia kabisa kuwa yule sio Mama yake....si wajua Mama wa Kinyakyusa alietoka Mbeya beak ya kwanza Shuleni hihihi hi akina Mwakaninini(naambiwa ninyi ni watani wangu upande wa Mama so usi-panic)! Eti "Children need role model Not a Model"....wacha uvivu, hebu jipende huko.....you can be both! By the path I AM FAR

Mwanaume ka' Mwanamke na Nyumba Ndogo!

Only Mwanaume husika akifanya jambo baya, la kizembe au akionyesha "emotions"! Mfano akisema ukweli pasipotakiwa (Umbea), akilia baada ya kuumia, akizimia Msibani (Wanaume hawazimii, huwa wenda wazimu hihihihihi) n.k. Tabia hiyo huwafanya Watoto wa Kiume kuwa na Tabia mbaya za Baba zao, kwasababu wanaogopa au hawataki kufananishwa na Wanawake. Kwenye Jamii yetu (Tz) Baba kuwa na Kimada siku hizi imekuwa suala la kawaida, jamii imelikubali hilo na kuwapa jina zuri eti "Nyumba Ndogo" which is sooooooo annoying, Yaani ndio kukata tamaa au?!! Sasa nyumba ndogo huwa haijengwi kwa siku moja, na mara zote Mtoto wa Kiume huwa wa kwanza kujua ikiwa Baba ana Kimada.....Vijana hujua mengi sana Mtaani/Vijiweni. Wengi huwa wanaumia kuona kuwa Mama zao wanakuwa cheated na Baba zao lakini kwa vile wanaogopa kuitwa "Wanawake" wanaamua Kuuchubua (do you still use this word??). Baadhi ya Vijana (watoto wa kiume) husi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mungu ni wa Afrika tu?

Umewahi kujiuliza kwanini sisi Waafrika Mataifa Mengine ambayo ni Masikini kuwa pamoja na kuamini Mungu na kusali kwetu kote bado hakuna Maendeleo? Kwanini Mataifa hayo yanaendelea kuwa Tegemezi wa Nchi za Ulaya Magharibi na Marekani?(Wacha sababu za Kisiasa na Historia hapa sio mahali pake).... Leo hapa (kwako itakuwa Jana) Mimi na Asali wa Moyo tulikuwa tunajadili kuhusu Ubinafsi wa sisi wanadamu, tukafikia mahali tukakubaliana (kwa kawaida huwa hatukubaliani)! Wazungu ni Washenzi kote-kote na wengi wao hawaamini Mungu as in kusali kucha kutwa na kwenda kutoa Sadaka kanisani kila J'2 lakini linapokuja suala la kusaidia Binadamu wengine wenye Matatizo huwa mstari wa Mbele! Huenda hilo ndilo linalowafanya waendelee kufanikiwa, kwamba hawakai(kupoteza muda) kusali na kutegemea Mungu awashushie Mahela ili wawasaidie wengine au kukesha na kuomba ili Mungu awape Makazi wakimbizi mahali palipo na Vita. Wanafanya yote hayo kwa Vitendo.... kuna Maduka kibao ya Misaada ambapo watu hujitole

Na-admire sana watu wa Medical...

Nakupenda kwa kuichagua Blog hii... Unajua wale wadada wakubwa inatokea unawapenda, unatamani kuwa kama wao (Kielimu) utakapokuwa Mkubwa?!! Mie nilikuwa nawapenda sana Wadada Wanasheria, Waandishi wa Habari na Young Docs (au tuliwaita Medical assistants sababu walikuwa hawajafuzu).....sasa kuna mmoja alikuwa jirani yetu enzi hizo bado kabinti, alikuwa anasoma Russia. Kwasababu alikuwa Mkubwa sana kwangu hatukuwa na utaratibu wa kuongea lakini tulikuwa karibu sana na alionyesha kunipenda kweli-kweli! Kila J'Mosi alikuwa ananiita "Dinah Mdogo wangu unakazi?(Za shule)... ukimaliza naomba uje unikwangue Mba"!! Usicheke tafadhali (hihihihihihihahahahahaha)...Basi mwenyewe nafurahi naenda kumkwangua "dada MA" Mba....honestly!!! Namkwangua, nikimaliza nampaka mafuta halafu namsuka....heee! Najua kusuka blaa tangu nina miaka 7 shukurani kwa Bibi na MSesere(Doll) wangu....nika-master Kusuka Mitindo nilipofika miaka 1

Nguvu ya Mama....

Sio aliekuzaa bali uliezaa nae (Mwanaume) na wewe Mkimama mwenye mtoto au watoto. Embu ngoja kwanza!!....Mama aliekuzaa ndio chanzo cha ninachotaka kusema hapa siku hii ya leo. Nilibahatika kulelewa kwenye Mazingira ya Imani Kuu Mbili za Dini (Wazazi walikuwa na Imani tofauti za Dini), hali ambayo ilitufanya watoto kuwa na Dini ya Baba mpaka tulipofikisha Umri wa Miaka 18!!! Aiii.....angalau tulikuwa na kitu cha ku-look forward to....errr 18th birthday na 1st Key for your own house au kuanza kulipa Kodi ya chumba unacholala hapo kwenu (nisikuchanganye na mambo ya Ulayani). Kabla ya Miaka 18 sote tukahamia Dini ya Mama...Mzee akabaki peke yake na Dini yake masikini.....hapo ndio "nguvu" ya mama inapokuja sasa. Mama akiamua watoto wasitambue baadhi ya Ndugu anaweza kufanya hivyo kirahisi kabisa na kufanikiwa. Mama akiamua kumkufanya mtoto amchukie Baba yake anaweza kufanya hivyo like pie! Mama akiamua kukua

Raha ya Tako Kubwa kutikisika...

Sanaaa ila sio kila siku though! Kuna siku mwanamke unahisi hitaji la "kikaza" Maungo huko nyuma katikati....maana mtikisiko unazidi kiwango cha kawaida(au ni mimi tu?!!). Kwa wale ambao hatukujaaliwa "Choo" huwa hatuvai "kyupi" ili kuongeza "mtetemeko".....lakini waaapi bana, kitako kigumuuu ka' Jiwe.....ila angalau halipo. Sasa usiombe uwe umebebeshwa "lichoo" halafu halitikisiki!! Au linaenda Ti------Ti-----Ti badala ya "SingidaDododoma-SingidaDodoma" Anyway! Kama wewe huna "Litako" na ungependa mtikisiko time to time (pale unataka attention) bila kubadilisha mwendo na kuendelea kuvaa "kyupi" yako.....Hongera sana kwa kuichagua Blog hii hihihihi! Unapotembea mbele ya "mhusika" achia sehemu ya Haja kubwa kama Vile unataka "Kushusha Mzigo".....Hakika tumbo lako liposawa maana.....!!! And oh....unafanya hivyo ukimkaribia Mlen

Ijumaa moja Baada ya Mauaji ya MwembeChai!

Maisha haya! Nimekumbuka 1996/97 Mauaji ya Mwembe Chai (siku mbuki vema na sitaki ku-google vilevile)! Siku chache baada ya Mauaji yale bado kulikuwa na Maandamano ya Siri ya "Waislamu wenye Hasira".....Kile kifo cha yule Kijana pale Mwembe chai akianguka LIVE baada ya kupigwa Risasi na Polisi (FFU sijui) akiwa amevaa shati la Bluu Mpauko(light Blue) kamwe haitonitoka Kichwani! Ni kifo cha kwanza nilishuhudia live(on Tv)!! Sasa bila kujua si tukaenda Kariakoo siku ya Ijumaa! Ile tumemaliza manunuzi si tukakutana na Waandamanaji na FFU...wakayaachia Mabomu ya "Machozi"....oh boy! Nilihisi Vita kuu ya Mwisho wa Dunia ambayo sina Uzoefu nayo ndio imefika!!! Kimbia, huku na kule mara Tukakutana na jamaa (sijui Katibu au Mlinzi, ila alikuwa Mhindi) Wa SSC pale Msimbazi, akatufungulia Mlango kwenye Jengo la Simba....akawa anaita akina Mama na Watoto waende kupata Huduma ya kwanza....hihihihi kunawishwa Maji Usoni(wasn't a laughing matter then)! Anyway! Baada ya hapo k

Kujikanganya nako!

Kuna siku nilisikilizishwa Nyimbo za Bi Rozi Mhando akizungumzia "Kunyang'anywa" Mali zao na Wageni..."Wao kuwa Wageni Nchini mwao". Aliendelea na kuimba kuhusu kuchukua na Kunyang'anya vilivyo vyao kwa Jina la Yesu!.....Nkajiuliza Kunyang'anya(kutumia nguvu) si ni Dhambi?!! Halafu nikakumbuka Ubunge ni Career Path kwa watu Mashuhuri ila issue nzima inayonifanya niandike hapa ni ile ya kuji-contradict!! Isitoshe kuwa Mlokole kwa Miaka zaidi ya 20 lazma utarudi nyuma (utachoka) kumsubiri Yetu (hihihihi my ribs... Wapendwa na Watumishi habari gani?) na hivyo kuhama Kanisa, Kuanzisha Kanisa Lako au kujiingiza kwenye mambo mengine ambayo ni tofauti na Misimamo yako. Si walokole tu wanaoji-contradict kwa kukataa "Mikorosho" lakini wakati huohuo Kumuita Yesu ni Mume wa Wajane (Wajane sio Wanawake tu kama ulikuwa hujui, kuna Wajane wanaume) kwa mfano tu!! Kujikanganya ni kitu cha kawaida ailimradi

Kizazi cha Santuri, Kaseti CD Vs MP3...

Nimekatiza mahali mtaa wa ki-Posh nikakutana na "Bei Nanini CafE" haraka haraka akilini ikaja "Price and what's not"....not exactly what they meant ni mimi tu na Utamu wa Kiswahili.....liwache hili! Unakumbuka enzi zako ulipokuwa unakuwa miaka ya 92+ hapo ndio Tv zinaanza kuchanganya(sio Vituo) bali watu kumiliki Tv(wageni wa Jioni wakapungua nyumbani kwetu). Kila ulichokuwa ukifanya Mzazi wako anakukatalia akisema "enzi zetu tulikuwa hivi na vile....sio nyie watoto wa siku hizi"! Halafu unatamani kumuambia "sasa Mama enzi zako si zimeisha, hizi zetu" lakini huwezi, unaishia kununa. Nakumbuka Baba(Marehemu) alikuwa anasema "hivi huko Madukani hakuna nguo za wakubwa, zote ni za watoto tu?" Akimaanisha zinabana au fupi!....tukamwambia "Baba hii ndio mitindo ya kileo".....alisema "vaeni mtakavyo lakini mkija Ofinisi kwangu sitaki kuona chupi ndefu" (Suruali za Kubana).

Kizazi cha Miaka ya 90!

Na haraka zao!! Yaani wapo mbio-mbio tu japo mbio zao zinatofautiana.....kuna wale wa starehe(Now) na wa maisha yajayo(Future)!! Mdogo wangu wa Mwisho anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Nilipopata habari za yeye Kuposwa nilipata hasira za ajabu! Nikabaki nalalamika "yaani mdogo wangu mdogo hivi anaolewa"...."Vipi huyo mwanaume akienda kumtesa"? "Kwanini asisubiri kidogo jamani akue (huku nalia) bado mdogoooooooo" she's 23yrs! Mama akaniuliza(Simuni), ningekupa taarifa kuwa anamimba au kazaa ugelia kiasi gani?!! Kabla sijajibu!! Asali wa Moyo nae akauliza swali hilo hilo(live).....nikasema but she's my little sister....can she just wait another 2yrs?!!! Anyway, ilinichukua mwezi Mzima kukubali kuwa my baby little sister-o anaenda kuolewa!! Sasa leo naongea nae, ananiambia "nipo site dada" Nkauliza Site ya maandalizi ya Ndoa? Akanijibu "Hapana Da Dinah, tunajenga"!!

Nimeachwa na Teknolojia...

Ah! Nimebanwa kweli siku mbili hizi....ila nafurahi kuwa nimepata muda wa kuongea na wewe kabla sijaenda kulala.....mmh! Tangu nimekuwa Mama wala hakuna kulala ni kujilaza tu. Kuna tuwimbo tuwili twa Ali Kiba tunanikuna kweli yaani "Mwana Daslama" na "Kimaso" ingekuwa zile Kanda za enzi ninge-rewind kwa Penseli mpaka Kanda ikatike....ujue kuna Wasanii wa Bongo Flava halafu kuna Ali Kiba(I just love that Kid). Achana na hili. Jana nikaenda Dukani kuangalia Simu....Teknolojia imenishinda au niseme tu imenipita! Simu yangu ya mwisho ilikuwa (usicheke) Blackberry Bold 9900, ikatumbukia chooni (umama siku za mwanzo uliniCost!!!). Siku naenda mtembeza mwanangu City center kwa mara ya kwanza si nilipanda Treni heheheheheeeeeeee mwanamke nashuka na "Pram" lenye Mwanangu obviously!!....nikaacha Hand bag kwenye Treni(walinirudishia though)! Turudi kwenye Teknolojia ya Simu, wala siamini kama nimekaa Miaka 3 bila

Mtu chake...

Kwa kawaida mimi sina tabia ya kuangalia watu ninapokuwa natembea na hata kama nimekaa mahali nitakuangalia kama nimependa ulichovaa....na kuangalia kwenyewe ni kwa Sekunde chache tu. Kuna watu wanajua kukodolea macho wenzao bila kupepesa! Yaani anakukazia macho mpaka unaona aibu kwa ajili yake! Ukitaka ugomvi na watoto wa London wale wa Uswahilini bana wakazie Macho hivyo....anakufuata na kukuuliza "what you looking at?" huku kashikilia Kisu! Kisu bit pale juu nimeongezea tu chumvi, ila kuna vipigo na vifo kadhaa vilitokea kutokana na mtu kumkodolea macho mwenzie. Stori time: Sasa jana tupo mtaani tunatembea na watoto....nyie mnatoka Weekend sie twatoka J'tatu....kisa na sababu? Ili tusiwe sawa, hakuna lingine wacha kutuJAJI eeh! Nasikia Asali wa Moyo analalamika "mijaume ya kiafrika sijui ikoje (yeye mwenye Muafrika) inamkodolea macho mke wa mtu wakati inaona kabisa yupo na Mtu wake" Hee! Nka

The why's!

Nilijua siku nikizaa mmoja kati ya wanangu (au wote) watakuwa waongeaji sana kama errr Mimi?!! Well, najua kuwa napenda kuongea (labda kwa vile sinywi pombe au sina nguvu ya kupigana) lakini sio muongeaji kihiiivyo. Nakumbuka Marehemu Baba alikuwa anawaambia watu "aah kuwa makini, binti yangu huyu anamaneno sana". Kiukweli kabisa na admit mimi ni Mbishi sana....nope! wala sina asili na watu wa Kibondo, Kigoma! Labda kwa vile sina Nguvu za kupigana lakini wakati huohuo sipendi kuonewa, sipendi kudanganywa na siamni katika "kubali yaishe" BS na wala sio "ndio bwana"....sasa nikiwa na uhakika na ninachokisema nitakubishia mpaka kesho muda kama huu. Turudi kwenye uongeaji ambapo ndipo Babuu(my 1st born) anapokuja sasa....Laaaa! Mwanangu anaongea jamaniiiii....akianza stori zake....halafu ana "why's" za kutosha. Maana nilikuwa nahofia Hisabati akianza shule, sasa nina shughuli ya kujibu wh

Mama wa Nyumbani...

Kwa mwaka mmoja na nusu (au tuseme miwili maana nilianza likizo ya Uzazi nikiwa na Mimba ya Miezi 5) nimekuwa Mama wa Nyumbani. Mie kuwa Mama wa nyumbani ilikuwa choice kutokana na moja ya Misimamo yangu ya kimaisha ambayo wengi hushindwa kunielewa....kwamba miaka 3 ya mwanzo ya wanangu ni lazima niifaidi (as in kuona wanavyobadilika kila siku, kuwafunza manners n.k kabla hawajaanza shule rasmi). Pia ile hali ya mimi kutoamini mtu mwingine kuangalia wanangu, nahisi kuwa hawatawapa huduma, upendo na attention inavyotakiwa, na wao hawataniambia kwani bado wadogo. Hiyo ilikuja baada ya kujifungua mtoto wa Pili, yule wa kwanza bado nilikuwa na ile "lazima nirudi kazini, am financially independent working Mum" hivyo Babuu akawa Day care akiwa bado mchanga. Back to Mama wa kunyumba! Heeeeeeee! Nawaheshimu wote, kazi yenu ni ngumu, Kuzaa is nothing compared to Mama wa Nyumbani na anashatili malipo ya juu ambayo ni zaidi ya £60,000 kwa mwaka....well sio wote bali wale ambao hawana

Maghorofa-2

Siku nimekatiza mahali nkasikia sauti ya Kike kwa Lafudhi ya Kipemba "Bwana Dullah wee panda basi mwenzio nipo hoi".....nkajisemea eh watu na shughuli zao asubuhi-asubuhi. Wacha mawazo machafu! Bwana Dulla alikuwa Chini ya Ghorofa akitaka Bibie amfuate kwani aogopa panda Lift-ini peke yake! Sasa Glasgow-Scotigo kama nilivyogusia jana ni Jiji (lililozubaa) lakini linamajengo Marefu mengi kuliko Majiji mengine ndani ya UK. Pamoja na sifa hiyo wataalam wanadai hayakujengwa vema na mbaya zaidi yana reputation mbaya ya "Komando Yoso" Vijana wakorofi na familia mbazo ni masikini(wanaotegemea Benefit). Wananchi wakaanza kuzikimbia nyumba za Maghorofani na kukimbia maeneo ambayo kuna majengo hayo Marefu kwa kuhofia "status" zao na kuibiwa au kuuwawa. Baada ya Muda Serikali(almashauri ya Jiji husika) wakaamua kuyabomoa yale ambayo waliona ni ghali sana kuyatengeneza na Mengine kuyagawa(kuyauza) kwa Mashirika

Majengo marefu(Maghorofa)!

Kuna yale yaliyojengwa kati ya Miaka ya 40s na 70s ( I guess) Ilala, na yale pale kati ya Mnazi Mmoja na Stesheni, Posta, Kariakoo, Tandika, Keko, Upanga, Ostabei. Halafu kuna yale ya Miaka ya 80-90 maeneo ya Tabata, Mbezi Beach.....tulia, nazungumzia Maghorofa ya NHC na ya Kampuni kubwa kama vile TTCL, PPF na kadhalika sio yake binafsi. Ninayoyataka hapa ni yale ya 40s-70s, ambayo hayakujengwa katika mfumo mzuri wa Maji safi na Maji taka, Nyaya za umeme zimekaa kihatari-hatari na Juu ya Ghorofa ya Mwisho kuna uwazi kwa ajili ya eer "kupunga hewa" " kufurahia the view"?!!! in which kwa nchi yenye watu wenye ma-stress na ma-depression kama UK ingekuwa rahisi kujipoteza (kujirusha ili kufa).....mbona tungewa-sue NHC mpaka wangekoma. Pamoja na hasi hizo bado majengo yale yana sifa ya kujengwa kwa kutumia Malighafi Imara ukilinganisha na Maghorofa yanayojengwa Karne hii. Magorofa hayo yakikarabatiwa mmmh itakuwa gharama kuu na pengine kulipuliwa na yaanza kuanguka labd

Reality Tv Shows....

Haiyaaaaa (Waswahili wa huku ndio wanasalimiana hivyo)....Wakishua wanasema how do yo do.....asa nani anamuda wa "hau-du-yu-du Maisha haya?!! Unakumbuka enzi Reality shoo zinaanza kulikuwa na slogan ya "Movies are boring, Reality is exciting"....well not exactly ila ili-sound hivyo bana eh! Basi bana si Ndio akina Kadarshian* wakaanza na mimi nikiwa mmoja wa watazamaji wa mwanzo kabisa nikiamini kuwa nilichokuwa nakiona ni uhalisia wa Maisha yao....kwa miaka miwili.....mai miaka Miwili naangalia scripted "reality" Tv shoo (nalia hapa kwa aibu). Basi bwana, nikaacha kuangalia na kuchukia Reality Tv shoo zote ikiwemo Big Brother! Sasa nilipomimbika 2012 nilianza Likizo ya Uzazi nikiwa na Mimba ya Miezi 5.....unataka kujua kwanini? Hehehehehe aiii nilikuwa "rough" sana na kazi yangu inahitaji u-smart bana, nkaona mmh ntakosa Maternity Leave hapa, mwanamke wacha nikimbie mapemaa(natania). 2012 ndio nikaanza tena

Kupenda kusifiwa....

Ah! Kama wewe ni mzuri wa jambo fulani hakika utakuwa unajijua hivyo sio mbaya kujisifia mwenyewe.....au subiri Mpaka urudishe namba (ufariki) ndio watu wakusifie kwa Mema na hata kwa yale mabaya yako. Mmh! Lamini ukifariki unakuwa umemaliza ya Duniani, sasa sifa za Walimwengu uliowaacha zitakusaidia nini? Kungekuwa na uhakika wa Sifa hizo kukupunguzia Madhambi uliyofanya au Ukali wa Moto siku ya Kihama, ingekuwa Poa! Sasa, kuna Watu wameumbwa kuzitafuta Sifa kwa nguvu.....yaani mtu anatengwa, anafanyiwa maovu na mabaya yote lakini yeye yumo tu kujionyesha Mwema kwa hao Walimwengu.....wacha kujipendekeza, fanya yako....hutakiwi na huna umuhimu kwao! Unawajua wale Jamaa wanafanyiwa mabaya, wanaharibiwa familia zao au Mradi ambao ulikuwa Tegemeo kiuchumi....Jamaa waharibifu wakirudi na kuomba Msamaha wanasamehewa na Ujamaa unarudi upya. Mie siwezi bana, ukinitenda ama nalipiza Kisasi kwa Jamii yako Nzima au nakufuta akilini (nachukulia kuwa

Kuwekana...

Heloooooooo there! Mie huwa sishangai mtu akimchomekeza Jamaa yake (binamu, mtoto wa ba' mdogo).....nilishakuambia Ndugu ni wale mnaochangia Damu kwa Baba na Mama vinginevyo nyie ni jamaa tu! Hii haina "Dinah kakaa sana Ulaya kabadilika"....tangu Mdogo mie huwa siwachukulii Jamaa kuwa Ndugu! Ndugu zangu ni wale tuliotoka Tumbo Moja au Baba na Mama Mmoja.....kama hutaki kukubali bana shauri yako! Mambo ya kulazimisha Undugu bana ni kumaskishana (kutiana umasikini) na kuongezeana ma-stress tu.....hii ndio huwakosesha watu "bahati" ya kufanikiwa. Bana mie ningekuwa sijui nani ni nani Serikalini halafu kuna nafasi za kazi zinapatikana unadhani nitakuajiri wewe wakati nina Mpwa wangu (Jamaa) anaelimu na ujuzi ka' wako nyumbani? Aiii nitampa nafasi yeye kwanza, akiikataa ndio wewe wa Nje utafikiriwa. Najua sheria za kazi na kadhalika BUT Mpwa wangu sio Ndugu yangu, hatu-shei damu wala Ubini sasa undugu unatoka w

Umewahi ombwa Mchango wa Birthday?

Huu ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa heshima wa Vipato vya watu....hii kwa Michango yote isipokuwa Ada ya Shule. Kama humudu kulisha watu kwenye sherehe ya kuadhimisha siku yako ya kuzaliwa si uachane na issue nzima ya Sherehe!! Kujitegemea Kiuchumi kumegawanyika katika makundi mbali mbali ujue...(sina uhakika, najaribu kulazimisha tu hapa hihihihihi).....! Kuna baadhi ya watu ambao huishi kutegemea wenzao ili kufanikisha mambo au jambo kwa faida zao Binafsi......wandugu jitegemeeni kiuchumi EBO!!! Mchango wa Harusi: Wakati harusi(Bikira) yenyewe wewe na mtarajiwa wako hamna hiyo HARUSI. Kama hamuwezi kulisha wageni wenu kwa kutumia vipato venu basi fungeni Ndoa mkiwa peke yenu wawili na mashahidi....eti? Siiiiiiimple + no stress. Birthday Party: hii sinimeisha isema kule juu? Eeeh kuna hii hapa chini: Michango ya Baby Shower: Kwa kawaida ukialikwa unaenda na Zawadi inayomhusu Mtoto mtarajiwa si ndio? Sasa hii biashara

Religious vs Believe in God

Nilikuambia nipo Michezoni Glasgow-Scotigo, basi bwana si nkakutana na jamaa wakaniuliza kama mimi ni Religious, nkasema hapana ila naamini Mungu.....acha washtuke!!! Udini unatutenga, Udini unasababisha watu wasifanye mambo kwa uhuru, Udini hukosesha watu wake/waume wema n.k. Hivi unajua kuwa Dini zililetwa na Wageni ambao sasa ama hawazifuati au wameamua kubadilisha waliotuaminisha kuwa "yaliandikwa" na nani sijui nani. Halafu Waafrika tunaanza kuwaona namna gani vipi hawa jamaa wanatubadilishia Maneno ya kwenye Vitabu vyetu vitakatifu ili kuendana na "maisha" ya sasa! Ama kweli Dunia imefikia mwisho. Tunajipa Moyo na kushikilia Imani zetu tukiamini kuwa ni za kweli na kuponda hao Wageni (Wamagharibi na Waarabu waliotuletea hizo Dini) kuwa ni Wafuasi wa Shetwani. Baada ya wao kuchoshwa na Imani mbili tangu Miaka 2000 iliyopita wengi wao wakaamua ama kuachana nazo au kuanzisha nyingine ili ku-suit maisha yao ya Nyakati hizi. Sasa wewe unapoteza Muda wako wote kuja

Review Undugu wako...

Familia/koo nyingi huwa kuna mtu ambae karibu wote wanaMshuku....wanamuona hatari....kutokana na mambo yake Kiuchumi kuwa safi na kila anachosema basi ni "sheria" au hupewa "umuhimu" au "umakini" hata kama alichosema ni upuuzi! Yaani watu kwenye Familia\Ukoo husika hawaishi kwenda kwa huyo mtu, watoto wake, Mke/Mume wake wote wanapewa attention tofauti na akina nyie Hohehahe. Mtu huyu na Familia yake hufurahia yote hayo na huwa on the look out kuona nani anakuja speed ili kuwa kama yeye au kumpita Kiuchumi....basi akigundua atafanya kila alijualo kuzuia Ndugu (tumbo moja) au Jamaa(ndugu wa mbali wale wa kuunganisha mjomba, binamu etc) asifanikiwe. Umewahi kumpa Ndugu yako wa hivyo idea ya Biashara au Mradi halafu akakukatisha tamaa kisha yeye anaifanya hiyo Biashara au ule mradi ambao alikuambia kuwa huwezi kufanikiwa ukiufanya, kwamba utapoteza pesa tu??.....hihihiihi sasa amka na review Undugu wenu! Mtu

Glasgow 2014....

Siku ya Pili ya Mashindano ya Jumuiya ya Madola, nipo eneo la Tukio kwa Wiki 2....interested?....me neither! Kama umewahi kufanya kazi au kutembelea Jiji la London au NY au hata Dar(City Centres sio Keko sijui Masaki huko, nazungumzia "kiini")....ukija Glasgow bana.....ka' sio Jiji, yaani hakujachamgamka kiviiiiiile(ka' Jiji)..... Ila kuna kama "fun fair" kwa kids(sijui wanaitaje bana), nadhani hiki ndicho kitakachonileta huku mara kwa mara. Michezo imeingiliwa na watu kutoka "Makabatini" bwana, wamefanya watu tushindwe ku-concentrate na Mashindano.....yaani "ukorosho" wao una distract kimtindo....maana wengine tulikuwa tunapenda Mbio na Kuogelea....kuangalia "zile maumbile" za Wakaka pale kati na Miguu (au ni mimi tu nakua pervert wa Kike....hihihihi). Siku hizi bana mtu unajisikia vibaya hata kuangalia mchezaji, akili kama inahamia kwenye akifanyacho private! Kwani lazima watuambie wao wana

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Chuki....

Ni sehemu ya Ubinaadamu si eti! Kama unaweza kupenda basi ujue unaweza kuchukia pia....zote ni hisia! Mie bana ukiniudhi kwa kiwango cha kutosha na ukijaribu kuingilia Maisha yangu binafsi nakuchukia wewe, Familia yako, Ukoo wako, Jamii yako, Kabila lako na Nchi yako kwa Ujumla. Yaani watu wanaotoka huko unakotoka wewe wote wanakuwa Maadui, yaani siwaPENDIIIIII mf ni Wanajeria.....Mungu anisamehe ila daa! Nawachukia balaa.....wengine ni wale Majirani zetu waliozima ka' umeme wa Tanesco (what does it mean) ambao hatutaniani na Kiswahili kwao ni sawa na kuwa Malaya the Nigerian of East Africa....BOY I HATE THEM. Alafu kuna Wazimb hihihihihihi nikupe stori? Ni washenzi.....hapa hapatoshi kwa stori, maana ninazo nyingi. Huyo mimi, halafu kuna wewe (sio wewe bali yule)....ambae unamchukia tu mtu wakati wala humjui, hujawahi kukutana nae na wala hajawahi kujihusisha na lolote linalokuhusu! Unaanza Vita!.....aah! Kuna jamaa namkumbuka alikuwa namuandama mwenzie kwa chuki ya wazi kabisa ha

Nipo mtaani kwako, upo home?...

Sipendi hii tabia kwa Moyo Mkunjufu kabisa!!! Nilikuwa namkimbia rafiki yangu Mghana kwa tabia hii....niambie basi siku moja kabla hujaja kuwa unapanga kuja kwangu....sio unafika Mtaani kwangu au pengine Mlangoni halafu ndio unaniambia kwa Simu! Sio peke yake, hata ndugu (wa mbali) na jamaa wanatabia hiyo....kuna siku (nikiwa bado Nyumbani) nilimrudisha mtu kwao on next flight....the next Bus bana, hela ya next flight mie ninayo?!!....nikaambiwa nina Roho Mbaya. Katoka huko Mwanza sijui wapi eti kaja kutafuta Kazi, asa kwanini usituambie mapema tujiandae na Bajeti!....anyway achana na hilo. Mie huwa sifanyi jambo ambalo najua sipendi kufanyiwa, tatizo linakuja pale Mwenza wako sasa anatabia hiyo....hehehehe Baba Babuu Asali wa Moyo wangu bana anaudhi kweli!!! Mnaweza mkawa safarini mara akakumbuka fulani anakaa karibu na hapo mnapopumzika labda....ananyanyua simu "eh bwana fulani! Upo nyumbani?....tupo hapa karibu kama vipi tuje kuwasa